Monday, 22 August 2016

Re: [wanabidii] Dola zote kubwa zilizowahi kujengwa duniani zilijengwa na watawala kama Mhe. Magufuli.

Hakuna sababu ya kuzuia maandamano na Mikutano ya hadhara kunapokuwa na hoja ya kitanzania (kitaifa). Hapa ndugu zetu waliozoea kukwepa kodi na kutumia siasa kujilinda. Waliozoea kuwahujumu watanzania kwa kuharibu Reli yetu ili malori yao yapate tenda. Waliozoea kumwaga maji ya Mtera ili waendelee kupata mgao kutoka capacity Charges na nchi iendelee kupata umeme wa mgao. waliohakikisha meli ya Victoria haitengenezwi kwa kuelekeza fedha ya serikali ya kukarabati meli inalipa mishahara wameshikwa pabaya na wanazua sera mpya na kutaka watanzania wawaunge mkono wanapoteza muda. Nitamlaumu JPM kama watarudi majimbani na sio hospitali baada ya maandamano. Baada ya Demokrasia ya kuamua uingereza kubaki au kujitoa umoja wa ulaya sasa ni udikteta wa kutekeleza waliloamua kidemokrasia. Tunahitaji udictator wa kutekeleza kauli mbiu tuliyoichagua kwa demokrasia yaani HAPA KAZI TU. Mikutano ya kutafuta wanachama ruksa. Mikutano ya ndani ruksa. Ya kutukana rais wetu hapana. Kama JPM akishidhwa kuidhibiti basi aseme. Itadhibitiwa na nguvu inayodharauliwa. Ipo.
--------------------------------------------
On Sun, 8/21/16, 'mpombe mtalika' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: [wanabidii] Dola zote kubwa zilizowahi kujengwa duniani zilijengwa na watawala kama Mhe. Magufuli.
To: "ELISA MUHINGO' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Sunday, August 21, 2016, 6:22 PM
Fuatilia
nchi zote zilizoendelea anzia, Marekani, China, Urusi na
kwinginepo
walitanguliza maendeleo kabla ya Demokrasia. Kwan chi nyingi
za Afrika
tulitanguliza Demokrasia badala ya maendeleo.

Kwa sasa
nchi yenye mafanikio makubwa katika ukanda wa Afrika
Mashariki ni Rwanda.

Ukiambiwa miaka
ya 1990 kulikuwepo na vita vya wenyewe kwa wenyewe
hutokubali
kwa jinsi inavyokimbia kimaendeleo. Unajua kwa nini? Ndani
ya Rwanda kuna baba
mmoja tu kwa sasa akisema wakalime wanaenda kulima kulima,
hakuna atakaebaki
kwa kucheza pooltable au kuandamana, akisema rushwa stop
watu wanafunga wallet
zao.


Tanzania
tumezoea kubembelezana sana, JK alituparuhusa ya kuzurura
zurura usiku na
mchana tunapiga domo. Kwa miaka yote kumi ni maandamano tu,
mara operation
sangara kama si sato au M4C na kadhalika, hata wapinzani
wenyewe walidiliki
kusema tunahitaji rais  mkali zaidi ya JK
na yeye mwenyewe alituahidi  kuwa atakuja
na leo tumempata tunaanza kutafuta kick za hovyo  hovyo kabisa wakati shida kubwa ya
sisi
watanzania ni maendeleo wala si UKUTA kama wanavyotaka
kutuaminisha.


Nani
aliyekuwa anaifahamu Libya ya mliyekuwa mnamuita dikteta??
Ni Libya hipi ya
kukumbukwa hii ya leo inayoruhusu maandamano ya vurugu kila
leo na kushindwa
kuyadhibiti na kulinda usalama wa raia wake na mali zao au
ile Libya ya
aliyekuwa akiitwa dikteta Gadafi?


Nendeni
Misri ya leo nao kuanzia January hadi decemba 
wapo mitaani wanaandama pamoja na kutafutana kwa
mitutu ya bunduki
halafu linganisheni na Misri ya aliyekuwa akiitwa dikteta
Mubarak akiwa
madarakani.


Dola zote
kubwa zilizowahi kujengwa duniani zilijengwa na watawala
kama Mhe. Magufuli.
Tafuta dola yeyote kubwa ya zamani halafu tafuta staili zao
za uongozi
iliyokuwepo na maendeleo wanayojivunia leo.


Lakini leo
hii wanasiasa wetu wanataka na kutamani kufanya damu za
watoto wa masikini kuwa
daraja la wao kupata umaarufu, Serikali imeruhusu maandamano
kwa sharti la
Mbowe mna Lowassa pamoja na familia zao ikiwemo wake na
watoto wao kuwa mstali
wa mbele katika maandamano, natamani tulione hilo September
1 lakini
hawatathubutu ni waoga, wanapenda kuonyesha ujasiri katika
kamera za wanahabari
huku wakiwafanya watoto wa masikini kuwa chambo cha wao
kupata front page za
magazeti na umaarufu.


Natamani
maandamano yao ya Septemba mosi  yaanzie
kule Hai mkoani kililimanjaro, Mbowe awaitekina Sugu,
Msingwa, Lema, Prof
Baregu na wengineo pale nyumbani kwake au hotelini kwakwe
Protea kule Machame.


Namshangaa
sana Mbowe, anahubirije demokrasia wakati wakati yeye haishi
katika yale
anayoyazungumza? Kama Kitilya,Mwigamba na Zitto watu watau
hao waliandika
waraka na kuusevu kwenye PC zao ila waliishia kufukuzwa kama
mbwa hiyo ndiyo
demokrasia anayoihubiri?


Hivi Mbowe
anapogombeaga uenyekiti wa chama huwa anashindanisahwa na
nani? Lowassa
alipopewa nafasi yay a kugombea urais Chadema mwaka jana
alishindanishwa na
nani?


Watanzania
wenzangu kwa kweli atakayekutana na mkono wa dola kwenye
maandamno ya tarehe
1/9/2016 shauri yake na msianze kutusumbua kwa kututumia
picha mikiwa mmelowa
damu nahilo ndilo wanalolitaka Mbowe na
Lowassa.


Ndudu zangu
Watanzania hakuna hoja yeyote ya msingi ya kutufanya
tuandamane nchi nzima hiyo
tarehe 1/9/2016 hili ni jaribio la UHAINI.

Kama swala
la Tulia walimkimbia wenyewe na kama hakufuata kanuni
zilizotungwa na bunge,
hicho chombo kina taratibu zake za kudili naye na si kuja
kutusumbua wananchi.


"Kila mmoja
afanye siasa kwenye eneo alilochaguliwa, Kingu mbunge wa
Ikungi Magharibi
afanye mikutano yake ale pale kwake alipoahidi shughuli za
maendeleo, Mbowe
afanye siasa pale pale Hai aliochaguliwa na kuahidi kuwapa
maendeleo, kila
mmoja aliyechaguliwa afanye siasa eneo lake."


"Sitaki
kuona mtu anatoka HAI kwenda KAHAMA kufanya mikutano n.k
Mbunge au diwani wa
HAI au Mbeya  hana mamlaka ya kuingia
ndani ya majimbo ya yao. Huwezi kuwa mbunge wa Ubungo
ukaenda kufanya vikao vya
maendeleo kwenye eneo ambalo si lako".


"Wanaotaka
kuandamana au kufanya mikutano kiholela kwanini wasubiri
mwezi wa 9? Wafanye mikutano
hata leo ili wajue mimi ni nani. Siwezi kuigeuza hii nchi ya
sisa, nataka nchi
ya maendeleo tu. Siasa zilishakwisha wakati wa KAMPENI muda
huu ni wa KAZI TU".

Hiyo ndiyo kauli
Rais Magufuli, nafikiri ndio siku Mbowe atabatizwa kwa moto
kama atakuwa mstari
wa mbele, ikiwa hawezi kuwa mstari wa mbele aache kuwafanya
chambo watoto wa
masikini manufaa yao ya kisiasa na kupata
umaarufu.

--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment