Monday 29 October 2012

Re: [wanabidii] UJINGA WA OIC NA MAHAKAMA YA KADHI

HK hilo nalo neno, mimi nikionaga Hilda Kiwasila na urefu wa maneno, kusema kweli huwa napita au na-delete! Too long!! LKK
 
From: "hkigwangalla@gmail.com" <hkigwangalla@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Monday, October 29, 2012 5:51 PM
Subject: Re: [wanabidii] UJINGA WA OIC NA MAHAKAMA YA KADHI

Dada Hilda,

Huwa una michango mizuri sana sema mirefu kupita maelezo matokeo yake mimi huwa siwezi kusoma mpaka mwisho, jaribu ku-summarize basi ili tuwe tunasoma bila kupotelea humo kwenye mchango wako! Usidhani nimo katika lile kundi la waTZ wavivu wa kusoma, la hasha ukweli ni kwamba mjadala unapendeza kama kila mtu akichangia senti mbili zake humo kuliko tajiri mmoja akatupia mamilioni yeye peke yake!
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania

From: Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Mon, 29 Oct 2012 09:17:32 +0000 (GMT)
To: <wanabidii@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] UJINGA WA OIC NA MAHAKAMA YA KADHI

Lakini wakristu wana umoja wao hapa nchini (CCT) na finances zinatoka kwao makanisa na donors wao; Wengine ni wanachama wa Lutheran World Federation (LWF) ya dini yao hiyo ya Kilutheri ambayo huwapa Grants za miradi kama hiyo OIC inavyotakiwa iwe na ifanye. Sio Nchi ya TZ iliyojiunga na LWF!!
 
Waislamu wana-Bakwata. Wakristu wana mahakama zao wanazogharimia wenyewe-kamati za ushauri za makanisa (wazee wasikilizao kesi za waumini wao), ikishindikana katika kamati ya kanisa hilo itakwenda Jimboni kwa Askofu, Kardinari-Roma kwa Baba Mtakatifu. Hakuna hela ya serikali hapo wala ya mtoa kodi wa dini si yake. Na Padri akikosea- inaamuliwa kikao cha kanisa, jimbo, baraza la maaskofu etc-anakwenda kula kifungo Roma kwa gharama za Kanisa ikiamuliwa au anafukuzwa. Hivyo, haina haja ya kuiingiza nchi zima kuiingiza katika vyama vya dini kama utawala si wa dini moja na kuna madhehebu kibao. Wala haitokuwa haki nchi imlipie Kadhi kwa hela za walipa kodi na ilipe mishahara ya wafanyakazi wa madhehebu hayo maana kila dhehebu-Katoliki, Aglican, Lutheran, Sabato, Hindu, Bohora, Ismailia whatever wana mahakama zao mahekaluni mwao kwa michango yao ktk mahekalu hao. Jee Hindu etc wadai nao mahakama ilipiwe na GVT, aina zote za makanisa zinai, Bohora nao na wasio na dini wadai za mila zao-tutafika. Vurugu hii ya nini. Mbona kitu kipo wazi ila hakieleweki. Panatafutiwa pa kuanzishia vita isiyokwisha tu. Hata zikianzishwa za Kadhi, bado watakimbilia mahakama ya GVT ili kupata haki hasa akina mama kama wafanyavyo wa dini ya kikristo. wajiunge kama Bakwata lakini sio nchi na ndio wakristo humpokea Papa, Wengine Aga Khan, wengine Dharai Lama, kiongozi wa Kibohora na akija TZ anakuwa mgeni wao na wa Taifa anaonwa na viongozi wa nchi. Licha ya wakristo kuwa na miradi ya maendeleo na kuonekana wanapendelewa lakini ni kwa hela zao binafsi za kuchanga kanisani, wenzetu wahindi-hutoa michango mikubwa ya maendeleo nchini kupitia dhehebu lao. hawa hawachomewi mahekalu yao pamoja kuwa ndio matajiri wakubwa na mkoloni aliwapendelea.
 
Kuwe na mjadala wa wazi basi wa mashirika ya dini kuwaelimisha au kuelimishana jinsi wanavyopata hela na misaada na kuendeleza miradi yao ya dini yao, wanavyojiunga na mashirika ya dini zao duniani ili ndugu zetu waislam wajue kuwa hawaonewi kwa hili.

--- On Mon, 29/10/12, Ellay Mnyamoga <mnyamoga@live.com> wrote:

From: Ellay Mnyamoga <mnyamoga@live.com>
Subject: Re: [wanabidii] UJINGA WA OIC NA MAHAKAMA YA KADHI
To: "wanabidii@googlegroups.com " <wanabidii@googlegroups.com>, "matinyi@hotmail.com " <matinyi@hotmail.com>
Date: Monday, 29 October, 2012, 6:25

Sasa my bro kama oic hakuna misaada kwanini tung'ang'anie ni sawa na kung'ang'ania kuunge tusilolijua,kama marejeo yako yanaonesha kuwa hakuna faida,lets shit! Oic ni jumuia ya kiislam na misimamo,itikadi ni za kiislam nakini katika hali ya upeo vikundi vingi vya kiislam vinatuhumiwa kuwa na fujo mara kwa mara,mfano alshabab,boko haram,uamsho hivo si hekima kuruhusu tena organisation kama hivo,na mi ninachoamini tanzania haijafikia hatua ya kuwatesa waislam hadi watake kuwa na vikundi maalum vya kudai haki zao kwa mabavu sana,hatupendi kuzozana sana jamani! Na kama watu wanahoja binafsi basi watumie njia ya busara na katiba ya jamhuri ipo.

-----Original Message-----
From: Mobhare Matinyi
Sent: 10/29/2012 5:37:32 AM
To: Wanabidii googlegroups
Subject: RE: [wanabidii] UJINGA WA OIC NA MAHAKAMA YA KADHI
Jamani Watanzania wenzangu,
 
Tusiite wazo la wenzetu ujinga.
 
Watanzania tumejijengea tabia ya kwua ombaomba na hoja ya OIC ilianzia Zanzibar kwa madai kwamba kuna misaada ingawa hakuna aliyekwishachambua hiyo misaada kama kweli ina uzito wowote. Ninachojua mimi ni kwamba siku moja OIC ilifanya mkutano wake mwaka 2008 nchini Senegal na ukazua kashfa ya wizi wa hela na Senegal iliumia sana kwenye kuandaa mkutano. Nchi wanachama ni nyingi mno na karibu zote ni maskini na zinayategemea mataifa yaliyomo kwenye The Arab League ambayo nayo ina maslahi yake. Mbaya zaidi matajiri wa OIC ndio hao hao wanaoibeba hiyo ya Waarabu lakini mbaya mbaya mbaya zaidi ni kwamba matajiri wa hiyo ya Waarabu wana maslahi mengine kwenye Umoja wa Ghuba ambako kuna maskini wa kusaidia pia tena kwa mabilioni.
 
Sielewi hiyo misaada itatoka wapi? Hivi, Msumbiji inaweza kutuonesha faida iliyokwishapata? Uganda je? Kodivaa je? Kameruni je? Ukweli ni kwamba OIC hakuna misaada kama wengi wanavyodhani; misaada imo kwenye akili zetu na nguvu zetu. Mungu alishatupa, hii tabia ya kuombaomba tuache kabisa!
 
Lakini zaidi ya hapo, kama OIC ina sifa zisizokuwa na mgogoro, tuingie kila mtu afurahi. Kwa nini tusipekue kwanza?
 
Matinyi.
 
Date: Sun, 28 Oct 2012 22:15:07 -0700
From: jrtuvana@yahoo.com
Subject: [wanabidii] UJINGA WA OIC NA MAHAKAMA YA KADHI
To: wanabidii@googlegroups.com

UJINGA MTUPU KAMA KUNA MTU ANATAKA KUJIUNGA NA OIC AANZE KUUNGA MKONO HOJA YA URAIA WA NCHI MBILI TANZANIA, ILI IKIPITA HIYO NA KUWA SHERIA WAKAHAMIE NCHI YOYOTE DUNIANI ILIYO MWANACHAMA WA OIC WAKAKAE HUKO, KWENYE NCHI YOYOTE  YENYE UANACHAMA WA OIC, SIO KULAZIMISHA NCHI NZIMA YA TANZANIA KUWA MWANACHAMA WA OIC AU KUNDI FLANI KUTAKA TANZANIA NZIMA KUWA WANACHAMA WA OIC? NA OIC NI NINI? 

HIVI UNATEGEMEA NCHI MOJA MIRENGO MIWILI YA SHERIA INAWEZEKANA WAPI? NIKUTOKUWA NA FIKIRA NDIO KUNA LETA YOTE HAYO
.
IKIANZA MAHAKAMA YA KADHI, BASI PIA MAHAKAMA YA KIRUMI IWEPO, sbb taratibu za usimamizi wa sheria wa tanzania utakuwa hauna maana tena.

A SPADE CALL IT BY ITS NAME, NOT A BIG SPOON

From: Ellay Mnyamoga <mnyamoga@live.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com " <wanabidii@googlegroups.com>; "ngupula@yahoo.co.uk " <ngupula@yahoo.co.uk>
Sent: Sunday, October 28, 2012 4:49 PM
Subject: Re: [wanabidii] TAMKO LA WAISLAMU : KUHUSU KUJIUNGA NA OIC NA KUREJESHWA KWA MAHAKAMA ZA KADHI

Tusijadili ujinga wa oic
----------
Sent from my Nokia phone

-----Original Message-----
From: Godfrey Ngupula
Sent: 10/28/2012 3:46:25 PM
To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] TAMKO LA WAISLAMU : KUHUSU KUJIUNGA NA OIC NA KUREJESHWA KWA MAHAKAMA ZA KADHI

kiukweli ni kuwa Tanzania haiwez ikajiunga na OIC shirika ambalo haliamini uwepo wa taifa jingine ktk ramani ya dunia.Kujiunga na shirika au chama fulani ni lazima uamini shirika au chama hicho inachoamini.Na kama ni lazima Tanzania kufanya hivyo basi OIC iondoe kipengele cha kulaani na kutolitambua taifa la Israeli.Hakuna mkristo yeyote anayetambua uhalali wa kuwepo taifa la israeli kisha akaafiki Tz kujiunga na shirika la OIC,ni labda awe mkristo jina kama Membe ambaye yupoyupo tu ari mradi mkono unaenda kinywani.
pili,wakristo hawaping hata kidogo uanzishwaji wa mahakama za kadhi nchini.Wanachopinga ni kuingiza vipengere suppotive kwenye katiba yetu which in fact vitaifanya katiba yetu neutral kuwa sensitive.Jambo hili wakristo hawatalikubali hata kidogo. Ni kwa nini wakristo wanapinga mambo hayo mawili kuwemo ndani ya katiba?jawabu rahisi kupita yote ni kwa sababu jamii ya kiislam kihistoria na kimatendo imejihidhirisha kuwa sio jamii ya watu waliostaarabika.All the time handle them with care.Huu ndio ukweli,and that is cost waislam have to bare.Nina imani kwa 100% wakristo wako tayari ubaloz wa vatican uondolewa Tz kuliko nchi kujiunga na Oic au mahakama za kadhi kuanzishwa tz chini ya mfumo wa serikali. wakristo wanaamini kuwa upotevu mwelekeo wa nchi kama n4eria,ivorycost,benin ni laana ya kimaandiko kwa sababu ya kutokuwa na tahadhali ktk kufanya maamuzi.Hivyo,hiyo mifano ya nch zenye wakristo weng zilizojiunga na oic in fact stand as the negative
 example,the side effect of the decision towards...

Godfrey Ngupula
------------------------------
On Sun, Oct 28, 2012 4:58 PM EET Ellay Mnyamoga wrote:

>Acha kuandika ujinga usio na maana kwani wewe ukiishi katika uislam mi inanisaidia nini? Umeambiwa hizi ni mahakama za kikristo?
>
>
>-----Original Message-----
>From: Abdalah Hamis
>Sent: 10/28/2012 2:01:10 PM
>To: wanabidii@googlegroups.com
>Subject: [wanabidii] TAMKO LA WAISLAMU : KUHUSU KUJIUNGA NA OIC NA KUREJESHWA KWA MAHAKAMA ZA KADHI
>BARAZA KUU LA JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAMU TANZANIA
>
>TAMKO LA WAISLAMU TANZANIA
>
>KUHUSU KADHIA YA TANZANIA KUJIUNGA NA OIC NA KUREJESHWA KWA MAHAKAMA ZA KADHI
>
>BARAZA KUU LA JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAMU TANZANIA
>
>I. UTANGULIZI
>
>Tanzania inapita katika kipindi cha mivutano mikubwa kati ya Waislamu kwa upande mmoja, na serikali na Wakiristo kwa upande mwingine.
>
>Tafauti hizo ni juu ya uhalalali wa urejeshwaji wa Taasisi ya Waislamu ya Mahakama za Kadhi na mchakato wa Tanzania kujiunga na Jumuiya ya misaada ya Waislamu duniani Organization of the Islamic Conference OIC.
>Historia inaonesha kuwa kufutwa kwa Mahakama ya Kadhi mwaka 1963 kunatokana na maamuzi ya Bunge kupitia The Magistrates Courts Act, 1963.
>
>Suala jingine ni uhalali na ubora kwa Jamuhuri ya muungano wa Tanganyika na Zanzibari (Tanzania) kujiunga na Shirika la misaada la Waislamu duniani OIC.
>
>Kutokana na madai ya muda mrefu ya Waislamu ya kutaka kurejeshwa Mahakama ya Kadhi nchini, Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania lilitoa jukumu kwa Kamati ya Katiba na Sheria kushughulikia suala hilo chini ya uongozi wa Muheshimiwa Arcado Ntagazwa mwaka 1994. Mwaka 2004 kamati iliendelea na jukumu hilo chini ya uongozi wa Muheshimiwa Athumani Janguo.
>
>Suala hili pia lilijitokeza katika Ilani ya Chama tawala CCM kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2005.
>
>Kamati hiyo chini ya uongozi wa awamu zote mbili ilikutana na Jumuiya za Kiislamu kwa uelewa halisi wa suala husika na vilevile wadau wengine kwa faida za kiutendaji.
>
>Taarifa tulizonazo ni kwamba waraka wa kamati hiyo uliwasilishwa kwa Spika wa Bunge (wa wakati huo) Mh. Pius Msekwa.
>
>Novemba 11, 2007 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia katika hafla ya 'kusimikwa' Askofu mkuu wa Kanisa la KKKT Alex Malasusa aliwataarifu watanzania kuwa mapitio ya vyombo husika juu suala la Mahakama ya
>Kadhi yamekamilika, akaongeza kuwa wananchi watapatiwa jawabu ya suala hili Februari mwakani, yaani 2008.
>
>Tokea mchakato wa suala hili uanze, na mpaka Rais Kikwete alipotoa tarehe ya kutoa jawabu katika hafla iliyotajwa hapo juu, ni zaidi ya miaka 13 sasa.  Aidha, suala la OIC nalo limepewa urasimu wa aina yake.
>
>Mwaka 1993 Zanzibar ambayo ni moja ya nchi zilizounda serikali ya muungano inayoitwa Tanzania, iliamua kujiunga na OIC kama Zanzibar.  Tanzania bara ilipinga kwa hoja kuwa ni vema ufanyike utafiti wa kina ili maamuzi ya kujiunga au kutojiunga yawe ya pamoja.
>
>Baada ya utafiti wa miaka 15 serikali ya Tanzania kupitia Waziri wake wa mambo ya nje imetamka hadharani kuridhika kwake na sababu zote za kujiunga OIC zikiwemo za kisheria na kiusalama.
>
>Nchi ambazo kwa muda mrefu raia wake wamekuwa wakifaidika kwa misaada ya OIC ni pamoja na Benin, Cameroon, Cote d'Ivoire,  Gabon, Guinea, Guinea Bissau, Msumbiji, Nigeria, Sierra leone, Uganda, Urusi. Nchi hizi ni sehemu ya nchi 57 wanachama wa OIC zikiwemo zenye idadi kubwa ya raia Wakiristo.
>
>Tarehe 24 Oktoba 2008 Maaskofu Tanzania walitoa tamko kali kupinga Mahakama ya Kadhi na OIC. Wameionya serikali kuwa endapo itaridhia kurejeshwa kwa Mahakama ya Kadhi na nchi kujiunga na OIC, mahusiano kati ya Wakristo na Waislamu yatavunjika na uwezekano mkubwa wa kutokea umwagikaji wa damu.
>
>Katika masuala haya, Waislamu wameendelea kusimama kwenye rejea za Sheria, Sharia, Mantiki na Historia. Wakristo wameendelea kusimama katika wasiwasi wa kuwepo kwa itikadi yao na madai ya 'uvunjwaji wa katiba' ya nchi. Serikali inaendelea kusuasua katika ahadi za muda mrefu na sura isiyoeleweka.
>
>Waraka huu ambao unakamilika kwa Tamko la Waislamu, unapitia hoja zote tegemezi kwa Wakiristo, Waislamu na mtazamo wa sheria za nchi ili kuitanabahisha serikali itekeleze ahadi zote kama ilivyoahidi, kwa maslahi ya wananchi wote.
>
>II. HOJA ZA MAASKOFU
>
>1. Udini
>
>
>Miongoni mwa hoja za Maaskofu ni kuwa suala la Kadhi kutambuliwa na katiba ya nchi ni kuleta udini miongoni mwa watanzania. Rejea gazeti la Msema Kweli, na. 578 Jumapili, Septemba 28-Oktoba, 2008, uk. 5.
>
>'Akitoa tamko hilo Jijini Dar es Salaam, kwa niaba ya Maaskofu wa Kipentekoste nchini, Mwenyekiti wa PCT mkoani hapa Askofu David Mwasota alisema katika awamu nne za uongozi wa nchi, kumekuwapo na juhudi za makusudi kwa baadhi ya viongozi wa serikali, Wabunge na Viongozi wa Dini ya Kiislamu kujaribu kushinikiza udini.'
>
>'Aliutaja udini huo kuwa ni kutaka kuiingiza Mahakama ya Kadhi ndani ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano na pia Tanzania kujiunga na OIC.'
>
>2. Ukiukwaji wa Katiba
>
>Ukiukwaji wa katiba ni moja ya madai ya Maaskofu katika kupinga kurejeshwa kwa Mahakama ya Kadhi na Tanzania kujiunga na OIC. Rejea gazeti la Jibu la Maisha, na.37, Jumapili, Septemba 28 Oktoba 4, 2008, uk. 2.
>
>'Na wala hatutaki kabisa kuona kinaingizwa kipengele cha kuwa na Mahakama ya Kadhi ndani ya Katiba, maana kwa kufanya hivyo ni kukiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 toleo la Novemba 1, 2000, Sehemu ya Pili Ibara ya 9 kifungu 'a' na Ibara ya 20 (2) a. Kukiuka vifungu hivyo, kutasababisha uvunjifu wa amani na kubomoa mihimili mikuu ya utulivu iliyosimamishwa ndani ya nchi yetu.'
>
>3. Uvunjifu wa Amani
>
>Maaskofu pia wametowa hoja ya uvunjifu wa amani, rejea gazeti la Utatu, Na 044, Jumapili, Septemba 28 - Okotoba 4, 2008 uk. 5.
>
>'Kwa kuwa Katiba ya nchi yetu hairuhusu serikali ya kidini hatujui linalotafutwa ni nini hasa na serikali kuendelea kuachilia jambo kurudia rudia bungeni, inaashiria nini, hata kama jambo limekubaliwa na chama tawala katika ilani yake, lakini suala hili si la kichama, bali ni la kitaifa na halina maslahi kitaifa maana lina malengo ya kuwagawa Watanzania kidini, hivyo kuchafua amani tunayojivunia muda mrefu.'
>
>4. Kunajisi Katiba
>
>Maaskofu pia wamefika mbali zaidi kwa kutowa hoja kuwa kuingizwa OIC na Mahakama ya Kadhi ni kunajisi katiba ya nchi. Rejea gazeti la Utatu - Na 044, Jumapili, Septemba 28 - Oktoba 4, 2008, uk. 5.
>
>'Akionyesha wazi msimamo usioyumba wa baraza hilo, Mwenyekiti wa PCT, Dar es Salaam, Askofu David Mwasota aliwaambia waandishi wa habari kuwa uvumilivu wa Wakristo umefikia mwisho na sasa wanasema hapana, hawataki Katiba ya nchi itiwe unajisi na sheria za dini.'
>
>Aidha, kwenye Tahariri ya gazeti hilo Uk. 4. imeeleza kama ifuatavyo.
>
>'Tusikubali kutia unajisi katiba ya nchi, iachwe ikibaki kama katiba na dini zetu zibaki kama zilivyo, kwani kucheza na eneo hilo ni kuchezea aliyeumba mbingu na nchi ambaye ana mamlaka juu ya yeyote na chochote.'
>
>5. Kujitafutia laana ya Biblia, Tanzania
>
>Imeelezwa kuwa 'Yabainika Tanzania kujiunga na OIC ni kujitafutia laana ya biblia.' Rejea gazeti la Msema Kweli Na. 579 Jumapili, Oktoba 5-11, 2008, Ukurasa wa mbele na Uk. 5,
>
>'Imebainika kuwa malengo ya Shirika la Umoja wa Kiislamu (OIC) yatailetea laana kubwa Tanzania iwapo itajiunga nalo, kutokana na moja ya malengo yake kupinga uwepo wa taifa la Kiyahudi la Israeli katika eneo la Mashariki ya Kati, huku tayari Biblia Tukufu ikiwa imetahadharisha kuwa yeyote atakayekwenda kinyume na taifa hilo atakuwa amejipatia laana.'
>
>'Ukweli wa laana ambayo Tanzania itajipatia ikiwa itajiunga na OIC inaelezwa vyema katika Biblia kwenye Kitabu cha Mwanzo 12:3 ambapo baada ya Mungu kumwahidi baraka kuu Nabii Abrahamu ambaye ni chimbuko la taifa la Israeli, alisisitiza ahadi zake kwa kuweka Agano kwamba atawabariki wote watakaombariki na kuwalaani wote watakaomlaani.'
>
>6. Kuisilimisha nchi
>
>Rejea gazeti la Msema Kweli - Na. 578, Jumapili, Septemba 28 Oktoba 4, 2008, Ukurasa wa mbele na Uk 5, chini ya kichwa cha habari:
>
>'Katiba ya OIC kuibadilisha Tanzania kuwa dola ya kiislamu.'
>
>'Juhudi zinazoendelea hivi sasa za kutaka Tanzania ijiunge na Shirika la Umoja wa Kiislamu maarufu kama Organization of the Islamic Conference (OIC), hu

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment