Wednesday, 17 August 2016

[wanabidii] PEPO WA BONGO DANSI KAWAGANDA WASHABIKI ULAYA

Pepo wa Bongo Dansi bado anasumbua washabiki ulaya !
NGOMA AFRICA BAND AKA FFU ndio wanaopeperusha !

Utamu wa muziki wa dansi wa kiafrika umegeuka kuwa pepo asiye sikia
ubani wala uvumba mbele ya washabiki wa muziki wa kiafrika kule ughaibuni,kwa takribanimiaka 23 sasa Ngoma Africa band imekuwa katika medani ya muziki katika majukwaa ya kimataifa kule ughaibuni na kufanikiwa kujizolea umaarufu kwa kuwanasa washabiki wa kimataifa katika kila kona. urimbo wanaoutumia kuwanasa washabiki wao ni "Muziki wa dansi" au Bongo dansi kutoka uswahilini na jirani mwa afrika mashariki. bendi hiyo mashughuli iliyoanzishwa mwaka 1993 na kiongozi wake mwanamuziki  mtanzania Ebrahim Makunja kwa majina ya usanii Kamanda Ras Makunja mkuu wa viumbe wa ajabu Anunnaki Aliens, bendi ya Ngoma Africa band na muziki wake imegeuka kuwa pepo aliyewaganda washabiki wa kila umri na kila jinsia, na kuifanya bendi hiyo kujiwekea historia ya bendu pekee ya kiafrika katika majukwaa ya kimataifa ,bendi ambayo mara nyingine usababisha ulinzi kuwa mkubwa kila wanapotumbuiza.bendi hiyo iliyobatizwa majina mengi ya utani na washabiki wake,majina kama vile FFU-Ughaibuni,aka "Viumbe wa ajabu Anunnaki Aliens kutoka "Special Planet Bongo land".
Kikosi kazi cha Ngoma Africa band kinapokwea jukwaani kinakuwa na kazi moja tu hakuna kuremba remba bali kushambulia kwa muziki moto mpaka
washabiki wanachanganyikiwa.
usikose kuwasikiliza at www.ngoma-africa.com
jarida moja la ujerumani limeitaja bendi ya ngoma africa kuwa yenye mafanikio na imeshinda mapambano kwa kuwa bendi pekee ya kiarika kuteka soko la muziki ujerumani na ulaya som at http://www.afrikaportal.eu/portraet-ngoma-africa-band/--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment