Sunday 30 August 2015

[wanabidii] Kuelekea uchaguzi Mkuu 2015: UKAWA yadhibitisha-Lowasa anaumwa.

Nakumbuka wakati Jakaya Mrisho Kikwete anaomba kuingia madarakani mwaka 2005 alizushiwa kuwa alikuwa anaumwa UKIMWI. Maana yake siyo kwamba alikuwa na HIV tu, virusi vinavyosababisha UKIMWI, bali alikuwa ameshafikia hali mbaya ya kuumwa UKIMWI kabisa na alizushiwa kuwa muda wowote angeondoka duniani kabla hata ya kumaliza miezi sita ya mwaka wa kwanza madarakani.

Lakini ni miaka kumi sasa yupo anadunda. Hata Tezi Dume (kansa) ambayo yeye mwenyewe amewathibitishia Watanzania kwamba anayo haijamzuia kufanya kazi za Urais. Lakini zaidi ingawa ametuthibitishia Watanzania kuwa ana tezi dume, kuondoka kwake duniani anakujua Mwenyenzi Mungu, tunaweza kushangaa sisi binadamu kuona Mungu anampa kuishi miaka 40 hata 50 ijayo.

Ninachotaka kusema hapa ni kwamba maisha ya binadamu uzima wake anaujua Mungu. Rais mstaafu wa Kenya Mwai Kibaki alikuwa mgonjwa mahututi wakati anaingia madarakani. Lakini Wakenye waliokuwa wanataka madadiliko walimchagua. Lakini leo yupo Kibaki yuko hai na zaidi miaka yake aliyoitumikia Kenya hakuna Rais aliyewahi kumfikia kwa kiwango cha kuwaletea Wakenya maendeleo.

Hivyo wanaodhani kuwa kwa kusema Edward Lowassa ni mgonjwa eti hawezi kuongoza Tanzania kwa miaka 5 ijayo, hiyo ni kete tu ya kuwadanganya wapiga kura ili kuzuia mabadiliko. Lakini Watanzania wengi wa leo HAWADANGANYIKI. Hivyo ni vema wenye hoja ya ugonjwa waachane nayo maana itakufa kama ile hoja ya ufisadi wa Richmond ilivyokufa baada ya kubaini aliyekuwa kinara wa Richmond ni mkuu wa nchi na siyo Waziri Mkuu (Edward Lowassa). Wananchi wanajua serikali ya CCM ndiyo fisadi kamili anayekwapua fedha za wananchi kila uchao. Mfano ufisadi wa Tegeta escrow kinara wa ufisadi huo alikuwa ofisi kuu ya nchi Ikulu Wapiga kura wanauliza je Lowassa alikuwa Ikulu mwaka jana 2014?


Ananilea Nkya
 E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com

--------------------------------------------
On Sun, 8/30/15, De kleinson kim <dekleinson@gmail.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] Kuelekea uchaguzi Mkuu 2015: UKAWA yadhibitisha-Lowasa anaumwa.
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Sunday, August 30, 2015, 9:55 AM

Kwanza
tukubaliane hali ya Edo sio nzuri. Nadhani inaathiri hata
mfumo wake wa akili kwa mbaali.
Jana alikuwa anaongea kama amekariri, haraka
haraka, limited, its like he was running out of time!!!

Mwenye akili zake akiri kuumwa kwake, halafu arudi na kuanza
kutetea ugonjwa wake (kama anaujua) ni jinsi gani hauna
athari zozote za muda mfupi.
Mambo mengine yapo wazi bandugu.

ha ha ha haaaaa. hata angekuwa na ugonjwa wa kuonekana bado
raia mngeweka ngumu.



--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment