Tuesday 30 October 2012

Re: [wanabidii] UKWELI KUHUSU RIDHWANI KIKWETE KUKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA CHINA

Tony,
I agree with your candid analysis. Na Ile statement ya "don't bring me that Swahili boy"  is also true na 
ilikuwa part of his initial stand, alizidiwa kete na ujanja na mitandao yenye fedha na iliyo jmonopolize media. Jiandae, history repeats itself 

From LR

On 30 Okt 2012, at 8:13, "Tony PT" <tony_uk45@yahoo.co.uk> wrote:

Emma,

Mkapa alibadilika baada ya taarifa za usalama kumwambia ikiwa atalazimisha mtu mwingine kuchukua nchi atakigawa chama maana camp ya JK ilikuwa imetanda kuliko alivyotarajia! Alibadilika siku 6 kabla ya mkutano mkuu na sio kwa kupoteza mafaili! Ukumbuke kuwa usalama wa Taifa chini ya Apson haukumtaka JK, lakini hali ya kisiasa iliwalazimisha wakubali kushindwa.

Hakuna jingine na upo sahihi kabla ya hapo Che Mkapa alikuwa against JK na uwezekano wa kutamka maneno uliyoyasema ulikuwapo!
Sent wirelessly from my BlackBerry device on the Bell network.
Envoyé sans fil par mon terminal mobile BlackBerry sur le réseau de Bell.

From: Emmanuel Muganda <emuganda@gmail.com>
Date: Mon, 29 Oct 2012 14:57:12 -0400
Subject: Re: [wanabidii] UKWELI KUHUSU RIDHWANI KIKWETE KUKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA CHINA

Tony,
Hiyo habari nimeipata kutoka kwa watu wa karibu na Mkapa. Mpaka leo anasema kuwa alilazimika kula matapishi yake.
Hata katika mkutano wangu na Mkapa mara ya mwisho 2004 aliapa kuwa Kikwete atakuwa rais "over my dead body."
Siwezi kueneza uwongo au kusema kitu ambacho sina uhakika nacho. Fani yangu na nafsi vinanikataza.
em

2012/10/29 Tony PT <tony_uk45@yahoo.co.uk>
Emmanuel,

Usiongope hata kidogo JK au mwingine hakuna yeyote alitumia mafaili ya biashara za Che mkapa kumshinikiza ampitishe JK. JK alipitishwa na wapiga kura mkutano wa Nec na mkuu wa wa ccm! Acheni kudakia maneno ya mitaani licha ya kutumia jina la mtangazaji wa zamani wa VOA! Unapotosha mada tamu tunayoendelea kuisoma hapa!
Au wewe ndiye uliyachukua mafaili hayo! Kampuni za Mkapa zinajulikana Brela, ndio maana wapinzani wake baada ya kuacha madaraka walipekua Brela kwa kulipia na kupata taarifa zote.
Sent wirelessly from my BlackBerry device on the Bell network.
Envoyé sans fil par mon terminal mobile BlackBerry sur le réseau de Bell.

From: Emmanuel Muganda <emuganda@gmail.com>
Date: Mon, 29 Oct 2012 05:35:03 -0400
Subject: Re: [wanabidii] UKWELI KUHUSU RIDHWANI KIKWETE KUKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA CHINA

Abdallah,
Kabla ya kumhukumu Dr. Slaa nakushauri uangalie uwezekano kwamba hii story kama imetungwa, basi imetungwa na afisa mwandamizi katika idara ya usalama wa taifa. Hapo ndipo ninaona kuna tatizo. Ndio maana nimeuliza katika bandiko
langu la awali, watu wenye akili watujulishe, ilikuwaje wakati Ikulu inaungua, kilichochukuliwa ni mafaili kuhusu biashara za Mkapa ambayo yalikuja kutumiwa na Kikwete na Rostum kumshinikiza Mkapa ampitishe Kikwete mwaka 2005. The problem is bigger than shutuma zako kuhusu uwongo wa Mheshimiwa Slaa.
em

2012/10/29 Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
Hii Ndiyo Fact Check Sahihi na ya Wazi

WAHENGA waliamini kuwa tabia na hulka ya binadamu haibadiliki hata akiwa na umri mkubwa kiasi gani. Chukulia mfano wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Wilbroad Slaa.  Huyu kwa umri wake, kwa asili yake ya kupitia mifumo ya dini ya Kikristo madhehebu ya Kikatoliki, asingekuwa mtu wa kutunga, kusema na kuwaaminisha watu ukweli. Huyo ni mtu ambaye alikuwa padre, kiongozi mkubwa wa kiroho. Usingemtegemea kabisa kutunga na kuwaambia watu uongo. Kwa hakika, tabia yake hiiya kutunga na kusema uongo inazua maswali kuhusu mfumo mzima wa kulea watoto katika Seminari na kufundisha mapadre katika Kanisa hili.

Mtu kama Slaa – mzushi, mwongo, mnafiki asiyeheshimu watu anaweza vipi kufikia hatua ya kuwa padre; baya zaidi aliweza vipi kupanda ndani ya mfumo huo hadi kufikia kuwa Katibu wa Baraza la Maaskofu (TEC). Nasema haheshimu watu kwa sababu mtu anayetaka watu wamchangue awaongoze, hawezi tena kushiriki katika tabia ya kuwadanganya na kuwafanya wapumbavu. Lakini Bwana Salaa hili halimnyimi usingizi. Majuzi, Ijumaa, kule Sikonge, Tabora amezua na kutunga jipya. Amedai kuwa Julai 2, mwaka huu, 2012, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alisafiri kwenda Hong Kong kumwokoa mtoto wake wa kiume, Ridhiwani Kikwete ambaye anadaiwa kuwa alikuwa amekamatwa na mihadarati siku moja kabla, yaani Julai Mosi.

Huu ni uongo wa dhahiri kwa sababu ratiba ya Mhe. Rais Kikwete katika siku hizo anazozitaja Slaa iko wazi.

Julai Mosi, akitumia Ndege ya Rais, alisafiri kwenda Rwanda ambako alihudhuria Sherehe za Miaka 50 ya nchi hiyo na akalala mjini Kigali. Julai 2 alisafiri kwenda Bujumbura kuhudhuria Sherehe za Miaka 50 ya Burundi.  Alirejea Dar es Salaam Julai 3 na Julai 4 alikutana na ujumbe wa Kampuni ya IBM na Mjumbe Maalum kutoka Zimbabwe. Julai 5, alikwenda Dodoma ambako aliendesha Kikao cha Baraza la Mawaziri na kurejea Dar es Salaam siku hiyo hiyo. Sasa alikwenda Hong Kong lini? Ama alikuwa Burundi na Hong Kong siku hiyo hiyo? Slaa anadai pia kuwa alipowasili Hong Kong, Mheshimiwa Rais Kikwete alipokelewa na Balozi wa Tanzania nchini China, Mheshimiwa Philip Marmo ambaye alimpeleka kwenye mkutano na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Mheshimiwa Hu Jintao. Huu ni uongo mwingine wa dhahiri na ambayo sijui unamsaidia nini Slaa. Slaa anasema uongo kuhusu Balozi Marmo kwa sababu ratiba ya Mheshimiwa Marmo kwa siku sita za mwezi Julai nayo iko wazi na siyo kificho.

Kwanza, Ubalozi wa Tanzania katika China hauko Hong Kong bali uko mjini Beijing na Mheshimiwa Marmo hajawahi hata kufika Hong Kong. Taarifa kutoka Hong Kong amekuwa anazipata kutoka kwa Balozi Mdogo wa heshima wa Tanzania Mheshimiwa Clement Chan. Hata juzi, Ijumaa, Oktoba 26, Balozi Marmo alikutana na Bwana Clement Chan. Balozi Marmo anapanga kutembelea Hong Kong kwa mara ya kwanza mwishoni mwa mwezi ujao, Novemba, 2012. Angalia ratiba ya Mheshimiwa Marmo katika wiki ya kwanza ya mwezi Julai mwaka huu:

Julai Mosi, Balozi Mamro alikuwa ofisini Beijing. Julai 2, Balozi alihudhuria Sherehe za Siku ya Mongolia mchana na usiku alihudhuria Sherehe za Siku ya Djibouti kwenye Hoteli ya Lengedane mjini Beijing. Siku nzima ya Julai 3 alishiriki katika warsha ya Kampuni ya China Chemicals Techonologies Group ambayo inataka  kufungua viwanda cha madawa na mbolea nchini Tanzania. Asubuhi ya Julai 4, Balozi Marmo alikutana na ujumbe wa Kampuni ya Sichaun Honda Group inayowekeza katika miradi ya Mchuchuma na Liganga na jioni ya siku hiyo alikutana na ujumbe wa Kampuni ya Mawasiliano ya ZTE. Julai 5, Balozi  alihudhuria Sherehe za Siku ya Venezuala Day na Julai 6 alijiunga na Mabalozi wa Nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki katika mkutano wa Forum on Trade na Cooperation na jioni alihudhuria Sherehe za Rwanda Day. Sasa, Balozi Marmo alikwenda lini Hong Kong kumpokea Mheshimiwa Rais kama siyo uongo?

Katika siku zinazotajwa, Bwana Ridhiwan alikuwa Dar es salaam muda wote.  Kwa hakika, Ridhiwan hajapata kufika Hong Kong ama China katika maisha yake yote. Nchi pekee inayokaribia China ambayo amewahi kuitembelea ni Dubai kwa sababu hata India hajapata kufika. Ratiba hizi za Mhe. Rais na Mheshimiwa Marmo na ukweli kuwa Ridhiwan hajapata hata kufika China ama Hong Kong ni ushahidi usiopingika kuwa Mzee Slaa kwa mara nyingine ametunga, yeye amekuwa bingwa wa goofing. Huyu ni mtu anayezeeka vibaya. Tunaamini kuwa ameanza kuchanganyikiwa pengine kwa kuzidiwa na jukumu ya kulea mtoto-mjukuu na kumtunza mchumba Bi Josephine ambaye wanaishi kama vimanda kwa sababu huyo mama bado anayo ndoa halali. Pole sana Mzee Slaa kama Josephine na mwanae amekushinda mrudishie mwenye mali yake.

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
0 comments:

Post a Comment