Tuesday, 10 March 2015

[wanabidii] Re: [Mabadiliko] Kufukuzwa Kwa Zitto Chadema: Nimepokea Taarifa Kwa Masikitiko..

Magid, 

Suala la Zitto sio jipya. Ninakwenda sambamba na Kitila na wenzake. Lakini kubwa zaidi ni kwamba anayekosea anaomba radhi na radhi inapokelewa kulingana na aina ya kosa. Tumeshuhudia juhudi za kutaka kukiua CHADEMA kwa makusudi mtu kama huyu anayekojoa au kunyea sahani yake ya kulia chakula hana msamaha dawa yake ni aidha kumtibisha kichwa kama yuko tayari kutibiwa.

Sakata la Zitto ni tabia na ugonjwa mbaya ambao vyama makini haviwezi kuufumbia macho. Tabia hizo ndizo zinadumaza mabadiliko kwa kuusaliti upinzani. Zitto na wenzake walitaka kufanya mapinduzi ndani ya chama. Marafiki zake tumewasikia huko ACT walikoenda. 

Ktk mapambano heri kupoteza askari mmoja mzembe kuliko kuangamiza kikosi kizima. 




Sent from Samsung Mobile



-------- Original message --------
From: Maggid Mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com>
Date:
To: wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>,mabadilikotanzania <mabadilikotanzania@googlegroups.com>,Wanazuoni@yahoogroups.com
Subject: [Mabadiliko] Kufukuzwa Kwa Zitto Chadema: Nimepokea Taarifa Kwa Masikitiko..


Nimepokea kwa masikitiko taarifa kuwa ndugu yangu Zitto Kabwe amefukuzwa kwenye chama cha Chadema. Ni habari ya kusikitisha unapotafakari demokrasia tunayojitahidi kuijenga.

Zitto amekuwa mwanachama wa Chadema tangu akiwa kijana mdogo. Mwenyekiti wa chama hicho , Freeman Mbowe, amenukuliwa mara kadhaa akikumbushia jinsi alivyoshirikiana na Zitto kuhamasisha vijana wengine waliokuwa vyuoni kujiunga na Chadema.

Kwenye siasa za vyama kuna kutofautiana kifikra na kimitazamo. Na mara nyingine migongano huwa inahusu kugombania nafasi za uongozi. Haya ni mambo ya kawaida kwa chama cha siasa. Hayapaswi kuwa sababu za viongozi wa vyama kuwafukuza wanachama.

Kwenye siasa tofauti humalizwa kwa hoja, kwenye vikao. Na anayekiuka taratibu za chama kumfukuza kwenye chama ni adhabu kubwa na kali kama ya kifo. Maana, anayejiunga na chama hufanya hivyo kwa mapenzi. Anapokosea anaweza kuonywa au kuadhibiwa, lakini, kufukuzwa kwa misingi ya kutofautiana kifikra na kimitazano si hulka njema.

Zitto Kabwe ni mwanasiasa kijana na mahiri. Chadema ilipaswa imvumilie na ishindane nae kwa hoja, lakini, si kumtupa nje kwa staili tuliyoishuhudia.

Chadema, kama chama cha siasa, isijiandalie mazingira ya wanachama wake kuwa na hofu ya kufukuzwa pindi wanapotofautiana na viongozi wa juu. Itapoteza kisiasa.

Na hili la Zitto Kabwe linatukumbusha kile ambacho binafsi nimeandika mara kadhaa, juu ya udhaifu kwenye Katiba yetu. Kwamba Mbunge aliyechaguliwa na Wananchi anaishi kwa hofu ya rungu la chama.

Kwamba leo Wananchi wa Kigoma Kaskazini wanampoteza Mbunge wao waliyemchagua kwa maamuzi ya Chama anachotoka Mbunge wao. Haya ni mapungufu makubwa. Wananchi hapaswi kuadhibiwa kwa maamuzi ya vyama.

Nachukua fursa hii kumtakia kila la heri ndugu yangu Zitto Kabwe, nikimuasa asikate tamaa, akipata fursa nyingine, aendelee na siasa na hususan uongozi wa uwakilishi wa wananchi. Aendelee kuwa sauti ya wasio na sauti, popote pale.

Maggid Mjengwa,

Dar Es Salaam.

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CAMD-ye7WpzasmKLQapWvO7FYpGtR3MD0jjWpVRLb8k%2BBt-ZYbw%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment