Bam
On 1 Oct 2015 13:44, "'mpombe mtalika' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
-- --Privatus Karugendo
TUNAPOELEKEA Uchaguzi Mkuu wa 2015, tutayasikia mengi. Na tumeanza kuyasikia na tutaendelea kuyasikia kufikia tarehe yenyewe ya uchaguzi, Oktoba 25, 2015. Mengine ya ukweli na mengine ya uongo. Watu wataanza kupakana matope na kuharibiana majina. Kutakuwa na mapambano makali kati ya chama na chama. Vyama vikubwa vinakabana .
Kila mtu anataka ashinde na kila chama kinataka kishinde. Hiyo ndiyo siasa na huo ndiyo ubinadamu. La msingi ni kusema ukweli.Tusipindishe mambo. Wezi wa nchi hii wanafahamika, mafisadi wa nchi hii wanafahamika, wazalendo na watu safi wasiohongeka wanafahamika na ni wengi. La msingi ni kuacha siasa za chuki na kumshambulia mtu binafsi. Vile vile ni vyama kutangaza sera na kuyaeleza yale watakayoyafanya wakiingia madarakani.
Maisha ya mtu binafsi, maisha ya familia yake, maisha ya afya yake si suala la kisiasa. Pamoja na uangalifu wa kuzuia kurudia uchaguzi kwa kipindi kifupi, mengine tumwachie Mwenyezi Mungu, yeye akitaka, tunaweza kuurudia uchaguzi hata mara tatu kwa mwaka. Tuache siasa za uongo na chuki. Siasa hizi za uongo, chuki, umbea na uhasama, zimeanza kujitokeza kwa nguvu.
Tumeweka mambo ya msingi pembeni na kuanza kushughulikia umbea na uhasama. Baadhi ya vyombo vya habari vinavyoaminika vimeanza kupotea njia. Magazeti yanaandika uongo na kueneza chuki. Watu tulioambiwa ni magamba, wakatangazwa na vyombo vya habari kwamba ni mafisadi, leo hii wamesafishwa na watu wale wale walio watangaza. Tunaambiwa wametubu na kusamehewa.
Wametubu wapi? Fedha za Richmond zimerudi? Aliyepitisha mkataba huo mbovu amekamatwa na kufikishwa mbele ya sheria? Sifa za Edward Lowassa, tunazifahamu.
Hata ukirudi nyuma kwenye vyombo vya habari utauona ukweli huo. Leo hii ndiye anapamba magazeti yote. Leo hii ndiye baadhi ya watu wanamtaka awe Rais wa Tanzania. Huku ni kuupotosha ukweli na kuwapotosha wananchi. Hizi ndizo tunaita siasa za uongo na siasa za hatari.
Tumekuwa tukisikia sifa za Dk. John Magufuli. Hata ukirudi nyuma na kupekuwa magazeti yote, utakuta Magufuli, mchapakazi. Magufuli, anayejenga barabara na kupambana dhidi ya wezi kama alivyoshika meli iliyokuwa ikivua samaki kwenye Bahari ya Hindi. Leo hii tunaanza kusikia uongo juu yake kwa vile anapambana na mtu mwenye nguvu za kifedha.
Tuseme ukweli na kuacha uongo. Lowassa na Magufuli, wamekuwa ndani ya serikali. Ni wazi kwa wagombea urais waliojitokeza, hawa wawili wana nafasi kubwa mmoja wao kutokea mshindi. Sote tunajua utendaji kazi wao. Tukiacha ushabiki wa vyama vyao vya siasa na kulitanguliza taifa letu. Tutakubaliana kwamba sifa za Magufuli ziko juu zaidi. Na kama kweli tunayataka mabadiliko, tunayoyalilia, tunalazimika kumchagua Magufuli.
Jambo la msingi ambalo tunapaswa kuliangalia kwa makini ili tuhesabike kati ya jamii iliyostaarabika na inayoheshimika duniani ni lazima tufanye siasa zinazozingatia ukweli. Ni jambo la kawaida katika ushindani wa kisiasa watu kutafuta kuangushana, na kila mmoja anataka kushinda, ili ushindi uwe wa amani, ni lazima washindani kueleza ukweli dhidi ya wapinzani wao. Maana kama lengo ni kuijenga Tanzania bora, yenye amani na utulivu, hakuna haja ya kuupindisha ukweli. Gharama ya kupindisha ukweli ni kubwa na yenye hasara kuliko faida.
Ni ukweli kwamba Lowassa, aliachia ngazi ya Uwaziri Mkuu, kwa kashifa ya Richmond. Hadi ninapoandika makala hii, hatujamsikia akifafanua juu ya suala hili.
Nani alihusika na Richmond? Ni ukweli kwamba Lowassa, ndiye baba wa mtandao. Mashabiki wake wanatamba kwa hili hadi kusema kwamba mtandao huo, aliouanzisha Lowassa na kuendelea kuuratibu ndio ulimwingiza madarakani Rais Jakaya Kikwete.
Mtandao umekivuruga Chama Cha Mapinduzi, mtandao umelivuruga taifa letu. Kama una kitu cha kujutia ni mtandao. Mfumo huu ndio uliozaa "kichaa" cha kila mtu kufikiri anaweza kuwa rais wa nchi, kila mtu anaweza kuwa mbunge. Mtandao umezaa utamaduni mpya wa kutumia fedha kwenye uchaguzi, utamaduni wa kununua kura na kununua shahada za uchaguzi.
Huu ni mfumo mchafu ambao hauwezi kuanzishwa na mtu msafi, mtu wa kuwa na sifa za kuliongoza taifa letu.Uchunguzi wa kina unaonyesha Magufuli, si sehemu ya mtandao huu, ndiyo maana maadui zake wanasema hana mizizi ngani ya CCM. Kuwa na mizizi ni kuwa kwenye mtandao, na kuwa kwenye makundi. Hivyo huyu ana nafasi ya pekee ya kukiunganisha chama chake na kuliunganisha taifa zaidi ya baba wa mtandao. Huyu ndiye anayefaa kuliongoza taifa letu.
Haya tunayasema bila ushabiki wowote na bila lengo au nia ya kuomba fedha kutoka sehemu yoyote ile. Tunayesema bila kuangalia vyama vya siasa, nguvu na ushawishi wa vya hivi. Tunaangalia uhai wa taifa letu. Tunaiangalia Tanzania ya leo na kesho. Huu ni ukweli ambao ni lazima kuusema na ni ukweli utakaotuweka huru.
Hapa Tanzania, ukiachia mbali kiti cha rais, nafasi nyingine zinazokuwa na ushindani mkubwa ni ubunge na udiwani. Hizi zote ni nafasi za uwakilishi. Mbunge anawawakilisha watu wa jimbo lake bungeni na diwani anawawakilishia watu wa kata yake kati vikao vya halmashauri ya wilaya. Nafasi hizi zinakuwa na siasa za uongo, chuki, umbea na uhasama.
Ni bahati mbaya kwamba baadhi ya wale wanaochaguliwa kwenye nafasi hizi wanafikiria zaidi juu ya posho kuliko kuuzingatia na kuutafakari wajibu wao wa kuwawakilisha wananchi, wajibu wa kuelezea ukweli, kulinda ukweli na kuusimamia ukweli. Kazi hii ni ngumu kiasi kwamba kama watu wangeifahamu vizuri, ni wachache wangeikimbilia!
Ni bora wananchi wakatambua hili kwamba wanapomtafuta mbunge wa kuwakilisha jimbo lao ni lazima wamtafute mtu mwenye uwezo na karama ya kutetea ukweli na kuusimamia bila kuyumbishwa na vitisho, rushwa, upendeleo au ubinafsi. Bunge ni chombo muhimu katika taifa letu. Katiba inasema:
"Sehemu ya pili ya Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katitika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii" (Ibara 63(2)).
Tumekuwa na utamaduni wa mafiga matatu. Kila chama cha siasa kina kauli mbiu ya mafiga matatu. Utatu mtakatifu wa kura ya rais, mbunge na diwani. Yawezekana ni utamaduni mbaya au mzuri, la msingi ni kuchagua kwa kuzingatia vigezo. Tusichague kwa ushabiki wa vyama vya siasa.
Tuchague kwa kulitanguliza taifa letu la Tanzania. Tumchague rais wa kuliongoza taifa letu, rais wa vyama vyote vya siasa, rais wa makabila yote, rais wa waumini wote. Hii ndiyo kazi kubwa iliyo mbele yetu. Ni kazi inayohitaji ukweli zaidi ya upotoshaji
Raia Mwema
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment