Wednesday, 27 November 2013

Re: [wanabidii] TUSIRUHUSU WOGA KUWA SIFA MPYA YA UONGOZI TANZANIA

Safi kabisa. Tena mazingira yanastahili kuwa bora zaidi kwa Serikali kuhakikisha vyombo vya dola havitumiki kuhujumu vyama vya siasa. Tunaiga mifumo ya magharibi wa umri wangu tunafahamu kashfa ya Watergate iliypomuondoa Nixon kwa kuhujumu chama cha upinzani. Pasipo kuliangalia hivyo tutakuwa tunajidanganya pia. Tena hili tunaliacha pembeni sijui ni ushiriki wetu au lina joto kali?

From: Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Thursday, November 28, 2013 9:53 AM
Subject: [wanabidii] TUSIRUHUSU WOGA KUWA SIFA MPYA YA UONGOZI TANZANIA

TUSIRUHUSU WOGA KUWA SIFA MPYA YA UONGOZI TANZANIA 

Vijana tuwe na mawazo huru na tusimamie yale tunayoyaamini yana tija kwa Taifa hili. Hatuwezi kupata viongozi wazuri na imara kwa njia ya kujipendekeza. Vyama visimeze uwezo, ujasiri na uthubutu wa vijana katika ujenzi wa nchi yetu ambayo kimsingi inahujumiwa na wachumia tumbo. Ni wakati wa kujitambua na kuacha ushabiki wa kijinga maamuzi yetu na sapoti yetu katika siasa, serikali na viongozi wetu yasimamie uhalisia na si ushabiki. Wananchi wananafasi kubwa ya kuwashape viongozi wao, wananchi wanaojitambua hawaburuzwi na viongozi wao bali wanasimamia viongozi wao kuzingatia misingi ya uongozi. 

Demokrasia ianzie ndani ya vyama vya siasa, kama kuna chama kitashindwa kusimamia haki na demokrasia kwa wanachama wake basi hakitaweza kuwatendea haki wananchi ikiwa kitapata fursa ya kuongoza dola.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.


0 comments:

Post a Comment