Monday, 18 July 2016

Re: [wanabidii] KUWAFUNGIA MATABIBU CLINIC ZAO: NI mkakati wa kukuza ubunifu au tunafanya tusichokijua?

Nimemaliza kujifuta machozi. Umenikosea sana Misango. Umenikumbusha ya Dr. Masau. Baada ya kummbaliza wakajiita majina ya hospitali ambayo alikuwa anataka iwasaidie watanzania. Mungu apishe mbali hata siku moja nisilale katika hospitali hiyo Kila ikitamkwa taasisi ya moyo na nanihii nasikia ki9chefuchefu.
--------------------------------------------
On Mon, 7/18/16, 'Charles Misango' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] KUWAFUNGIA MATABIBU CLINIC ZAO: NI mkakati wa kukuza ubunifu au tunafanya tusichokijua?
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Monday, July 18, 2016, 3:24 PM

Naungana
nawe Elisa kwa maoni yako. Kinachotusumbua watanzania wengi
naweza sema ni 'ushamba' uliopitiliza ukawa
'ujinga'.. Ujinga uliotusukuma wengi kuwa na wivu wa
kipuuzi uliozaa roho mbaya.

Enzi ya
Mwalimu, utawala wake na hasa yeye mwenyewe alikuwa na moyo
wa kuwainua watanzania. kuwaonyesha wazungu kwamba ngozi
nyeusi sio laana wala kukosa akili, ujuzi na maarifa. Yeye
katika umri mdogo aliwahenyesha na wanalijua hilo. Kitendo
cha kumteua kijana mdogo kwa umri wakati huo, Salim Ahmed
Salim kuwa balozi kilishangaza wengi. Au alipomtuma kijana
mdogo wakati ule kwenda israel kusomea uhandisi, marehemu
Beda Amuri kilikuwa ni kitendo cha kuutambulisha ulimwengu
kuwa ipo siku tutakwenda huko kwa weupe kuwafundisha
kazi.Mzee
kaondoka na ujasiri huo. Nyuma wakabaki wasaidizi wake
waliohusudu sana, wageni. Jambo likifanywa na mtanzania
mwenye uchu wa kuchuma mali za halali kwa bidii yake,
atakwamishwa sana. Reginard Mengi hata kama ana matatizo
yake, kama sio kusimama imara asingefika hapo alipo.
Serikali iseme imeweka mkono gani kwake kufika hapo? Dk
Masau, mtaalamu bingwa wa magonjwa ya moyo alitendewa unyama
wa kutisha na waliotakiwa kumuunga mkono kwa nguvu zote.
Nina uhakika Dk Masau angekuwa mweupe, angelambwa hata miguu
na kupewa kila ambacho angetaka. Lakini mswahi wa Majita,
wapi na wapi.Mzee wa
kikombe cha Loliondo, alikimbiliwa kwa sababu aliegemea
mambo ya Imani na Kanisa lake akiwemo askofu wake,
wakamuunga mkono.Kumbe
akina Mwaka walitakiwa kusaidiwa pale walipokosea, kusudi
waweze sasa kutenda vyema. sio kufungia bila kuangalia mtu
huyu kasota vipi kufanikisha kazi yake


On Saturday, July 16,
2016 6:40 PM, 'Hildegarda Kiwasila' via Wanabidii
<wanabidii@googlegroups.com> wrote:Kuna dreva mmoja wa chuo kikuu Dar (UDSM)
katibiwa cancer ya mguu kwa dawa ya miti shamba. Maisha yake
yamekuwa mapya kwani hata kutembea alikuwa hawezi wakati
Muhimbili na Ocean road wanatumia miale na mbinu sa kisasa.
Hebu fikiria ni raha na furaha kiasi gani Tiba Asili
imemponya! Full doze ni 450,000/= kwa matibabu ya miezi
3.

Cha kufanya ni Wizara ya
Afya na Jinsia kutafuta mwekezaji au hela kujenga kiwanda
cha kufyatua dawa ziwe katika unga, maji, mafuta etc na kuwa
packaged kama inavyotakiwa. Mbona zinafanyiwa utafiti na
kuthibitishwa na Muhimbili na Taasisi ya Utafiti wa Tiba
asili kuthibitishwa na NIMR na TFDA? Zipo za kutoka nchi
mbali mbali zinauzwa kariakoo. Baadhi ya tabibu hawakusoma
kabisa wamerithi kutoka wazazi, bibi na babu na watu
wanatibiwa wanapona. Madaktari wa Tanzania walipelekwa China
kusomea barefoot doctors na kujua masuala ya Tiba Asilina
Mbadala na ndio wapo wizarani kitengo cha Tiba Asili. Ulaya
unanunua dawa asili packaged. Wajenge kiwanda kifyatue dawa
kiusalama zaidi. Badala ya kushindana na kufungiana-dialogue
inahitajika. Mbona Baraza la Wizara la Tiba Asili lipo na
Vyama vya Waganga au Tabibu Asili vipo na vimeandikishwa
kisheria. Wanakutana na Wizara kupitia wawakilishi wao ktk
Baraza-dialogue inashindikana kivipi.

Kwenye waganga wa Tiba Asili kuna
specialization pia-kutibu magonjwa mbali mbali na wengi
wamesaidiwa kwa bei nafuu badala ya kwenda India kutibiwa 
matibabu ya kisasa. Wanaotibu  pumu, malaria, parkinsons,
uzazi, kupooza, kichwa kuuma etc kwa miti shamba/miti dawa
na madini asilia au dawa asilia.

Tutatue matatizo kwa majadiliano na makubaliano
kabla ya wahusika wa kuwafungia hawajaanza kwenda mwendo
kazi barabarani na kuyapita magari ya sasa ya jiji ya mwendo
kasi ili Tiba Asili aje kuonyesha mfano wa kumtibu ili apate
kuheshimiwa!

Kama Kawa

--------------------------------------------
On Sat, 16/7/16, Emmanuel Muganda <emuganda@gmail.com>
wrote:

Subject: Re:
[wanabidii] KUWAFUNGIA MATABIBU CLINIC ZAO: NI mkakati wa
kukuza ubunifu au tunafanya tusichokijua?

To: "wanabidii@googlegroups.com"
<wanabidii@googlegroups.com>
Date: Saturday, 16 July, 2016, 16:53

Elisa,Nakuunga mkono. We are
our own worst
enemy.em

2016-07-16 3:30 GMT-04:00
'ELISA
MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:
Zamani
fulani niliwahi
kuandika makala katika moja ya magazeti

iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho: Wabunifu wetu
wa
magobole wamo magerezani wakilindwa na
magobole ya wabunifu
wenzao kutoka
India.

Nilichosema ni
kuwa Tanzania imewakamata watengeneza

magobole ambayo (magobole) yalikuwa hayakutengenezwa kwa
kibali. Na India hivyohivyo. Sisi
watengenezaji hao wa
magobole tukawashtaki
kwa kutengeneza magobole hayo bila
kibali
cha serikali. India wa kwao ikawatafutia nyenzo
wakaendelea kutengeneza magobole na (India)
kuanza kuyauza
nje. Sisi kwa kuwa tulikuwa
tunatafuta bunduki za kulinda
magereza yetu
tukagundua kuwa zile zinazouzwa India

zinatufaa. Tukazinunua na zikasaidia maaskari magereza
wetu
kulinda wafungwa wetu wakiwemo
wabunifu wetu wa magobole.
Nilipokuwa
naandika makala hiyo kulikuwa na kesi mahakamani
na watu hao walihukumiwa vifungo kweli. Siyo
India peke yake
inayogeuza 'uhalifu'
kuwa Fursa. Uganda enzi za Obote
ilikuwa na
shida ya waganda kutengeneza gongo wakati gongo
hilo ni haramu. Baadaye uongozi wa Obote
ukachemsha kichwa
(okufumba omutwe).
Wakawageuza wapika gongo kuwa wakala wa

'Uganda Waragi'. (kwetu ni Konyagi) hivyo Uganda
waragi
ikawa inanunua Gongo na kulichuja na
kuliweka kwenye chupa
hivyo tatizo
likapungua, (halikuisha).


Tanzania ina dira yake sasa. Tunataka kujenga uchumi wa
kati
ifikapo 2025. Njia moja wapo ni kukuza
viwanda. Huo ni
mpango wa Taifa. Si
serikali peke yake inayotekeleza pango
huo.
La! Serikali, Taasisi za kidini, Wananchi, wataalamu wa
kila sekta, wanasiasa-wote tunatekeleza hilo.
Ndiyo maana
wanaoona; vyama vya siasa
walipofungiwa kufanya mikutano ya

kikampeni-tuliunga mkono. Tunaona wanataka kutupotezea
muda
kwa kisingizio cha demokrasia.

Moja kati ya mikakati ya
kutekeleza lengo hilo la taifa
wakajitokeza
watanzania wenzetu wasomi wa mambo ya afya

katika ngazi ya kati (Matabibu) wakafanya utafiti kwa
kuoanisha magonjwa wanayoyajua kitabibu; na
matibabu ya
kienyeji (Kiasili). Serikali
kwa kutambua hilo ikawawekea
utaratibu.
Waitwe watoa tiba ya asili au tiba mbadala.


Dawa ya kutibu malaria (kwa mfano) kwa
dawa ya kienyeji, ni
bakuli moja ya lita
moja mara mbili kwa siku. Wao kwa
kuangalia
ukubwa wa lita na uwezo wa kuitumia wakajitahidi
wakaiweka katika unga na sasa wamefikia hatua
ya kutumia
unga wa kijiko kimoja kwenye
glass ya maji. Ni hatua
hiyo.

Watu hawa wameendelea na
sasa wana clinics nyingi na
zinatibu
magonjwa ambayo baadhi yameshindikana katika
hospitali zinazoitwa za kisasa.

Dawa zao zimepiga hatua
kutoka kibakuli cha lita moja mpaka
glass
moja. Wamepiga hatua kiasi cha kutengeneza vifungashio
vizuri tu vya kisasa. Wakasema sasa huduma zao
ni za
'kisasa'. Kwa neno hilo
wakafungiwa.

Majuzi rais
wetu amewakaribisha wahindi kuja kuwekeza katika
viwanda vya madawa, badala ya kuendelea
kutuuzia dawa.
Ukienda India baadhi ya
viwanda vinavyotuuzia madawa hayo
viko
uwani mwa nyumba za kuishi. Wanachofanya ni kutumia
majina ya viwanda vikubwa na luweka
'label' zao na
kuwalipa kamisheni.
Ndizo tunazotumia na huwezi kujua labda

Mwijage (waziri wa viwanda) akienda huko. (Namuamini ana
uwezo wa kugundua hilo. Wengine hamna).

Miti inayotumika kutengeneza
dawa ya Malaria ni Cinchona na
imezagaa na
ndiyo Bukoba wanatengeneza dawa za

'Omushana' lakini China wanatuletea Malaraquine. Dawa
za
Dr Mwaka tunasema za asili na akisema za
kisasa tunamfungia
lakini za Mchina
tunazikubali na kuziita za kisasa. Tofauti

ya dawa hizi ni moja: za wachina hatujui
wanakozitengenezea.
Ndiyo tofauti. Kumbe
akina 'Dr. Mwaka' wa China
walisaidiwa
na serikali yao na sasa wanatuuzia dawa na sisi
tumefaulu kuwanyamazisha wabunifu wetu sasa
tunataka 'Dr.
Mwaka' wa kichina na wetu
tunaua. Dr. Mwaka akikosea
akaenda china na
kuanzisha kiwanda akaiita 'hwa ngwi

chi', dawa zake zitanunuliwa tena kwa garama kubwa na
kutumika katika hospitali zetu za kisasa.

Hivi muda tunaotumia
kumlaumu Dr. Mwaka na wenzake kwa
kutumia
neno 'matibabu ya kisasa' badala ya

'asili/mbadala' kwa nini tusiutumie kumsaidia
kuzifanya
dawa zake za kisasa? Kama
tumehakikisha zinatibu; kama
tumehakikisha
zinaboreshwa kutoka bulkiness mpaka small

packages; Kama amefikia hatua ya kuzifungasha
vizuri-tunashindwa nini kumpeleka mbele akawa
wa kiwango cha
kisasa?

Kwa kuzima ubunifu Tanzania inaweza kusifika.
Ukiondoa swala
la magobole, tunakumbuka
jinsi Mafuta ya Ubuyu ulivyozimwa.
Ukienda
Dodoma vijijini kukutana na mzee wa myaka 120
anakimbizana na mbuzi kama kijana ni jambo la
kawaida.
'Watafiti' wa
kyenyeji/asili/mbadala wa kitanzania

wakahusishaa matumizi ya mbegu za ubuyu na uzee mwema
huo.
Wakafanya utafiti; wakayakamua na
yakaanza kuwasaidia
watanzania kiafya na
kiuchumi. Akakurupuka huko mtu na
kusema
mafuta hayo ni 'hatari kwa binadamu'. Kulikuwa na
uvumi kuwa kuna mtu mmoja alitaka kuhodhi soko
la mafuta
hayo na akaanza kwa kuzima
wanaoyauza. Kwamba ni kweli au
sio hiyo
siri kubwa.

Sipendi
kuamini kuwa katika amri hii ya matibabu kufungiwa
ina swala la mahusiano ya mtu na mtu kwa
makusudi ya
kukomoana. Tunafahamu kuwa
kuliwahi kutokea mzozo kati ya
uongozi mpya
wa wizara ya Afya na Clinic ya Dr. Mwaka.

Lakini nadhani hakuna mahusiano na si kusudi la makala
hii
kulijadili. Kalamu imeteleza tu.

Ninachosema ni kuwa Tanzania
inahitaji kufanya zaidi ili
kukuza sayansi.
Lazima tujipe nafasi ya kutumia akili

zetu.

Nimesikia habari za
uanzishwaji wa ''Jiji la sayansi'.

Nilisikiliza sana nikahofu tunaanza jiji hilo na kosa la
msingi ambalo litatupoteza njia. Mpango wa
jiji hilo ni kuwa
Mtu mwenye degree akiwa
na wazo la ubunifu atapeleka wazo
hilo.
Wataalamu wenzake watalipitia na lifanyiwe kazi.
Najiuliza Wasomi wetu wenye degree wamewahi
kubuni nini
kinachosaidia jamii.
Waliofungiwa wote wako ngazi ya kati.

Matabibu; yaani Clinical officers (au Clinical
Assistants).
Kama tutajikita kuwatumia
wenye degree tu basi kukwama kwa
kutimiza
lengo la kuanzisha jiji hilo kutaanzia hapo.Elisa Muhingo

0767 187 507-- Send Emails to wanabidii@googlegroups.com   Kujiondoa Tuma Email
kwenda
 wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya

 kudhibitisha ukishatuma   Disclaimer: Everyone
posting to this Forum bears the sole

responsibility

 for any
legal consequences of his or her postings, and
hence


 statements and facts must be presented responsibly.
Your


 continued membership signifies that you agree to this

 disclaimer and pledge to
abide by our Rules and
Guidelines. --- You received this message
because you are subscribed to
the

 Google Groups
"Wanabidii" group. To
unsubscribe from this group and stop receiving
emails


 from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com. For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.comKujiondoa Tuma Email kwenda


wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatumaDisclaimer:


Everyone posting to this Forum bears the sole
responsibility
for any legal consequences
of his or her postings, and hence

statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree
to this
disclaimer and pledge to abide by
our Rules and
Guidelines.


---

You
received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this
group and stop receiving emails
from it,
send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.


--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda


wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:


Everyone posting to this Forum bears the sole
responsibility
for any legal consequences
of his or her postings, and hence

statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree
to this
disclaimer and pledge to abide by
our Rules and
Guidelines.


---


You received this message because you are subscribed to
the
Google Groups "Wanabidii"
group.

To unsubscribe
from this group and stop receiving emails

from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to
this Forum bears the sole responsibility for any legal
consequences of his or her postings, and hence statements
and facts must be presented responsibly. Your continued
membership signifies that you agree to this disclaimer and
pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message
because you are subscribed to the Google Groups
"Wanabidii" group.
To unsubscribe
from this group and stop receiving emails from it, send an
email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.
--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment