Thursday, 28 November 2013

Re: [wanabidii] Ripoti ya Siri juu ya Zito: Kosa la CHADEMA

Mgonge Mgonge ndugu na Mtanzania Mwenzangu, pole pole mkuu, Kama CHADEMA itafanya haya uliyoandika, ni dhahiri kabikisa kitakuwa kwenye hali mbaya. Nina sema hivyo kwa kuunga pia hoja nzuri aliyo itoa ndugu Elisa Muhingo. 

CHADEMA walikuwa wanajua ni nini kinafanyika na ambacho anakifanya Zitto, tukianzia kwenye Uchaguzi wa mwaka 2010, yapo mengi yalizungumzwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu Zitto na tabia yake. Mengi tuliyasoma na mengi tuliyasikia na wengine kudiriki hata kuona Adhari zake. Nirejeee kunukuu hili swahili la ndugu Elisa Muhingo "Hebu jiulize Zitto wa hoja ya Buzwagi ndiye huyu tunayemuona siku hizi?" 

Ni wazi kabisa hili linajulikuna na CHADEMA wanalijua, kuwa ni kitu gani huyu Zitto kilimfanya anyamaze kuitetea/ ama kuizungumzia hii hoja ya Buzwagi?

Kama Chama kilifahamu, na kikaka kimya kumsoma ili kujua anaelekea wapi, Basi kingeshahili pia kumwacha na kuamua tuu kuchukua jukumu la kumuonyesha waraka aliokuwa ameundika na wenzake, halafu chama kikae kimya, ili mwenyewe Zitto ajikanyaje na kujiharibia . 
Lakini kwasasa ni dhahiri na ni wazi kuwa Watanzania walio wengi walikuwa wanamuona huyu Zitto alikuwa mwanaharati shupavu, leo hii CHADEMA wanamvua uongozi ghafla na kumtaka ajitetee laa sivyo anafutwa uanachama. Je hawaoni kuwa walio wengi wanaomjua Zitto kuwa ni Mwanaharakati mzuri watakikimbia Chama?

Je Mtoto wako ndani ya nyumba yako akiwa anatoa siri za chumbani mwako ama kujititimua na kutaka aitwe Baba, utamfukuza nyumbani mwako? Ama utamuita na kumuonya na kuchukua tahadhari kwakwe na kuwa makini na yeye? 

Mimi sipo kwenye chama chochote kile, sio CCM wala CHADEMA, ni mpenda maendeleo yanayoletwa na vyama vya Siasa, chama kikiwa makini lazima nikisifie. Kwamfano CHADEMA. Lakini sasa napatwa na kigugumizi maana mwendo wa kuelekea kwenye Ukombozi naona unapata vikwazo vingi na vikubwa, ukizingatia tunaelekea kwenye uchanguzi mkuu soon?.
Kwa mawazo yangu, CHADEMA ama uongozi wa CHADEMA ukae chini upya, na kujaribu kutumia Busara zaidi ya hii iliyotumika awali.

2013/11/26 mngonge <mngonge@gmail.com>
Hakuna sababu ya kuogopa kujisafisha kama kuna uchafu, ili chama kikomae lazima kipitie mapito kama haya. Ni hatari kukaa nyumba moja na mtu usiyemuamini wacha kila kitu kiwekwe hadharani, majipu yapasuliwe ili amani ipatikane. Ni fundisho kwa vyama vingine vya upinzani vipate kuelewa nini hasa tatizo ndani ya vyama vyao na mwisho watakuwa salama.

2013/11/26 Mike Zunzu <mikezunzu@yahoo.co.uk>
Elisa,
Umesema sahihi kwamba vurugu hizi zinatokea wakati mbaya sana karibu na uchaguzi mkuu, hadi vumbi likatulie si leo, umesema sahihi pia kwamba si watanzania wote wanaotambua maana ya sera, sera kwa wengini inamaana chama, ukimuuliza ni sera za cha kipi zimekufurahisha, anakujibu; sera yangu mimi ni chama Fulani.
Ni wazi wako wengi wanaounga mkono chama Fulani kwa sababu ya mtu Fulani, nawafahamu jamaa zangu huko kijijini ilitokea uchaguzi mdogo nikawa maeneo ya nyumbani, jamaa zangu hata wanakwaya kwa ajili ya chama ambacho hata hakikuwa na matumaini ya kuleta upizani , nilipowauliza kuwa nini wanaunga mkono chama hicho, walichojibu; kiongozi wa chama hicho anatoka mkoa wao.
Ni wazi kuna kundi la watu watakao ondoa mkono wao kwenye kuunga mkono kwa sababu wat Fulani wamenyofolewa nyazifa zao, lakini cha mhimu kwa CHADEMA ilikuwa ni kuchukua hatua kama kutakuwa kulikuwa na ukweli wa kutosha juu ya jambo, unachosema Elisa kwamba wangelimwita wamuonye, huwezi kufahamu pengine walishafanya hivyo je, na pengine siyo mara moja?
Kinachonishangaza mimi kama yanayosemwa yanaukweli, ni ujasiri wa hao walioshikiki kufanya hizo hujuma, hata kama ingelifanikiwa, pengine waliofanyiwa hujuma nao wangeli react, ni kipi kingelitokea? Siyo mfarakamo mkubwa wa hata kukivunja chama, je nini yangelikuwa matumaini ya huyo mwenye kiti mpya wa chama ambacho kingelimegeka vipande vipande?

On Tuesday, 26 November 2013, 9:03, ELISA MUHINGO <elisamuhingo@yahoo.com> wrote:
Hatimaye Tunasoma ripoti ya Ujasusi aliofanyiwa Zitto wakati akipanga kukihujumu chama chake.
Mimi si jasusi wa CHADEMA wala si mwanachama wa CHADEMA. Ni mwana CCM lakini ni Mtanzania zaidi. Hii iko wazi katika michango yangu. Licha ya kutokuwa jasusi wa CHADEMA dalili za uasi wa Zitto ulikuwa unaonekana wazi. Wakati mwingine nilikuwa nawashangaa wasiouona na wakati mwingine nilikuwa nawashangaa wanaouonyesha bila kukusudia.
 
Hebu jiulize Zitto wa hoja ya Buzwagi ndiye huyu tunayemuana siku hizi?
Jiulize tena-Humu jukwaani na nje magazetini watu gani walikuwa wanasema nini juu ya Zitto? WanaCCM walikuwa wanamsemaje Zitto? na mengine mengi.
 
Kosa la Majasusi wa CHADEMA:
Mara kadhaa nimeandika humu kuwa CHADEMA inafanya vyema kwenda na Zitto hivihivi bila kumgusa.
 
Ningekuwa naishauri CHADEMA ningewaambia wamwite wamuonyeshe ripoti ya Ujasusi halafu wanyamaze. Asingeweza kufanya zaidi.
Au wangeweza kuitoa hadharani halafu wakanyamaza.
Kitendo cha kumuondolea madaraka na wajibu wake  ni dalili kuwa CHADEMA haijawasoma watanzania. Kinachotarajiwa sasa ambacho CHADEMA ilistahili kukiepuka ni kuwagawa wanachama kwa kutenda walichotenda. Sio wanachama wote na waTanzania wote walikuwa wamemuelewa ZITTO. Na sio watanzania wote watakaoelewa maana ya ripoti ya Ujasusi. Bado kuna upofu. Ngoja 2015 ije. Bado kuna watanzania wanashabikia rangi za vyama sio sera.
Kama CHADEMA wangemuonyesha zitto wanavyomuelewa au wakaweka ripoti hadharani wakamuacha angefanya kosa yeye. Sasa wamefanya wao. Lazima mtikisiko utatokea na utatokea wakati mbaya. Karibu na uchaguzi wa Chama na karibu na uchaguzi Mkuu. 2014 na 2015 si mbali sana. Wanaojadili watavhusisha kitendo cha CHADEMA na uchaguzi. Hii sio afya kwa CHADEMA.
 
Nawatakia waTanzania kuisaidia Taasisi yao hii muhimu kabla ya Uchaguzi ili uweze kwenda kwa haki. Ikiwa matatizoni watanzania watachagua kitakachokuwepo.
Haifai
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment