Monday, 22 August 2016

Re: [wanabidii] Mbinu za Rais Magufuli zinawaumiza wapinzani

Ushauri wako unaweza kuchukuliwa na watu majasiri na waliotayari kuona kosa lao.
CDM walishindwa kusoma watanzania wakati wa kampeni za uchaguzi. Walishindwa pia kumsoma magufuli ambaye anajulikana toka zamani. Ujasiri wake wa kumtumbua naibu wake alipokuwa wizara ya ardhi na huku wote wakiwa wateule wa Rais CDM walistahili kujiuliza wataendaje naye. Wanakunja ngumi bila GLOVU kupambana na aliyevaa glovu. Kwanza kabisa wangefanya analysis ya mambo wasingesusia bunge. Pili wanlipoona anatekeleza maswala ya kero za watanzania wangeibuka kwa nguvu kumuunga mkono kwa utendaji wake huku wakisubiri akosee makosa ambayo wananchi watayaona.
Hiyo ingewasaidia kuendelea kuungwsa mkono na watanzania. CDM walishindwa kujua toka mwanzo wa kampeni kuwa kutelekeza kelele zao kuhusu ufisadi na kumtafuta fisadi kusimamia mabadiliko hayo ya sera imechangia na inaendelea kuchangia kuporomoka kwake.
Ninafikiri kuwa huenda magufuli anawasaidia sana kuzuia maandamano na mikutano yao. Ikitokea wakaifanya hakuna walilo nalo la kuwaeleza watanzania kwa sasa mpaka wakawaunga mkono. Wanachokipigania ndicho kiliwaumiza watanzania. Demokrasia iliyoruhusu uhujumu wa uchumi na wati wakaishia kutozwa kodi na tozi watu wa chini na wakubwa wakikwepoa kodi. Ninafikiri wapinzani wana tatizo la zidumu fikra za mwenyekiti. Ni wazi kila aliyempinga alitimuliwa anzia kwa Zitto, mwigamba, Dr. Slaa na wengine. Wao kuendelea kujitambulisha hivyo ni kuendelea kutengeneza njia ya kuelekea kaburini.
Tulisema wakati wa kampeni hawakusikia. sasa tunasema tena na waendelee kutosikia
--------------------------------------------
On Mon, 8/22/16, 'mpombe mtalika' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: [wanabidii] Mbinu za Rais Magufuli zinawaumiza wapinzani
To: "ELISA MUHINGO' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Monday, August 22, 2016, 12:11 AM

Rais Magufuli amekuwa na mbinu tofauti za kuongoza
nchi hii, mbinu zake
zimekuwa tofauti na zile za Rais Mstaafu Jakaya Kikwete.
Zipo dhana
mbili katika uongozi wa kisiasa dhidi ya wapinzani ndani ya
mataifa
mbali mbali.



Kwa mfano mwanasiasa anaweza kukabiliana na wapinzani wake
kwa njia kuu
mbili, mosi ni kuwaweka karibu wapinzani wake. Pili ni
kuwatupilia mbali
wapinzani wake.



Mpaka sasa kuna mabo mawili nimeyaona kwa Rais Magufuli.
Katika utawala
wa Rais mstaafu Kikwete mara nyingi alikuwa akitumia mbinu
ya kuwaweka
karibu wainzani wake kisiasa iwew ndani ya chama au nje ya
chama.



Ndani ya chama Kikwete alifanikiwa kuangamiza polepole kundi
la mtandao
lililokuwa na kina Edward Lowassa, Rostam Azizi, Samweli
Sita na
wengineo wengi tu ambao siwezi kuwataja hapa, Kikwete
alifanikiwa
kulingamiza kundi hilo la mtandao polepole mpaka
likamalizika huku
akiwaacha watu na mshangao mkubwa kwa mbinu hiyo kwa kuwa
kundi hilo
ndilo lilifanikisha kumfanyia kampeni 2005.



Kwa hiyo Kikwete aliishi na wainzani zake ndani ya chama kwa
kuhakikisha
anawapunguza nguvu na umahiri wao taratibu. Kwa upande wa
wapinzani wan
je ya chama Kikwete alikuwa akitumia mbinu hiyo hiyo ambayo
ilijitokeza
zaidi mwaka 2010 wakati wanasiasa wa kambi ya upinzani
walipoamua
kususia hotuba yake.



Licha ya kususiwa hotuba pale bungeni, Rais mstaafu Kikwete
aliwaambia
mtakwenda na mtarudi mimi ndio Rais wenu. Kauli hiyo ilikuja

kujidhihirisha baadaye baada ya wapinzani kuomwomba sana
Rais kuzungumza
naye.



Kikwete hakuweza kuzuia alichofanya ni kuchelewesha kidogo
kuonana nao
kabla ya kukutana nao. Kikwete alikutana wapinzani
walikokuwa
wakimkejeli na kumsusia hotuba.



Katika majadiliano ya muundo wa bunge la katiba pamoja na
sheria zake,
wapinzani waliomba kukutana na Rais Kikwete, naye bila ya
hiyana
akawaita ikulu na kufanya mazungumzo kuhusu hilo.



Hoja kubwa ya wapinzani ilikuwa ni kupinga sheria
iliyopitishwa na bunge
la katiba. Pamoja na mabo mengine Kikwete alikubaliana nao
na
kusisitiza kuwa mabo waliowasilisha kwakwe yaliwezekana
kufanyika
bungeni.



Kikwete aliwaahidi wanasiasa hao wazito kweli wakiongozwa
na Freman
Mbowe, Wilboard Slaa na Tundu Lissu, ambapo walikunywa chai,
wakanywa
juisi ya ikulu mazungumzo yakenda vizuri. Licha ya kuahidi
kutosaini
sheria hiyo, Rais Mstaafu Kikwete alitumia mamlaka yake
kusaini na kisha
kutumika kama sheria ya kuunda Bunge la katiba.



Hali hiyo iliwashitua ya wanasiasa wa upinzani, lakini
Kikwete
alisistiza mambo yaliyopaswa kupitishwa bungeni hayakutakiwa
kufika
kwake, badala yake yaliofika kwake huku muswaada ukiwa
umeshapitishwa
maana yake ulikuwa umekubaliwa na wabunge wote.



Wapinzani walijaribu kujenga hoja katika hilo kuwa Kikwete
aliwekwa kiti
moto na chama chake katika hilo lakini haikuwasaidia kitu
na pia
hakukuwa na uthibitisho wowote mpaka leo hii.



Kimsingi hii ilikuwa mbinu ya Kikwete kuwaweka karibu
wapinzani wake.
Aliwakaribisha ikulu na kuwapa Chai na juisi na kuwasikiliza
kabla ya
kuamua tofauti na matarajio yao.



Hiyo pekee ilikuwa njia iliyokuwa ikiwajaza matumaini lakini
ikawa
kinyume na matarajio yao na kumfanya Kikwete kuwa master wa
siasa. Mara
kadha Kikwete aliweza kula sahani na moja na wapinzani wake
na mwisho wa
siku aliweza kuwaacha kwenye mataa wakishangaa huku yeye
akiwaachia
tabasamu lake likiwachoma katika mioyo yao, sitaki kuandika
yaliyomkuta
Lowassa Dodoma akinuna na kundi lake huku Kikwete akimuibua
Magufuli na
tabasau la dhihaka kwa wanamtandao waliokuwa wakidhani
Lowassa
hawezekaniki.



Mbinu aliyokuwa akitumia Kikwete kuwaweka karibu wapinzani
ni ya
wanasiasa wachache sana, inahitaji uvumilivu wa hali ya juu,
pia
ianahitaji werevu na ujanja kumudu kwenda nao kisiasa
wapinzani wako wa
ndani ya chama na nje ya chama.Ingewezekana kabisa kutumia
mbinu ya
watupilie mbali, kwamba hakuna kuwadekeza wala kuwaeka
karibu.



Sasa turudi kwa rais wetu wa sasa John Magufuli, kihukla na
mwendo wake
ni tofauti kabisa na mtangulizi wake Kikwete. Kwa namna
Fulani Magufuli
anafanana kimwenendo na Raias Mstaafu Benjamini Mkapa.



Kwamba wawioi hao wameamua kuwaeka mbali kwa maana ya
kuwatupilia mbali
wapinzani wao kisiasa hususani wa vyama vya upinzani (nje ya
chama
chao). Mbinu hii inaungwa mkono na mawaziri wakuu wastaafu
na wakongwe
hapa nchini kina Cleopa Msuya, John Malecela na Spika
mstaafu iusi
Msekwa.



Kwa maana hiyo wanaccm sasa wanatakiwa kutumia mbinu hii ya
watupilie
mbali, kwa kuchapa kazi na majukumu yao kwa mujibu wa ilani
yao. Mbinu
ya kuwatupilia mbali wakati mwingine inaleta shida kubwa kwa
wapinzani.



Na shida hiyo tumeiona katika kipindi hiki Chadema wakiwa
wamepigwa nha
butwaa. Ikwa na maana wanadhafirika na kuona hawapewi fursa
wala heshima
yeyote na utawala mpya. Kwa hofu ya kufunikwa kisisa ndipo
wanaibua
operation za kupambana zenye nia ya kuonyeshana ubabe na
serikali
iliyopo madaraki.



Kwa maana hiyo vyama vya upinzani kama Chadema kimejikuta
kikipambana
peke yake bila kushirikisha wengine kutafuta kukubalika
mbele ya Rais
Magufuli. Lakini hadi sasa inaonekana Rais Magufuli yupo
mbali sana na
wapinzani kama ilivyokuwa enzi za Rais Mstaafu Benjamini
Mkapa, hivyo
inazidi kuwaumiza vichwa sana Chadema na kutafuta namna gani
ya kuwa
karibu naye.



Kiukweli Magufuli haonyeshi kwa namanma yeyote ile kuwa
karibu na
wapinzani kwa njia wanayotaka wao ya kubembelezana, badala
yake anataka
kuchapa kazi tu na kuwaletea maendeleo watanzania
waliomchagua, na hivyo
kutupilia mbali siasa zinazotakiwa na wapinzani ili
ziwanufaishe,
badala yake anataka kunufaisha wananchi kwa uchapaji kazi
tu.



Kwa vyovyote wapinzani haswa chadema wanatafuta mbinu ya
kukubalika na
Rais Magufuli angalau waweze kuvuna japo punje ya heshima
kutoka
kwakwe. Na jambo hilo linaonekana kuwaumiza vichwa sana
kwani Rais
Magufuli haonyeshi dalili za kuwaweka karibu kisisa kama
zilivyokuwa
enzi za Kikwete.



Mbinu hiyo pia ilitumiwa na Rais Mstaafu Benjamini Mkapa
ambaye hakuna
karibu na wapinzani wake nje ya chama, hali iliyotafsiriwa
kuwa ni ya
kibabe na tuambizane ukweli tatizo si ubabe ila ni uchaguzi
wa mbinu ya
kuongoza ya kuwaweka mbali wapinzani wake.



Jambo hilo linawaa wakati mgumu chadema na ndio kiini cha
operationi
ukuta.Nionavyo, hakuna dalili ya Rais Magufuli kutumia mbinu
ya
mtangulizi wake, Rais Kikwete ya kuwaweka karibu wapinzani.
Naona mbinu
hii ya watupilie mbali, iliyojitokeza wakati wautawala wa
Mkapa
ikiwaumiza kichwa wapinzani wake na ndio inayochukua hatamu
wakati huu .



Ni suala la uchagiuzi wa mbinu tu ndilo linalowaumiza kichwa
wapinzani
na kujaribu kutafuta kutafuta kila njia ya kutaka
kumuonyesha Magufuli
kuwa na wao ni wababe Fulani kisiasa, yaani vishindo vyao
vikubwa kwenye
siasa.



Mwisho nimalizie kwa kuawaasa na kuwashauri Chadema, wafuate
msemo wa
wafanyabiashara wa kihindi, ukiwa na mpinzani wako halafu
hauna nyenzo
za kushindana nae ni bora kuungana naye ili mambo yakle
yaende sawa
lasivyo utapotea.



Hivyo basi Chadema nao wanapswa kuungana na Rais Magufuli
kwa Kuchapa
kazi na kupeleka maendeleo katika majimbo yao na kata na
mitaa
wanayoiongoza kwani rais Magufuli alishawaeka wazi
atashirikiana na
yeyote katika kuleta maendeleo kwa kusema maendeleo hayana
chama.



--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment