Sunday 21 August 2016

[wanabidii] Mbinu za Rais Magufuli zinawaumiza wapinzani

Rais Magufuli amekuwa na mbinu tofauti za kuongoza nchi hii, mbinu zake zimekuwa tofauti na zile za Rais Mstaafu Jakaya Kikwete. Zipo dhana mbili katika uongozi wa kisiasa dhidi ya wapinzani ndani ya mataifa mbali mbali.

Kwa mfano mwanasiasa anaweza kukabiliana na wapinzani wake kwa njia kuu mbili, mosi ni kuwaweka karibu wapinzani wake. Pili ni kuwatupilia mbali wapinzani wake.

Mpaka sasa kuna mabo mawili nimeyaona kwa Rais Magufuli. Katika utawala wa Rais mstaafu Kikwete mara nyingi alikuwa akitumia mbinu ya kuwaweka karibu wainzani wake kisiasa iwew ndani ya chama au nje ya chama.

Ndani ya chama Kikwete alifanikiwa kuangamiza polepole kundi la mtandao lililokuwa na kina Edward Lowassa, Rostam Azizi, Samweli Sita na wengineo wengi tu ambao siwezi kuwataja hapa, Kikwete alifanikiwa kulingamiza kundi hilo la mtandao polepole mpaka likamalizika huku akiwaacha watu na mshangao mkubwa kwa mbinu hiyo kwa kuwa kundi hilo ndilo lilifanikisha kumfanyia kampeni 2005.

Kwa hiyo Kikwete aliishi na wainzani zake ndani ya chama kwa kuhakikisha anawapunguza nguvu na umahiri wao taratibu. Kwa upande wa wapinzani wan je ya chama Kikwete alikuwa akitumia mbinu hiyo hiyo ambayo ilijitokeza zaidi mwaka 2010 wakati wanasiasa wa kambi ya upinzani walipoamua kususia hotuba yake.

Licha ya kususiwa hotuba pale bungeni, Rais mstaafu Kikwete aliwaambia mtakwenda na mtarudi mimi ndio Rais wenu. Kauli hiyo ilikuja kujidhihirisha baadaye baada ya wapinzani kuomwomba sana Rais kuzungumza naye.

Kikwete hakuweza kuzuia alichofanya ni kuchelewesha kidogo kuonana nao kabla ya kukutana nao. Kikwete alikutana wapinzani walikokuwa wakimkejeli na kumsusia hotuba.

Katika majadiliano ya muundo wa bunge la katiba pamoja na sheria zake, wapinzani waliomba kukutana na Rais Kikwete, naye bila ya hiyana akawaita ikulu na kufanya mazungumzo kuhusu hilo.

Hoja kubwa ya wapinzani ilikuwa ni kupinga sheria iliyopitishwa na bunge la katiba. Pamoja na mabo mengine Kikwete alikubaliana nao na kusisitiza kuwa mabo waliowasilisha kwakwe yaliwezekana kufanyika bungeni.

Kikwete aliwaahidi wanasiasa hao wazito kweli wakiongozwa na Freman Mbowe, Wilboard Slaa na Tundu Lissu, ambapo walikunywa chai, wakanywa juisi ya ikulu mazungumzo yakenda vizuri. Licha ya kuahidi kutosaini sheria hiyo, Rais Mstaafu Kikwete alitumia mamlaka yake kusaini na kisha kutumika kama sheria ya kuunda Bunge la katiba.

Hali hiyo iliwashitua ya wanasiasa wa upinzani, lakini Kikwete alisistiza mambo yaliyopaswa kupitishwa bungeni hayakutakiwa kufika kwake, badala yake yaliofika kwake huku muswaada ukiwa umeshapitishwa maana yake ulikuwa umekubaliwa na wabunge wote.

Wapinzani walijaribu kujenga hoja katika hilo kuwa Kikwete aliwekwa kiti moto na chama chake katika hilo lakini haikuwasaidia kitu na pia hakukuwa na uthibitisho wowote mpaka leo hii.

Kimsingi hii ilikuwa mbinu ya Kikwete kuwaweka karibu wapinzani wake. Aliwakaribisha ikulu na kuwapa Chai na juisi na kuwasikiliza kabla ya kuamua tofauti na matarajio yao.

Hiyo pekee ilikuwa njia iliyokuwa ikiwajaza matumaini lakini ikawa kinyume na matarajio yao na kumfanya Kikwete kuwa master wa siasa. Mara kadha Kikwete aliweza kula sahani na moja na wapinzani wake na mwisho wa siku aliweza kuwaacha kwenye mataa wakishangaa huku yeye akiwaachia tabasamu lake likiwachoma katika mioyo yao, sitaki kuandika yaliyomkuta Lowassa Dodoma akinuna na kundi lake huku Kikwete akimuibua Magufuli na tabasau la dhihaka kwa wanamtandao waliokuwa wakidhani Lowassa hawezekaniki.

Mbinu aliyokuwa akitumia Kikwete kuwaweka karibu wapinzani ni ya wanasiasa wachache sana, inahitaji uvumilivu wa hali ya juu, pia ianahitaji werevu na ujanja kumudu kwenda nao kisiasa wapinzani wako wa ndani ya chama na nje ya chama.Ingewezekana kabisa kutumia mbinu ya watupilie mbali, kwamba hakuna kuwadekeza wala kuwaeka karibu.

Sasa turudi kwa rais wetu wa sasa John Magufuli, kihukla na mwendo wake ni tofauti kabisa na mtangulizi wake Kikwete. Kwa namna Fulani Magufuli anafanana kimwenendo na Raias Mstaafu Benjamini Mkapa.

Kwamba wawioi hao wameamua kuwaeka mbali kwa maana ya kuwatupilia mbali wapinzani wao kisiasa hususani wa vyama vya upinzani (nje ya chama chao). Mbinu hii inaungwa mkono na mawaziri wakuu wastaafu na wakongwe hapa nchini kina Cleopa Msuya, John Malecela na Spika mstaafu iusi Msekwa.

Kwa maana hiyo wanaccm sasa wanatakiwa kutumia mbinu hii ya watupilie mbali, kwa kuchapa kazi na majukumu yao kwa mujibu wa ilani yao. Mbinu ya kuwatupilia mbali wakati mwingine inaleta shida kubwa kwa wapinzani.

Na shida hiyo tumeiona katika kipindi hiki Chadema wakiwa wamepigwa nha butwaa. Ikwa na maana wanadhafirika na kuona hawapewi fursa wala heshima yeyote na utawala mpya. Kwa hofu ya kufunikwa kisisa ndipo wanaibua operation za kupambana zenye nia ya kuonyeshana ubabe na serikali iliyopo madaraki.

Kwa maana hiyo vyama vya upinzani kama Chadema kimejikuta kikipambana peke yake bila kushirikisha wengine kutafuta kukubalika mbele ya Rais Magufuli. Lakini hadi sasa inaonekana Rais Magufuli yupo mbali sana na wapinzani kama ilivyokuwa enzi za Rais Mstaafu Benjamini Mkapa, hivyo inazidi kuwaumiza vichwa sana Chadema na kutafuta namna gani ya kuwa karibu naye.

Kiukweli Magufuli haonyeshi kwa namanma yeyote ile kuwa karibu na wapinzani kwa njia wanayotaka wao ya kubembelezana, badala yake anataka kuchapa kazi tu na kuwaletea maendeleo watanzania waliomchagua, na hivyo kutupilia mbali siasa zinazotakiwa na wapinzani ili ziwanufaishe, badala yake anataka kunufaisha wananchi kwa uchapaji kazi tu.

Kwa vyovyote wapinzani haswa chadema wanatafuta mbinu ya kukubalika na Rais Magufuli angalau waweze kuvuna japo punje ya heshima kutoka kwakwe. Na jambo hilo linaonekana kuwaumiza vichwa sana kwani Rais Magufuli haonyeshi dalili za kuwaweka karibu kisisa kama zilivyokuwa enzi za Kikwete.

Mbinu hiyo pia ilitumiwa na Rais Mstaafu Benjamini Mkapa ambaye hakuna karibu na wapinzani wake nje ya chama, hali iliyotafsiriwa kuwa ni ya kibabe na tuambizane ukweli tatizo si ubabe ila ni uchaguzi wa mbinu ya kuongoza ya kuwaweka mbali wapinzani wake.

Jambo hilo linawaa wakati mgumu chadema na ndio kiini cha operationi ukuta.Nionavyo, hakuna dalili ya Rais Magufuli kutumia mbinu ya mtangulizi wake, Rais Kikwete ya kuwaweka karibu wapinzani. Naona mbinu hii ya watupilie mbali, iliyojitokeza wakati wautawala wa Mkapa ikiwaumiza kichwa wapinzani wake na ndio inayochukua hatamu wakati huu .

Ni suala la uchagiuzi wa mbinu tu ndilo linalowaumiza kichwa wapinzani na kujaribu kutafuta kutafuta kila njia ya kutaka kumuonyesha Magufuli kuwa na wao ni wababe Fulani kisiasa, yaani vishindo vyao vikubwa kwenye siasa.

Mwisho nimalizie kwa kuawaasa na kuwashauri Chadema, wafuate msemo wa wafanyabiashara wa kihindi, ukiwa na mpinzani wako halafu hauna nyenzo za kushindana nae ni bora kuungana naye ili mambo yakle yaende sawa lasivyo utapotea.

Hivyo basi Chadema nao wanapswa kuungana na Rais Magufuli kwa Kuchapa kazi na kupeleka maendeleo katika majimbo yao na kata na mitaa wanayoiongoza kwani rais Magufuli alishawaeka wazi atashirikiana na yeyote katika kuleta maendeleo kwa kusema maendeleo hayana chama.

0 comments:

Post a Comment