Tuesday 16 October 2012

Re: [wanabidii] Mhe PETER KAFUMU ANAOMBA RADHI AU .........?


-----Original Message-----
From: Peter
Sent: 10/16/2012 1:56:33 PM
To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Mhe PETER KAFUMU ANAOMBA RADHI AU .........?
Bert

Huna chama lakini ni mwenezi wa cdm hongera sana. Tunataka mabadiliko ya amani, cdm wakiingia madarakani kwa amani ndiyo hamu yetu. Lakini kwa siasa za kujenga chuki na matusi kwa kila mmoja aliyeko ccm, nchi itaingia kwenye vurugu.. Ni matumaini yangu tutajifunza siasa za amani bila matusi na kiusingiziana. Matusi, masingizio, na chuki hivyo ndivyo ninavyovikataa sana. 

Sipendi kulumbana nawe unazo hoja nzuri na za msingi za kuchangia lakini unachangia kwa jazba na chuki... Mimi nitaendelea kupigana na uovu na ufisadi kwanza kuanza ndani ya maisha  mwenyewe hatimaye mfumo.. Na mfumo unaweza kubadilishwa toka ndani kwa kubadili mioyo. Moyo Adili ni Dawa ya Rushwa. Watendaji wa serikali na vyama lazima wabadilike waione rushwa kuwa na dhambi, unaweza kuwa na mfumo lakini kama watu wako hawama maadili hakuna unaloweza kufanya.

Yaliyotokea igunga si ccm tu walifanya mambo ya ovyo lakini cdm nao walifanya mambo ya hovyo, kumvua dc hijab, kumwagia tindikali wengine na mengine. Wote kabisa tunahitaji kuacha vitendo hivi ili siasa za vyama vingi zilete matunda yanayotakiwa, lakini kwa mtindo huu taifa liko hatariri kupigana na kusambaratika. Huwa nasema  na narudia tena hapa ndani ha cdm kuna waadilifu lakini pia wamo maisadi wengi, na ndani ya ccm kuna waadifu lakini pia wamo mafisadi, na kuwa cdm malaika na ccm mashetani ni makosa makubwa. Kenya na Zimbabwe ni mifano halisi ya ushindani wa vyama unatawaliwa na chuki, matusi na propaganda za uongo.

Ninavyoamini mimi, ni maadili ya watu toka kijijini hadi taifani yatakayolinusuru taifa na mapigano yenye chuki za kisiasa.  Wenye maadili wamebaki wachache, tunahitaji mtawala wa kiimla zaidi kuwafanya watanzania wafanye kazi badala ya kucheza pool wakisubiri cdm iwaletee fedha, mishahara mizuri, masilahi makubwa - sijui kutoka wapi. Kazi, uwerevu, uadilifu na kufanyakazi ndiyo misingi ya maendeleo. 

Nakupongeza kwa msimamo dhidi ya ccm. Kaza uzi, utafika.. Lakini siasa za chuki, matusi na masingizio hazina tija na zitaleta vita.  Yeyote anayeleta matusi, chuki, fitina, choyo, masingizio analiweka taifa la tanzania katika uwezekano wa kusambaratika na ni wa kuogopwa huyo. Yeyote nina maana kutoka kote ccm, cdm na wengine, tuache siasa za matusi, tujifunze siasa za amani ili tutunze amani na mabadiliko ya kweli ya kiutawala yatakuja na tutakuwa salama kama taifa.

Endelea kutoa maoni yako lakii kwa upole na hekima.

Mungu akubariki

DPK Ng'wizukulushilinde

On 16 Oct 2012, at 11:11, "Ellay Mnyamoga " <mnyamoga@live.com> wrote:

Ni kweli unaweza kujitetea kuwa wewe huna chama chochote ili uweze kujinasua katika andamo fulani linalokukabili lakini sisi tukichambua maono na wawazo yako tunabaini kuwa wewe unaitikadi fulani na kuna kitu fulani unakikosa jambo linalopekekea ufanye hivyo,haidhuru kwanini huna chama? Utajibu kwani ni kosa kutokuwa na chama? Hapana na kwanini sasa kama si mwanachama unakunwa sana na siasa za vyama huo ni mlango tosha uliofungua wananchi kama mimi waanze kukudahiri moja kwa moja ndugu yangu.

----------
Sent from my Nokia phone


-----Original Message-----
From: Bart Mkinga
Sent: 10/16/2012 7:55:28 AM
To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Mhe PETER KAFUMU ANAOMBA RADHI AU .........?
Dr. Kafumu,
 
Unaamini kuwa mimi natoa maoni kishabiki, wakati kiuhalisia, mimi si shabiki wa siasa za vyama. Faraja yangu kubwa ni pale siku moja nitakapoona kuna Tanzania yenye matumaini makubwa kwa vizazi vya sasa na baadaye. Usishangae siku ambapo CHADEMA wataingia madarakani, na mambo yakawa ovyo, utaniona nikiilaumu serikali na chama kilichopo madarakani kama nifanyavyo sasa. Mimi naunga mkono sana mawazo mapya, mfumo mpya wa uongozi, na mbinu mpya za usimamizi wa sheria, kanuni na rasilimali zetu. Nina imani kubwa kuwa serikali ya sasa na Chama tawala hawayatekelezi majukumu yao kwa matarajio na matakwa ya Watanzania walio wengi, na wala hakuna dalili ya kupatikana mabadiliko makubwa ambayo wananchi wanayataka kwa kupitia CCM.
 
Lililo baya zaidi na la kukatisha tamaa, serikali yetu na CCM wamekuwa wakijisifia kuwa wanafanya vizuri sana. Hapo ndipo penye tatizo kubwa la msingi. CCM na serikali wanaamini mambo yanakwenda vizuri sana, hawa hawawezi kufanya mabadiliko makubwa. Siku zote ukitaka kufanikiwa na kufanya mabadiliko makubwa ni lazima kwanza ujichunguze, ukiri mapungufu, ndipo uweke malengo na mikakati mipya ya kutoka mahali ulipo. Na hii ndiyo sababu yangu kubwa kabisa ya msingi ya kusema kuwa CCM ndiyo adui namba 1 wa maendeleo ya Tanzania. Sababu kubwa CCM kama chama chenye serikali inazuia mabadiliko na kutuaminisha Watanzania wote kuwa tunaenda vizuri sana. Hawataki kukiri kuwa tunavyoenda sivyo, na kisha kama Taifa tukae na kujadili kwa pamoja kuona wapi tulipokosea na twende mbele namna gani. Hili haliweza kutokea kwa sababu CCM wameridhika na mwendo wa konokono tunaoenda nao. Hawataki kuleta mfumo mpya wa utawala utakaoongeza ufanisi, hatuoni dhamira ya dhati ya kuweka na kusimamia sera na sheria zinazoongeza uwajibikaji, kupunguza matumizi ya anasa, kuondoa rushwa na ufisadi. Hatuoni dhamira ya uwekaji mikakati mipya ya usimamizi wa sheria na kanuni. Hatuoni mawazo mapya yanayotuaminisha kuwa kesho tutakuwa bora zaidi kuliko tulivyo leo, kwa sababu namna ya utendaji wa serikali wa leo hauna tofauti na namna ya utendaji wa jana - kama matendo yetu ya leo hayana tofauti na ya jana, kwa nini tuamini kuwa maisha yetu ya kesho yatakuwa tofauti na ya jana na leo?
 
Dr. umeeleza juu ya siasa za ghiliba na uwongo wakati wa kampeni, na hasa wewe kuhusishwa na mikataba mibaya ya madini, mimi nikiwa mmoja wa wadau wakubwa kwenye sekta hii, nafahamu siyo kweli hata kidogo. Pia natambua juhudi zako, na pia nafahamu ukomo wa uwezo wako ulipokuwa kamishna katika kuleta mabadiliko. Dr. kama mtu binafsi, sina lawama yeyote ninayoweza kuielekeza kwako binafsi lakini daima lawama zangu nazielekeza kwa serikali na CCM kama taasisi za uongozi na utawala juu ya kutokuwa tayari kuleta mabadiliko makubwa yatakayowaletea matumaini Watanzania na uhakika wa maisha. Japo siungi mkono siasa za ghiliba lakini pia nikukumbushe Dr. kuwa kinara wa siasa za ghiliba Tanzania ni CCM. Ni CCM kwa miaka mingi ndiyo imekuwa ikiwadanganya wananchi kuwa vyama vingi vya siasa vitaleta vita. Ni CCM kwa kutumia vyombo vya dola, ilitangaza kuwa CUFwalikamatwa na makontena ya majambia, tena walikuwa wakiyatamka hayo kipindi cha kampeni. Kwenye uchaguzi wa Igunga, ni CCM ndiyo iliyotangaza kuwa CHADEMA waliingiza makomandoo toka mataifa ya nje ili kuanzisha vita. CCM haina usafi, haina usafi hata kidogo kulaumu vyama vya upinzani kueneza uwongo kwa sababu wao ni vinara katika matendo hayo. CCM kama chama kikonge, chama chenye dola, kilistahili kuonesha mfano wa siasa za kistaarabu lakini kwa bahati mbaya zaidi hakijaweza kufanya hivyo.
 
Kwangu mimi, hatua ya kwanza kuleta mabadilko katika Tanzania, ni lazima kupunguza nguvu za CCM ili CCM iweze kuridhia matakwa ya Watanzania. Kwa sasa CCM haioni umuhimu huo kwa vile inahodhi kila nyanja ya mamlaka, kuanzia uundwaji wa sera, utungaji wa sheria na usimamizi. CCM imeondoka kwenye jukumu la uzalendo kwa Taifa, inaangalia zaidi maslahi ya Chama hata kama maslahi hayo yana madhara makubwa kwa Watanzania.
 
Bado narudi kwenye imani yangu kubwa kuwa CCM haiwezi kutuongoza katika vita ya kuondoa rushwa kwa sababu CCM yenyewe, ndani ya chama imeridhia matumizi ya rushwa kimatendo, japo kinadharia kinakataa, lakini daima matendo huongea zaidi kuliko maneno. Hakuna chama wala nchi ya watu wasafi watupu, lakini wana mifumo ya kudhibiti uchafu. Mifumo ya dhibiti wa maovu inayofanya kazi, ndicho kinachokosekana ndani ya serikali yetu na CCM. Wanatamka mdomoni kuchukia rushwa lakini mioyo yao inafurahia rushwa. Ni rahisi kuondoa rushwa ya mtu mmoja mmoja lakini ni ngumu sana kuondoa rushwa ya kimfumo. CCM kwa sasa ina mfumo wa kujenga, kuendekeeza na kuulinda mfumo wa rushwa. Ndiyo maana Dr. Kafumu leo hii ukitaka kupigana na mfumo wa rushwa ndani ya CCM huwezi kufika mbali. Sumaye ameshindwa, amebaki kuulalamikia, Mkurugenzi wa TAKUKURU ameshindwa (aliwahi kutamka kuwa mafisadi wote wakishughulikiwa, nchi itayumba). Mtu mmoja hawezi kuyumbisha nchi lakini kwa sababu rushwa yetu ni ya kimfumo, ndiyo maana mkurugenzi wa TAKUKURU naye anakuwa mwoga kupambana nayo kikamilifu.
 
Rai yangu ni ile ile, kama tunataka nchi yetu iendeshwe kwa matakwa ya walio wengi ni lazima kufifisha nguvu za kupindukia za kundi moja katika jamii, kwa sasa ni CCM. Kupunguza nguvu za CCM, kutasaidia sana nchi yetu kuwa na utawala wa watu kimatendo na siyo kinadharia kama ulivyo sasa. CCM wala vyama vingine vya kisiasa havistahili kufa, maana vikifa, hata CHADEMA nayo baadaye inaweza kugeuka kama ilivyo CCM sasa.
 
Bart

From: Peter <kafumu@yahoo.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Tuesday, October 16, 2012 9:59 AM
Subject: Re: [wanabidii] Mhe PETER KAFUMU ANAOMBA RADHI AU .........?
Makundi

Asannte kwa ujumbe wako, bado uko majuu? Kama ndivyo sisi tuliorudi nchi yetu kuhudumu, haya ndiyo tunakutana nayo, mambo ya matusi, masingizoo, chuki tukiongozwa na siasa za kimagharibi za vyama vingi. Lakini hatujakata tamaaa, bado tutafika tunakotarajia...

Unajua mkakati wa upinzani ni kututaka watu wote tutoke ccm na tukikataa wote twaitwa mafisadi.. Hiyo siyo sawa. Na wakati wote nimejaribu kueleza kuwa pamoja na kuonekana uwepo wa ufisadi unaptokana na kutumia madaraka vibaya, bado imani na visions za ccm ni zilezile za kuamini katika usawa wa binadamu, kupinga rushwa, na mengine mengi kama yalivyoelezwa kwenye imani ya ccm na hata azimiao la arusha. Kurekebisha uovu si lazima utoke waweza kubadilisha pale ulipo ili mradi uteseke kuishi katika ubaya huo kwa uadilifu ukilenga kuleta mabadiliko ya kweli.

Ufisadi upo kila sehemu cdm wamejaa mafisadi wenye mali na makasri ya ajabu. Wengi wamepata mali hizo kwa dhuluma na biashara haramu, katika nchi ambayo usimamizi wa biashaara ni hafifu. Hwa kwa macho ya upinzani wa kisiasa ni malaika ilimradi tu wapo nje ya ccm na utawala.

Huwa ninasikitika sina nikiona siasa za tanzania zinazoendeshwa na upnzani ni siasa za matusi na kusingiziana. Kila wakati na kila kijana wa cdm - angalia vijana wa JF wakielezea kuhusu kafumu utadhani wanamfahamu. Wanasema fisadi huyo aliingia mikataba mibovu ya madini. Huu ni uzushi mkubwa na uongo uliojaa ushabiki ulio tayari kuua. Mimi nimekuwa kamishna wa madini kuanzia oktoba 2006, wakati huo mikataba yote ya madini ilishaingiwa tena na waziri wala siyo kamishna kulingana na sheria ya madini ya mwaka 1998, iliyotungwa na bunge la vyama vingi. Nilikuwa kamishna wa madini kusimamia sheria hiyo, wala siyo kuingia mikataba. 

Katika kipindi cha miaka mitano ya kuhudumu nafasi hiyo nilishiriki kuishauri serikali kurekebisha sheria hiyo na serikaliilitunga sheria ya madini ya mwaka 2010, yenye masharti na maelekezo ya kuitaka jamii ya watanzania kushiri zaidi katika sekta ya madini qqna hususan tasnia ya uchimbaji wa madini.

Mzee Makundi, tulipokuwa kwenye kampeni za uchaguzi mdogo wa igunga vijana wa cdm wakiongozwa na kijana mnyika walipita kila kona ya nyumbani kwetu kwa ndugu zangu wakisema huyu mtoto wenu amekuwa kamishna wa madini kwa miaka 18 ametunga sheria mbaya ya madini na ameingia mikataba mibovu. Nayasema haya kukuoanesha kuwa siasa zetu ni za propaganda mbaya iliyojaa uongo wenye nia ya kuamsha hasira ya wananchi. Hii siyo sawa.

Nionavyo mimi tunahitaji kuajifunza kushiriki kwenye siasa hizi kwa ukweli na uwazi, aliyekosa, au aliye fisadi asongwe, asontwe ili aadhibiwe na jamii, lakini siyo kila aliyeccm ni fisadi hata raia wa kawaida kijijini.

Siala la kuwa na fedha uswiss hata mafisadi waliopao cdm wanazo fedha huko, kwa vile wao hawahusiani na utawala basi wao malaika hii siyo sawa. Willy, nashukuru kwa ushauri wako, wa kuwasonta na kuandama mafisadi pale nilipo, kwanza kabla hujafanya hivyo ani lazima kuishi maisha ya mateso maisha ya kuwa mwadilifu katikati ya uozo ili uwe taa na mfano wa wazi wa kushindana na maovu. 

Tumekubali kuteseka ndani ya ccm ili Mungu atutumie kuleta mabadiliko ya kweli yasiyo na uwezekano wa kumwaga damu. Tunaitwa mafisadi wakati hatuhusikin kama unavyosema, tunanuka na mafisadi, lakini tutashinda tu. Uasi wakati mwingine siyo jibu la kusahihisha mambo.. Goberchev alibaki ndani na akausanbaratisha ukomunisti wa urusi. 

Nawaomba vijana waache kutukana kila mtu.

Unisamehe kwa makala ndefu.

Mungu akubariki

DPK Ng'wizukulushilinde
On 12 Oct 2012, at 23:56, Willy Makundi <wrlmakundi@aol.com> wrote:
Daktari naomba kusema neno..

CCM kuna mafisadi na watumiaji madaraka vibaya, vile vile kuna watu wema. Wakubwa wa ufisadi wametajwa hadharani na upinzani na hata baadhi ya wanaCCM. Kumbuka NAPE na kampeni ya kujivua gamba. Tunachowaomba wale wema ni kuwataja na kujitenga na wale mafisadi hadharani. Muanze kupigana kuwaondoa kwenye nchama, na kama ikiwezekana kuwachukulia hatua za kisheria.

Vile vile tungeomba wanaCCM wanaowajua mafisadi wa upinzani wawataje hadharani, na tutegemee upinzani kuwafukuzia mbali. Kwa namna hii wale wema wa CCM na wa upinzani wanaweza kuaminiana na kuwa wapinzani wenye lengo la ustawi wa taifa.

Kwa sasa, alimradi waizi wa EPA, MEREMETA, Import Export Fund, IPTL, Richmond/Dowans, Radar, Ndege ya Rais, pesa za Swiss Banks, viongozi wenye mabilioni na makasri, nk wako huru na tena kwenye nafasi za uongozi wa CCM, wale wema wananuka pamoja na hao mafisadi. Unashangaa nini nyote mnaonekana muozo hata kama binafsi nakufahamu kwa unadhifu wako?

Daktari, huna choice ila ile ya kuwaaibisha hadharani na kusema yale maovu wanayofanya. Mwisho wa siku wale wema wa CCM na Upinzani watarithi hii nchi, au kwa zamu au kwa kujiunga. Lifikirie.


mchilyi7.0



-----Original Message----- From: Dr Peter D Kafumu <kafumu@yahoo.com> To: wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> Sent: Fri, Oct 12, 2012 10:22 pm Subject: Re: [wanabidii] Mhe PETER KAFUMU ANAOMBA RADHI AU .........?
Selemani,
 
Nakubaliana nawe sana kuwa ccm kuna mafisadi wakubwa lakini siyo sote. Nasema tena cdm nako kuna mafisadi wengi tu, waliojilimbikizia mali na watanzania wengi wakilala na njaa, wanaendesaha magari mahammer kutoka marekani lakini hawa ni malaika. siyo kweli. Lakini pia cdm wapo waadilifu wa kweli. Naomba nawe uwe objective usimchukie lila aliye ccm, ni kujenga chuki.
 
Nw'izukulushilinde --- On Fri, 10/12/12, Leonard E. Mboera <lmboera@nimr.or.tz> wrote:

From: Leonard E. Mboera <lmboera@nimr.or.tz>
Subject: Re: [wanabidii] Mhe PETER KAFUMU ANAOMBA RADHI AU .........?
To: wanabidii@googlegroups.com, "Selemani Rehani" <srehani@hotmail.com>
Date: Friday, October 12, 2012, 9:47 AM

Tukumbushane tu kuwa: Na hata siasa za Chama Kimoja si utamaduni wa Kiafrika. Swala si vyama vingapi, bali ni uzalendo na maadili ya kiongozi mkuu na viongozi wenzake wa nchi. On Fri, 12 Oct 2012 08:22:31 +0000 Selemani Rehani <srehani@hotmail.com> wrote: > > Kafumu, > > Kama kawaida yako mtazamo HASI uliopindukia juu ya vyama vya upinzani na hasa Chadema. Inastajabisha sana na hasa kwa msomi kama wewe. Chuki haziwezi kuondoka kwa mitazamo kama yako; hasa unapoamua kuyaona ya upande mmoja tu, yaani yale yanayofanywa na Chadema. Yale maovu yanayofanywa na CCM unaamua kujenga upofu na kuamua kutoyaona. Vitendo hivyo vinafanywa hata na wanachama wa CCM pia, mbona hilo hulisemi!! mbona upo biased sana kiasi hicho? Jaribu kuwa fair na objective ndio tutaweza kutatua tatizo hilo. > > Dr. ni muhimu ukajiuliza kwa nini CCM inahusishwa na ufisadi kiasi hicho? kwa nini? jaribu kuwa objective na nina hakika utayapata majibu. Hivi unataka tuseme vipi? je tukisema TLP ndio mafisadi ni sawa? au CUF? au Chadema? ni sawa? je kesi zilizopo mahakamani za kutumia madaraka vibaya au za ufisadi zinawakabili wanachama na viongozi wa chama gani? Jamani huu upofu ni wa kustajabisha sana. Inaoenekana ukiingia CCM hata ukiwa msomi namna gani, haijalishi, baada ya muda kidogo tu unajenga upofu na fikra kongwe za ajabu kabisa. Hivi kweli Dr unashindwa kuelewa kwa nini CCM inahusishwa na ufisadi? angalia kinachoendelea katika changuzi zake za ndani? hizo pesa za kuhongana na kutoleana bastola ni kwa ajili ya nini? wanazipata wapi? kama si ufisadi? > Vyama vingine havina access ya raslimali za Taifa, vyama vingine havina uwezo wa kuamua kandarasi na kushughulika na kodi za wananchi, vyama vingine havina power wala mamlaka ya kuwatishia wafanya biashara ili wavichangie wala haviwezi kuwaahidi kuwa vitawapa kandarasi. Ufisadi upo CCM na hata viongozi mbalimbali ndani ya CCM wanaliona hilo na wanalisema, Waziri Mkuu mstaafu amelisema. Philip Mangula aliwahi kusema kuwa itafikia muda ili kupata viongozi ndani ya CCM itabidi watangaze zabuni na mwenye hela nyingi ndio atashinda na kuwa kiongozi. Ni Ufisadi mtupu. Inasikitisha umeshindwa kuona hilo. Ni juu yenu kuamua kubadilika au kuendelea na vitendo vya ufisadi na kukosa maadili. > > Selemani > > > > > Date: Fri, 12 Oct 2012 00:58:42 -0700 > From: kafumu@yahoo.com > Subject: Re: [wanabidii] Mhe PETER KAFUMU ANAOMBA RADHI AU .........? > To: wanabidii@googlegroups.com > > > > > > > Anael wa Nzega > > Pole, siasa za vyama vyingi siyo utamaduni wa mwafrika, ni jinamizi kutoka kwa wakoloni mamboleo, tunavyolikumbatia kiasi cha kuwagawanya watu wetu ni hatari kwa amani na ustawi wa nchi yetu. > Huwa niashangaa ninapoona viongozi na vijana wenye imani kali ya cdm wanapomwita kila mwanaccm hata kama anaatoka kijiji cha Karitu (nzega) kuwa ni fisadi kwa vile ni mwanachama wa ccm ni kitu cha kutisha, > Ninapoona mara nyingi mama wa ccm kavaa kitenge chake cha ccm anatukanwa na kupigwa mawe na vijana wa cdm ninashangaa. Hali hiyo inajenga uhasama miongoni mwa wananchi wa kawaida na uhasama huo utakapokolea na wananchi wakaanza kubaguana kwa kufuata vyama hatutapona. > Wakati wote ninawaomba wenzangu ndani ya ccm na ndani ya cdm ninao marafiki, tujitahidi kuujenga mfumo huu bila chuki ili tuweze kubadilisha utawala wakati ukifika bila kumwaga damu. Chuki na matusi kwa sababu ya vyama havifai, vitalibomoa taifa letu... > > Anael ubarikiwe > Nitakuletea kitabu nzega, Niarifu namba yako ya simu nitamtuma mtu akuletee > > Kitabu ni katika llugha ya kingereza na bei yake ni sh 15,000 tu > > Asante sana > > Ngw'izukulushilinde > > --- On Thu, 10/11/12, Anael Macha <kowiri@hotmail.com> wrote: > > > From: Anael Macha <kowiri@hotmail.com> > Subject: Re: [wanabidii] Mhe PETER KAFUMU ANAOMBA RADHI AU .........? > To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com> > Date: Thursday, October 11, 2012, 8:07 PM > > > > > Dr. Kafumu, > > > Nitakinunua kitabu, tafadhali kifikishe nzega. > > > Unasema upinzani kuwa wanajenga chuki, sawa ila ccm unataka kujitenga nao. Wewe msafi ila wao walisema/walifanya. Ccm wanajenga nn? Kazi ipo, siasa zinawenyewe bana. > > > Ok, nashukuru na ubarikiwe nawe pia > > AM > > On Oct 11, 2012, at 21:43, "Dr Peter D Kafumu" <kafumu@yahoo.com> wrote: > > > > > > > > > > Bw. Nkumbaro. > > Nilishawahi kusema kwenye mabadiliko, cdm imejaa watu wema na pia mafisadi, kwa sababu hao ni binadamu wenye damu na nyama. Pia ccm imejaa wema na pia mafisadi kwani nao ni watu. Maandishi yako yanaonesha wewe sasa umegandamana na siasa za upinzani, zenye chuki na hasira iliyokithiri na ushabiki unaoona kuwa CDM malaika CCM mashetani. > Katka uchaguzi mdogo wa Igunga mimi mgombea sikutoa rushwa yoyote, sikutukana mtu yoyote na sikukiuka kanuni zozote za uchaguzi. Hukumu imetolewa dhidi yangu kwa tuhuma siyo za rushwa bali za maneno ya watu wengine siyo mimi. Lakini pia kulikuwa na tuhuma zilizotolewa na washitaki kuhusu kutolewa kwa rushwa na baadhi ya wanccm (siyo mimi) lakini jaji alizikataa akasema hazina ushahidi. > > Kwa maoni ya jaji; maneno ya wengine yalitosha yeye kuhukumu alivyohukumu. Maneno yako yamejaa ushabiki na hasira dhidi ya ccm na wanaccm. Huo siyo utamaduni wa ushindani wa vyama vingi tunaotarajia kuujenga Tanzania, utamaduni wa kuita watu wote wa ccm au chama kisicho chako kuwa waovu na wazuri wote wako cdm.  Sipendi kulumbana nawe kwa sababu sitaki kujenga chuki dhidi ya mtu yoyote. > Nakushukuru kwa mchango wako. > > Mungu akubariki > > Ngw'izukulushilinde > > --- On Thu, 10/11/12, John Nkumbaruko <nkumbaruko@yahoo.com> wrote: > > > From: John Nkumbaruko <nkumbaruko@yahoo.com> > Subject: Re: [wanabidii] Mhe PETER KAFUMU ANAOMBA RADHI AU .........? > To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com> > Date: Thursday, October 11, 2012, 2:21 PM > > > > > > > Dear Kaka Kafumu, > Kaka  HK anaandika kuwa, hakukuwa na tuhuma za rushwa kwako wala kiongozi yoyote wa CCM ama serikali aliyetuhumiwa na kukutwa na hatia ya kutoa rushwa kule Igunga. > Definitely Kaka HK hajui nini rushwa. Kwake yeye labda ukikutwa unatoa pesa ndio unaweza kutuhumiwa na hatia ya rushwa. Rushwa, Kaka Kafumu, is any dishonest act committed in return for personal gain. Hata yule aliesema kuwa daraja halitomalizwa Igunga kama CCM haitoshinda - nae pia alitenda kitendo cha rushwa kwa upande wako. > Mahkama Kuu imegundua kuwa dishonest acts (yaani rushwa) zilitumika na ndio maana ikapinduwa ushindi wako. > Kaka HK nae anaeleza kuwa yumo katika kuandika kitabu chake pia. Hili ni jambo zuri sana na ninampongeza kama ninavyokupongeza wewe, kwani 'vizazi na vizazi vitapata kusoma na kujifunza', > lakini sijui kitabu chake kitakuwa kuhusu nini - most probably his book will be titled - How fast a Cowboy draws his  gun on his enemy. > Hapa netini, mimi nilikuwa katika watu wa mwanzo kukupa hongera baada ya ule ushindi wako na nilikuwa peke yangu nilie-withdraw hongera zangu baada ya kufahamu nini kilitokea Igunga na kuwa kumbe ulishinda kwa mazonge na rushwa. Ninastaajabu, vipi mtu anaandika kitabu kuhusu ubaya na extent ya rushwa nchini na huku anakuenda kugombania ubunge kupitia CCM na sio Chadema. Are we serious? The only CCM member ambae alikuwa free of rushwa kwa bahati mbaya amefariki tokea 1999. Sidhani kama yupo mwengine. Mwengine ambae tungelimdhania juzi aliadhirika Kisutu kuenda kudai kodi zake alizotapeliwa. Sisi tulimpa usukani ndugu yetu kumbe mwenzetu alikuwa busy kujenga nyumba za kukodisha katika kila corner ya DSM. Kama ni mimi nisingelikuenda Kisutu kujiadhirisha na ningelimuachia tu huyo mwizi hicho alichochukuwa - kama vile na yeye amechukua chake mapema kutoka kwangu! > > > http://zanzibarnikwetu.blogspot.ca/2012/10/mzee-sio-muachie-tu-raia-wako.html > > > > Anyway, najua mpo wengi hapa ukumbini (Tony, HK, etc) na kwahivyo bora nikimbie kwa haraka! > > > //Nkumba. > > > > > > > > From: Dr Peter D Kafumu <kafumu@yahoo.com> > To: wanabidii@googlegroups.com Sent: Wednesday, October 10, 2012 3:55:48 PM > Subject: Re: [wanabidii] Mhe PETER KAFUMU ANAOMBA RADHI AU .........? > > > > > > > > Waungwana > > Nawaomba mnunue kitabu kwanza msome, na kufanya "a book review" na mjadili na kutoa maoni yenu. Kitabu ni cha kingereza mwandishi wa gazeti kajaribu kutafsiri - ni vizuri kusoma mwenyewe. Tuwasiliane mpate kitabu. Kinauzwa Shs 15,000 tu. Karibuni.. > > Ng'wizukulushilinde > > --- On Wed, 10/10/12, mngonge <mngonge@gmail.com> wrote: > > > From: mngonge <mngonge@gmail.com> > Subject: Re: [wanabidii] Mhe PETER KAFUMU ANAOMBA RADHI AU .........? > To: wanabidii@googlegroups.com > Date: Wednesday, October 10, 2012, 5:05 PM > > > Mimi siyo Kafumu na wala sijabahatika kusoma kitabu chake lakini kwa > kuiangalia sehemu uliyonukuu "...kwamba kuishi kwa uaminifu katika > jamii iliyokithiri kwa rushwa ni sawa na tone la damu ya samaki > aliyejeruhiwa baharini" unaweza kutoa tafakari.  Maneno hayo ni ya > kiswahili yanayoweza kueleweka kwa wasomaji japo mwandishi anaweza > kuwa na tafsiri zaidi. > > Kwa vile katuandikia wasomaji ili tusome kitabu chake na bila shaka > kuelewa ujumbe anaokusudia tuupate. Binafsi namuelewa kwamba si rahisi > kuuona uaminifu wa mtu au watu waaminifu wachache wanaoishi na jamii > kubwa isiyokuwa na uaminifu (wala rushwa). Kwa kufafanua > anachokimaanisha akafananisha mchango wa mtu mwaminifu na tone la damu > ya samaki baharini. > Kwa ufupi kama mada inahusu rushwa na tukiamua kujielekeza katika > tukio lililompata mwandishi wa kitabu hicho tunaweza kupata maana > zaidi. Yeye Kafumu amevuliwa ubunge kwa sababu ya ukiukwaji wa > taratibu za uchaguzi yumkini ikiwemo rushwa. > > Maana pana zaidi tunayoweza kupata ni kama waziri mstaafu (Sumaye) > alivyosema juma lililopita kwamba rushwa inanuka katika chaguzi za > CCM. Inawezekana Kafumu alianza kudaiwa rushwa tangu kuteuliwa na > chama chake hadi kwenye uchaguzi wenyewe. Hivyo anavyosema mtu > mwaminifu hawezi kutokea kwenye kundi la wala rushwa maana > hawatampitisha na hivyo hawezi kuonekana au kueleweka kwa namna > yoyote. > > Lakini pia Kafumu anaweza kuwa na maana pana zaidi ya kwamba > watanzania kwa ujumla wetu tulikofikia ni mwendo wa kutoa chochote ili > uchaguliwe "Toa kula nikupe kura" > Kwamba nchi imekuwa ya watu wasiokuwa waaminifu na hivyo mchango wa > mtu mwaminifu hauwezi kuonekana kwa namna yoyote. Nafikiri Kafumu hana > mpango wa kuomba radhi bali ameamua kuanika alichokiona ndani na nje > ya CCM > > Naamini Kafumu mwenyewe atatueleza nini hasa alichokimaanisha ili > tuweze kununua na kukisoma kitabu chake kwa uelewa zaidi > > 2012/10/10 Said Issa <saidissa100@yahoo.com>: >> Hi All, >> Nd. Peter Kafumu ameandika kitabu kuhusu rushwa nchini kinachoitwa "Sauti >> Inayolia-Tafakuri Binafsi" (a Crying Voice-personal reflections). >> Maelezo yake ya mbio mbio yananipa fikra kama huyu Mhe anatubia labda kwa >> kushinda kule Igunga kwa kupitia mambo ya rushwa na sasa anaomba radhi. >> Anyway, kila mtu atafahamu kivyake, lakini mimi ninamuona kama anaomba >> radhi, hasa pale alipoandika kuwa...."...kwamba kuishi kwa uaminifu katika >> jamii >> iliyokithiri kwa rushwa ni sawa na tone la damu ya samaki aliyejeruhiwa >> baharini". >> >> Najua Mhe Kafumu yupo hapa ukumbini. Ningelimuomba atupe briefing ya kitabu >> chake ambacho kidogo hakifahamiki - yaani haeleweki kama anai-expose >> rushwa au anaomba radhi kwa rushwa iliyotendeka Igunga mpaka akashinda? >> >> >> http://zanzibarnikwetu.blogspot.ca/2012/10/peter-kafumu-alishinda-kutokana-na.html >> >> -- >> Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/ >> Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/ >> Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/ >> >> Kujiondoa Tuma Email kwenda >> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha >> ukishatuma >> >> Disclaimer: >> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal >> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be >> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to >> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines. >> >> > > -- Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/ > Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/ > Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/ > > Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma > > Disclaimer: > Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines. > > > > -- Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/ > Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/ > Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/ > > Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma > > Disclaimer: > Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines. > > > > > > -- Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/ > Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/ > Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/ > > Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma > > Disclaimer: > Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines. > > > > -- Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/ > Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/ > Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/ > > Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma > > Disclaimer: > Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines. > > > > -- Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/ > Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/ > Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/ > > Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma > > Disclaimer: > Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines. > > > > -- Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/ > Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/ > Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/ > > Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma > > Disclaimer: > Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines. > > >                           > -- Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/ > Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/ > Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/ > > Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma > > Disclaimer: > Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines. > > -- Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/ Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/ Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/ Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
-- Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/ Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/ Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/   Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma   Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.    
-- Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/ Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/ Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/   Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma   Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.    
-- Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com   Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma   Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.    

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment