Sunday 30 August 2015

Re: [wanabidii] Huku Sumaye na Lowassa, kule Mengi na Rostam, tusubiri

Kichwa hiki cha habari kinaonekana kinachochoea ukaburu na ubaguzi.
Ananilea Nkya
 E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com

--------------------------------------------
On Sun, 8/30/15, 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] Huku Sumaye na Lowassa, kule Mengi na Rostam, tusubiri
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Sunday, August 30, 2015, 6:53 AM

Watanzania wameikasirikia
CCM. Wamekasirika na kuweka bifu vifuani mwao. Tuombe kuja
kufika uchaguzi wawe wameamua kuua kunguni wala si kuchoka
kitanda chote. Watakosa pa kulala.
Ni haki
na kweli kuwa mchanganyiko wa Lowasa na Sumaye utakuja
kuleta ya Sudani ya kusini. Yaani ugomvi kati ya Kir na
machari. Hawa wamepatanishwa na nini na lini? Wote walikuwa
CCM. hao wao ndiyo CCM. Wakishatoka CCM basi inabaki CCM
mpya. Lakini kwa umbumbumbu wa wengine wanaweza kuendelea
kuishambulia CCM kumbe CCM iko UKAWA inaendesha uCCM
huko.
Kila mtanzania anatarajia mabadiliko.
Na lazima atayapata. Yanaweza kuletwa na UKAWA (CCM B) au
CCM original. Yani CCM iliyorekebishwa. Tunahitaji
kuwasaidia watanzania kuliona hilo. Bahati nzuri wameanza
kuliona.
--------------------------------------------
On Sun, 8/30/15, 'mpombe mtalika' via
Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
wrote:

Subject:
[wanabidii] Huku Sumaye na Lowassa, kule Mengi na Rostam,
tusubiri
To: "ELISA MUHINGO' via
Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Sunday, August 30, 2015, 7:56 AM



Huku Sumaye na
Lowassa, kule
Mengi na Rostam, tusubiri


AMA kweli Wahenga walisema; ndugu

wakigombana chukua jembe
ukalime,siku
wakipatana chukua kapu ukavune.


Lakini pia upo usemi wa
wanasiasa kote
duniani wa kwamba
katika siasa,hakuna urafiki wala uadui wa
kudumu, bali
kinachoangaliwa zaidi
nimaslahi ya kisiasa!

Historia inashuhudia misemo yote hiyo
miwili kwa sasa
ikitimia
katikakipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa
Oktoba 25, mwaka huu.


Huku tunawaona wanasiasa
wawili
mahasimu, Edward Lowassa na
FrederickSumaye wakiungana na kuwa wamoja,
kule tunawaona
wafanyabiasharawawili
mahasimu, Dk. Reginald Mengi na Rostam Aziz
nao
wakiwawameungana. Tusubiri
tuone huko tuendako!


Wiki iliyopita, Agosti
22,
mwaka huu, waziri mkuu mstaafu,
Sumaye,alitangaza
rasmi
kuachana na Chama cha Mapinduzi
(CCM),
akisemaameamua
kujiunga na Umoja wa Katiba
ya Wananchi (Ukawa), unaoundwa
navyama
vinne vya
siasa nchini vya Chadema, CUF,
NCCR-Mageuzi na NLD kwa lengo
kuongeza
nguvu ya
kisiasa upande wa Upinzani ili
hatimayekupatikane huko chama
chenye nguvu
na
kinachoweza kuaminiwa

naWatanzania.


Niseme mapema hapa kwamba binafsi,
hadi sasa sijui ni

Watanzaniawangapi wanaweza kushawishika na kukiamini
chama
chochote cha

Upinzani katika idadi ya vyama hivi tulivyonavyo
atakachojiunganacho

Sumayeambaye hakuwahi kuaminiwa na Watanzania hao hata
katika miaka yakeyote 10
ya
uwaziri mkuu.


Ninachokikumbuka, huyu ndiye waziri
mkuu
pekee katika
uongozi wakealiyepachikwa jina
la waziri mkuu zero au sifuri
na Watanzania
hao
haopamoja na wachora vikatuni katika
baadhi ya magazeti
yetu.



Ninachoamini bado, kama
alivyosema
Sumaye mwenyewe wakati wa
akitoatamko lake hilo la kuhama CCM wiki
iliyopita, huyu ni
mwanasiasasisimizi
tu katika wanasiasa wa nchi hii!

Ndugu zangu, huko Ukawa
alikokwenda
Sumaye ndiko aliko
aliyekuwahasimu wake mkuu wa kisiasa katika
siasa za ndani
ya CCM,

Lowassa,ambaye alitangaza rasmi kuhamia huko Julai 28,
mwaka
huu, kabla yaumoja

huo kumkabidhi mikoba ya kuwa mgombea pekee wa urais wa
Jamhuriya Muungano wa

Tanzania kwa tiketi ya Ukawa.


Kabla ya wawili hao kuchukua
uamuzi
huo, wakiwa bado makada
wa CCM,wote walijitokeza na kuwa miongoni mwa
makada 38 wa
chama

hichowaliochukua na kurejesha fomu za kuomba kuteuliwa
kuwa
wagombea waurais

katika uchaguzi wa mwaka huu.

Hata hivyo, kutokana na haiba yao ya
kisiasa ndani na nje ya
CCM,
wotewawili hao majina yao yalikatwa katika hatua za
mwanzo kabisa, wala hayakuingia
hata ndani ya kikao cha Kamati Kuu
kujadiliwa!


Kwa yeyote anayefuatilia siasa za
ndani ya CCM, anafahamu

kwambaLowassa na Sumaye, walikuwa hawaivi kisiasa. Mara
kadhaa,
Sumayeamejiapiza
mbele ya chama chake na mbele ya waliokuwa

wanachamawenzake,
akisema endapo CCM
ingemteua Lowassa kuwa mgombea wa

urais,basi yeye
angejitenga na chama
hicho.



Kama ambavyo karibu viongozi wakuu
wote wa
Chadema na kambi
yaupinzani kwa ujumla
ilivyokuwa ikimtuhumu Lowassa kwamba
ni
fisadiasiyestahili kukabidhiwa madaraka ya juu
ya kuongoza
nchi, ndivyo pia
Sumaye alivyokuwa akimnanga Lowassa kila
anapopata fursa
yakuzungumzia masuala
ya rushwa na ufisadi.

Kwa mfano, Novemba 2013, katika
mkutano mmoja na waandishi
wa
habari,Sumaye alilalamika kuhujumiwa na watu aliodai kuwa
mahasimu wake
wakisiasa
katika mbio za urais za mwaka 2015, hasa kwa
kuingilia katimialiko
yake ya
kijamii anayoipata ili kuwa mgeni rasmi.



Malalamiko hayo ni mbali
na yale
aliyoyatoa mwaka 2012 baada
yakushindwa katika nafasi ya Mjumbe wa
Halmashauri Kuu (NEC)
Taifakuwakilisha
Wilaya ya Hannang, mkoani Manyara, akisema
wazi kuwa
baadhiya mafisadi wa ndani
ya CCM, walitumia fedha nyingi kuhakikisha
kwambamshindani
wake, Dk. Mary Nagu,
anamwangusha.


"Siwataji, hata ninyi
mnawajua,"
aliwahi kukaririwa Sumaye
baada yakutakiwa na wandishi wa habari
kuwataja mafisadi
wanaomjumu
kwenyemialiko yake ya shughuli za kijamii
pamoja na kumwaga
fedha wilayanikwake
ili ashindwe ujumbe wa NEC.



Wakati fulani pia, mbele
ya wandishi
wa habari, Sumaye, bila
kutajajina la Lowassa, aliwahi kukaririwa
akisema: "Fisadi
huliibia taifafedha
nyingi kiasi cha wananchi kutaabika, halafu
akiitwa
kwenyeharambee anatoa
kijisehemu tu cha fedha alizofisadi kwa njia
ya
rushwakukandamiza maendeleo ya
watu.


"Rais Kikwete amesema kuwa rushwa
inaweza ikafanya CCM

ikashindwa.

Mimi naamini,
kama CCM itapitisha
majina (ya wagombea
wake
wa urais2015) kwa kuangalia rushwa,
chama kitaanguka, bahati
nzuri
Mwenyekitiameliona hilo, siamini kama
watapitisha watu ambao
watakiangusha.



Wakipitishwa hao, sitaweza kukaa nao,
hata
kama sitahama."

Hizo ni
baadhi tu ya nukuu za Sumaye
katika matukio
na
nyakatimbalimbali akizungumzia msimamo
wake kuhusu rushwa na
mafisadi,
lakininyingi ya kauli zake hizo, kwa vyovyote
vile
akizielekeza kwa Lowassa.


Hata
hivyo, Sumaye huyu wa sasa,
aliyeamua
kumfuata Lowassa
Ukawa,amekaririwa na
baadhi ya vyombo vya habari nchini
katika
tukio hilo
lawiki iliyopita akisema:
"Ambaye ameshakaa serikalini
katika
nafasi mbalimbali
ni Lowassa. Hawa wengine
(aliogombea nao urais ndani yaCCM)

hawajaendesha
Serikali, wamekwenda shule
tu."

Kwamba Lowassa
ambaye siku zote Sumaye
alikuwa
akikiaminisha
chamachake, CCM, kwamba ni
fisadi na mtoa rushwa mkubwa,
akisema
kama
CCMitampitisha mwanasiasa huyo
kugombea urais, yeye hatakuwa
sehemu
yachama
hicho, leo hii ndiye tunayeambiwa
na Sumaye kwamba
alikuwaanafaa kuteuliwa
kwa
sababu tu amekwishashika nafasi
mbalimbali

serikalini,
anafahamu kuendesha
Serikali!


Huyo ni
Sumaye na Lowassa, wanasiasa
ambao huko
nyuma
walikuwa katikamkoa mmoja wa Arusha,
wakiwa na uhasama
mkubwa wa kisiasa,
kabla
yaMkoa huo kugawanywa na kupatikana
mkoa mwingine wa
Manyarauliowatenganisha
kiutawala.



Katikati ya mshangao huo wa Sumaye na
Lowassa, katika
kipindi
hikihiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2015,
tunawaona pia mahasimu

wawiliwa kibiashara hapa nchini, Dk. Mengi na Rostam Aziz
wakiweka tofautizao
za muda
mrefu pembeni na kuungana kumtafuta mgombea wao wa
uraismwaka huu.


Kwa wenye kumbukumbu na
wanaofuatilia
matukio mbalimbali
yanayoendelea nchini watakuwa wanakumbuka
tukio la Mei 26,
mwaka huu, siku
ambayo wafanyabiashara wawili hao maarufu
nchini walivyokaa
mezakuu moja. Hilo
lilikuwa tukio la kutano wa wamiliki wa vyombo
binafsi
vyahabari nchini,

kupitia umoja wao wa MOAT na waandishi wa vyombo vya
habari
vya ndani na nje,

uliolenga kuzungumzia, pamoja na mambo mengine, hisia za
MOAT kuhusu miswada
miwili
iliyokuwa ikitazamiwa kuwasilishwa na Serikali
bungeni ili kuwa sheria

kamili. Muswada wa Huduma za Vyombo vya Habari pamoja na
Muswada wa Haki ya

KupataHabari.


Swali kuu lililotawala vichwani mwa
baadhi ya wadadisi wa

mambowalioshuhudia tukio lile la Mei 26, 2015, la Dk.
Mengi
na

Rostamkukumbatiana na kukaa meza moja, lilikuwa ni, je;
miswada hiyo miwiliya

Serikali ndiyo iliyowaleta pamoja wafanyabiashara hao
wawili
maarufu katika
nchi
hii au ni Uchaguzi Mkuu wa Oktoba na vitalu vya gesi
asilia na mafuta?


Kwanini swali hilo?
Itakumbukwa kwamba
Aprili 23, 2009, Dk
Mengi, ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji wa
Makampuni ya IPP,
alitaja kwa majina
wafanyabiashara watano akiwatuhumu kuwa
mafisadi papa hatari
kwa uchumi wa
Taifa hili, miongoni mwa mafisadi wasiopungua
10 aliodai
kuuyumbisha utawala wa
Rais Jakaya Kikwete.


Katika madai yake hayo, Dk.
Mengi
alikaririwa na baadhi ya
vyombo vya habari nchini akisema: "Nchi hii
ina mafisadi
ambao kila kukicha
wanaiyumbisha nchi. Hawazidi hata kumi. Lakini
kuna watano
ambao ni mafisadi
papa. Ukitokea kupingana nao tu kutokana na
ufisadi wao,
wanakuona wewe ni adui
mkubwa."


Dk Mengi, siku hiyo akiwa kwenye
mkutano
mkubwa na vyombo
vya habari, alitaja majina
ya mafisadi papa hao watano,
wakiongozwa na
Rostam
Aziz na wengine wanne ambao sina
sababu ya kuwataja
hapa.



Baada ya kutaja orodha
hiyo ya
wafanyabiashara mafisadi
papa, Dk. Mengi alieleweka vyema kwa
Watanzania, hasa wale
waliokuwa
wakimwamini na kumkubali kutokana na msimamo
wake wa
'uzalendo' na 'utetezi wa
wazawa.'


Wakati Watanzania hao wakiendelea

kutafakari orodha hiyo ya
mafisadi papa
pamoja na matendo yao kwa Taifa hili, siku 10
baadaye, yaani Mei
2, 2009,
Rostam Aziz naye aliitisha mkutano mkubwa pia wa
waandishi vyombo
mbalimbali
vya habari vya ndani na nje na kumrushia

makombora mazito Mwenyekiti
Mtendaji huyo
wa IPP.



Dk Mengi alitajwa na Rostam Aziz
kwamba
yeye ndiye fisadi
mkubwa ndani ya nchi hii,
akimfananisha na fisadi nyangumi.
Rostam
alikwenda
mbali zaidi, akidai kuwa na
vielelezo kibao ambavyo
angeviwakilisha
mikononi
mwa Jeshi la Polisi ili waanze
kumchunguza dhidi ya vitendo
vyake hivyo
vya
kifisadi nyangumi.


Katika kipindi hicho cha
misuguano
baina ya wafanyabiashara
hao wawili, kiasi cha kupachikana majina ya
mafisadi papa na
mafisadi nyangumi,
Rostam alikuwa bado ni Mbunge wa Igunga na pia
Mjumbe wa
Kamati Kuu na

Halmashauri Kuu ya CCM.



Takriban miaka mitatu

baadaye, baada ya Rostam Aziz kudaiwa
na
Dk.Mengi kwamba amekuwa akishiriki katika vitendo
vinavyoiyumbisha nchi hii,

kwa maana ya Julai 13, 2011, mwanasiasa huyo aliamua
kujiuzulu ubunge huo wa

Igunga pamoja na nyadhifa nyingine zote hizo alizokuwa
nazo
ndani ya CCM,
akidai
kuwa dhamira yake ya dhati kabisa imemtuma


aachane na siasa uchwara za ndani ya
chama chake hicho ili
sasa
aweze kutumia muda wake kushughulika na biashara
zake.


Je, uhusiano huu mpya wa Dk Mengi na
Rostam Aziz,
uliowafanya
wazike tofauti zao na uhasama wao na kwa pamoja
kuamua kumuunga
mkono kisiasa
Lowassa katika mbio zake za kuusaka urais,

unabeba siri gani?


Nihitimishe makala haya kwa
kuwakumbusha
Watanzania kwa
ujumla wa imani zote, kwamba
katika Biblia (Mathayo 7:6,
12-14),
imeandikwa
hivi: "Msimpe mbwa kilicho
kitakatifu, wala msiwape
nguruwe lulu zenu
wasije
wakawakanyaga, wakawageuka na
kuwararua."


Ikulu ni mahali patakatifu, watu wasio
wasafi si mahali pao.
Gesi
asilia na mafuta yaliyopatikana Mtwara pamoja na maeneo
mengine ya nchi
hii, Bara na
Visiwani, ni lulu ya uchumi wa nchi hii, ambayo
kamwe Watanzania
hawawezi
kuitoa lulu yao hiyo na kuwakabidhi wasiofaa!
Tutafakari sasa na hata

Oktoba 25.

Chanzo
RaiaMwema

Toleo la 420,28
Aug 2015





--

Send
Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda


wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:


Everyone posting to this Forum bears the sole
responsibility
for any legal consequences
of his or her postings, and hence

statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree
to this
disclaimer and pledge to abide by
our Rules and Guidelines.


---

You received this
message because you are subscribed to the

Google Groups "Wanabidii" group.


To unsubscribe from this group and stop
receiving emails
from it, send an email to
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.


--
Send
Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to
this Forum bears the sole responsibility for any legal
consequences of his or her postings, and hence statements
and facts must be presented responsibly. Your continued
membership signifies that you agree to this disclaimer and
pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message
because you are subscribed to the Google Groups
"Wanabidii" group.
To unsubscribe
from this group and stop receiving emails from it, send an
email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment