Monday 31 August 2015

Re: [wanabidii] Kweli fedha fedhea, Kaka yangu Mpendazoe leo anaposahau maandishi yake wakati wasomaji hatujasahau

Mama Nkya
Hawa kina elisa na wenzake kama kina mbwambo nahisi ndio walionunuliwa kwa kua ukweli kuhusu Richmlndo ushaanikwa na tena na mawaziri wakuu wawili na wakihitaji zaidi waseme, ushahidi upo lakin kwakua washalishwa na kushiba basi wanakua kama zitto na act yake kua badala ya kuipinga ccm yenye dola unapambana na ukawa isio na doka are a serious political party, au mmehongwa kuja kuharibu mabadiliko, sasa kwa taarifa yenu, mm natembea sana na juz tu niliweza kuzunguka mikoa 5 ya kanda ya nyanda za juu kusini tena vijijn haswaaa, watanzania wengi wanamtaka lowasa hivyo hivyo alivyo awe amekuka pesa sawa, awe ana kashfa sawa, awe anatuhumiwa wanasema sawa, kwakua hakuna msafiiii, magufulo hawamjui na hawamtakiii, hatoweza kubadilisha nchi kwa kua ccm ishachukulia watanzania ni waoga na hawana uthubutu wa kufanya mabadiliko, to tell you the truth vijana wengi sana wamejiandikisha, unajua kwann waje waiathibu ccm kwa kuikataa kwa kuraa
Wanasema wanapewa mikopo hewa, pesa za vijna hawajawahi ona
Kina mama wengi saa wamejiandikisha mnajua kwann wanasema vikatio vyao oct 25 lazima waikate ccm, ishachoka haiwajali wajawazito, watoto na vikongwe
Wasome wengi wamejiandikisha tena kwa fujo,'mnajua kwann, wanasema mikopo wanapata kwa mbinde na kwa kujuana,so watatumia vikatio oct 25
Kundi hiki jingine ni waaakimu hawa wamejiandikisha tena kwahasira wakisema haki zao watapata punde watakapoitoa ccm madarakani
Pole ccm na magufuli safari hii kukalia benji la uoinzani ni ka lazima si hiari bao la mkono ni ngumu kwan kioa kajipanga kukamata penalty ya mguu sembuse bao la mkono
Tchao
Lesian

'ananilea nkya' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

>Elisa,
>Kama ulisoma ile makala yangu iliyokuwa yenye kichwa cha habari LOWASA kafara wa CCM kujaribu kuzuia mabadiliko kwa kudanganya Watanzania kwamba CCM ni safi isipokuwa mchafu ni Lowassa na wenzake wachache utabaini kuwa CCM ilitumia vyama vya upinzani na vyombo vya habari kukamilisha ajenda yake ya kumpakazia Lowassa na kumtoa kafara kwa kutumia ufisadi wa Richmond. Lakini zama hizi ukweli wa Richmond uko wazi--ni ufisadi uliofanya na serikali ya CCM kama serikali hiyo ilivyoshiriki pia kikamilifu katika ufisadi wa Tegeta Escrow mwaka jana 2014 na ufisadi wa EPA 2005. Kwa sasa wananchi wanajua vema kwamba fisadi CCM yenyewe na serikali yake kama taasisi.
>
>Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye kaweka vizuri sana kuhusu CCM na ufisadi wake wakati wa ufunguzi wa kampeni za UKAWA. Hivyo usijisumbue kuweka maandishi ya zamani hapa kuhusu watu waliomkandia Lowassa kuwa ni fisadi wa Richmond. Mpendazoe aliandika hii makala wakati akiwa gizani --wakati wapinzani kwa kutokujua walipokuwa wakiisaidia serikali ya CCM kucheza siasa za maji taka--kumtoa kafara Lowassa kupumbaza umma kuwa CCM siyo chama cha kifisadi bali fisadi ni mtu mmoja tu--Edward Lowassa. Sasa hivi umma umeshaamka-HATUDANGANYIKI. Unaposema Mpendazoe kanunuliwa kwa maoni yangu hata kama Lowassa angekuwa na fedha nyingi kama Bill Gate wa Marekani asingeweza kuwanunua Watanzania wote. Hapo ni haki tu inachukua mkondo wake maana uongo hufa kifo kibaya na ukweli hudumu daima. Tafuta hoja nyingine Lowassa siyo fisadi wa Richmond. Sisi wananchi tumeshaujua ukweli na ukweli humuweka mtu huru.
>
>Ananilea Nkya
E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com
>
>--------------------------------------------
>On Mon, 8/31/15, 'mpombe mtalika' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
>
> Subject: [wanabidii] Kweli fedha fedhea, Kaka yangu Mpendazoe leo anaposahau maandishi yake wakati wasomaji hatujasahau
> To: "ELISA MUHINGO' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
> Date: Monday, August 31, 2015, 9:44 PM
>
>
>
> Hatutaki mgombea urais anayekimbilia
> Ikulu
>
>
> Fred Mpendazoe
>
> Toleo la 402
>
> 22 Apr 2015
>
>  
>
> PLATO alikuwa kati ya wanafalsafa
> muhimu zaidi huko Ugiriki
> ya kale. Plato aliishi kati ya mwaka 427 hadi 447 KK.
> Alikuwa mwanafunzi wa
> Socrates na mwalimu wa Aristotle. Alibuni mawazo mengi
> ambayo yana maana hadi
> leo. Moja ya falsafa ya Plato ni kwamba mafilosofa ndio
> wanaofaa kuwa watawala
> wa nchi, maana wana sifa mbili muhimu. Kwanza wana uwezo wa
> kutawala na pili
> hawapendi kutawala.
>
>
> Ni sheria ya mafilosofa
> kutawala kwa zamu . Na mtu zamu yake
> ya kutawala ikiisha, atafurahi sana kurudia shughuli zake za
> kifalsafa ambazo
> hasa ndizo anazipenda. Hivyo, Plato aliamini kwamba, zipo
> sifa kuu mbili au
> vigezo vya kumpata kiongozi awe rais, mbunge, diwani au
> nafasi yoyote ya
> kuchaguliwa.
>
>
> Sifa ya kwanza ni lazima
> tunayetaka kumpa uongozi awe na
> uwezo wa kuongoza. Na sifa ya pili, mtu huyo sharti awe
> hataki kabisa kuwa
> rais, anatambua kuongoza watu ni utumishi na huyo ndiye watu
> wamfuate,
> wamshauri, wamwombe, ndipo atakuwa kiongozi bora, kwani
> atawaheshimu
> waliomwomba awaongoze. Na ataheshimu na kuiogopa dhamana
> aliyokabidhiwa.
>
>
> Mwalimu Nyerere, katika
> kitabu chake, Uongozi Wetu na Hatma
> ya Tanzania, anasema wanasiasa kwa kawaida hupenda kutawala
> hata kama hawana
> uwezo wa kutawala. Kwa hiyo, wako tayari hata kuhonga ili
> wachaguliwe kuwa
> watawala au wako tayari kuchakachua kura ili watangazwe
> washindi na
> wakishachaguliwa au kutangazwa washindi hawatoki bila
> kulazimishwa.
>
>
> Wanaotaka sana uongozi kwa
> gharama yoyote mara nyingi ni
> wanasiasa ambao hawana uwezo wa kuongoza. Hata hivyo, wapo
> wanasiasa
> wanaoutamani uongozi kisha wakawa viongozi bora, kama
> aliyekuwa Rais wa
> Marekani, hayati John F Kennedy, lakini nitahadharishe kuwa
> watu wa aina hiyo
> ni adimu sana duniani.
>
> Kuna wakati Mwalimu Nyerere
> alikaririwa akisema kwamba
> alikuwa mwalimu taaluma aliyoipenda kwa kuichagua mwenyewe ,
> lakini aliingia
> kwenye siasa kama ajali.
> Hakutaka kuwa rais.
> Ilikuwa ni bahati mbaya kwake.
>
> Katika makala yangu ya tarehe 15 April
> 22015 kwenye gazeti
> la Raia Mwema niliandika juu ya nini nilichoona kilikuwa ni
> chanzo cha nchi
> yetu kuyumba. Imebaki miezi takribani sita watanzania
> watachagua viongozi wao
> akiwemo Rais. Wananchi wana jukumu la kwanza kuhakikisha
> wanapata viongozi
> wazuri.
>
>
> Hivyo ni mhimu wananchi
> waelimishwe ili waweze kuchagua
> viongozi wenye uwezo wa kuongoza na wanaofaa. Katika makala
> hii ninapenda kutoa
> ushauri wangu kwa Watanzania tunapoelekea katika uchaguzi
> mkuu wa mwaka 2015
> sifa muhimu wanazotakiwa wawe nazo wanaofaa kuwa viongozi.
> Ushauri wangu
> unaegemea katika falfasa ya Plato.
>
>
> Watanzania mnashuhudia
> minyukano ya kuwania kuteuliwa
> kugombea nafasi ya urais ndani ya CCM na mbinu chafu
> zinazotumika leo kuelekea
> uchaguzi mkuu mwaka wa Oktoba 2015 ambazo Watanzania
> tunazishudia ni mbinu
> zilezile zilizotumika mwaka 1995 na 2005 na zinatumiwa na
> watu walewale na ni
> chanzo cha CCM kuanguka na taifa letu kuyumba. Wapo wana CCM
> wengi walionyesha nia ya kutaka kuchaguliwa
> kuongoza taifa letu.
>
> Waziri Mkuu aliyejiuzulu,
> Edward Lowassa pia ameonyesha
> nia ya kutaka kugombea urais kupitia CCM. Zipo dalili za
> wazi kwamba CCM
> isingependa kumpitisha Lowassa kutokana na tuhuma za mbinu
> chafu. Wapo
> wanaomtetea kwamba hana tuhuma na wapo wanaoona kwamba
> tuhuma hizo ni za kweli.
> CCM imegawanyika.
>
>
> Mgawanyiko huu umeingia
> hadi nyumba za ibada, vyuo vikuu,
> vyombo vya usalama nakadhalika. CCM nzima imegawanyika.
> Taifa limegawanyika.
> Sababu za kugawanyika kwa Taifa zinatokana na mbinu chafu
> zinazotumika wala si
> kwamba jamii inamhitaji sana Lowassa.
>
>
> Makundi yanayotangaza
> kwamba anafaa na yanayokwenda
> kumshawishi kila mara baadaye yamedhibitika siyo kweli bali
> yametengenezwa na
> yamepewa fedha au yamenunuliwa. Ni ujinga.
>
>
> Ningependa kusisitiza na
> tujiulize kwamba, Lowassa aliwania
> kugombea urais mwaka 1995 lakini akaondolewa na CCM kwa
> tuhuma za kutumia mbinu
> chafu ikiwemo kujilimbikiza mali. Mwaka 2007 akajiuzulu
> Uwaziri Mkuu kwa tuhuma
> za ufisadi. Kwa sasa anataka kugombea tena urais na bado
> anatuhumiwa na chama
> chake kwa kutumia mbinu chafu.
>
>
> Kwa nini mwenzetu huyu,
> Edward Ngoyai Lowassa anataka sana
> kwenda Ikulu kwa gharama yoyote? Tunafahamu uongozi ni
> utumishi. Huwezi
> kung'ang'ania au kulazimisha kuongoza au kuitumikia
> jamii wakati huo huo jamii
> hiyo ina mashaka na uadilifu wako. Haiwezekani. Nyerere
> aliyekaa Ikulu miaka 24 alisema, kwa mtu
> muungwana kabisa Ikulu si pa kukimbilia. Hakuna biashara
> Ikulu.
>
>
> Kwenye makala iliyopita ya
> tarehe 15 April 2015 kwenye Raia
> Mwema nilieleza kwamba kikao cha NEC cha mwaka 1995
> kiliondoa jina la Lowassa
> kwa kuwa alikuwa na tuhuma za rushwa, kujilimbikizia mali na
> kupungukiwa na
> maadili, kinyume na katiba ya CCM na chama hicho kikawateua
> Benjamin William
> Mkapa, Cleopa David Msuya na Jakaya Mrisho Kikwete kuwa
> wagombea.
>
>
> Ukweli kwamba kuna matajiri
> au watu wanaotumia pesa kumiliki
> siasa na uongozi katika nchi yetu, ni jambo lililo wazi.
> Mathalani, kulikuwa na
> matumizi makubwa ya fedha katika uchaguzi mkuu wa mwaka
> 2005.
>
> Baada ya kutangazwa mshindi wa kiti
> cha urais katika
> uchaguzi huo, Rais Jakaya
>
> Mrisho Kikwete, akizindua
> Bunge Desemba 30, 2005,
> alisema: "Yameanza mawazo kuwa uongozi unaweza kununuliwa
> kwa fedha. Tusipokuwa
> waangalifu, nchi yetu inaweza kuwekwa rehani kwa watu wenye
> fedha za kununua
> uongozi au wanaoweza kupata fedha za kufanya hivyo, maana
> unaweza kufadhiliwa
> na mtu ili ununue uongozi, ni vema sasa tulishughulikie
> suala hili".
>
>
> Nchi kuwekwa rehani kwa
> matajiri ni jambo la hatari sana,
> kwa maana serikali itaongozwa na matajiri na haitawajibika
> kwa wananchi.
> Demokrasia itakoma na udikteta utatawala. Jambo
> linalojitokeza hapa na ambalo
> ni matokeo ya matumizi makubwa ya fedha na rushwa kwenye
> chaguzi, ni kupatikana
> kwa viongozi ambao hawakuchaguliwa na wananchi bali
> walinunua uongozi au
> waliotoa rushwa kushawishi wapiga kura wawape uongozi.
>
>
> Pia Mwalimu Nyerere, wakati
> wa uhai wake, aliwahi kuonya juu
> ya hatari ya watu wachache wenye pesa kujaribu kutafuta
> uongozi kwa manufaa
> yao. Alisema: "Tanzania halijawa taifa imara sana na
> adilifu kiasi cha kuruhusu
> matajiri kuingia kwenye uongozi wa nchi kama ilivyo Marekani
> na Ulaya. Wakati
> huo bado uko mbali sana na tukitaka kuuvuta kwa kamba huko
> ndiko kuliingiza
> taifa letu changa kwenye kiwango cha ufisadi kama ilivyo
> sasa.
>
>
> Katika kitabu cha Uongozi
> Wetu na Hatma ya Tanzania, Mwalimu
> J.K Nyerere, alisema hivi: "Utajiri unaweza kupatikana
> kutokana na rushwa kwa
> watumishi wa umma au kutokana na wafanyabiashara ambao
> wanawania nafasi za
> kisiasa ili wawe wadeni wa rais aliyeko madarakani". Maana
> ya maneno haya ni
> kwamba kiongozi akipatikana kwa kupewa fedha na matajiri,
> atapaswa alipe
> fadhila kwa matajiri hao waliokifadhili chama chake au yeye
> mwenyewe wakati wa
> uchaguzi.
>
>
> Serikali inayopatikana kwa
> rushwa haiwajibiki kwa wananchi.
> Hutumikishwa na matajiri walionunua uongozi na waliotoa
> rushwa. Serikali hiyo
> huwaabudu matajiri walioiweka madarakani, haiwezi kufanya
> maamuzi yenye maslahi
> kwa wananchi. Serikali hiyo hulinda maslahi ya watu
> wachache, haiwezi kuchukua
> hatua dhidi ya ufisadi.
>
>
> Hivi karibuni tumeshuhudia
> uteuzi wa hovyo wa wakuu wa
> wilaya, pia siku za nyuma tumeshuhudia kwenye utawala wa
> Kikwete uteuzi wa kushangaza
> wa mawaziri , watendaji wa serikali na taasisi za serikali.
> Uteuzi wa ajabu
> kabisa hadi unajiuliza watoto wetu wanajifunza nini kwa watu
> wa aina hiyo
> wanaopewa dhamana kubwa wakati hawana uwezo na wamepungukiwa
> maadili?
>
>
> Ni bayana walipewa dhamana
> hizo kwa kulipa fadhila kwani
> walikuwa kwenye mtandao uliomwingiza Kikwete madarakani.
> Mtandao wa sasa wa
> Lowassa ni mkubwa kuliko wa mwaka 2005 uliomwingiza Kikwete
> madarakani na fedha
> zinatumika sasa pia ni nyingi kuliko zile zilzotumika mwaka
> 2005. Je Watanzania
> tunategemea nini baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015 ikiwa
> Lowassa atakuwa
> Rais?
>
>
> Hivyo ninashawishika
> kukubaliana na wale wanaotabiri kwamba
> utawala wa Lowassa utakuwa mgumu kuliko wa Kikwete kwani
> utaendeleza yale yale
> ambayo Kikwete ameyafanya, mfano kulipa fadhila kwa
> wanamtandao waliomwingiza
> madarakani bila kujali uwezo wao wa kuongoza.
>
>
> Rais wetu ambaye pia ni
> Mwenyekiti wa CCM anao wajibu na
> nafasi ya kusaidia kutoa ufafanuzi na hatimaye kufikia
> maamuzi ya kuliponya
> taifa letu kama alivyofanya Mwalimu Nyerere. Nyerere
> alipotanguliza utaifa
> kwanza, akasema ukweli na maamuzi sahihi yakafanyika. A
> friend in power is a
> friend lost. Taifa letu kwanza urafiki baadaye. Kikwete
> amshauri Lowassa aache
> kugombea urais kwa ajili ya kuliponya Taifa letu.
>
>
> Madhumuni ya makala hii ni kuendelea
> na ushawishi na ushauri
> wangu nilioutoa katika makala iliyopita kwa kuzingatia
> falfasa ya Plato na
> ushauri wa Mwalimu Nyerere alioutoa kwenye kitabu
> chake.
>
>
> Tunamhitaji Mtanzania ambaye ana uwezo
> wa kuongoza lakini ambaye
> anajua Ikulu ni mahali patakatifu na hakimbilii au
> halazimishi kwenda huko kwa
> kujua ugumu wa kazi hiyo na si kazi ya kuomba kienyeji kwa
> matakwa yake
> binafsi. Tunahitaji mtu mwadilifu wa mkweli siyo kama watia
> nia wengine
> wanavyoigiza kukubalika na jamii na wanatumia uwezo wa
> kifedha kuutafuta urais.
>
>
> Hivyo, ningependa kusisitiza ushauri
> wa Mwalimu Nyerere
> unaozingatia falsafa ya Plato kwamba ni muhimu wananchi
> waelimishwe ili waweze
> kuchagua viongozi wenye uwezo wa kuongoza na wanaofaa na
> wasio na tamaa ya
> kwenda Ikulu kwa kuwahonga watu.
>
>
> Ikulu ni mahali patakatifu na hakuna
> biashara Ikulu bali ni
> mahali pa kuwatumikia watu. Si kila tajiri ana uwezo wa
> kuongoza.
> Chanzo Raia Mwema
> Toleo la 402
>
> 22 Apr 2015
>
>
>
>
>
> --
>
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
>  
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
> kudhibitisha ukishatuma
>
>  
>
> Disclaimer:
>
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
> for any legal consequences of his or her postings, and hence
> statements and facts must be presented responsibly. Your
> continued membership signifies that you agree to this
> disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
> ---
>
> You received this message because you are subscribed to the
> Google Groups "Wanabidii" group.
>
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails
> from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>
> For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
>
>
>--
>Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
>Kujiondoa Tuma Email kwenda
>wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
>Disclaimer:
>Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>---
>You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
>To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment