Saturday 29 August 2015

[wanabidii] Huku Sumaye na Lowassa, kule Mengi na Rostam, tusubiri

Huku Sumaye na Lowassa, kule Mengi na Rostam, tusubiri
AMA kweli Wahenga walisema; ndugu wakigombana chukua jembe ukalime,siku wakipatana chukua kapu ukavune.

Lakini pia upo usemi wa wanasiasa kote duniani wa kwamba katika siasa,hakuna urafiki wala uadui wa kudumu, bali kinachoangaliwa zaidi nimaslahi ya kisiasa!
Historia inashuhudia misemo yote hiyo miwili kwa sasa ikitimia katikakipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu.

Huku tunawaona wanasiasa wawili mahasimu, Edward Lowassa na FrederickSumaye wakiungana na kuwa wamoja, kule tunawaona wafanyabiasharawawili mahasimu, Dk. Reginald Mengi na Rostam Aziz nao wakiwawameungana. Tusubiri tuone huko tuendako!

Wiki iliyopita, Agosti 22, mwaka huu, waziri mkuu mstaafu, Sumaye,alitangaza
rasmi kuachana na Chama cha Mapinduzi (CCM), akisemaameamua kujiunga na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), unaoundwa navyama vinne vya siasa nchini vya Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD kwa lengo kuongeza nguvu ya kisiasa upande wa Upinzani ili hatimayekupatikane huko chama chenye nguvu na
kinachoweza kuaminiwa naWatanzania.

Niseme mapema hapa kwamba binafsi, hadi sasa sijui ni Watanzaniawangapi wanaweza kushawishika na kukiamini chama chochote cha Upinzani katika idadi ya vyama hivi tulivyonavyo atakachojiunganacho Sumayeambaye hakuwahi kuaminiwa na Watanzania hao hata katika miaka yakeyote 10 ya uwaziri mkuu.
Ninachokikumbuka, huyu ndiye waziri mkuu pekee katika uongozi wakealiyepachikwa jina la waziri mkuu zero au sifuri na Watanzania hao haopamoja na wachora vikatuni katika baadhi ya magazeti yetu.

Ninachoamini bado, kama alivyosema Sumaye mwenyewe wakati wa akitoatamko lake hilo la kuhama CCM wiki iliyopita, huyu ni mwanasiasasisimizi tu katika wanasiasa wa nchi hii!
Ndugu zangu, huko Ukawa alikokwenda Sumaye ndiko aliko aliyekuwahasimu wake mkuu wa kisiasa katika siasa za ndani ya CCM, Lowassa,ambaye alitangaza rasmi kuhamia huko Julai 28, mwaka huu, kabla yaumoja huo kumkabidhi mikoba ya kuwa mgombea pekee wa urais wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Ukawa.

Kabla ya wawili hao kuchukua uamuzi huo, wakiwa bado makada wa CCM,wote walijitokeza na kuwa miongoni mwa makada 38 wa chama hichowaliochukua na kurejesha fomu za kuomba kuteuliwa kuwa wagombea waurais katika uchaguzi wa mwaka huu.
Hata hivyo, kutokana na haiba yao ya kisiasa ndani na nje ya CCM, wotewawili hao majina yao yalikatwa katika hatua za mwanzo kabisa, wala hayakuingia hata ndani ya kikao cha Kamati Kuu kujadiliwa!

Kwa yeyote anayefuatilia siasa za ndani ya CCM, anafahamu kwambaLowassa na Sumaye, walikuwa hawaivi kisiasa. Mara kadhaa, Sumayeamejiapiza mbele ya chama chake na mbele ya waliokuwa wanachamawenzake, akisema endapo CCM ingemteua Lowassa kuwa mgombea wa urais,basi yeye angejitenga na chama hicho.

Kama ambavyo karibu viongozi wakuu wote wa Chadema na kambi yaupinzani kwa ujumla ilivyokuwa ikimtuhumu Lowassa kwamba ni fisadiasiyestahili kukabidhiwa madaraka ya juu ya kuongoza nchi, ndivyo pia Sumaye alivyokuwa akimnanga Lowassa kila anapopata fursa yakuzungumzia masuala ya rushwa na ufisadi.
Kwa mfano, Novemba 2013, katika mkutano mmoja na waandishi wa habari,Sumaye alilalamika kuhujumiwa na watu aliodai kuwa mahasimu wake wakisiasa katika mbio za urais za mwaka 2015, hasa kwa kuingilia katimialiko yake ya kijamii anayoipata ili kuwa mgeni rasmi.

Malalamiko hayo ni mbali na yale aliyoyatoa mwaka 2012 baada yakushindwa katika nafasi ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) Taifakuwakilisha Wilaya ya Hannang, mkoani Manyara, akisema wazi kuwa baadhiya mafisadi wa ndani ya CCM, walitumia fedha nyingi kuhakikisha kwambamshindani wake, Dk. Mary Nagu, anamwangusha.

"Siwataji, hata ninyi mnawajua," aliwahi kukaririwa Sumaye baada yakutakiwa na wandishi wa habari kuwataja mafisadi wanaomjumu kwenyemialiko yake ya shughuli za kijamii pamoja na kumwaga fedha wilayanikwake ili ashindwe ujumbe wa NEC.

Wakati fulani pia, mbele ya wandishi wa habari, Sumaye, bila kutajajina la Lowassa, aliwahi kukaririwa akisema: "Fisadi huliibia taifafedha nyingi kiasi cha wananchi kutaabika, halafu akiitwa kwenyeharambee anatoa kijisehemu tu cha fedha alizofisadi kwa njia ya rushwakukandamiza maendeleo ya watu.

"Rais Kikwete amesema kuwa rushwa inaweza ikafanya CCM ikashindwa.
Mimi naamini, kama CCM itapitisha majina (ya wagombea wake wa urais2015) kwa kuangalia rushwa, chama kitaanguka, bahati nzuri Mwenyekitiameliona hilo, siamini kama watapitisha watu ambao watakiangusha.

Wakipitishwa hao, sitaweza kukaa nao, hata kama sitahama."
Hizo ni baadhi tu ya nukuu za Sumaye katika matukio na nyakatimbalimbali akizungumzia msimamo wake kuhusu rushwa na mafisadi, lakininyingi ya kauli zake hizo, kwa vyovyote vile akizielekeza kwa Lowassa.

Hata hivyo, Sumaye huyu wa sasa, aliyeamua kumfuata Lowassa Ukawa,amekaririwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini katika tukio hilo lawiki iliyopita akisema: "Ambaye ameshakaa serikalini katika nafasi mbalimbali ni Lowassa. Hawa wengine (aliogombea nao urais ndani yaCCM) hawajaendesha Serikali, wamekwenda shule tu."
Kwamba Lowassa ambaye siku zote Sumaye alikuwa akikiaminisha chamachake, CCM, kwamba ni fisadi na mtoa rushwa mkubwa, akisema kama CCMitampitisha mwanasiasa huyo kugombea urais, yeye hatakuwa sehemu yachama hicho, leo hii ndiye tunayeambiwa na Sumaye kwamba alikuwaanafaa kuteuliwa kwa sababu tu amekwishashika nafasi mbalimbali
serikalini, anafahamu kuendesha Serikali!

Huyo ni Sumaye na Lowassa, wanasiasa ambao huko nyuma walikuwa katikamkoa mmoja wa Arusha, wakiwa na uhasama mkubwa wa kisiasa, kabla yaMkoa huo kugawanywa na kupatikana mkoa mwingine wa Manyarauliowatenganisha kiutawala.

Katikati ya mshangao huo wa Sumaye na Lowassa, katika kipindi hikihiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2015, tunawaona pia mahasimu wawiliwa kibiashara hapa nchini, Dk. Mengi na Rostam Aziz wakiweka tofautizao za muda mrefu pembeni na kuungana kumtafuta mgombea wao wa uraismwaka huu.

Kwa wenye kumbukumbu na wanaofuatilia matukio mbalimbali yanayoendelea nchini watakuwa wanakumbuka tukio la Mei 26, mwaka huu, siku ambayo wafanyabiashara wawili hao maarufu nchini walivyokaa mezakuu moja. Hilo lilikuwa tukio la kutano wa wamiliki wa vyombo binafsi vyahabari nchini, kupitia umoja wao wa MOAT na waandishi wa vyombo vya habari vya ndani na nje, uliolenga kuzungumzia, pamoja na mambo mengine, hisia za MOAT kuhusu miswada miwili iliyokuwa ikitazamiwa kuwasilishwa na Serikali bungeni ili kuwa sheria kamili. Muswada wa Huduma za Vyombo vya Habari pamoja na Muswada wa Haki ya KupataHabari.

Swali kuu lililotawala vichwani mwa baadhi ya wadadisi wa mambowalioshuhudia tukio lile la Mei 26, 2015, la Dk. Mengi na Rostamkukumbatiana na kukaa meza moja, lilikuwa ni, je; miswada hiyo miwiliya Serikali ndiyo iliyowaleta pamoja wafanyabiashara hao wawili maarufu katika nchi hii au ni Uchaguzi Mkuu wa Oktoba na vitalu vya gesi asilia na mafuta?

Kwanini swali hilo? Itakumbukwa kwamba Aprili 23, 2009, Dk Mengi, ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, alitaja kwa majina wafanyabiashara watano akiwatuhumu kuwa mafisadi papa hatari kwa uchumi wa Taifa hili, miongoni mwa mafisadi wasiopungua 10 aliodai kuuyumbisha utawala wa Rais Jakaya Kikwete.

Katika madai yake hayo, Dk. Mengi alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini akisema: "Nchi hii ina mafisadi ambao kila kukicha wanaiyumbisha nchi. Hawazidi hata kumi. Lakini kuna watano ambao ni mafisadi papa. Ukitokea kupingana nao tu kutokana na ufisadi wao, wanakuona wewe ni adui mkubwa."
Dk Mengi, siku hiyo akiwa kwenye mkutano mkubwa na vyombo vya habari, alitaja majina ya mafisadi papa hao watano, wakiongozwa na Rostam Aziz na wengine wanne ambao sina sababu ya kuwataja hapa.

Baada ya kutaja orodha hiyo ya wafanyabiashara mafisadi papa, Dk. Mengi alieleweka vyema kwa Watanzania, hasa wale waliokuwa wakimwamini na kumkubali kutokana na msimamo wake wa 'uzalendo' na 'utetezi wa wazawa.'
Wakati Watanzania hao wakiendelea kutafakari orodha hiyo ya mafisadi papa pamoja na matendo yao kwa Taifa hili, siku 10 baadaye, yaani Mei 2, 2009, Rostam Aziz naye aliitisha mkutano mkubwa pia wa waandishi vyombo mbalimbali vya habari vya ndani na nje na kumrushia makombora mazito Mwenyekiti Mtendaji huyo wa IPP.

Dk Mengi alitajwa na Rostam Aziz kwamba yeye ndiye fisadi mkubwa ndani ya nchi hii, akimfananisha na fisadi nyangumi. Rostam alikwenda mbali zaidi, akidai kuwa na vielelezo kibao ambavyo angeviwakilisha mikononi mwa Jeshi la Polisi ili waanze kumchunguza dhidi ya vitendo vyake hivyo vya kifisadi nyangumi.

Katika kipindi hicho cha misuguano baina ya wafanyabiashara hao wawili, kiasi cha kupachikana majina ya mafisadi papa na mafisadi nyangumi, Rostam alikuwa bado ni Mbunge wa Igunga na pia Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM.

Takriban miaka mitatu baadaye, baada ya Rostam Aziz kudaiwa na Dk.Mengi kwamba amekuwa akishiriki katika vitendo vinavyoiyumbisha nchi hii, kwa maana ya Julai 13, 2011, mwanasiasa huyo aliamua kujiuzulu ubunge huo wa Igunga pamoja na nyadhifa nyingine zote hizo alizokuwa nazo ndani ya CCM, akidai kuwa dhamira yake ya dhati kabisa imemtuma
aachane na siasa uchwara za ndani ya chama chake hicho ili sasa aweze kutumia muda wake kushughulika na biashara zake.

Je, uhusiano huu mpya wa Dk Mengi na Rostam Aziz, uliowafanya wazike tofauti zao na uhasama wao na kwa pamoja kuamua kumuunga mkono kisiasa Lowassa katika mbio zake za kuusaka urais, unabeba siri gani?
Nihitimishe makala haya kwa kuwakumbusha Watanzania kwa ujumla wa imani zote, kwamba katika Biblia (Mathayo 7:6, 12-14), imeandikwa hivi: "Msimpe mbwa kilicho kitakatifu, wala msiwape nguruwe lulu zenu wasije wakawakanyaga, wakawageuka na kuwararua."

Ikulu ni mahali patakatifu, watu wasio wasafi si mahali pao. Gesi asilia na mafuta yaliyopatikana Mtwara pamoja na maeneo mengine ya nchi hii, Bara na Visiwani, ni lulu ya uchumi wa nchi hii, ambayo kamwe Watanzania hawawezi kuitoa lulu yao hiyo na kuwakabidhi wasiofaa! Tutafakari sasa na hata Oktoba 25.
Chanzo RaiaMwema
Toleo la 420,28 Aug 2015

0 comments:

Post a Comment