Monday, 3 August 2015

Re: [wanabidii] DK.MAKONGORO MAHANGA USITUZEVEZE

Happyness na wanaJamvi wote na watanzania kwa ujumla.
Ukiondoa ngazi ya Urais kwa kweli wagombea wa CCM wanatia kichefuchefu. nakubaliana na Katabazi kuwa uongozi wa juu wa CCM ufanye kweli katika kupitisha wagombea. la sivyo watanzania wafuatilie vyama vingine kama huko rushwa haitatumika basi tutapata viongozi huko. Hapana rushwa imetembea kama karanga zinavyotembezwa. Sijui kama nao watakuwa wahuni kutaka kupelekwa mahakamani.

Tuklimrudia Makongoro mahanga naye katia aibu ya mwaka. Yaani anajiona kama Afisa kilimo ambaye nalistahili kupandishwa cheo na kuwa waziri kamili kwa sababu tu ya kuwa naibu toka 2006. Tunasubiri kuupima uwezo wa kufikiri wa CHADEMA. Wampokee kwa mbwembwe tuzid kuwajua.. Niliandika kwenye facebook yangu kuwa CHADEMA inahitaji UNHCR kukabiliana na wakimbizi. nikasema wasipoangalia mazingira yake (Chadema) yataharibika kama ya Ngara na kigoma kwa wakimbizi wa 1994-2004. Wako wakuu wa Wilaya wanaoweza nao kudai kwa nini hawakupandishwa kuwa wakuu wa Mikoa. labda katika makubaliano ya wanamtandao aliahidiewa hivyo? Anajuaje kama Lowasa akipata atampa uwaziri? haoni kuwa mtandao umepanuka?

--------------------------------------------
On Mon, 8/3/15, 'Happiness Katabazi' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: [wanabidii] DK.MAKONGORO MAHANGA USITUZEVEZE
To: "WANABIDII" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Monday, August 3, 2015, 10:52 AM



DK.MAKONGORO
MAHANGA USITUZEVEZE
Na
Happiness Katabazi
AGOSTI
Mosi Mwaka huu ,Chama Cha Mapinduzi (CCM), kiliendesha kura
za maoni kwa wagombea wake kwa ngazi za Ubunge na Udiwani
kote nchini.
Kwa
tuliofutilia harakati za kupatikana kwa wagombea hao kwa
zaidi ya miezi mitatu sasa katika baadhi ya maeneo hapa
nchini tumelishuhudia matumizi ya fedha kwa baadhi ya
wapambe wa wagombea kuandaa mikutano ya wapiga kura wa CCM
katika Matawi,Kata ambao walikuwa na Kadi za CCM.
Wiki
iliyopita mimi mibanfsi nilikuwa nikishinda mitaani ,kwenye
vijiwe,kuzungumza  na baadhi ya wanaume na wanawake
ambao wengine ni wake za watu ambao ilipokuwa ikifika saa
nane mchana kutwa kiguu na njia kwenda kwenye vikao
vilivyokuwa vinaandaliwa na wapambe wa wagombea na wanawake
hao walikuwa wakienda haraka haraka kwenye vikao hivyo vya
kukutanishwa na baadhi ya wagombea kwasababu mwisho wa vikao
hivyo walikuwa wakihongwa Sh.5,000,10,0000 na
Sh.3,000.
Tumesikia
Madai ya tuhuma za Rushwa na uhuni wa kila aina Katika
mchakato huo wa kura za maoni ndani ya CCM.
Baada
ya baadhi ya wagombea walioshinda Katika kura za maoni
wametuhumiwa na wapambe wa kambi za wagombea wenzao Kuwa
wametumia Rushwa na figisufigisu.
Lakini
hata Hao walioshindwa Katika kura hizo za maoni ambao
wapambe wao wanalalamika Kuwa washindi walitumia Rushwa,nao
pia walitumia Rushwa Katika kampeni zao kwa kuwahonga baadhi
ya Wapiga kura,wajumbe wa nyumba Kumi ,mawakala wao na
baadhi ya viongozi wa CCM ili wamsaidie washinde ila tu
Fedha zao zimeliwa na ushindi hawajapata.
Naomba
vikao Vya juu Vya CCM chini ya Rais Jakaya Kikwete na Timu
yake vichunguze vizuri wale wote walioshinda kura za maoni
Kama walishinda kwa njia chafu basi wahenguliwe.
Maana
 siyo Siri uchafu na matumizi ya Rushwa Kabla na wakati
wa uchaguzi huo yalitawala katika baadhi ya majimbo na Kata
vitendo ambavyo vimethibitisha Kuwa ni Ngumu sana kupata
madaraka ndani ya CCM bila kumwaga Fedha na kufanya ghiriba
maana Takukuru nikama walikuwa mbingu nyingine.
Turejee
Katika mada Kuu ambayo ni Agosti Mosi Mwaka
huu,  aliyekuwa
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Segerea kwa vipindi viwili
mfululizo tangu mwaka 2000-2010 ambaye ni Naibu Waziri wa
Wizara ya Kazi na Ajira, Dk.Makongoro Mahanga kwa tiketi ya
CCM, alishindwa katika kura za maoni .
Agosti
2 Mwaka huu, yaani Jana Dk.Mahanga aliitisha mkutano wake na
waandishi wa Habari na kutoa shutuma kuwa uchaguzi
ulitawaliwa na Rushwa, hira, mizengwe na kwamba Kabla ya
uchaguzi huo kufanyika Juzi .
Mara
kwa Mara alikuwa akilalamika Kwenye Ofisi za CCM Wilaya ya
Ilala Kuwa kuna baadhi ya wagombea wenzake wa Ubunge
wanavunja Kanuni za chama lakini uongozi wa CCM Wilaya ya
Ilala ulimpuuza.
Na
kwasababu hiyo ametangaza rasmi kuhama CCM anakwenda zake
kujiunga na Chadema.
Kwa
mujibu wa Ibara ya 20 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ya Mwaka 1977, inatoa Haki ya Mtanzania yoyote
kujiunga na Chama chochote cha siasa.Hivyo Kwenda kwako
Chadema wala ujafuvunja Sheria za nchi.
Siyo
Siri baada ya kumsikia Dk.Makongoro Kwenye  Redio na
kumshuhudia Kwenye Televisheni akizungumza maneno hayo na
uamuzi huo, niliishia Kusema kweli 'Mungu wa siku hizi
ni kijana analipa hapa hapa Duniani'  na Kwamba
Muosha uwoshwa tena wakati wa kuoshwa ulipuliwa.
Leo
Dk.Mahanga  analalamika Rushwa  hira zimesababisha
ashindwe?.Lini we Makongoro na wewe na genge Lako mliacha
kucheza Michezo hiyo unayowatuhumu wenzio wamejifanya
 ? 
Mahanga
huyu huyu ninae mfahamu Mimi anadiriki Kusema hayo?Nimecheka
sana.Kweli Dk.Mahanga safari hii umempata Kiboko yako
mwanamke wa Shoka Bonna Kalua  ambae amekuangusha
Katika kura za maoni nafasi ya Ubunge.Kalua umetoa kamasi
Makongoro hadi ameamua CCM ,safi sana Kalua ,wanawake
tunaweza Kuwa wabunge majimboni sio siku zote Kuwa wabunge
wa viti Maalum.   
Minamuuliza
huyu Bwana Makongoro huo ujasiri wa kukemea figisufisu na
Rushwa Katika uchaguzi Katika Jimbo la  Segerea
ameupata wapi?
Ina
maana ujasiri huu wa kuona Rushwa ,figisufigisu Katika
uchaguzi CCM, Dk.Mahanga ameupata baada ya kubwagwa na
aliyekuwa mgombea mwenzake ambaye ni binti Mdogo
Juzi?
Kweli
Mtenda akitendewa uisi kaonewa na Yale yote aliyoyatenda uwa
yanamrudia alijiimbiaga Mwanamuziki Ally Choki.
We
Dk.Makongoro Mahanga kweli Leo hii unapata ujasiri wa kutoa
malalamiko hayo tena hadharani   Wewe Huyo?
Minimuulize
Mtani wangu Dk.Mahanga Ina maana wewe na genge Lako
lililokuwa likikupigia  kampeni hamkutoa hata Sh.100
kwa Wapiga kura ili kuwashawishi wakipigie  kura za
ndiyo?
Maana
wakati mwingine Nyie wanasiasa muwe mnamuogopa Mungu na muwe
wa kweli.  Sema Dk. Makongoro  Kama kweli hukutoa
hata senti Moja kwa baadhi ya Wapiga kura ili
wakuchague?
Minakufahamu
vizuri sana na wewe tangu Enzi zile nakuja kuandika Habari
za jimbo Lako na waandishi wenzangu ambao hivi  sasa ni
marehemu Jackline Mwingira(Nipashe), Agnes Yamo ( Tanzania
Damia) na Veronica Charles ( Majira).
Au
Katika uchaguzi wa kura za maoni Mwaka 2015 ulishampokea
Bwana Yesu ,umeokoka unampenda Yesu hivyo Figisufisu
'ghiriba' za uchaguzi wewe na kambi yako
hamkuzifanya Mwaka huu?
Lakini
Mtani wangu wakati wewe ukiwatuhumu waliokushinda na
mchakato huo Kuwa ulighubikwa na Rushwa, pia kuna Wapiga
kura wa jimbo la Segerea baadhi Yao na wanakutuhumu Kuwa
nawewe na kambi yako mlishiriki kucheza Michezo hiyo haramu
' Figisufisu' Katika uchaguzi huo uliomalizika
Juzi.
Ila
 tu uchaguzi 2010 , wana CCM Jimbo la Segerea
wamekuchoka waliamua kutafuna Fedha zako kwa makusudi na
Kisha  KUIBWAGA na kweli wamekubwagwa kama zigo hadi
umeonekana kukumbwa na kiwewe?
Watu
wamechoka za Fedha  zako sasa uende nazo uko Chadema,na
Chadema wameishafanya uchaguzi wa kura za maoni za Ubunge na
Udiwani, sasa sijui  utaweza kuvumilia Kuwa
Mwanachadema wakati Huna Cheo cha Ubunge wala
Udiwani?
Maana
siyo Siri kilichokuamisha CCM ni baada ya kushindwa Katika
kura za maoni ya Ubunge yaani ni kukosa madaraka ndani ya
CCM ndiko kulikosababisha uame CCM .
Sasa
ndiyo  Sultani wenu Mkuu mnayemfuata huko Chadema
ambaye aliamia Chadema kwa kishindo Jumanne iliyopita kwa
kile alichodai aliamua kuhama CCM baada ya jina lake
kuenguliwa Katika Hatua za awali za mchakato wa kumpata
mgombea Urais CCM.
Sasa
Kama Chanzo cha kuhama CCM ni baada ya wewe kushindwa kura
za maoni Jimbo la Segerea, umeamua kuhamia Chadema, sasa
kwakuwa wewe mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa
mmeonyesha Kuwa Shida  yenu Kuu ni Kupata madaraka tu
.
Ikitokea
Chadema wakakunyima madaraka siutaihama Chadema kwa Kigezo
Kuwa hawajakupa madaraka? 
Tamaa
na Kupenda madaraka itakuja kuwadhuru siku Moja.Yaani mjue
mnawashangaza sana watu wanaofikiri sawa
sawa. 
Dk.Mahanga
 ,waziri mzima umekaa Katika baraza la Mawaziri Katika
serikali ya awamu ya nne yote Kama Niabu Waziri eti
umeshindwa kura za maoni basi bila haya wala hujui vibaya
unasema Rushwa ilitawala Katika uchaguzi na kwamba unahama
 CCM. Unamdanganya nani na unamkomoa nani?
Mimi
nimekuwa nikikufuatilia nyendo zako muda mrefu kisiasa wewe
Makongoro ulikuwa Team Lowassa na siyo dhambi.Na ni mbunge
ambaye Wapiga Kuwa wa Jimbo la Segerea walikuwa
wameishakukinai na Ndio maana wamekubwaga.
Mpango
wenu wa kitoto wa kuhama CCM Kama aliyekuwa mgombea wenu wa
urais jina lake lisipopitishwa na CCM Kuwa mgombea urais,
ule hajulikani NA  watu wenye akili timamu .
Watu
wakawa  wanawatazama nakuwaacha mjazane Ujinga,
matumaini makubwa ya kupeana madaraka na mtekeketeze fedha
zenu sasa mgombea wenu alipokatwa jina na vikao Vya juu vya
CCM Dodoma ndiyo kambi yenu mkaanza kupata wazimu Msijue
pakukamata maana mkijiamini sana na Fedha nyingi mkateketeza
na mlilolitaka hamkulipata.
Sisi
wajuzi wa mambo ulipotangaza Jana unahama CCM ,tuliishia
kucheka na kukuonea huruma tu Manaa Miaka yote mlivyoenda
Timu Lowassa mlifikiri mmejificha Kwenye  Giza Kumbe
mlijificha Kwenye Mawingu mnaonekana,watu wana Wachora
wanajua wanawakona wapi.Na ndiyo basi Mtani wangu Ubunge na
unaibu waziri umeutema.
Waswahili
wanamsemo wao usemao " Aliyejamba atakunya tu".
 Siku zote ulijidai ni CCM Damu na upo na CCM Katika
Shida na raha lakini Juzi baada ya kushindwa Katika kura za
maoni ( Ndio wakati wa Shida), umeamua kuitosa CCM na kwenda
Chadema mchana kweupe .Balaa.
Licha
ni Haki yako ya Kikatiba kuamia Chama chochote
unachotaka. lla
Mimi Kama Mtani wako nakwambia hivi  uamuzi wako wa
kuamia Chadema hautakuwa  na faida kwako zaidi ya
Majuto muda Si mrefu,tusubiri Tuone na hili litatokea usije
kulia na Mtu.
Leo
Dk.Mahanga Unaiona Chadema ni nzuri na umeamua kujiunga nayo
wakati mi nakumbuka ni hawa hawa Chadema ndiyo walikuwa
wakikutukana matusi usiku kucha Katika mitandao na magazeti
Kuwa wewe ni "Fisadi wa Elimu" , umeghushi Vyeti
Vya elimu .
Na
kwamba Katika uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010 hukushinda,
ulimuibia kura aliyekuwa Mgombea Ubunge (Fredy
Mpendazoe)? 
Na
kila ulipopita walikuwa wanakuchafua hasa  na hadi siku
ile Mahakama Kuu Kitengo cha Biashara,Dar Es
Salaam,ulioposhinda Kesi ya kupinga Bunge wako iliyokuwa
imefunguliwa na Mpendazoe dhidi yako na wenzako?Kesi ya
kupinga Ubunge wako na zile Kesi zote za kudhalilishwa na
Kaineruba.
Lini
Chadema wamekusafisha wewe? Mtani wangu Mahanga sio kila
siku lazima uwe Mbunge ,Naibu waziri.
Siku
 nyingine Unatakiwa uwe Mwananchi wa kawaida na wewe
watu wakuongoze.Mahanga acha kutuzeveza.
Tamaa
ya madaraka itakuja kuwawaisha  Kuzimu maana unaweza
kujikuta unaanguka ghafla na kufariki kwa BP baada ya kupata
taarifa umeshindwa Katika uchaguzi uliokuwa
ukigombea.
Nakushauri
wewe na wenzio ambao ni wazi mna onyesha mnapenda sana
kupata madaraka nendeni katika makanisa ya Kiroho mkakemewe
hili hiyo roho ya Kupenda madaraka iwatoke. 
Maana
hiyo roho ya Kupenda madaraka  inawasumbua ,kuwatesa na
kuwadhalilisha sana .Na Kwa Mungu hakuna
linashindikana.
Mtani
wangu  Hupaswi Kulalamika Katika uchaguzi huu
ulioshindwa eti uligubikwa Na
figisufigisu, inakupasa ukae chini ujiulize ni kwanini hizo
figisufigisu unazodai zilikuwepo zikasababisha ushindwe ni
kwanini zimetokea na ni kwanini wewe kambi yako na mawakala
wako ,mamlaka husika mlishindwa  kuthibiti figisufigisu
hizo unazodai zilishamiri?
Uoni
figisufigisu hizo ni malipo  kwako kutokana na
figisufigisu  ulizotuhumiwa kumfanyia aliyekuwa mgombea
Ubunge (Chadema) Mwaka 2010 ? 
Watoto
wa mjini tunasema " Malipo ni Dunia akhera kuhesabiwa
usijigeuze nyani kucheka uliyoumbiwa".  Sasa basi
figisufigisu zilizokupaa Katika kura za maoni CCM Juzi ni
malipo ya figisufigisu zile.

Minawashauri
watu walionizidi umri,na viongozi wetu Nyie msipende
kuchukua maamuzi wakati mnahasira na machungu moyoni
 Kwani mwisho wa siku mtajikuta mnajutia maamuzi hayo
mliyoyachukua wakati mnahasira na uchungu moyoni.
Mtani
wangu Mahanga Nakutakia kila lakheri katika makazi mapya ya
siasa huko ulikosema anaenda kuamia Chadema, Mungu
akutangulie.Ila tabia ya kuama Chama na kutoa kashfa dhidi
ya CCM baada ya kushindwa kura za maoni uache haitokufikisha
Kokote Kwani hata huko uendako Kama kuna viongozi wenye
akili timamu na wenye busara wana Haki ya kukataa usijiunge
na Chama chao kwasababu kupitia maelezo yako ni wazi unaamia
Chadema siyo kwasababu unaipenda Chadema kutoka
moyoni.
Unahama
Chadema baada ya kushindwa Katika kura za maoni za Ubunge
CCM Juzi, na Jana ukatangaza unahama CCM unaenda
Chadema.
Hivi
nikikuuliza wewe Dk.Mahanga lini ulijipa muda ukaisoma
Katiba ya Chadema na Kanuni zake ukazielewa vyema na
zikakuvutia ndani ya saa 24 ukaamua kujiunga na
Chadema?
Chadema
muwe makini sana na hili Wimbo la makada wa CCM waliokosa
fursa za uongozi ndani ya CCM wanaamua kujiunga na
Chadema.
Kuweni
nao makini sana, Wengi wao wana uchu na tamaa ya madaraka na
viongozi wa aina hii mnavyozidi kuwakaribisha misiwakatazi
msiwakatibishe ila Mkae mkijua hipo siku
watawasumbua.
Mwenye
 Kilema abadili Mwendo. Lowassa,Dk.Mahanga tayari
wameisha jidhihirisha ni aina ya binadamu wanaopenda
madaraka kupita kiasi.Hivyo licha wamekuja Chadema
 Lowassa mmempa nafasi Adimu ya Kuwa mgombea urais
ambayo nafasi hiyo Ina malizika Oktoba 25 Mwaka huu
.
Fedha
na mali wanazo lakini wanachokisaka kwa kwa udi na uvumba ni
madaraka.Watu wenye akili timamu na tunaofikiri sawa sawa tu
nawaogopa sana sana.
Mimi
binafsi naamini Lowassa hawezi Kuwa rais kupitia Chadema.Huo
ndiyo ukweli mchungu nafahamu itawakera sana Chadema na
baadhi ya watu wa Kanda ya Kaskazini ambao huku mitaani hivi
sasa wanasema wanaeneza siasa za ukanda wa Kaskazini lakini
vumilieni.
Swali
Je, Cheo hicho cha ugombea urais wa Chadema ambacho anacho
Lowassa kwa sasa kikimalizika Oktoba 25 Mwaka
huu. 
Je
Mzee wangu Lowassa atavumulia kuishi Chadema bila kupewa
Cheo chochote kikubwa ? 
Kweli
nimeamini wanasiasa Wengi ni walafi wa madaraka,hawajui
kukosa ,wanajua kupata tu siku zote. CCM  Kwao uwa ni
nzuri  pale inapowapa madaraka    lakini CCM
 hiyo ugeuka Kuwa Mbaya Kwao pindi anapokosa madaraka
au Kama wanapoona kuna Dalili za kushindwa Katika uchaguzi
wa CCM.
Ndiyo
Lowassa na Mahanga,Ester Bulaya, James Lembeli  CCM ni
Mbaya kwasababu wamekosa madaraka ila Kipindi kile wana
madaraka ndani ya CCM  , walikuwa wakitamba majukwani
kuwa CCM ni Chama bora na Hakuna Kama CCM na hawatahama CCM
.
 
Mei Mwaka huu, Lowassa Katika mikutano yake na waandishi wa
Habari ambayo imerekodiwa  alijiapiza  kuwa Katu
 hawezi kuhama CCM hata kidogo. 
Miuwa
nawasikitikiaga sana watu wa aina hii na kuwaombea kwa Mungu
awatengeneze upya kiroho.
Itakumbukwa
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ,Julai 28 Mwaka huu,
wakati akihutubia umma Katika mkutano wa kumkabidhi rasmi
Kadi ya Chadema, Lowassa,pamoja na mambo mengine Mbowe
alinukuliwa akisema Kuwa alitumia Miezi mitatu kufanya
mawasiliano na Lowassa ya kumshawishi Lowassaa ajiunge na
Chadema.
Wenye
akili timamu tumeitafakari hiyo Kauli ya Mbowe Kuwa alitumia
Miezi mitatu kufanyamawasiliano na Lowassa ajiunge na
Chadema na kweli Chadema umefanyikiwa kumnasa mgombea
Lowassa.
Julai
10 Mwaka huu, CCM ndiyo ilichuja Majina ya wagombea urais
ikiwemo jina la Lowassa kwa kuyakata na kupata tano bora
ambapo Lowassa akufika tano Bora.
Ndani
ya Miezi hiyo mitatu aliyotueleza Mbowe, Lowassa alikuwa ni
miongoni mwa wagombea urais kwa CCM na ni wazi CCM ilikuwa
ikiwafuatilia nyendo za wagombea wake wote kwa
karibu.
Ikiwa
Hali ndiyo ilikuwa baina ya Lowassa aliyekuwa mgombea urais
CCM alikuwa na mawasiliano Mwenyekiti wa Chadema ,Mbowe ili
Lowassa aame CCM.Mnafikiri wanausalama wa CCM walikuwa
hawajabaini Njama hiyo chafu ya Lowassa ya kusaliti CCM kwa
Chadema?

Kama
CCM walibaini mawasiliano hayo ya Lowassa na Mbowe ya kuhama
CCM hatuoni nayo hiyo ni miongoni mwa Sababu uenda
zilizotumiwa na Kikao CCM kumuhuengua Lowassa mapema Katika
kinyang'anyiro cha ugombea urais CCM?
Minafananisha
hiyo  alilolisema Mbowe Kuwa alikuwa akimtongoza
Lowassa ili aamie Chadema, ni sawa Mke wa Mtu Aliyepo ndani
ya ndoa ila kwakuwa tu ni Malaya Akaamua Kuwa anasaliti ndoa
yake kwa bwana mwingine.Maana huwezi Kuwa Mke wa Mtu au mume
wa Mtu halafu ukaanza kutongozwa Mara kwa Mara  na
bwana mwingine ukakubari wakati ukijua una ndoa
yako,ukifanya hivyo ukae ukijua jina unalostahili kupachikwa
ni mwanamke au mwanaume Malaya. 
Maana
haiwezekani uwe mgombea urais CCM mwenye hadhi ya madaraka
aliyowahi kushika Lowassa ambaye hadi sasa analindwa na
walinzi waliokula kiapo cha kutii serikali iliyopo
madarakani na Amir Jeshi Mkuu ,halafu uwe unafanya mipango
ya kuhamia Chama cha upinzani halafu vyombo Vya Ulinzi na
Usalama visibaini Usaliti huu. 
 Vilibaini
Njama yake hiyo  mapema vikawa vinamtazama kwasababu
Tayari walikuwa wanajua wakati wanaoutaka wao   utafika
na watamtia adabu, na kweli adabu waliomshikisha  kwa
Kulikata jina lake mapema bila kuogopa Kuwa anaungwa mkono
na baadhi ya watu.
Chadema
Mnapaswa mjiulize Lowassa huyu ambaye ndiye mgombea wenu wa
urais wa sasa Enzi zile alipokuwa mgombea wa CCM aliweza
kurubuniwa na Mbowe ili aamie Chadema na kweli amerubunika
baada ya CCM kuchinja jina lake Kahamia Chadema, hamuoni
 huyu mgombea wenu wa urais Lowassa akitokea Mtu
mwingine amshawishi aihame Chadema anaweza kuhama?
Mungu
Ibariki Tanzania
0716 774494Blogg: www.katabazihappy.blogspot.comFacebook:
Happy Katabazi3/8/2015.






Sent from my iPad



--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment