Katika hilotunawasubiri wanaosema watatumia nguvu za umma kumuingiza madarakani.
--------------------------------------------
On Mon, 8/3/15, fadhil fadhil <fadhil.fadhil96@gmail.com> wrote:
Subject: Re: [wanabidii] jamani hivi ukawa wameshindwa hata kusoma report ya Mwakyembe au ndio tumboni streets?
To: "'Hildegarda Kiwasila' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Monday, August 3, 2015, 4:39 PM
halafu leo
wanakuja watu kwa maneno mepesi na laini wanatwambia dili
lilikuwa la bosi wake kwa hiyo angepata urais kupitia ccm
asingesema.
kaka mpombe safi sana kwa kutukumbusha machungu
yanauma tena sana lakini yanatufundisha haswa katika kipindi
hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu
2015-08-03 16:25
GMT+03:00 Victor Mwita <victormwita@gmail.com>:
Hili jukwaa huwa linapendeza likijadili issues of
national interest na sio kujadili watu. Kaka Mpombe Mtalika
asante kwa mada moto moto. Na sisi wengine tunaelemika na
uchambuzi wako wa kina
2015-08-03 16:07
GMT+03:00 'mpombe mtalika' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:
3.2 Mzigo wa Malipo wa TANESCO
Mheshimiwa Spika, nimeeleza awali kuwa mbali na kulipia
gharama ya umeme
wenyewe, TANESCO inawajibika chini ya Mkataba huo kulipa
gharama za
uwezo wa mitambo (capacity charges) ambazo ni sh. milioni
152 kila siku
hadi mwisho wa Mkataba. Aidha, chini ya Mkataba huo, TANESCO
inabebeshwa
mzingo wote wa kodi, malipo na gharama mbalimbali
zinazoweza kumkabili
mwekezaji! Kifungu cha 3.4 cha Mkataba wa TANESCO na
Richmond kinasema:
"All taxes and charges arising in relation to the
importation and
exportation of the plant, equipment, tools, spare parts,
consumables,
testing and monitoring equipment or in connection with the
supplier's
performance of its obligations under this Agreement
generally that
become due in accordance with the laws of Tanzania shall be
paid for by
TANESCO at its sole cost and expense".
Mheshimiwa Spika, Tafsiri ya jumla ya kifungu hiki cha
Mkataba ni
kwamba: kodi na ada zote zinazohusiana na uingizaji ndani ya
nchi na
usafirishaji nje ya nchi wa mitambo yote, vifaa, vipuli n.k.
na gharama
zote zinazohusiana na utekelezaji wa wajibu wa Richmond
(sasa Dowans)
chini ya Mkataba, yaani gharama za uendeshaji (operations),
za
matengenezo (maintenance) ya mitambo na gharama ya gesi
inayotumika
kuzalishia umeme, ni wajibu wa TANESCO kuzibeba!
Mheshimiwa Spika, mzigo mkubwa ambao TANESCO inabeba chini
ya mkataba na
Richmond (sasa Dowans) unajirudia katika mikataba mingine
kati ya
TANESCO na makampuni mengine ya umeme kama vile IPTL,
AGGREKO, ALSTOM na
SONGAS ambayo kwa ujumla yanachukua sehemu kubwa ya mapato
ya shirika
hilo, hivyo kuvuruga kabisa mizania yake. Kwa wigo wa
tafsiri wa
mikataba hii inayotuumiza kwa kujitakia, TANESCO inawajibika
kuwalipia
hawa wanaojiita wawekezaji hata gharama za bima na ada za
mawakili wao!
Mheshimiwa Spika, tumefikishwa hapa tulipofika na mikataba
mibovu,
maamuzi ya kiimla na papara ya baadhi ya watendaji
waandamizi wa
Serikali wasiozingatia maslahi ya muda mrefu ya Taifa. Net
Group
Solution (PTY) ambayo kwa kiwango kikubwa imechangia sana
katika
kuidumaza TANESCO kiutaalamu na kifedha, iliingizwa TANESCO
kwa ubabe
bila kujali hoja za msingi za wataalamu na wafanyakazi wa
TANESCO.
Matokeo yake wote tunayaelewa. Vivyo hivyo, Richmond
Development Company
LLC, kampuni isiyo na rekodi yoyote ya kiufundi hata ya
kuchomeka
"bulb" kwenye kishikio chake, ikapewa mradi mkubwa na
Serikali wa
kuzalisha umeme wa dharura bila kujali kuhusu ufanisi wake
tena katika
kipindi ambacho nchi ilikuwa gizani! Huu ni ujasiri wa
kifisadi.
4.0 UTEKELEZAJI WA MRADI
4.1 Barua ya Dhamana ya Benki (Letter of Credit)
Mheshimiwa Spika, ili kufanikisha utekelezaji wa haraka wa
mradi wa
umeme wa dharura, Mkataba kati ya TANESCO na Richmond
Development
Company LLC, ulitoa fursa ya kufunguliwa kwa Barua ya
Dhamana ya Benki
(Letter of Credit), kwa kifupi nitaiita LC, kwa madhumuni ya
kulipia
gharama za maandalizi na za usafirishaji wa mitambo ya
uzalishaji wa
umeme huo wa dharura. Mkataba ulitaka TANESCO, Benki Kuu ya
Tanzania,
Wizara ya Fedha na Richmond Development Company LLC waketi
pamoja
kukubaliana masharti ya LC hiyo.
Mheshimiwa Spika, vyombo hivyo vya Serikali vilikaa tarehe 7
Julai, 2006
baada ya kupokea mapendekezo kutoka Richmond Development
Company LLC ya
namna ambavyo ingetaka ilipwe. Vyombo hivyo vya Serikali
vikarekebisha
kidogo madai ya Richmond na kuamua kuwa kampuni hiyo ilipwe
Dola za
Kimarekani 30,000,000 (milioni thelathini), sawa na asilimia
30 ya
thamani ya malipo ya Mkataba kwa kipindi cha miaka miwili
kwa masharti
kwamba: asilimia 12 ya fedha hizo ilipwe kama malipo ya
awali (Advance
Payment) baada ya kuwasilishwa hati ya madai (Invoice), hati
ya
Uthibitisho wa Udhamini wa Benki (Bank Guarantee) kwa
TANESCO na
uthibitisho wa kusafirisha mitambo kuleta Tanzania; asilimia
10 ilipwe
baada ya kuwasilishwa hati za kusafirishia mitambo kwa
mpangilio wa
awamu; asilimia 8 ilipwe mara baada ya uzinduzi wa mitambo.
Mheshimiwa Spika, siku tatu baadaye Richmond Development
Company LLC
ikataka masharti hayo yarekebishwe ili kuipa kampuni hiyo
unafuu zaidi,
wazo ambalo TANESCO ililikataa kwa kuhofia kuwa kampuni hiyo
ingeweza
kupotea baada ya kupata malipo ya awali yasiyo na masharti
magumu.
Tarehe 27 Julai, 2007 Wizara ya Nishati na Madini ikaingilia
kati
mvutano huo na kuitisha kikao kilichosimamiwa na Waziri Mhe.
Dr. Ibrahim
Msabaha, Mb kama Mwenyekiti. Kikao hiki kilihusisha wajumbe
kutoka
Wizara ya Fedha, TANESCO, Benki Kuu ya Tanzania, Mwakilishi
kutoka CTI
na Richmond Development Company LLC. Kama ilivyokuwa kwa
kikao cha
tarehe 7 Julai, 2006, Mwanasheria Mkuu wa Serikali wala
mwakilishi wake
hakuhudhuria.
Mheshimiwa Spika, kikao hiki kikaamua kurekebishwa kwa
masharti ya LC
kama ilivyopendekezwa na Richmond Development Company LLC.
Baadhi ya
marekebisho yalikuwa:
(i) Kampuni hiyo ilipwe asilimia 17.5 ya jumla ya thamani ya
Mkataba
baada ya Benki ya kampuni hiyo kupokea hati za usafirishaji
wa mitambo
(shipping documents), hati ya bima, orodha ya vifungashio
(packing
list), hati za uasili wa bidhaa (Certificate of origin),
hati za
upangaji wa mizigo (packing lists), pamoja na hati ya madai
(Invoice)
kwa mtambo wa MW 22.
(ii) Kampuni hiyo ilipwe vilevile asilimia 17.5 ya jumla ya
thamani ya
Mkataba baada ya TANESCO kutoa hati ya uthibitisho ya
mitambo kuwasili
eneo la kazi (Ubungo, Dar-es-Salaam).
4.2 Mchakato wa Kufungua Barua ya Dhamana ya Benki
Mheshimiwa Spika, baada ya makubaliano hayo, tarehe 23
Agosti, 2006
TANESCO iliiomba Citibank (Tanzania) kufungua LC kwa ajili
ya Richmond
Development Company LLC yenye thamani ya Dola za Kimarekani
30,696,598.00. Siku hiyo hiyo ya terehe 23 Agosti 2006,
Citibank
(Tanzania) iliwajulisha TANESCO kwamba isingeweza kufungua
LC kwa ajili
ya Richmond Development Company LLC, kutokana na kile
walichoeleza kuwa
ni kutopata muda wa kutosha kuchunguza kwa kina uwezo wa
mteja
anayehusishwa na dhamana ya malipo hayo (due diligence)
kabla ya kuingia
Mkataba huo.
Mheshimiwa Spika, baada ya kukataliwa na Citibank, TANESCO
waliiomba
Benki ya CRDB kufungua Barua ya Dhamana ya Benki hiyo kwa
masharti sawa
na yale yaliyopelekwa Citibank (Tanzania). Tarehe 25 Agosti,
2006 CRDB
ikafanya mawasiliano Citibank (New York). Lakini tarehe 2
Septemba 2006,
Citibank (New York) ikaifahamisha CRDB kuwa wao pia
wasingeweza
kushiriki katika kufungua LC kwa Richmond Development
Company LLC
kutokana na mahitaji ya lazima ya kuzingatiwa chini ya
Kifungu Namba 7
cha Kanuni za UCP 500. Kifungu hicho ndicho kilichowafanya
Citibank
(Tanzania) kukataa kufungua Barua kama hiyo.
Mheshimiwa Spika, kitendo cha benki hizo mbili za Kimarekani
kukataa
kufungua LC kwa jili ya kampuni ya Kimarekani, kilitosha
kuzua wasiwasi
wa msingi kuhusu kampuni hiyo. Kwa kuwa Watanzania
tuliishaamua kufa na
Richmond, tukasonga mbele! Hivyo, tarehe 2 Septemba 2006,
CRDB ikafungua
upya LC kwa ajili ya Richmond Development Company LLC
kupitia Benki
nyingine ya nje iitwayo HSBC kwa masharti yale yale ambayo
CRDB ilipokea
kutoka TANESCO. Hatimaye HSBC ikafungua LC kwa ajili ya
kampuni hiyo
lakini kwa kutumia jina lingine la RDEVCO na siyo Richmond
Development
Company LLC!
4.3 Maombi ya Mapya ya Richmond kubadilisha tena Masharti
ya LLC.
Mheshimiwa Spika, baada ya LC kufunguliwa na kuthibitishwa
uwajibikaji
kwa utekelezaji wa masharti ya Mkataba ulianza rasmi. Hata
hivyo, tarehe
4 Oktoba 2006, Richmond Development Company LLC kwa mara
nyingine tena,
iliipelekea TANESCO maombi ya kutaka kuifanyia marekebisho
ya LC
kwamba:-
(i) LC iruhusu malipo ya awali (upfront payment) ya Dola
za Kimarekani milioni 10;
(ii) Richmond Development Company LLC iruhusiwe kusafirisha
mtambo wa
kwanza kwa njia ya ndege kwa gharama ya Dola za Kimarekani
5,696,568.00;
(iii) Asilimia 50 ya Barua ya Dhamana ya Benki ilipwe baada
ya uthibitisho kutoka TANESCO juu ya kupokelewa kwa mitambo
nchini.
Mheshimiwa Spika, tarehe hiyo hiyo ya 4 Oktoba, 2006 Wizara
ya Nishati
na Madini ikaitisha kikao kujadili maombi hayo. Kikao hiki
kilichohudhuriwa na wawakilishi kutoka Wizara ya Nishati na
Madini,
TANESCO, Benki ya CRDB na Richmond Development Company LLC,
kikakubali
maombi yote ya Richmond Development Company LLC na kuagiza
kuwa hatua za
utekelezaji zifuatie mara moja.
Mheshimiwa Spika, pamoja na ukweli kwamba mchakato mzima
ulitawaliwa na
udharura, Kamati Teule haielewi ni vipi Wizara ya Nishati na
Madini
ilikuwa ikitekeleza kila pendekezo jipya lililotolewa na
Richmond
Development Company LLC bila kujali madhara ambayo yangewea
kutokea
pindi kampuni hiyo ingelipwa na kuingia mitini.
Mheshimiwa Spika, baada ya kubaini kwamba mapendekezo hayo
mapya ya
kuibeba Richmond yalikuwa nje ya masharti ya LC
yaliyoainishwa katika
Mkataba wa malipo kati ya TANESCO, Benki Kuu ya Tanzania,
Wizara ya
Fedha na CRDB Bank, Wizara ya Nishati na Madini ikaijulisha
Wizara ya
Fedha kuhusu maamuzi mapya ya LC kutokana na maombi ya
Richmond
Development Company LLC.
Mheshimiwa Spika, Wizara ya Fedha haikuridhishwa na
mapendekezo
yaliyotolewa kwani malipo yoyote ya awali kutoka fungu
maalum la
Multilateral Debt Relief Initiative ni lazima yafanyike kwa
uthibitisho
wa kuridhisha. Sehemu ya barua hiyo iliyoandikwa na Katibu
Mkuu wa
Wizara ya Fedha, Ndugu Gray Mgonja, inasema:
: "... tunaona kuwa tofauti na taarifa zilizotolewa wakati
wa
majadiliano ya Mkataba kuwa mkandarasi aliyechaguliwa
alikuwa na vifaa
tayari kuvileta nchini, sasa ni wazi kuwa si hivyo.
Kama unavyojua, msingi wa malipo kuhusu mitambo ya kununua
au kukodisha
chini ya Mradi wa Nishati ya Dharura unaofadhiliwa kupitia
IMF MDRI, ni
mkataba unaotokana na majadiliano.
Napenda kupendekeza kuwa malipo yoyote ya awali kutoka
akaunti ya MDRI
lazima yaandamane na dhamana ya kuridhisha kutoka kwa
mkandarasi. Sharti
hili linaonyesha kutokuzingatiwa chini ya mapendekezo
yenu".
Mheshimiwa Spika, pamoja na maelekezo na ushauri huu wa
Wizara ya Fedha,
Wizara ya Nishati na Madini siku hiyo hiyo ikaiandikia
barua TANESCO
kuitaka itekeleze maombi ya Richmond Development Company LLC
mara moja
kubadilisha masharti ya malipo:-
" . . . I wish to inform you that the proposed amendments
to the
existing Letter of Credit are acceptable and you are advised
to liaise
with CRDB Bank to effect the changes as soon as is
practical. . . ."
Barua ya Katibu Mkuu wa Nishati na Madini (Kumb. Na.
CBD.214/324/01 ya
tarehe 6/10/2006) inasomeka.
Mheshimiwa Spika, Kamati Teule imejiuliza bila kupata
majibu: Ni nini
kilifanyika hadi Wizara ya Nishati na Madini ikatoa kauli
hii ambayo ni
tofauti kabisa na ushauri ilioupata kutoka Wizara ya Fedha?
Nini msingi
wa ukereketwa au ufukukutwa bayana wa Wizara ya Nishati na
Madini kuhusu
Richmond?
Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza maagizo ya Wizara,
TANESCO
iliiandikia barua Benki ya CRDB tarehe 6 Oktoba, 2006
kuitaka kufanya
mabadiliko hayo mapya kwenye LC ya Richmond. Tarehe 9
Oktoba, 2006 Benki
ya CRDB iliijibu TANESCO na kuikumbusha kwamba LC
inasimamiwa na
makubaliano ya pamoja chini ya uangalizi wa Benki Kuu ya
Tanzania. Kwa
msingi huo TANESCO ikatakiwa kufuata taratibu kwa kuiomba
Benki Kuu ya
Tanzania kibali cha kufanya marekebisho katika Kifungu 1(a)
cha Mkataba
wa makubaliano ya taratibu za malipo ili kuwezesha maombi
yaliyopendekezwa kufanyiwa kazi. Jibu hilo likailazimu
TANESCO kufuta
maombi hayo.
Mheshimiwa Spika, hadi LC hiyo ya Richmond inaisha muda wake
(tarehe 30
Novemba, 2006), kampuni hiyo ya Kimarekani haikuweza
kutekeleza sharti
hata moja na hivyo kushindwa kuchukua fedha kama ilivyokuwa
imepangwa.
Swali linalojitokeza ni: Iwapo CRDB ingekubali kubadilisha
masharti ya
LC na kuipa Richmond Development Company LLC fedha ilizoomba
bila kibali
cha Benki Kuu ya Tanzania; Je, Richmond ingeleta nchini
mitambo kama
ilivyokusudiwa au ingekuwa ni hasara kwa Taifa?
Kwa upande mwingine, mchakato mzima wa Richmond Development
Company LLC
wa kutaka kufanya mabadiliko katika Barua ya Dhamana ya
Benki mara kwa
mara unadhihirisha nia yao ya kutaka kupata mtaji. Pia
inadhihirisha
kwamba Richmond Development Company, LLC haikuwa na uwezo wa
kifedha wa
kutekeleza Mkataba huu kinyume na tamko kwenye Mkataba
kuwa:-
"The Supplier (i.e. Richmond) has the equipment and the
financial and
technical capability to construct, install, commission,
operate and
maintain such a plant as required by TANESCO". (Msambazaji
(yaani
Richmond) ana vifaa na uwezo wa kifedha na wa kitaalam
kujenga,
kusimika, kuiwasha, kuendesha na kuendeleza mtambo huo kama
TANESCO
inavyohitaji.)
Mheshimiwa Spika, kwa msingi huo Kamati Teule ilijiuliza
maswali yafuatayo:-
(i) Je, utafiti ulifanywa kufahamu gharama halisi za mitambo
mipya
kutoka kwa watengenezaji wenyewe bila ya kupitia kwa
mawakala? Kamati
Teule ilibaini kuwa zoezi hilo liliwahi kufanyika mwaka 1998
tu ambapo
Wizara ya Nishati na Madini ilitoa kazi hiyo kwa wataalam wa
sekta
(consultants) na kufanikisha kugundua kuwa bei ya mitambo ya
umeme ya
IPTL (400 MW) ambayo ilitakiwa kuuzwa kwa Dola za Kimarekani
milioni 150
(Tsh. 187.5 bilioni) bei yake halisi ilikuwa ni Dola za
Kimarekani
milioni 85 (Tsh.106.2 bilioni) tu na hivyo kupata kigezo cha
kukataa bei
yao. Hivyo basi, kutokana uzoefu huo, Wizara ya Nishati na
Madini kwa
kushirikiana na TANESCO walitakiwa kufuatilia bei hizo za
mitambo na pia
makadirio ya kazi za ujenzi ili kupata picha ya gharama
halisi ya mradi
jambo, ambalo halikufanyika.
Mheshimiwa Spika, kwa viongozi wa Wizara na TANESCO
kushindwa kujua bei
halisi ya mitambo kutoka kwa watengenezaji wenyewe kwa
takribani miaka
10 huku wakisafiri kwenda nje ya nchi kila kukicha kwa
mikutano, warsha,
makongamano, n.k, na kwa Wizara kung'ang'ania kutumia
mawakala badala
ya watengenezaji wa mitambo, nchi yetu imegeuzwa gulio la
wajanja
kuikamua na kuwabebesha wananchi mzigo wa kodi.
Mheshimiwa Spika, Kamati Teule ilipotembelea Marekani,
iliamua
kuwatembelea baadhi ya watengenezaji wa mitambo ya
uzalishaji wa umeme
huko huko Houston Marekani kujua bei za mitambo yao. Mmoja
wa
watengenezaji wenye jina kubwa duniani, Kawasaki Gas
Turbines –
Americas, anatengeneza na kuuza Mtambo mpya aina ya GPB180
wenye uwezo
wa kuzalisha MW 17.5 kwa Dola za Kimarekani 7.5 milioni
(Tsh. 9.4
bilioni). Mawakala huwa wanatuletea mitambo ya aina hiyo
hiyo kwa bei
mara mbili ya bei halisi.
(ii) Iwapo TANESCO au Serikali iliweza kufungua LC ya Dola
za Kimarekani
30,696,598; je, fedha hizo zisingeweza kutosheleza kununua
mitambo
mipya ya uzalishaji umeme, na mitambo hiyo kubakia mali ya
TANESCO,
badala ya kuingia katika Mikataba ya ghali ya kukodisha
mitambo?
Aidha, taarifa za watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini
kwamba wakati
wa kipindi cha mchakato wa zabuni ya umeme wa dharura
kulikuwa na ugumu
wa kupatikana mitambo ya umeme wa dharura zimethibitishwa
na Kamati
Teule kuwa sio za kweli.
Mheshimiwa Spika, ni ukweli kwamba kulikuwa na ukame, lakini
ukame huo
haukuwa wa mitambo ya kuzalisha umeme kwani mitambo hiyo
hutengenezwa
muda wote na sio kwa kutegemea mvua. Aidha, utafiti wetu
umebaini kuwa
katika kipindi hicho cha matatizo ya umeme nchini, kampuni
zote za
kutengeneza mitambo hiyo ya umeme zilikuwa zina mitambo
kadhaa ikisubiri
wateja. Kawasaki ilikuwa na mitambo 8 ya kisasa tena yenye
kutumia gesi
na dizeli (dual fuel plant). Serikali nyingi, ikiwemo ya
Nigeria, ni
wateja wazuri wa kampuni hiyo ambao huteremshiwa bei kwa
mtambo moja
hadi Dola za Kimarekani milioni 6.7 milioni badala ya Dola
za Kimarekani
milioni 7.5 bei ya kawaida.
Mheshimiwa Spika, kwa thamani ya LC iliyofunguliwa kwa
Richmond
Development Company LLC ya Dola za Kimarekani milioni 30.7
au Tsh 38.4
bilioni, TANESCO ingeweza kununua mitambo mipya yote minne
pamoja na
kumudu kulipia gharama za kusafirisha kwa meli hadi
Dar-es-Salaam. Hivyo
ili zipatikane MW 105.6 zilizohitajiwa na TANESCO
ingehitajika mitambo
sita (6) ambayo ni sawa sawa Dola za Kimarekani milioni 45
au Tsh. 56.25
bilioni badala ya Dola za Kimarekani milioni 87 au Tsh.
108.7 bilioni
tulizobebeshwa na Richmond Development Company LLC.
Mheshimiwa Spika, Je, si dhahiri kuwa hii ndiyo ilikuwa nia
ya Richmond
Development Company LLC, yaani kupata fedha za malipo ya
awali (advance
payment) ili ikatununulie mtambo mmoja na kuja kutukodisha
sisi wenyewe,
hivyo kufaidika na capacity charge ya kila mwezi kwa
Mkataba wa miaka
miwili? Kwa mtambo mmoja wa MW 22, capacity charge ni Dola
za Kimarekani
takriban 730,871 au Tsh. Milioni 913.6 kwa mwezi, hivyo kwa
miezi 24 ni
wastani wa Dola za Kimarekani 17,540,912 au Tsh. Bilioni
21.9.
(iii) Kwa kuwa thamani ya LC inalipwa kama malipo ya awali
(advance
payment), Je, hii si sawa na kutoa mkopo kwa Richmond
Development
Company LLC? Kamati Teule inaona kwamba hiyo ni sawa na
kutoa mkopo usio
na riba kwa mfanyabiashara wa nje ili awe mwekezaji.
(iv) Kwa nini katika Mkataba wa Richmond Development Company
LLC kifungu
cha kufidia malipo ya awali (advance payment) ya LC
hakikuwekwa bayana
ndani ya Mkataba tofauti na Mikataba mingine, badala yake
ikawekwa fursa
ya kujadiliana na mkandarasi? Kamati Teule haioni sababu
yeyote ya
msingi mbali na wahusika kujiwekea fursa ya kukidhi maslahi
yao binafsi.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Victor Caleb Mwita
Ministry of Livestock and Fisheries Development
P.O. Box 9152
Dar Es Salaam
Tel: 0766750673, 0789142275
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment