Sunday 21 August 2016

Re: [wanabidii] Dola zote kubwa zilizowahi kujengwa duniani zilijengwa na watawala kama Mhe. Magufuli.

Marekani ilijengwa kwa katiba madhubuti. Ingawa kuna wakati ilikuwa inakiukwa lakini katiba hiyo hiyo ilitumiwa kuirudisha nchi kwenye mstari wa mwelekeo wake.
Bila katiba ndugu zangu weusi wangeendelea kuishi maisha ya kunyanyaswa. Bila katiba wanawake wasingeruhusiwa kupiga kura.
em,

2016-08-21 12:07 GMT-04:00 Edgar Mbegu <embegu@hotmail.com>:
Hakuna jipya hapa! Mbona hujasema mandeleo ya Zimbabwe wakati huu wa Mugabe? Mbona hujasema maendeleo ya Malawi wakati wa Kamuzu Banda? Mbona hujasema maendeleo ya Uganda wakati wa Idd Amin? Maendeleo ya Kongo (DRC) wakati wa Mobutu? Husemi maendeleo ya Burundi sasa ? Maendeleo ya Marekani kabla ya Demokrasia maana yake nini? Husemi yaliyotokea DDR (Ujerumani Mashariki) wakati wa  Erich Hönecker ukilinganisha na BRD (Ujerumani Magharibi) wakati wa Helmut Kohl? Husemi Jugoslavia wakati wa Tito, Husemi Romania wakati wa Nikolai Ciausescu ukilinganisha na sasa? Husemi Philipines wakati wa Ferdinand Marcos? 

Date: Sun, 21 Aug 2016 15:22:48 +0000
From: wanabidii@googlegroups.com
To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: [wanabidii] Dola zote kubwa zilizowahi kujengwa duniani zilijengwa na watawala kama Mhe. Magufuli.

Fuatilia nchi zote zilizoendelea anzia, Marekani, China, Urusi na kwinginepo walitanguliza maendeleo kabla ya Demokrasia. Kwan chi nyingi za Afrika tulitanguliza Demokrasia badala ya maendeleo.
Kwa sasa nchi yenye mafanikio makubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki ni Rwanda.

Ukiambiwa miaka ya 1990 kulikuwepo na vita vya wenyewe kwa wenyewe hutokubali kwa jinsi inavyokimbia kimaendeleo. Unajua kwa nini? Ndani ya Rwanda kuna baba mmoja tu kwa sasa akisema wakalime wanaenda kulima kulima, hakuna atakaebaki kwa kucheza pooltable au kuandamana, akisema rushwa stop watu wanafunga wallet zao.

Tanzania tumezoea kubembelezana sana, JK alituparuhusa ya kuzurura zurura usiku na mchana tunapiga domo. Kwa miaka yote kumi ni maandamano tu, mara operation sangara kama si sato au M4C na kadhalika, hata wapinzani wenyewe walidiliki kusema tunahitaji rais  mkali zaidi ya JK na yeye mwenyewe alituahidi  kuwa atakuja na leo tumempata tunaanza kutafuta kick za hovyo  hovyo kabisa wakati shida kubwa ya sisi watanzania ni maendeleo wala si UKUTA kama wanavyotaka kutuaminisha.

Nani aliyekuwa anaifahamu Libya ya mliyekuwa mnamuita dikteta?? Ni Libya hipi ya kukumbukwa hii ya leo inayoruhusu maandamano ya vurugu kila leo na kushindwa kuyadhibiti na kulinda usalama wa raia wake na mali zao au ile Libya ya aliyekuwa akiitwa dikteta Gadafi?

Nendeni Misri ya leo nao kuanzia January hadi decemba  wapo mitaani wanaandama pamoja na kutafutana kwa mitutu ya bunduki halafu linganisheni na Misri ya aliyekuwa akiitwa dikteta Mubarak akiwa madarakani.

Dola zote kubwa zilizowahi kujengwa duniani zilijengwa na watawala kama Mhe. Magufuli. Tafuta dola yeyote kubwa ya zamani halafu tafuta staili zao za uongozi iliyokuwepo na maendeleo wanayojivunia leo.

Lakini leo hii wanasiasa wetu wanataka na kutamani kufanya damu za watoto wa masikini kuwa daraja la wao kupata umaarufu, Serikali imeruhusu maandamano kwa sharti la Mbowe mna Lowassa pamoja na familia zao ikiwemo wake na watoto wao kuwa mstali wa mbele katika maandamano, natamani tulione hilo September 1 lakini hawatathubutu ni waoga, wanapenda kuonyesha ujasiri katika kamera za wanahabari huku wakiwafanya watoto wa masikini kuwa chambo cha wao kupata front page za magazeti na umaarufu.

Natamani maandamano yao ya Septemba mosi  yaanzie kule Hai mkoani kililimanjaro, Mbowe awaitekina Sugu, Msingwa, Lema, Prof Baregu na wengineo pale nyumbani kwake au hotelini kwakwe Protea kule Machame.

Namshangaa sana Mbowe, anahubirije demokrasia wakati wakati yeye haishi katika yale anayoyazungumza? Kama Kitilya,Mwigamba na Zitto watu watau hao waliandika waraka na kuusevu kwenye PC zao ila waliishia kufukuzwa kama mbwa hiyo ndiyo demokrasia anayoihubiri?

Hivi Mbowe anapogombeaga uenyekiti wa chama huwa anashindanisahwa na nani? Lowassa alipopewa nafasi yay a kugombea urais Chadema mwaka jana alishindanishwa na nani?

Watanzania wenzangu kwa kweli atakayekutana na mkono wa dola kwenye maandamno ya tarehe 1/9/2016 shauri yake na msianze kutusumbua kwa kututumia picha mikiwa mmelowa damu nahilo ndilo wanalolitaka Mbowe na Lowassa.

Ndudu zangu Watanzania hakuna hoja yeyote ya msingi ya kutufanya tuandamane nchi nzima hiyo tarehe 1/9/2016 hili ni jaribio la UHAINI.
Kama swala la Tulia walimkimbia wenyewe na kama hakufuata kanuni zilizotungwa na bunge, hicho chombo kina taratibu zake za kudili naye na si kuja kutusumbua wananchi.

"Kila mmoja afanye siasa kwenye eneo alilochaguliwa, Kingu mbunge wa Ikungi Magharibi afanye mikutano yake ale pale kwake alipoahidi shughuli za maendeleo, Mbowe afanye siasa pale pale Hai aliochaguliwa na kuahidi kuwapa maendeleo, kila mmoja aliyechaguliwa afanye siasa eneo lake."

"Sitaki kuona mtu anatoka HAI kwenda KAHAMA kufanya mikutano n.k Mbunge au diwani wa HAI au Mbeya  hana mamlaka ya kuingia ndani ya majimbo ya yao. Huwezi kuwa mbunge wa Ubungo ukaenda kufanya vikao vya maendeleo kwenye eneo ambalo si lako".

"Wanaotaka kuandamana au kufanya mikutano kiholela kwanini wasubiri mwezi wa 9? Wafanye mikutano hata leo ili wajue mimi ni nani. Siwezi kuigeuza hii nchi ya sisa, nataka nchi ya maendeleo tu. Siasa zilishakwisha wakati wa KAMPENI muda huu ni wa KAZI TU".
Hiyo ndiyo kauli Rais Magufuli, nafikiri ndio siku Mbowe atabatizwa kwa moto kama atakuwa mstari wa mbele, ikiwa hawezi kuwa mstari wa mbele aache kuwafanya chambo watoto wa masikini manufaa yao ya kisiasa na kupata umaarufu.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment