Monday 22 August 2016

Re: [wanabidii] FRED MPENDAZOE: Kwanini nimeondoka CHADEMA?

Kweli Lesian, Mpendazoe angepata Ubunge angeacha na kurudi CCM? Je chama kikijisahihisha wote wanahama kuelekea huko na kuacha vyama vingine kufa? Wapi kuna Mafisadi wengi CDM au CCM? Kama ni uvundo uko wapi sasa?

Mpendazoe acha njaa ikuue tu.

Jovin Bifabusha

DIRECTOR
KWFF LTD
P. O. Box 313
Skype: jovin.bifabusha
Karagwe, Tanzania
+255 784 709200

--------------------------------------------
On Mon, 8/22/16, 'Lesian' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] FRED MPENDAZOE: Kwanini nimeondoka CHADEMA?
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Monday, August 22, 2016, 8:47 AM

Kilichokuondoa cdm mzee mpendezoa ni
njaaa na uchu wa madaraka na kiukweli huko uliko rudi
utasubiri sana, hupata hata udc ulilost mwenyewe.....kama
watu hawakutaki hawakautaki tu, usianze kutafuta mchawi,
kuondoka kwako cdm ni njaaaaaaa......uliiingia kwa uchu wa
kudhania ungeukwa ubunge ulipokosa ukaona urudi thinking kua
magufuli angekuonea huruma akupe udc...mmmh, nyie ndio
wanasiasa wanafiki msiokua na nia thabiti ya kusaidia
matatizo ya watanzania bali mmetanguliza mitumbo yenu, mtu
akikusoma hata usoni atakuona,'unafik ulionao...soma
maandika yako uliowahi kuyachapisha hayatafutika na huo ndio
unafik wako mzeee,'pole
Ushaur wangu achana na siasa, fannya kaz za kuzalisha kipata
tulia nyumbani mzeee, you are a lost sheep

'mpombe mtalika' via Wanabidii
<wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Tarehe 23 July 2016 nilishiriki
kwenye Mkutano Mkuu wa CCM. Kwenye
mkutano huo nilipata nafasi ya kuzungumza na haya Ndiyo
niliyoweza
kuyasema Kwenye mkutano huo:



Nilieleza kwamba kwa muda mrefu Nilikuwa nimeamua kurudi
CCM, siku hiyo
ilikuwa ni siku ya kutangaza tu. Nilikuwa nimeamua kurudi
CCM kwa
sababu kuu zifuatazo. Kwanza ni hatua ambazo CCM ilikuwa
imeanza
kuzichukua kupitia Katibu Mkuu wake Kinana. Kinana alifanya
ziara nchi
nzima akiwaeleza na kuwataka wanachama wa CCM kubadilika.
Akiwaeleza
wapige vita ufisadi, CCM iisimamie serikali yake. Aliwataka
mawaziri
wafanyekazi Kwa bidii. Aliikosoa serikali. Alisikiliza kero
za wananchi
wa chini na akawasemea Kwenye serikali yao. Watanzania
wakaanza kupata
matumaini.



Wakati Kinana akiendelea na ziara, CDM na UKAWA walihubiri
mabadiliko
majukwaani na kuzungusha mikono Lakini miyoni mwao hawakuwa
tayari
kubadilika. CCM kubadilika na kukubalika na wananchi.



Jambo jingine , CDM na UKAWA walimpokea mgombea aliyekuwa
ameondolewa
Kwenye kura za maoni ndani ya CCM. Mgombea huyo aliondolewa
kwa tuhuma
za ufisadi. UKAWA wakamchukua. Mtakumbuka, CDM walizunguka
nchi nzima na
wakadai wanao ushahidi kwamba mgombea huyo ni fisadi. CCM
walimuondoa
wao wakampokea akawa mgombea urais. Wasambaa wanao msemo
unaosema,
"ukitaka kuepuka nzi tupa kibudu". CCM ilitupa
kibudu kilichokuwa
kinasababisha harufu mbaya.



Hatua hii ya CDM na UKAWA kukumbatia kibudu kimesababisha
CDM na UKAWA
kimepoteza ajenda ya kupinga ufisadi na sasa ipo harufu ya
mzoga ndani
ya CDM na UKAWA.

Sababu nyingine ni hatua ambazo JPM na serikali yake
amechukua. JPM
amechukua hatua madhubuti kupiga vita ufisadi, uzembe na
ubadhirifu.
JPM ameleta matumaini kwa watanzania.

JPM Kama Mwenyekiti wa CCM amesema ni kweli CCM ilikuwa
imepoteza dira.
Nilipokuwa CCM pia nilisema kwamba CCM ilikuwa imeyumba.
Niliyoyapigia
kelele kwa sasa tunaye mtanzania ambaye amejitoa
kuyashughulikia.



Lakini, Nani asiyefahamu kwamba ndani ya CDM demokrasia
imeminywa kuliko Kwenye vyama vingine vya siasa?

Hahitaji utaalamu mkubwa kuchunguza na kubaini kwamba
maamuzi ya kumtoa
Dk Slaa kuwa mgombea hayakuwa ya kidemokrasia na ya harufu
ya rushwa?

Maamuzi ya kupata mgombea yalifanyika Kwenye chopa !?.

Hivi CDM na UKAWA wanapigania nini? Siyo demokrasia.
Hapana.



Ni Kwa sababu hizi nimerudi CCM.
 




--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment