Sunday 7 August 2016

Re: [wanabidii]

Kupoteza mwelekeo kwa CHADEMA kuko wazi wala usimshambulie Mpobe.Uanzie walikoaanzia kupoteza mwelekeo:
1) Chama kina misingi miwili; Deokrasia na Mandeleo. Fuatilia oune kinavyopotea kutoka kwenye dira ya demokrasia na maendeleo.
Zitto alipotaka kugombea uenyekiti alitokaje CHADEMA? Hiyo ni demikrasia?

Utaratibu wa kumpata mgombea urais 2015 ulikuwaje kwa kulinganisha na siku za nyuma? Hiyo ni demokrasia?

Sera za CHADEMA zilizoiletea kupendwa na watanzania ni zipi? Kupinga ufisadi, kuibua matatizo yaliyolikumba taifa ikiwa ni pamoja na list of shame. Ulivisikia kwenye kampeni za 2015 kama ulivyovisikia kampeni za 2010?

Sasa tuna rais. Anashughulikia habari za kuondoa shida zilizoibuliwana CHADEMA. Anakusanya kodi Chadema wanasema anawayima haki za kibinadamu wakwepa kodi. wanataka rais ajadiliane nao.
Rais anahimiza watu kufanya kazi ili wajiletee maendeleo ambayo ni nguzo ya dira ya CHADEMA, wao wanataka saa za kazi watu waandamane.
uo ndio msingi wa makala ya mpombe kuwa CHADEMA kimepoteza mwelekeo.

Lakini ndugu yangu Bifabusha. vyama hivi si mali ya wanachama. Ni mali a watanzania. Ndivyo vinavyochangia mabadiliko. Viongozi wenye akili ndani ya vyama hivi wanasikiliza wanaowaunga mkonokama wewe na wanaowapinga kama Mpombe. Hivyo huwezi kutumia akili sana halafu ukamwambia Mpombe aiache CHADEMA kwa wanachadea tu. hapana ni yetu sote. kumbuka CHADEMA imewasaidia watanzania kuisaihisha na kuirekebish CCM. Naamini viongozi makini wa CCM wanakiri hilo.
Upo?

--------------------------------------------
On Sun, 8/7/16, 'jbifabusha' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii]
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Sunday, August 7, 2016, 11:55 AM

Mpombe
hivi mada zako unaziandika ukiwa na hali gani? Wewe umeongea
na nani kujua kama CHADEMA inapoteza mwelekeo? Hivi kwako
Kada wa CCM unataka CHADEMA iwe na mwelekeo kwa faida ya
nani? Usipoteze muda wako kuijadili CHADEMA badala yake
sifia CCM yako yenye mwelekeo unaoutaka. Nakushauri wala
usiungane nao na uwaache wasio na mwelekeo waungane na
washikane mikono. Pia unatakiwa kujadili mantiki ya
kinachozungumzwa na sio hisia zisizokuwepo. Operesheni UKUTA
ni zao la Serikali ya CCM kupiga marufuku shughuli za
kisiasa hadi 2020. Je kwa akili yako nzuri unadhani amri
hiyo ya kupiga marufuku shughuli za kisiasa ni sahihi na
halali? Tujadili hilo alafu ndo tuone kama CHADEMA
wamepoteza mwelekeo au hapana. Hatuwezi kusema tu kama
mazuzu au wajinga au bendera fuata upepo,  lazima tuseme
kwa mantiki na ukweli.

Sent from Samsung
Mobile


-------- Original message
--------
From: 'mpombe mtalika' via
Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Date:
To: ELISA MUHINGO'
via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Subject: [wanabidii]


     
                       KUNA hatari kwamba endapo
Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) hakitajiangalia vizuri katika hali yake ya
kupoteza mwelekeo
ambao tunauona sasa hivi sasa kinaweza huko mbeleni kikaja
na harakati
nyingine za kuhamasisha watu kuandamana dhidi ya serikali au
juu ya
jambo fulani na wakaamua kuita harakati hizo
'Ukutiukuti'!



Tunaweza kuwaona siku moja wakishikana mikono na kuanza
kuzunguka kwa
pamoja huku wakitaka wengine nao washiriki kucheza na
kurukaruka huku
wote wakiimba "ukuti ukuti, wa mnazi wa mnazi, ukiingia
upepo watetema!"
Nina sababu ya kuhofia hili. Tulipokuwa watoto wadogo
tulicheza michezo
mbalimbali ambayo ilitufundisha misingi mbalimbali ya
kimaisha. Kupitia
michezo hiyo tulijifunza urafiki, kusaidiana, kushirikiana,
kuwa
mwangalifu, ujanja na hata mahusiano kati ya watu wa jinsia
tofauti.



Kwa kadiri tulivyokuwa ndivyo michezo mbalimbali tuliipita
tukaingia
katika aina nyingine za michezo hadi kwenye shule na vyuo
vya juu.
Michezo ambayo tulicheza ni mingi na ilikuwa na aina yake ya
ushindani;
kuanzia Kombolela, Kula mbakishie baba, Kioo alikivunja
nani,
Banchikicha, Turinge Bayoyo, na michezo mingine mingi ya
utotoni. Katika
michezo yote hiyo, naamini ipo ambayo hadi leo ukikumbuka
inakupa
tabasamu kwani inakurudisha miaka ile ya kutokuwa na hatia
na furaha ya
maisha; mmoja wa hiyo ni huu wa 'ukutiukuti'.



Watoto kutoka mtaani au hata mtaa wa jirani walijikusanya
pamoja mara
nyingi baada ya michezo mingine yote kuisha wanashikana
mikono katika
mduara na kuanza kuimba huku wakizunguka na kuruka ruka. Huu
ni miongoni
mwa michezo iliyohusisha watoto wa kike na wa kiume.
Wanapofika mwisho
watoto wameanguka, wanacheka na kuagana au kwenda majumbani
mwao wakiwa
na furaha. Ni miongoni mwa michezo ambayo hata dada na kaka
zao wakubwa
waliweza kujumuika nao na hivyo kuendeleza mahusiano
mazuri.



Siasa zetu sasa hivi zilipofika hasa kwenye chama kikuu cha
upinzani
nchini cha Chadema ni kuwa tusipoangalia wanaweza au tayari
wamefikia
mahali pa kuanza kuja na harakati kama burudani. Tangu
walipoanza na
Operesheni Sangara, Operesheni Mzizima, M4C, wengi tuliona
hatari ya
kampeni hizi zenye majina mbalimbali ambayo labda matokeo
yake yanaweza
kubishaniwa.



Kwa wanaojua, mimi sikuwahi kuwa shabiki wa lile dubwasha la
Ukawa
ambalo naamini lilichangia sana kuvuruga upinzani na
mwelekeo wa
upinzani kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana. Lakini kama
vile ndugu
zetu hawataki kujifunza au wamegoma kujifunza baada ya kikao
chao
kingine wameamua kuja na kampeni nyingine au operesheni
nyingine ambayo
sasa wameamua kuiita 'Ukuta' ukiwa ni Umoja wa Kupinga
Udikteta
Tanzania.



Kimsingi, wameamua kuja na operesheni ya kupinga uongozi wa
Rais
Magufuli. Nina uhakika wa kutosha kati ya operesheni
zitakazoshindwa
vibaya ni hii. Kwa sababu wakati ile nyingine kwa kiasi
ziliakisi hisia
za Watanzania wengi na zilibeba kwa kiasi maudhui ya
matamanio yao hii
ya sasa ni operesheni ya wasomi wachache (the few elite)
ambao wanaamini
kinadharia na kwa sababu zao za kisomi kuwa Magufuli ni
dikteta.
Wanaamini hivi na wanataka watu wa kawaida ambao hawaoni huo
udikteta wa
Magufuli waunge mkono.



Operesheni hii itafeli kwa sababu, mamilioni ya Watanzania
waliokuwa
wanalalamikia watoto wao kukosa madawati leo wanaona
madawati
yanatengenezwa na kupatikana kwa wingi, waliokuwa
wanalalamikia watu
kutokuwajibika au kuwajibishwa wanaona watu vigogo
wanawajibishwa kila
kona, na wale ambao walikuwa wanataka kuona serikali
inasimamia vizuri
watendaji wake wanaona hilo linatokea tena bila kupepeseana
macho.



Wale ambao wanafikiri kuna haki ya kuonekana kwenye runinga
mubashara
(live) na kuamua kugoma kwa sababu hawaonekani mubashara
wanaweza kupata
shida. Wananchi wa kawaida wanajua ipo haki ya kujua (right
to
information) lakini hakuna haki ya kuonekana. Kuandamana
kutaka watu
waonekane mubashara wakati watu wanapata nafasi ya kujua
hata bila kuona
kwa wengine ni kuanza kuchanganya mambo.



Wale ambao kwa muda mrefu walikuwa wanataka mafisadi
washughulikiwe bila
huruma leo hii wanaanza kupinga serikali ambayo imeanzisha
na kutenga
fedha tayari kwa ajili ya mahakama maalumu ya kushughulikia
wahujumu
uchumi na mafisadi. Sasa unagoma ili kiwe nini? Serikali
iache mpango
huo? Unagoma ili serikali isihamasishe ujenzi wa madarasa
mapya na kwa
haraka? Unagoma ili watu wabovu na wasio na weledi
wasiendelee
serikalini? Unagoma ili tuendelee tulikokuwa?



Ndio maana hofu yangu ni kuwa tusipoangalia baada ya
harakati hizi
kushindwa; ndugu zetu wapendwa hawa wanaweza wakaja na
operesheni
"Ukutiukuti". Hii itakuwa ni operesheni ya aina yake,
watu wataambiwa
wasimame pamoja kuonesha umoja lakini ni umoja katika
kuzunguka duara!
Tatizo la kuzunguka duara ni kuwa halikomi! Binafsi
ningependa kuiona
Chadema inarudi na kuwa chama cha siasa na kufanya mambo
yake kama
Chadema, na kupitia taasisi zake.



Hizi operesheni zake mbalimbali siyo tu zinapoteza muda
mrefu lakini pia
zinatishia zaidi uhai wake kama chama cha siasa na kwa vile
viongozi
wake hawajawajibishwa kwa madudu yao ya mwaka jana, basi
wanaweza kabisa
kwenda kuipoteza Chadema kuelekea 2020. Na wasije wakadhani
kumlaumu
Magufuli kwa madudu yao kutawapatia simanzi kwa wananchi;
Magufuli
amechaguliwa na kuungwa mkono na watu ambao walikuwa
wanatamani
mabadiliko ya kweli. Atahukumiwa na wananchi hao ifikapo
2020.



Na mabadiliko hayo watu wameyaona; hayahitaji kupewa jina la
operesheni.
Ni matumaini yangu baada ya kutoka M4C hadi Ukawa na kutoka
Ukawa hadi
Ukuta, wana-Chadema na wale wenye kuamini siasa za upinzani
watakuwa
wamechoka na hawatokuwa tayari kuimbishwa tena Ukutiukuti au
Kumbaya my
Lord Kumbaya! Kwani, tukianza kufanya siasa kama burudani,
wananchi na
watu wanaotuamini wanaweza waka wanasubiria kama watu
wanaosubiria wimbo
mpya wa Diamond, Ali Kiba na wasanii wengine.




--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.



--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment