Monday 15 October 2012

[wanabidii] ZANZIBAR NI KWETU - NI BLOG LA HATARI SANA! LA HATARI SANA!

Kaka bin Issa,
Natumai wewe ni mmoja kati ya administrators wa hili blog la ZANZIBAR NI KWETU 
linalosimamia maslahi ya Wazanzibari kwenye Cyber. Jambo moja ninataka kueleza, 
nalo ni kuwa: Nyinyi ni watu wa hatari sana, tena sana!
Hivyo mnapotangazia kuwa POMBE ni marufuku Zanzibar wakati sio kweli mnakusudia nini? 


Au ndio mnakusudia kutufukuza sisi kutoka Bara?
Fahamuni kwamba wengine tumeoa Visiwani na kutangaza pombe mmeipiga marufuku ni 
sawa na kutueleza kuwa tusije kuwatembelea wakwe zetu huko Visiwani.
SMZ au GNU ni yenu na mnaweza kupiga marufuku kitu chochote kile mkitakacho - 
kama vile ukahaba, sigara, etc, lakini kisiwe pombe. 
Mkitaka kuuvunja Muungano kwa haraka sana kabla hata ya kungojea Katiba Mpya basi pigeni 
marufuku pombe. Tupo tayari hata kutia sahihi MKATABA wowote ule na Maalim lakini pombe 
msiipige marufuku.
Tufikirieni ndugu zenu kwa huruma nyingi hasa baada ya miaka 48 ya kuwa pamoja.

Wako nduguyo,

//John Nkumbaruko.

0 comments:

Post a Comment