Monday 31 August 2015

Re: [wanabidii] Bi. Samia Suluhu Ahaidi Ujenzi Hospitali ya Wilaya Ikungi, Bandari Kavu Manyoni

Naomba niage Kabla ya tarehe 1.9.2015.
Sio tu uongo wa huko Manyoni, hata Bahi, ambako ndo kwetu, ahadi za uongo , Leo Samia amezitoa,  Kwa kuwa ni kati ya wanawake dhaifu wa CCM, waliopandikizwa, waonekane kuna wanawake!
Eti Bahi patawekwa bwawa  la uhakika.Wakati mie nimekulia Bahi kwa maji yenye rangi kama juice ya nanasi. Tunakunywa maji na ng'ombe.
Ahadi zinatolewa sasa na Samia na CCM, walishindwa nini miaka 53, wataweza Leo?
Mie Nimesoma kijiji cha Kilimatinde , wilayani Manyoni, miaka ya kuanzia 1973.Kilimatinde, wilaya ya Manyoni, na mkoa wa Singida hali ni ileile, kama wanavyoimba wenyewe, CCM ni ileile , kumbe kwa kuwa pia watu ni walewale, na mifumo ni ileile!  Mabadiliko yatapatikana kwa miujiza gani? Wana CCM wakiondoka madarakani kwa kifo, uzee,nk,  ma baba mtu au ma mama mtu, wanarithishwa watoto wao! Majina ni yaleyale.

Nani hajui Getrude Mongela Ndo mwanawe alikuwa DC, na sasa amekuwa RC , Kagera, asiyejua CCM, iliongozwa na Moses Nnauye, na sasa ni mtoto wake Nape Nnauye, Job Lusinde aliyekuwaga waziri na Balozi, na sasa kuna mbunge Lusinde, aliyeachiwa jimbo na Ba mkubwa wake , ambaye ni  John Malechela. Bado kuna wabunge kama Vita Kawawa, Mkapa, ma  Nyerere kama watatu hivi!, Malima, Mgimwa, na hatimaye mbunge Ridhiwani Kikwete , huku fast lady naye akiwa ni mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM.Ina maana, Watanzania ndo haohao tu, wanaoweza kuongoza CCM, na serikali yake out of watu ML 43 ! Duh! Hebu fungukeni bila kujali vyama huku mkikumbuka, umasikini sio ajali, na Tanzania inahitaji mabadiliko. Wengine wasio na watoto, ndo wanapiga watu bakora, hawataki kutoka madarakani, na bado kamati za maadili - CCM, zinawapitisha kuwa wanafaa!
Kweli Tanzania sasa siasa ni sawa na ile ngoma ya mdundiko, inasomba watu ovyo ovyo tu.
Kwa herini!

SB

On Aug 31, 2015 10:13 AM, Joachim Mushi <mushijoa@gmail.com> wrote:
Bi. Samia Suluhu Ahaidi Ujenzi Hospitali ya Wilaya Ikungi, Bandari Kavu Manyoni

[caption id="attachment_61296" align="aligncenter" width="800"]<img class="size-full wp-image-61296" src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2015/08/IMG_00031.jpg" alt="Mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu akiwahutubia wananchi katika mkutano wa kampeni ulofanyika Wilaya ya Ikungi." width="800" height="408" /> Mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu akiwahutubia wananchi katika mkutano wa kampeni ulofanyika Wilaya ya Ikungi.[/caption]

[caption id="attachment_61289" align="aligncenter" width="800"]<img class="size-full wp-image-61289" src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2015/08/IMG_00401.jpg" alt="Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhuwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea uliofanyika katika Wilaya ya Ikungi. " width="800" height="463" /> Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhuwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea uliofanyika katika Wilaya ya Ikungi.[/caption]

[caption id="attachment_61290" align="aligncenter" width="800"]<img class="size-full wp-image-61290" src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2015/08/IMG_0048.jpg" alt="Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhuwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea uliofanyika katika Wilaya ya Ikungi. " width="800" height="437" /> Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhuwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea uliofanyika katika Wilaya ya Ikungi.[/caption]

[caption id="attachment_61284" align="aligncenter" width="800"]<img class="size-full wp-image-61284" src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2015/08/IMG_00021.jpg" alt="Mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu akiwahutubia wananchi katika mkutano wa kampeni ulofanyika Wilaya ya Ikungi." width="800" height="383" /> Mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu akiwahutubia wananchi katika mkutano wa kampeni ulofanyika Wilaya ya Ikungi.[/caption]

<strong>MGOMBEA</strong> mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu ameendelea kunadi ilani ya chama chake huku akiahidi ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Ikungi pamoja na ujenzi wa bandari kavu wilayani Manyoni endapo wananchi watakipa ridhaa ya kuunda serikali mara baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, 2015.

Bi. Samia alitoa ahadi hizo jana katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika Kijiji cha Ikungi, wilayani Ikungi ikiwa ni jitihada za serikali ya CCM kuhakikisha inaendelea kuboresha huduma bora za afya kwa wananchi mjini na vijijini.

Alisema serikali watakayoiunda itaendelea kushughulikia kero ya maji katika vijiji vyenye ukame na kuhakikisha kila kijiji kinapata maji safi na salama kwa matumizi, pamoja na kuvipelekea umeme baadhi ya vijiji vya Singida Mashariki ambavyo bado vijafikiwa na huduma kupitia awamu ya pili ya mradi wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA) kuchochea maendeleo vijijini. Alisema katika kuboresha miundombinu wataikarabati barabara ya Mung'aa kwenda Nkiku ili iweze kupitika na kuwasaidia wananchi wanaoitegemea barabara hiyo.

Akihutubia katika mkutano mwingine wa kampeni Wilaya ya Manyoni, Bi, Suluhu aliahidi ujenzi wa bandari kavu eneo hilo ikiwa ni jitihada za kuongeza nafasi za ajira kwa vijana na kukuza uchumi na maendeleo ya wilaya hiyo. Alisema Serikali watakayoiunda itaunda mfuko wa maji ambao utashughulikia kero za huduma za maji safi na salama kwa wakazi wake.

Aidha watahakikisha vijiji ambavyo bado havina mawasiliano vinapata huduma hiyo ili kuchochea maendeleo ya wananchi katika mawasiliano. Bi. Samia amewataka Watanzania kutofanya makosa ya kuvichagua vyama vingine vya upinzani maana havina muelekeo na kuviita vya kuunga unga.

"...Tusifanye mchezo kwa kuvijaribu vyama vya kuungaunga kuingia madarakani, huwezi kufanya majaribio ya kuonja simu...hivi mlisha ona wa

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment