Sunday 30 August 2015

RE: [wanabidii] Kuelekea uchaguzi Mkuu 2015: UKAWA yadhibitisha-Lowasa anaumwa.

Mrema,

Nafikiri hivi,
1. Uchumi wa mtu mmoja mmoja kupitia kilimo, mpaka sasa tunategemea wengine kwa asilimia kubwa kuliko wanavyotutegemea sisi. Ukweli hatuna processing/manufacturing industries za kutupa viburi. na hata zingekuwepo bado raw materials hakuna.
Maana yangu,
Hatuwezi kukwepa 70% ya wananchi wanaotegemea kilimo, wengi ni kwa chakula bado hawajajua kilimo cha biashara. Kilimo kinahitaji kuelekezewa nguvu kwa zaidi katika budget yetu na iwafikie wakulima!! kama lengo litakuwa tuwainue 35% hatutakosa hata 15% za kuanza nao!! Mara 4 tu na tunalifikia lengo.
Kuinua Uchumi wa wananchi wote ni lazima tuanze ku-deal na kule ambapo wengi wao wanapatazama ambao wakiwezeshwa wataleta faida kubwa kwa serikali kimapato, na wao binafsi kujikimu. umetengeneza ajira kwao na mapato kwa serikali!!! Na haitahitaji gharama kubwa za kuanza kama ambavyo tungeanza kuwekeza upya.

2, Elimu,
Hakuna jamii inayoweza kuendelea bila kupeana maarifa vizazi na vizazi. kizazi kijacho kijue mmekwama wapi na wapi mlijikwaa, wao wakija wanafanya vinginevyo ili mradi lengo litimie huku wakizidi kubuni sera mpya za kimaendeleo. Mpaka sasa hakuna utaratibu unaoeleweka katika hili. si tu elimu, iwe elimu bora. Tuwe na wapanga sera wazuri, watu wa fedha waaminifu n.k.
Mfano; Nina uhakika kwa nchi kama Tanzania kama elimu ya kilimo ingetiliwa mkazo kuanzia ngazi ya chini, haya mapori tungekuwa tunapigania. mtaji wa kwanza katika kilimo ni ardhi. na ipo!!

3. Utawala, hapa ndio pagumu maana tikifeli kwenye viongozi makini, tumefeli kila kitu, kijamii na kiuchumi.
Mfumo wa utawala bora huanzia kwenye kuheshimu sheria, tena sheria zilizotungwa kwa umakini kujali maslahi ya Taifa, Kwa Tanzania kuanzia Katiba, na vijisheria vidogo vidogo vyote vinahitaji kufumuliwa upya. kuna sheria ndogo ndogo nyingi pia zinategemea mwongozo wa katiba. angalia kwenye uteuzi wa board members katika taasisi fulani fulani. usiniambie tutabadilisha ring piston halafu turudishie oil ile ile!! 
Pamoja na yote hayo, sheria inaweza kuwa nzuri na bado ikakanyagwa!

4, Wawakilishi wa wananchi, Bado siamini katika bunge la udaku, linatengenezwa na vimada, vitwana na vijakazi vya wanasiasa/wafanyabiashara. lazima tutengeneze mfumo thabiti wa kupata wawakilishi wanaojua wananchi na nchi yao, wenye elimu kiasi katika ngazi flani. na pia chama sio lazima sana!! vyama vinaweza vikawapa wananchi wagombea wabovu. wananchi hawana uamuzi zaidi ya kupokea kile kilchopo mezani. waachiwe huru kuamua hata akiwa nje ya chama cha siasa.

5. Bado siamini kama tupo huru. tuanze kupigania uhuru kwa kuanza kufundishana uzalendo kuanzia ngazi ya familia, matelevisheni, radio na kila mahali. Vijana wa ki-Africa hatujui thamani ya nyumbani. hatuelewi ni kwa nini tunapaswa kulinda nchi zetu na kuzipigania. badala yake tunatumiwa kujidhoofisha!!! kila mtu anaezaliwa akifundishwa dunia ni wewe na nchi yako na watu wake ni hakika tutafika mbali.
Tutaona matokeo yake miaka 30 ijayo. Watu watakuwa positive katika mambo yenye maslahi na taifa.

Lakini nani wa kuamua haya kama tuliowapa mamlaka ya kuamua haya hawataki?

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment