Monday, 12 October 2015

Re: [wanabidii] Mabadiliko tuliyokuwa tunayahitaji siyo ya udini ukanda na ukabila..ni ya kupinga ufisadi.

Mwesiga,
Akhsante mTanzania mwenzangu.

Kama Mwananchi wa kawaida natamani haya yatokee uchaguzi huu;

1. BUNGE liwe changanyikeni.
2. Rais ajue kilichompeleka Ikulu akiwa na sifa stahiki.
Baasi!!

Tuangalie namna ya kupata maslahi yetu kwa namna tunayoona sisi inafaa. Tusisikilize kile politicians wanatuambia!! Hao wanatuelekezea kibla watuchinje vizuri tu!!
RULE NO. 1; DONT TRUST ANYONE/ANYBODY.
Wanasiasa ni kabila jingine watanzania wenzangu. Dont put any trust kwake. Never ever.
"Acquaintance, n. A person whom we know well enough to borrow from, but not well enough to lend to." - Ambrose Bierce

Uchaguzi huu ni wa muhimu kwetu kuliko kitu chochote, tukishindwa kuamua hapa kwa usahihi ujue tumekwisha. Kuwapa nguvu kubwa chama chochote kikubwa ni kujichimbia kaburi. Iwe CCM au CDM.
Amin nawaambieni kuna watu mnawaona wazuri leo ila mjue wakishika madaraka hawatatoka kirahisi na mambo hayataenda vile tunavyotaka. CCM wakirudi na wabunge wengi watataka kujiimarisha maana wamewashiwa time alert tayari, CDM nao wanajua this is their last time, if they can't rise here, wamepotea. CDM ya 2020 ni NCCR/CUF ya 2010!! Tunajua pilika pilika za wabunge wao bungeni haswa kwenye mijadala tajiri japo baadhi wamelala kidogo majimboni, bado nina imani utendaji wa serikali ukiwa mzuri utafukia mapungufu yao. They reason good more than CCM MP's.

Sitaki CCM iwe na wabunge wengi bungeni, tena hawa ndio wabaya kabisa in term of decison making, wana vitabia vya kuhongana wawe na maamuzi ya aina moja. pia CDM na vyama vingine iwe na wabunge more than 45%. Tukiwa na bunge la changanyikeni lenye watu makini, hakuna kitakachoshindikana. Bunge lina nguvu sana kama litapangwa sawa sawa. Na mkumbuke ni wabunge hawa hawa tunawatumia kutengeneza Baraza la Mawaziri. Hofu yangu wabunge wasiwe wajinga wakaanza kushabikia hoja za mawaziri kulingana na pande za vyama vyao. Watu wa aina hii wapo tunawajua!!

Mambo yoote yanayopewa kipaumbele na wana UKAWA (watanzania wenzangu) yanaweza kufanywa na bunge la namna hii!! Kilichokuwa kinawashinda wabunge wa upinzani ni kura zao tu kuwa chache. Katiba iliwabana sana. Sasa waende, watuandalie katiba na kujadili sera zetu huko huko.

Huu sio muda wa tambo za huyu ni bora kuliko yule. Tuangalie NANI ni BORA katika NINI, apewe NAFASI yake anayoFIT na kustahili, sio anayoitaka!!!
Tunachagua wafanyakazi wetu wa kututumikia, hatupigi kura ya nani kasema nini.
"Ability may get you to the top, but it takes character to keep you there." - John Wooden

NB; Pamoja na kumuunga mkono Magufuli, bado nafikiri awekewe jopo la washauri, maana kichwa chake nacho tunakijua wenyewe. Ni mzuri sana kwenye utendaji, sana, sana, ila urais ni ufuatiliaji na busara za hali ya juu sana. Unaweza kufanya positive decision na bado ikawa na negative impact + loss au negative decision na ikawa na positive impact kubwa tu.
Ningependekeza  wagombea Urais watakaoshindwa waunde team yao ikutane na Rais baada ya kila mwaka wa Budget. Kama walikuwa na lengo zuri na sisi, hawana budi kuendelea kuchangia mawazo yao kuisukuma serikali kwa namna yoyote!! Isiwe wamemaliza uchaguzi na mambo yamekwisha. NO!! We can have any of our own political structure only that it can pay us something worth!! Hakuna wa kutuzuia. Tuwe mfano kwa wengine.

"An education isn't how much you have committed to memory, or even how much you know. It's being able to differentiate between what you know and what you don't." - Anatole France

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment