Friday, 1 November 2013

Re: [wanabidii] MWANAMKE APIGWA RISASI KATIKA OFISI ZA TRA ARUSHA

Mpya nyingine ya jana kutoka TV  ni vijana kuona lori linakuja kasi na kupaki pembeni mwa daraja na jirani na mapito ya lori bodaboda iliyobeba mtu. Wakagongwa na kufa mtu aliyepakiwa. Lakini jiulize-kwa nini mtu anaona lori laja kwa kasi asimame jirani atoe chambi badala ya kwenda kusimama mbali.

Hata mjini hapa Dar unaweza kuona mtu anapishana na gari tako lake karibu liguse gari na hajali hata anaona gari ndio impishe. Hivyo vijana wa boda boda wakalingo'a milingoti ya daraja kwa hasika eti daraja dogo linasababisha hatari. Yaani unabomoa daraja eti gari limemgonga dreva au abiria wa  bodaboda darajani!!

wapo waliochoma gari ya Hiace ya mpemba Dar baada ya kumgonga wa bodaboda njia ya Tangi bovu-Tegeta Mradi tu mtu alishika kitu kuchoma au kung'oa anadondoka hadi leo wanapakatika na kusimulia wenyewe mtaani mpemba alivyowafanya. Mpemba aliwaambia mimi siokoti mabaki ya Hiace yangu ila mtajiokota wenyewe kuwa maiti kama hilo mlilofanya kunipotezea mali yangu nanyi mtapotea. hakieleweki kafanya nini lakini kundi la uchomaji wanateketea kwa vifo visivyoeleweka.

 Kiserikali-inachomwa gari ya police, zima moto na kubomoa daraja ambalo wao wachomao wanalihitaji. Hivi tupoje? Wakigonga wao mtu-poa na wanazunguka foleni za magari hovyo na kugonga watu daily, ila wao wasigongwe hata kama wanakiuka usalama na kusababisha wagongwe.

 Nyumba zimeingia sana barabarani mno kama lori la mafuta likipotea njia na kugonga nyumba balaa na mibanano kuingia barabarani inazidi.  Watu wanaweka viti vya kunywa pombe mpaka feeder road na side roads/pavements za kupita waendao kwa miguu. Viongozi wa mtaa wapo lakini wanaogopa kisasi. Wakubwa wanapita wanaona lakini nani amfunge paka kengele?-waache wanaganga njaa. Subiri lori lianguke hapo ktk right of way ya barabara ambapo wao wamekaa.

Sijui ni kitu gani sisi wabongo kinatufanya tusione umuhimu wa kufuata sheria hata za makazi, usalama wetu na kutii tunapoombwa kuzingatia sheria ktk sekta zote iwe usalama wa moto, benki, ujenzi wa makazi, biashara, usafiri bila kujazana sana ktk meli, boat, magari, train. Kweli tusipobadilika tutajiingiza vitaji na pia hata tusipoingia vitani maisha yetu yatakuwa primitive, nchi jirani zitatuacha daima katika masuala mengi pamoja na kuwa na wasomi na raslimali nyingi kuliko wao.

 



On Wednesday, 30 October 2013, 17:26, ELISA MUHINGO <elisamuhingo@yahoo.com> wrote:
Yak mambo ya msingi:
mama huyo alikuwa na Pistal mbele ya Askari?- Inatosha kabisa kumfyatulia za kwao. Yuko salama mbele yao na aliingia au yuko mazingira ya Benki. Anafanya nini na silaha hiyo wakati halindi pale?
Hapo twaweza kurudi nyuma kidogo: Ni kweli aliambiwa asiegeshe pale na walinzi hao? Hata kama inaruhusiwa lakini wakikushtukia huna la kufanya zaidi ya kutii
. Wanaweza wakawa wamekushtukia kwa bahati mbaya lakini inabidi kutii hata kama huna hatia. hapo sio mahakama ni pa kujitafutia haki. kama kweli alipokuta gari limeondolewa upepo na Polisi maana yake lisitoke. Unaendaje kuwagombeza na umeshika silaha? Wamefanya vizuri kumuumiza mkono maana tungewazulia kama ninavyoona mjadala unaanza-Kuleta assumptions kwa sababu tumezoea askari wetu kufanya makosa. Si wameanza kujisahihisha sasa????????
From: Mwema Felix <mwema.felix@gmail.com>
To: Mailing List <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Wednesday, October 30, 2013 4:33 PM
Subject: Re: [wanabidii] MWANAMKE APIGWA RISASI KATIKA OFISI ZA TRA ARUSHA

inamaana alipoegesha gari lake lilikuwa peke yake au kulikuwa na magari mengine?
vinginenvyo mleta habari hii afafanue zaidi hali halisi ilivyokuwa.

On Wed, Oct 30, 2013 at 8:27 PM, <ezekielmassanja@gmail.com> wrote:
Hata kama kulikuwa hamna tangazo lakini aliambiwa,


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.


0 comments:

Post a Comment