Saturday, 1 August 2015

Re: [wanabidii] RE: [Mabadiliko] NINAMUUNGA MKONO LOWASSA KUGOMBEA URAIS

1. Cha muhimu kwangu ni kwamba kutokana na sababu na mazingira ya wakati ule viongozi wa Chadema walimsema Lowassa fisadi kwa nguvu zao zote.
2. Pamoja na haya yote, Lowassa na viongozi wa Chadema na Ukawa wameyamaliza kwa kukubaliana Lowassa awe mgombea Chadema na Ukawa.
3. Hivyo, kama wahusika wenyewe wame'reconcile' sisi tunataka nini? After all, Lowassa hajawalalamikia hao viongozi wa Chadema na Ukawa na inaonekana wameamua kuanza maisha upya (kama ilivyo pia kwa familia yenye mzozo wa muda mrefu inapoamua kubadilika na kuanza maisha mapya/ya heri).
4. Hata warring parties zinapo reconcile na kuacha mapigano huwa zinasaini a joint peace accord. Ni kitu cha ajabu kwa watu wengine kuanza kuhoji kwa nini hizo warring parties zimecha mapigano na ku'reconcile'.
5. Hali kadhalika ndivyo ninavyoona kwa Lowassa na Chadema na hata viongozi wengine wa Ukawa na Watanzania, ambao pia walimwona Lowassa fisadi.
6. Kama kwa miaka yote hii hajawahi kutiwa hatiani, je tuendelee tu kuimba kuwa Lowassa ni fisadi bila ushahidi? According to me, kwa vile a reasonable time has elapsed na kwa vile hakuna chombo chochote cha dola kimeshamshtaki au cha kutoa haki kutoa hukumu kuwa Lowassa ni fisadi, sioni sababu yoyote ya kuendeleza allegations. Maana kama hatutafika mwisho tuamue kama tuna ushahidi kuwa ni fisadi tuutoe na vyombo husika vichukue hatua na kama hatuna, basi tusiendelee kuimba ni fisadi maana hatuwezi kuendelea ku'allege' indefinitely. Inabidi after a reasonable time, tujiridhishe na tuamue jambo moja. Na kwa facts zilivyo kwa sasa hatuna sababu yoyote ya msingi kuendelea kuimba kuwa Lowassa ni fisadi.

2015-08-01 10:59 GMT+03:00 amour chamani <abachamani@gmail.com>:

Mushongi

Asante kwa ujumbe murua. Asante sana.
Kama vichwa vyetu vinaongozwa na hisia in hatari. Hivi hakika Leo CHADEMA wamefikia hapa?
Leo Lowasa in kila kitu.
Nakumbuka ile hadithi ya Mwenyenyumba alie msaidia tembo Mwishowe akatolewa nje.
Hivi Lowasa atakubali kuwa rais kwenye chama asiwe mwenyekiti?
Usalama wake utatoka wapi?
Hakumbuki ya Mrema na akina Marando Tanga?
Kama naona mwisho wa CHADEMA wakiwafuata wenzao NCCR na CUF.
Hili ni sawa na jaribio la mapinduzi ambalo likifeli ni kifo.

Walewale.

On Aug 1, 2015 10:46 AM, "Ireneus Mushongi" <ireneuskakurumushongi@gmail.com> wrote:
Mama Nkya
Haya yote Ni marudio Tu. Tumeshayasikia tokea vinywa mbali mbali.

Kwanini mnapindisha ukweli? Huyu huyu Dr Slaa alisema kuwa Ana ushahidi kuhusu Richmond Na Yuko tayari kuuwasilisha  mahakamani kama tu ENL atapelekwa kwa pilato.

Mbona hamuhoji hayo tena au siyo ya msingi sababu Mkaskazini huyu keshakuwa malaika na automatically msafi kwa kubadili jezi? Hawa jamaa ni wajanja wamecheza na nyakati wamehit kwenye msumari wa moto ukiwa haujapoa. Watu wamecheza na fursa adimu. Kimsingi wana malengo tofauti. Huyu ana hasira ya kuikomoa CCM hawa wanacheza na akili hiyo kujijenga kisiasa zaidi kwani popularity itaongezeka, status itapanda, watavuna wafuasi wengi at ago na si lazima waingie ikulu but watakuwa wamegain sana hata kuongeza wabunge 50 from the current number.

Next move atakuja Chenge. Ukihama CCM si unatakasika automatic? Huyu bwana ana team oliyojiuzuru naye. Sijawasikia wao kuhama au wanapima upepo bado hadi ufanyike uchaguzi. Hawa wote ndani ya Ukawa ni watukufu na wasafi hivi karibuni watajoin majeshi na kubadili jezi. Hawa hawa waliokuwa wanawaponda watawashangilia sana na kuwaita majembe!

Ninaamini Mbowe, Slaa, Lipumba, Mbatia,  na UKAWA top yote hawampendi ENL ila wametumia fursa hii kuachieve strategy zao za kisiasa. Time will tell. Kumsafisha au kutomsafisha haihusu sana. Washasema ilikuwa ni mambo ya kisiasa zaidi so watapima matokeo baadaye! Muhimu ni kugain tu kwa sasa kabla ENL hajarudi kwenye normal senses.

Tutaona mwisho wa haya... Heri sisi tusiofungamana na kipande yoyote.... Tunahitaji mabadiliko ya kweli sio ya kinafiki. Msituchanganye! Jana mlikuja kivingine, Leo mnakuja hivi kesho hatujui mtakuja na lipi. Tuonyeshe dira na dhamira sio mikakati ya fursa za zimamoto.
Umesababisha mke wa mtu aachwe,  alipopewa talaka tu, eti ndio na wewe unatangaza ndoa halafu eti tukuchangie. Tutafika? Siasa mchezo mchafu!

From: 'ananilea nkya' via Mabadiliko Forum
Sent: ‎01/‎08/‎2015 01:21
To: mabadilikotanzania@googlegroups.com
Cc: WANA BIDII
Subject: [Mabadiliko] NINAMUUNGA MKONO LOWASSA KUGOMBEA URAIS

Mimi Ananilea Nkya tatizo langu kubwa kwa Lowassa lilikuwa ni ufisadi wa Richmond uliotafuna zaidi ya shilingi bilion 172 za wananchi. Baada ya kusikia kauli yake alipohojiwa na wanahabari siku alipojiunga na CHADEMA, na baada ya kujiridhisha kuwa kama alikuwa amehusika na ufisadi wa Richmond leo angelikuwa jela kama Yona na Mramba, namuunga mkono kugombea Urais. Naamini hata Dr Slaa amemkubali Lowassa kuwa mgombea Urais wa vyama vinanyounda UKAWA baada ya kujiridhisha kuwa mamlaka ya juu ilimbebesha Lowassa kashfa ya Richmond ili kunusuru serikali nzima kuanguka.

Lakini zaidi nimeongeza imani yangu kwa Lowassa baada ya kubaini kuwa hata Baba wa Taifa Julius Kambarage Nyerere alimuona kama kijana makini mwenye maono na dhamira safi ya kuwatumikia Watanzania. Mwaka 1995 wakati Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi anamaliza muda wake  mwandishi wa habari Mwita Matinyi alimuliza Mwalimu Nyerere alikuwa anafikiri ni nani angeweza kumrithi Mwinyi kuiongoza Tanzania. Mwalimu alijibu Matinyi hivi. Nanukuu:
Ni kweli Mzee Mwinyi anaondoka lakini ndani ya CCM kuna viongozi wengi wenye sifa za kuwaongoza Watanzania, kikubwa tu awe na dhamira kwa mfano wapo wakina Warioba, Mzee Msuya na Mark Bomani na wapo vijana hodari na wenye upeo mkubwa sana kama Mkapa, Kikwete na Lowassa ni jambo la heri sana CCM kuwa na watu kama hawa (Majira 26/5/1995) ukurasa wa 3; na Nipashe 26/5/95 ukurasa wa 3).

Pia nikiwa ripota Radio Tanzania Dar es Salaam niliwahi kufanya kazi na Lowassa katika miaka ya 90. Nilivyouona utendaji wake wa kazi zama hizo nashawishika kwamba anafaa kuwa kiongozi wa nchi yetu. Nilishuhudia akijituma kweli kweli kwenye kazi za umma zama hizo.

Kadhalika namuunga mkono Lowassa kwa sababu hagombei Urais kupitia chama cha CCM ambacho kinakumbatia mfumo wa kuwadhawau na kuwafukarisha wananchi huku watawala wachache wakineemeka kwa kutumia rasilimali za nchi kama vile nchi hii ni mali ya watawala, familia zao na marafiki za. Ninaamini kwa kugombea Urais kupitia UKAWA, CCM itapunguziwa dharau na jeuri yake dhidi ya wananchi ambao ndio wenye mamlaka ya mwisho kuhusu hatma ya nchi yetu. Mfano CCM mwaka jana 2014 ilionyesha dharau kubwa sana kwa wananchi kwa kuizika Rasimu ya Katiba iliyotengenezwa kwa kutumia maoni ya wananchi wakati fedha zaidi ya bilioni 130 zilitumika. Kwa kutumia mabilioni hayo bila Katiba Mpya kupatikana ni kufisadi mali za wananchi mchana kweupe. Haikubaliki.

Vile vile namuunga mkono Lowassa kwa kwa sababu anaukataa hadharani umaskini wa kuchongwa ambao watawala wanautumia kwa faida yao ili waendelee kuwanunua wananchi mafukara wakati wa uchaguzi na wakishapata madaraka waendelee kujineemesha na mali za nchi.

Nchi yetu siyo maskini bali watawala wanaendekeza matakwa ya wawekezaji (wakoloni wa zama hizi za utandawazi wizi) ambao wanaliibia taifa rasilimali nyingi na na hatimaye nchi za wawekezaji hao (donors)wanawapoza watawala kwa vijimisaadaa uchwara. Ni aibu sana kwa kiongozi wa Tanzania kijipitisha nchi moja hadi nyingine Marekani, Ulaya, China, India na Ausralia n.k kutembeza bakuli (omba omba kama matonya vile) huku nchi yetu ikiwa na rasilimali tele. Tena wakati watawala wanakwenda kuomba eti wanapanda ndege daraja la kwanza. Huu ni wenda wazimu. Ni kuiaibisha Tanzania na Afrika.

Sina chama cha siasa ninachofungamana nacho kwa sasa, lakini namuunga mkono Lowassa kugombea Urais kupitia UKAWA kwa sababu naamini akiwa Rais wa nchi yetu upuuzi huu wa kuendekeza umaskini kwa kuomba omba nchi za nje huku tukitoa mali za nchi honyo hovyo kwa wageni na kuamini kuwa maendeleo ya nchi yetu yataletwa kwa misaada kutoka nje, kutakomeshwa. Naamini hata hao wakoloni wa zama hizi za utandawazi wizi wanajua Lowassa hatachekacheka nao.

Lakini zaidi namuunga mkono Lowassa kwa sababu Watanzania wakiridhia kwenye sanduku huru la kura hapo Oktoba awe Rais wa Tanzania, vyama vinavyounda UKAWA vitasimamia kuhakikisha kuwa mamlaka ya wanannchi hayaporwi hivyo hovyo tena. Kwa hiyo Rasimu ya Katiba ya wananchi itaheshimiwa na nchi yetu itapata Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi. Kwa kufanya hivyo taifa hili litaanza kupiga hatua kubwa ya kuondoa ufukarishwaji wa wananchi walio wengi unaofanya na watawala wa CCM kwa kushirikiana na wakoloni wa zama hizi za utandawazi wizi.

Naridhia andiko langu hili lichapishwe na yeyote anayetaka
Ananilea Nkya
 E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com


For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/1438381307.95951.YahooMailBasic%40web121006.mail.ne1.yahoo.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment