Tuesday 2 October 2012

Re: [wanabidii] Mahusiano yetu ya kifamilia hayahusiki na sababu na dhamira yetu ya kujiunga CHADEMA

Ndugu Kigwangalla kama umeyasoma maelezo yao kutoka mwanzo hadi mwisho
yanaeleweka kabisa. Stephen Wassira ni baba yao mdogo na wanayemtaja
kama mwanzilishi wa Chadema ni baba yao mzazi. Ina maana huwezi
kutofautisha babamdogo na babamzazi? Ebu rudia kusoma vizuri utaelewa
naona ulikuwa na haraka au mtizamo wako kabla ya kusoma maelezo yao
kwa ukamilifu

2012/10/2 Dr. Hamisi A. Kigwangalla <hkigwangalla@gmail.com>:
> mbona wanajichanganya hawa warembo? Maana kuna para moja hapo juu (para ya
> pili) wanakana kuwa si watoto wa Stephen Wassira na kwamba huyo ni baba yao
> mdogo, baadaye kule mwisho wanasema CDM ilianzishwa na baba yao mzazi...sasa
> which is which? Aliyeanzisha CDM ni Stephen ama ni George? na je Baba yao
> mzazi ni nani, ni Stephen ama ni George Wassira?
>
>
> 2012/10/2 Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
>>
>> Tarehe 30/09/2012 mimi Esther Wasira na dada yangu Lilian Wasira
>> tulijiunga na CHADEMA na kukabidhiwa kadi na Katibu Mkuu wa CHADEMA
>> Mh. Dr Willibrod Slaa. Tulielezea kwa kirefu sababu za sisi kujiunga
>> Chadema na tukasisitiza kuwa tumeridhika kuwa CHADEMA ni chama chenye
>> dhamira safi ya kuiongoza Tanzania na kwamba ni chama kinacholeta
>> matumaini mapya ya kuijenga Tanzania mpya yenye neema.
>>
>> Waandishi wa habari walijaribu sana kutudodosa kujua tuna uhusiano
>> gani na Waziri Steven Wasira. Tulielezea wazi kuwa mahusiano yetu ya
>> kifamilia hayahusiki na sababu na dhamira yetu ya kujiunga CHADEMA.
>> Hata hivyo tulielezea kuwa Waziri Steven Wasira ni baba yetu mdogo
>> ambaye alinyang'anyana ziwa na baba yetu mzazi, wakili George Wasira.
>> Tulidhani hiyo ilitosha na lisingekuwa swala tena la kujadili na
>> badala yake hoja ya kujadiliwa ingeweza kuwa sababu tulizozieleza za
>> kujiunga CHADEMA.
>>
>> Tunasikitishwa sana na malumbano yaliyofuata baada ya hapo kuhusu kama
>> sisi ni watoto wa Wasira au la. Kama tulivyoeleza, tumejiunga CHADEMA
>> kwa sababu tulizozieleza hapo awali na wala si kwa sababu nyingine
>> yeyote. Hatujajiunga CHADEMA kumdhalilisha mtu, kumfedhehesha mtu au
>> kukipatia umaarufu CHADEMA kwa vile tu tunatumia jina la Wasira.
>> CHADEMA ni chama cha siasa tena chenye wanachama na wafuasi wengi
>> Tanzania hivyo si kashfa bali ni fahari kubwa mtu kujiunga CHADEMA na
>> tena ni ushahidi wa mtu kujitambua.
>>
>> Pia CHADEMA ni Chama maarufu sana Tanzania kwa sasa hata pengine ni
>> maarufu kuliko CCM hivyo hakihitaji kujipatia umaarufu kwa mgongo
>> wetu. Sisi tunawaheshimu sana wazee wetu na tutaendelea kuwaheshimu
>> ila linapokuja swala la chama cha kujiunga linabaki kuwa hiari yetu
>> kwa kuzingatia sera za chama na uwezo wa chama husika katika kujenga
>> Tanzania tunayoitaka na hilo ndilo lililotupeleka CHADEMA. Na hii ni
>> haki yetu ya msingi kabisa inayolindwa na Katiba ya nchi hii chini ya
>> ibara ya 20(1).
>>
>> Ikumbukwe kuwa mmoja wa Waanzilishi wa CHADEMA ni Mzee Wasira. Dhamira
>> ya kuanzisha CHADEMA ilikuwa ni kushika dola na hili ndilo CHADEMA
>> imekuwa siku zote inajaribu kuwashawishi Watanzania kuwa sasa
>> wamekomaa na wanastahili kuchukua dola. Kwa vile kuchukua dola ilikuwa
>> ndio ndoto ya baba yetu mzazi Mwanzilishi wa CHADEMA, sisi kama watoto
>> tumejiunga na M4C ya CHADEMA ili tuweze kutimiza ndoto ya baba yetu
>> kuwa CHADEMA siku moja ichukue jukumu la kuiongoza Tanzania.
>>
>> Kwa maelezo zaidi wasiliana na:
>> Lilian Wasira 0719 604156
>> Esther Wasira 0655 048797
>>
>> --
>> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
>> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
>> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>>
>> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
>> ukishatuma
>>
>> Disclaimer:
>> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
>> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
>> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
>> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>>
>>
>
>
>
> --
> "Vision is the ability to see the invisible!"
> Hamisi A. Kigwangalla, MD, MPH, MBA
> P.O.Box 22499,
> Dar es salaam.
> Tanzania.
> Phone No: +255 754 636963
> +255 782 636963
> website: www.peercorpstrust.org or www.hamisikigwangalla.com
> Email: hamisi.kigwangalla@peercorpstrust.org or info@hamisikigwangalla.com
> Skype ID: hkigwangalla
> Blog: blog.hamisikigwangalla.com
>
>
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment