hatari sana, ndionakubali sana maneno ya Mh Arfi alipomwambia Mh Lisu kuwa aweke akiba ya maneno
2015-08-02 13:00 GMT+03:00 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:
Jamani muda tu ndio utaamua. Kinachoniumma ni watanzania kukikosa chama chao walichokipenda kwa sababu ya kumkaribisha ndugu yetu huyu basi.
--------------------------------------------
On Sun, 8/2/15, Ireneus Kakuru Mushongi <ireneuskakurumushongi@gmail.com> wrote:
Subject: Re: [wanabidii] Haya ndio maneno ya mnyika juu ya ufisadi wa Lowasa miaka miaka 7 iliyopita leo hii wnadai amekuwa mtakatifu
To: "wanabidii@googlegroups com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Sunday, August 2, 2015, 11:12 AM
"Kwa
niaba ya Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA), kwa taarifa
hii tunarudia
kukemea jitihada zozote za kumlinda na kumtangaza Lowassa
kuwa shujaa katika taifa letu kwani hali hii ikiachwa kuendelea inatoa
mfano mbaya kwa vijana wa Tanzania. Tusingependa kwa namna yoyote katika taifa
letu, mtuhumiwa wa ufisadi aliyetajwa pia katika orodha ya
mafisadi(list of shame) kulindwa na kuenziwa kama shujaa wa
Taifa letu kwani ni kuharibu maana nzima ya ushujaa katika
uwajibikaji."
Omukunirwa
Ireneus
2015-08-02 9:31 GMT+03:00
'mpombe mtalika' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:
Wednesday, September 3, 2008
SERIKALI IACHE KUMLINDA LOWASSA
Siku chache zilizopita. Nilitoa taarifa hii kwa vyombo
vya
habari. Hata hivyo, kwa sababu ambazo sizifahamu, habari hii
haikutoka katika
magazeti mengi ya kila siku. Pengine inaweza ikawa ni njia
iliyotumika
kufikisha ujumbe(barua pepe) lakini kuna uwezekano mkubwa
sababu ikawa ni kuwa
Lowassa hakutajwa kuchukuliwa hatua kama hizi ambazo
nimezieleza hapa katika
yale Maazimio 23 ya Bunge.
Yeye aliambiwa tu atakafakari na kuchukua maamuzi
ambayo
ataona yanafaa. Yeye akaamua kujiuzulu. Lakini bado
siridhiki sana na sababu
hii kwa kuwa maazimio hayo 23 hayajasema Karamagi na Msabaha
wachunguzwe kuhusu
Rushwa kama serikali ilivyoamua. Kama imeamualiwa na
Serikali hawa wachunguzwe,
kwanini serikali haikumjumuisha na Lowassa? Hii inafanya
niamini kwamba bado
msimamo huu hapa chini ni mwafaka:
TAARIFA KWA UMMA
SERIKALI IACHE KUMLINDA
LOWASSA
Ni mmoja wa mizizi
ya ufisadi wa Richmond
Akamatwe,
ahojiwiwe na achukuliwe hatua za kisheria.
Tarehe 25 Februari, 2008 Vijana wa CHADEMA tulitoa
taarifa
kwa umma tukikemea jitihada zilizokuwa zikiendelea za
Lowassa kujisafisha na
kusafishwa na tukahimiza achukuliwe hatua za haraka kutokana
na tuhuma za
ufisadi na/ama matumizi ya madaraka katika kashfa ya
RICHMOND. Pamoja na
taarifa yetu hiyo kwa umma katika kipindi chote ambacho
Serikali ilipewa na
Bunge kutekeleza maazimio ya Bunge kuhusu suala hilo hatua
tulizopendekeza
hazikuchuliwa.
Aidha
tumefadhaishwa zaidi na Taarifa ambayo Waziri Mkuu,
Mheshimiwa Mizengo ameiwasilisha Bungeni Alhamisi 28 Agosti,
2008 pamoja na
kutaja hatua ambazo zimechukuliwa kuhusu watuhumiwa wengine
ikiwemo kuandikiwa
Barua za kujieleza na/ama kuanza kuchunguzwa na vyombo vya
dola/usalama; Waziri
Mkuu hakueleza hatua ambazo zimeaanza kuchukuliwa dhidi ya
Bwana Lowassa.
Tunatambua kuwa Waziri Mkuu katika taarifa yake
ameeleza
kuhusu hatua ambazo serikali imeanza kuchukua ikiwemo za
marekebisho ya Sheria
ama mifumo ya uwajibikaji, ikiwemo ile ya manunuzi. Hata
hivyo, tungependa
kuweka bayana kwamba matatizo ya msingi ya taifa letu
hayasababishwi na
mapungufu katika sheria pekee, ila kwa kiasi kikubwa
yanasababishwa na kulegea
kwa misingi ya utawala wa sheria na uwajibikaji miongoni mwa
viongozi
. Hivyo,
tunapenda kuwajulisha Watanzania kuwa kama watuhumiwa wa
ufisadi
hawatachukuliwa hatua mapema, misingi ya utawala wa sheria
itazidi kutetereka
na matokeo yake ni kuwa mageuzi yoyote katika mifumo ya
kiutawala
hayatatekelezwa kikamilifu. Kwa ujumla tunaamini kwamba
utamaduni huu wa
kulindana katika serikali unatoa mfano mbaya kwa vijana wa
kitanzania kuhusu
uongozi na utawala bora.
Tungependa kusisitiza kuwa Bwana Lowassa, akiwa Waziri
Mkuu
wa nchi yetu wakati huo alikuwa mmoja wa mizizi mikuu ya
ufisadi wa RICHMOND.
Hivyo, tunaona kuwa Taarifa ya Utekelezaji ya Waziri Mkuu
Pinda imejikita
katika kushughulikia matokeo badala ya mzizi wa tatizo
lenyewe na hivyo kama
hali hii ikiendelea itaporomosha nidhamu na uwajibikaji
katika taifa letu.
Tunaamini kwamba kama Bwana Lowassa aliyekuwa kinara wa
Serikali wakati huo,
ataweza kuchukuliwa hatua kikamilifu basi itakuwa rahisi kwa
waliokuwa chini
yake kuweza kuchukuliwa hatua za haraka na hatimaye
kurejesha maadili katika
utawala. Lakini kama Serikali itaendelea kumlinda Bwana
Lowassa na kuwatoa
kafara maafisa wa chini, bado haitakuwa imetekeleza
kikamilifu dhana ya
uwajibikaji na utawala wa Sheria. Kujiuzulu kwa Waziri Mkuu
na mawaziri wenzake
kadhaa ni hatua ndogo sana katika kashfa iliyohusisha
uvunjaji wa Sheria za
nchi yetu, mazingira ya ufisadi na hasara kubwa kwa
taifa.
Sisi tunaona kutotajwa kikamilifu kwa hatua
zilizochuliwa
juu ya Bwana Lowassa ni mwendelezo wajitihada za miezi ya
karibuni za Bwana
Lowassa(Mb) kupita akijitetea kuanzia katika hotuba yake
alipokwenda Jimboni
Monduli na kunukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari na
hata mahojiano yake
maalumu na Televeshioni ya Taifa(TVT).
Aidha, taarifa ya Waziri Mkuu Pinda imeakisi uamuzi wa
Waziri Mkuu aliyejiuzulu Bwana Edward Lowassa kujitokeza
miezi ya karibuni
kujitetea kuhusu kuhusika kwake katika kashfa ya Richmond
ambayo kwa ujumla ni
ishara ya unafiki wa kisiasa.
Itakumbukwa kuwa baada ya Kamati
Teule
kuwasilisha taarifa yake, Bwana Lowassa alipata nafasi
bungeni takribani mara
mbili kama kiongozi wa shughuli za serikali bungeni wakati
akiwa Waziri
kuzungumzia suala hili lakini hakutoa utetezi ambao Mwezi
Februari alijaribu
kuutoa kwa umma
Waziri Mkuu Pinda inabidi auleze
Umma kama uamuzi wa
kumtomtaja katika Taarifa yake ya utekelezaji kuhusu hatua
ambazo amechuliwa ni
ishara kuwa serikali imekubaliana na utetezi wa Bwana
Lowassa.
Itakumbukwa kuwa Vijana wa CHADEMA tulieleza wazi
kwamba
katika kujitetea kwake mwezi Mei, Bwana Lowassa
alithibitisha wazi uzembe na
matumizi mabaya ya madaraka ambayo aliyafanya alipokuwa
Waziri Mkuu wakati wa
sakata zima la Richmond. Hivyo, tunarudia kutoa mwito kwa
vyombo vya dola
kuweza kumkamata, kumhoji na kumchukulia hatua za kisheria
dhidi ya uzembe na
matumizi hayo mabaya ya madaraka kwa mujibu wa sheria za
nchi yetu.
Badala ya
Bwana Lowassa kuendelea kupita akijitetea kuwa Kamati Teule
haikumuita kuweza
kujieleza; vyombo vya dola vimkamate akatoe maelezo yake
panapohusika. Vyombo vya
dola vimekuwa vikiwakamata raia wa kawaida wenye taarifa za
uhalifu kuweza
kuisadia polisi, inashangaza Bwana Lowassa amejieleza wazi
kuwa alikuwa
anafahamu uhalifu uliokuwa ukitendeka lakini bado yuko nje
akijitetea na pia
Taarifa za kiserikali zikielekea kumlinda
. Tunaamini akikamatwa yeye,
atawezesha watuhumiwa wakuu wa kashfa ya Richmond kuweza
kupatikana. Tulieza
wazi katika tamko letu na Mwezi Februari kuwa , jitahada
zozote za kumlinda na
kumtetea zingeweza kuathiri mwekekeo wa hatua ambazo
zitanatarajia kupendekezwa
na Kamati ya Waziri Mkuu mpya Mheshimiwa Mizengo Pinda.
Kutokana na Taarifa ya
Waziri Mkuu Pinda aliyowasilisha Bungeni Alhamisi tarehe 28
Agosti, 2008 ni
wazi kuwa kuna kila dalili kuwa mwelekeo huo umeanza
kuathiriwa, hivyo
tunarudia tena kutaka Bwana Lowassa achukuliwe hatua kabla
ya Bunge la Mwezi
Novemba, 2008.
Bwana Lowassa akiwa Waziri Mkuu amethibitisha kwamba
maneno
yake mwenyewe kuwa alikiuka Sheria ya Maadili ya Viongozi wa
Umma ya mwaka 1995
na Sheria ya Makosa ya Udhibiti wa Uhujumu wa Uchumi wa nchi
ya Mwaka 1984.
Bwana Lowassa alikiri kwamba alikuwa anafahamu kwamba
Richmond ni kampuni ya kitapeli, lakini katika kipindi chote
cha uongozi wake
aliinyamazia hali hii na kwa kiasi kikubwa aliitetea kampuni
hiyo mbele ya
macho ya umma. Wakati wa Viongozi mbalimbali wa upinzani
walipoweka bayana
kwamba Richmond ni kampuni isiyo na uwezo, serikali ilitetea
kampuni hiyo.
Vyombo mbalimbali vya habari vilimtuhumu Bwana Lowassa mwaka
2006 na 2007 kama
kiongozi wa Shughuli za serikali bungeni, kwamba alishiriki
'kuwaziba midomo'
wabunge wa CCM wasijadili suala hili.
Pia, ni Bwana Lowassa huyo huyo,
alinukuliwa akiwa Arusha akiwataka watanzania wasiijadili
kampuni ya Richmond
baada ya mvua kuanza kunyeshaKama Bwana Lowassa wakati wote
huo alijua kama
ni kampuni ya kitapeli kama anavyojaribu alivyojaribu
kujitetea, uamuzi wake wa
kuwaasa watanzania wasiijadili ulikuwa ni wa kulinda ufisadi
ambao aliufahamu.
Inashangaza pia ni Lowassa huyo huyo alisema alijua kuwa
Richmond ni kampuni ya
kitapeli; ni Lowassa huyo huyo alisema kwamba alishauriwa
vibaya na watumishi
wa umma aliowataja kuhusu uwezo wa Richmond; Ni Lowassa huyo
huyo aliyesema
kwamba alijua kuwa TANESCO chini ya Menejimenti ya Net Group
Solution walitaka
kuhujumu mchakato wa tenda na hivyo
'kuwanyang'anya'.
Lakini ni Lowassa huyo
huyo aliyekuwa Waziri Mkuu ambaye angeweza kuviagiza vyombo
vya dola kumwezesha
kuthibitisha 'utapeli wa Richmond'; hivyo, maelezo ya
sasa yanayotolewa kuhusu
ushiriki wake yanaonyesha kuwa sasa kuna mwelekeo wa
kumlinda.
Tunaendelea kushangazwa na Serikali na Bwana Lowassa
kutumia
utetezi wake kueleza tu nia yake ya kutaka mkataba wa
Richmond usitishwe; nia
ambayo kama ni kweli alikuwa na uwezo wa kuitekeleza na
hakuitekeleza.
Tunaitaka Serikali na Bwana Lowassa kuweka bayana ni kwa
vipi Richmond ilipewa
tenda hiyo na kwa shinikizo la nani. Bwana Lowassa anakwepa
kuyazungumzia haya
kwa kuwa anajua kabisa kwamba ni yeye aliyetumia madaraka
yake vibaya alipokuwa
Waziri Mkuu kwa kukiuka Sheria na Taratibu za Ununuzi kwa
'kupora' mchakato
uliokuwa ukiendeshwa na TANESCO, 'kuunda kamati yake' na
kuzisukuma mamlaka za
ununuzi hali iliyopelekea Richmond kupewa tenda ili hali
haikuwa na uwezo
uliotakiwa.
Ni uzembe
huu ambao umelisababishia hasara taifa kwa kulipa
shilingi milioni 152 kila siku kwa kampuni ya Dowans
iliyohamishiwa mkataba wa
kitapeli wa Richmond; na takribani bilioni 172 kwa ujumla
ambazo taifa
linawajibika kuzilipa kutokana na kukodisha mitambo hiyo.
Hvyo tunarudia tena
rai yetu ya kutaka fedha zilizozilipwa kizembe mpaka sasa
kurejesghwa
serikalini.
Kwa
vyovyote vile, jitihada za Bwana Lowassa za kuhamasisha
ujenzi
wa Sekondari Kata, na utumishi wake kama Waziri Mkuu katika
kipindi cha miaka
miwili, haviwezi kuzidi hasara aliyosababisha katika uchumi
wetu kipindi chote
tulichokosa umeme wa dharura na wala hailingani na hasara
ambayo tunaendelea
kuilipa kila siku iendayo kwa Mungu. Maamuzi haya ya Bwana
Lowassa yanaendelea
kuwaumiza wananchi wote ikiwemo wa Jimbo lake la Monduli
ambao wanataabika kwa
mzigo wa gharama za umeme.
Tunarudia tena kumkumbusha Rais Kikwete kwamba Sheria
ya
Maadili ya Viongozi wa Umma inamtaka Rais kuhakikisha kwamba
taratibu
zinatengenezwa zitakazojenga maadili na kuongeza imani ya
wananchi kwa uadilifu
wa viongozi wa umma na katika taratibu za utoaji maamuzi
ndani ya Serikali na
katika sekta ya umma.
Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma vile vile imeweka
kanuni zinazotakiwa kuongoza utendaji wa viongozi wa umma:
kwamba wanapokuwa
madarakani, viongozi wa umma watakuwa waadilifu, wenye
huruma, utulivu, umakini
na watakaoendeleza viwango vya juu vya maadili ili kujenga
na kuendeleza imani
ya umma kwa uadilifu wa Serikali.
Kuhusiana na utoaji wa maamuzi,
viongozi wa
umma watatekeleza wajibu wao kufuatana na sheria na kwa
maslahi ya umma. Hivyo,
taarifa ya Waziri Mkuu Pinda kutokueleza bayana hatua ambazo
Bwana Lowassa
ameshachukuliwa au atachukuliwa ni ishara kuwa kauli ya Rais
Kikwete aliyoitoa
wakati akizungumza na Wazee wa CCM mkoani Dar es Salaam
kwamba Bwana Lowassa
amepata tu 'ajali ya kisiasa', na kumsifu kwa utumishi
wake imechangia kumlinda
mhusika huyu mkubwa katika sakata zima la
RICHMOND.
Vijana wa
CHADEMA
tulitarajia kuwa, baada ya Bwana Lowassa kukiri mwenyewe
hadharani kuhusu
uzembe wake na matumizi mabaya ya madaraka Rais Kikwete
angelekeza hatua za
kuchukuliwa dhidi yake badala ya kuendelea kumpamba kama
"shujaa wa uwajibikaji',
kinyume na hayo tutaamini kwamba serikali yake inaendeshwa
kwa 'ubia wa
kulindana'.
Aidha
tunarudia kutoa rai kwamba Rais Kikwete kuwafukuza kazi
watumishi wote wa umma waandamizi ambao wametajwa na Bwana
Lowassa kushiriki
uzembe na matumizi mabaya ya madaraka; watumishi ambao
walitajwa pia na Kamati
Teule ya Bunge lakini mpaka sasa wanaendelea kutumikia
nafasi zao mbalimbali.
Kwa kuwa Waziri Mkuu Pinda ameshatangaza kwamba kwa wale
wateule wa Rais,
Kamati yake imeshapeleka suala zima kwake, tunategemea Rais
atachukua hatua za
haraka ili kuonyesha mfano kwa viongozi wengine wa chini
yake wanaotarajiwa
kuchukua hatua kwa watumishi wa chini.
Kadhalika tunapenda kuvikumbusha tena vyombo vya dola
kwamba
Sheria ya Udhibiti wa Makosa ya Kuhujumu Uchumi ya mwaka
1984 inatamka makosa
yafuatayo kuwa baadhi ya makosa ya kuhujumu uchumi ni pamoja
na yale yote yenye
kusababisha hasara kwa mamlaka ya Serikali. Pia Sheria ya
Kuzuia na Kupambana
na Rushwa Na. 11 ya mwaka 2007 inatamka kuwa ubadhirifu
na/au ufujaji wa mali
ya umma unaofanywa na watumishi wa umma na Matumizi mabaya
ya madaraka kwa
ajili ya manufaa binafsi, ni sehemu ya
ufisadi.
Bwana
Lowassa alithibitisha
kwamba maneno yake kwamba wapo viongozi waandamizi wa
Serikali ambao amewataja
kwa majina wamefanya maamuzi ya kifisadi, kitendo chake cha
kunyamazia ufisadi
huo- kinafanya iwe vigumu kwa yeye kutenganishwa na tuhuma
za ufisadi zilizomo
katika mchakato mzima wa kupewa tenda kwa kampuni ya
Richmond na mambo yote
yaliyotokea baada ya Mkataba huo kuhamishiwa kwa kampuni ya
Dowans.
Aidha tumefadhaishwa na Taarifa ya Waziri Mkuu Pindi
kwamba
kujiuzulu kwa Waziri Mkuu na Baadhi ya Mawaziri ilikuwa ni
ishara ya hatua
ambazo serikali imechukua kutekeleza maazimio ya Bunge
kuhusu suala husika.
Tunarudia kukumbusha kwamba toka sakata la Richmond
lilipoanza zaidi ya mwaka
mmoja uliopita tulimtaka Bwana Lowassa kujiuzulu kulinda
heshima yake lakini
alikaidi na kuitetea kampuni ya Richmond.
Uamuzi wa yeye kujiuzulu baada ya
kashfa yote kuwa hadharani, umesaidia tu kuilinda serikali
ya CCM lakini katu
hauwezi kumpatia heshima ya uwajibikaji na wala hakuwezi
kuwa ishara ya kwamba
Maazimio ya Bunge yameshatekelezwa.
Kwa niaba ya Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA), kwa
taarifa hii tunarudia kukemea jitihada zozote za kumlinda na
kumtangaza Lowassa
kuwa shujaa katika taifa letu kwani hali hii ikiachwa
kuendelea inatoa mfano
mbaya kwa vijana wa Tanzania. Tusingependa kwa namna yoyote
katika taifa letu,
mtuhumiwa wa ufisadi aliyetajwa pia katika orodha ya
mafisadi(list of shame)
kulindwa na kuenziwa kama shujaa wa Taifa letu kwani ni
kuharibu maana nzima ya
ushujaa katika uwajibikaji.
"Inasikitisha kwamba vijana wezi wadogo wadogo
wakijazana
magerezani. Vijana wamachinga kuendelea kukosa mitaji na
maeneo ya kufanyia
biashara; wanafunzi wa elimu ya juu wakipandishiwa ada na
wengine kukosa
mikopo- huku fedha za walipa kodi zikiendelea kuteketea kwa
ufisadi na
watuhumiwa wa ufisadi wakiendelea kutamba
hadharani.
Hali hii
ikiachwa,
itaharibu utawala wa sheria na kuleta matabaka katika taifa
letu. Vijana
tusingependa kuona nchi yetu inatumbukia kwenye migawanyiko
kwa sababu ya
kuwalinda watu wachache kwa kisingizio cha haki za
binadamu"
Imetolewa tarehe 31 Agosti 2008 safirini Kenya
na:
John Mnyika
Mkurugenzi wa Vijana
0754694553
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment