Monday 31 August 2015

Re: [wanabidii] Kweli fedha fedhea, Kaka yangu Mpendazoe leo anaposahau maandishi yake wakati wasomaji hatujasahau

Mtalika hizi ndizo habari zinazokukosha sana moyo wako, umemuona Loasa tu ndiye anayetaka kwa hali na mali ikulu, hebu tafuta kwenye habari za hivi karibuni, pale kiongozi aliposimama jukwaani na kukemea kauli zinzochochea uhasama. Nani ya hotuba hiyo kuna maneno "CCMtumejipanga kushinda na tutahakikisha tumeshinda" Kauli hiyo ime kakaaje, kwako haionyeshiwa imshatoa matokeo ya uchaguzi hata kabla ya mabox ya kura hayajategenezwa?


On Monday, 31 August 2015, 22:21, 'ananilea nkya' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:


Elisa,
Kama ulisoma ile makala yangu iliyokuwa yenye kichwa cha habari LOWASA kafara wa CCM kujaribu kuzuia mabadiliko kwa  kudanganya Watanzania  kwamba CCM ni safi isipokuwa mchafu ni  Lowassa na wenzake wachache utabaini kuwa  CCM ilitumia vyama vya upinzani na vyombo vya habari kukamilisha ajenda yake ya kumpakazia Lowassa na kumtoa kafara kwa kutumia  ufisadi wa Richmond. Lakini zama hizi ukweli wa Richmond uko wazi--ni ufisadi uliofanya na serikali ya CCM  kama serikali hiyo ilivyoshiriki pia kikamilifu katika ufisadi wa Tegeta Escrow mwaka jana 2014  na ufisadi wa EPA 2005.  Kwa sasa wananchi wanajua vema kwamba fisadi CCM yenyewe na serikali yake kama taasisi. 

Waziri Mkuu Mstaafu  Fredrick Sumaye kaweka vizuri sana  kuhusu CCM  na ufisadi wake wakati wa ufunguzi wa kampeni za UKAWA.  Hivyo usijisumbue  kuweka maandishi ya zamani hapa  kuhusu watu waliomkandia Lowassa kuwa ni fisadi wa Richmond. Mpendazoe  aliandika hii makala wakati akiwa gizani --wakati wapinzani kwa kutokujua walipokuwa  wakiisaidia serikali ya CCM kucheza siasa za maji taka--kumtoa kafara Lowassa kupumbaza umma kuwa CCM siyo chama cha kifisadi bali fisadi ni mtu mmoja tu--Edward Lowassa.  Sasa hivi umma  umeshaamka-HATUDANGANYIKI. Unaposema Mpendazoe kanunuliwa  kwa maoni yangu hata kama  Lowassa  angekuwa na fedha nyingi kama Bill Gate wa Marekani  asingeweza kuwanunua Watanzania wote. Hapo ni haki tu inachukua mkondo wake maana uongo hufa kifo kibaya na ukweli hudumu daima.  Tafuta hoja nyingine Lowassa siyo fisadi wa Richmond. Sisi wananchi tumeshaujua ukweli na ukweli humuweka mtu huru. 

Ananilea Nkya
 E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com

--------------------------------------------
On Mon, 8/31/15, 'mpombe mtalika' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: [wanabidii] Kweli fedha fedhea, Kaka yangu Mpendazoe leo anaposahau maandishi yake wakati wasomaji hatujasahau
To: "ELISA MUHINGO' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Monday, August 31, 2015, 9:44 PM



Hatutaki mgombea urais anayekimbilia
Ikulu


Fred Mpendazoe

Toleo la 402

22 Apr 2015

 

PLATO alikuwa kati ya wanafalsafa
muhimu zaidi huko Ugiriki
ya kale. Plato aliishi kati ya mwaka 427 hadi 447 KK.
Alikuwa mwanafunzi wa
Socrates na mwalimu wa Aristotle. Alibuni mawazo mengi
ambayo yana maana hadi
leo. Moja ya falsafa ya Plato ni kwamba mafilosofa ndio
wanaofaa kuwa watawala
wa nchi, maana wana sifa mbili muhimu. Kwanza wana uwezo wa
kutawala na pili
hawapendi kutawala.


Ni sheria ya mafilosofa
kutawala kwa zamu . Na mtu zamu yake
ya kutawala ikiisha, atafurahi sana kurudia shughuli zake za
kifalsafa ambazo
hasa ndizo anazipenda. Hivyo, Plato aliamini kwamba, zipo
sifa kuu mbili au
vigezo vya kumpata kiongozi awe rais, mbunge, diwani au
nafasi yoyote ya
kuchaguliwa.


Sifa ya kwanza ni lazima
tunayetaka kumpa uongozi awe na
uwezo wa kuongoza. Na sifa ya pili, mtu huyo sharti awe
hataki kabisa kuwa
rais, anatambua kuongoza watu ni utumishi na huyo ndiye watu
wamfuate,
wamshauri, wamwombe, ndipo atakuwa kiongozi bora, kwani
atawaheshimu
waliomwomba awaongoze. Na ataheshimu na kuiogopa dhamana
aliyokabidhiwa.


Mwalimu Nyerere, katika
kitabu chake, Uongozi Wetu na Hatma
ya Tanzania, anasema wanasiasa kwa kawaida hupenda kutawala
hata kama hawana
uwezo wa kutawala. Kwa hiyo, wako tayari hata kuhonga ili
wachaguliwe kuwa
watawala au wako tayari kuchakachua kura ili watangazwe
washindi na
wakishachaguliwa au kutangazwa washindi hawatoki bila
kulazimishwa.


Wanaotaka sana uongozi kwa
gharama yoyote mara nyingi ni
wanasiasa ambao hawana uwezo wa kuongoza. Hata hivyo, wapo
wanasiasa
wanaoutamani uongozi kisha wakawa viongozi bora, kama
aliyekuwa Rais wa
Marekani, hayati John F Kennedy, lakini nitahadharishe kuwa
watu wa aina hiyo
ni adimu sana duniani.

Kuna wakati Mwalimu Nyerere
alikaririwa akisema kwamba
alikuwa mwalimu taaluma aliyoipenda kwa kuichagua mwenyewe ,
lakini aliingia
kwenye siasa kama ajali.
  Hakutaka kuwa rais.
Ilikuwa ni bahati mbaya kwake.

Katika makala yangu ya tarehe 15 April
22015 kwenye gazeti
la Raia Mwema niliandika juu ya nini nilichoona kilikuwa ni
chanzo cha nchi
yetu kuyumba. Imebaki miezi takribani sita watanzania
watachagua viongozi wao
akiwemo Rais. Wananchi wana jukumu la kwanza kuhakikisha
wanapata viongozi
wazuri.


Hivyo ni mhimu wananchi
waelimishwe ili waweze kuchagua
viongozi wenye uwezo wa kuongoza na wanaofaa. Katika makala
hii ninapenda kutoa
ushauri wangu kwa Watanzania tunapoelekea katika uchaguzi
mkuu wa mwaka 2015
sifa muhimu wanazotakiwa wawe nazo wanaofaa kuwa viongozi.
Ushauri wangu
unaegemea katika falfasa ya Plato.


Watanzania mnashuhudia
minyukano ya kuwania kuteuliwa
kugombea nafasi ya urais ndani ya CCM na mbinu chafu
zinazotumika leo kuelekea
uchaguzi mkuu mwaka wa Oktoba 2015 ambazo Watanzania
tunazishudia ni mbinu
zilezile zilizotumika mwaka 1995 na 2005 na zinatumiwa na
watu walewale na ni
chanzo cha CCM kuanguka na taifa letu kuyumba. Wapo wana CCM
wengi walionyesha nia ya kutaka kuchaguliwa
kuongoza taifa letu.

Waziri Mkuu aliyejiuzulu,
Edward Lowassa pia ameonyesha
nia ya kutaka kugombea urais kupitia CCM. Zipo dalili za
wazi kwamba CCM
isingependa kumpitisha Lowassa kutokana na tuhuma za mbinu
chafu. Wapo
wanaomtetea kwamba hana tuhuma na wapo wanaoona kwamba
tuhuma hizo ni za kweli.
CCM imegawanyika.


Mgawanyiko huu umeingia
hadi nyumba za ibada, vyuo vikuu,
vyombo vya usalama nakadhalika. CCM nzima imegawanyika.
Taifa limegawanyika.
Sababu za kugawanyika kwa Taifa zinatokana na mbinu chafu
zinazotumika wala si
kwamba jamii inamhitaji sana Lowassa.


Makundi yanayotangaza
kwamba anafaa na yanayokwenda
kumshawishi kila mara baadaye yamedhibitika siyo kweli bali
yametengenezwa na
yamepewa fedha au yamenunuliwa. Ni ujinga.


Ningependa kusisitiza na
tujiulize kwamba, Lowassa aliwania
kugombea urais mwaka 1995 lakini akaondolewa na CCM kwa
tuhuma za kutumia mbinu
chafu ikiwemo kujilimbikiza mali. Mwaka 2007 akajiuzulu
Uwaziri Mkuu kwa tuhuma
za ufisadi. Kwa sasa anataka kugombea tena urais na bado
anatuhumiwa na chama
chake kwa kutumia mbinu chafu.


Kwa nini mwenzetu huyu,
Edward Ngoyai Lowassa anataka sana
kwenda Ikulu kwa gharama yoyote? Tunafahamu uongozi ni
utumishi. Huwezi
kung'ang'ania au kulazimisha kuongoza au kuitumikia
jamii wakati huo huo jamii
hiyo ina mashaka na uadilifu wako. Haiwezekani. Nyerere
aliyekaa Ikulu miaka 24 alisema, kwa mtu
muungwana kabisa Ikulu si pa kukimbilia. Hakuna biashara
Ikulu.


Kwenye makala iliyopita ya
tarehe 15 April 2015 kwenye Raia
Mwema nilieleza kwamba kikao cha NEC cha mwaka 1995
kiliondoa jina la Lowassa
kwa kuwa alikuwa na tuhuma za rushwa, kujilimbikizia mali na
kupungukiwa na
maadili, kinyume na katiba ya CCM na chama hicho kikawateua
Benjamin William
Mkapa, Cleopa David Msuya na Jakaya Mrisho Kikwete kuwa
wagombea.


Ukweli kwamba kuna matajiri
au watu wanaotumia pesa kumiliki
siasa na uongozi katika nchi yetu, ni jambo lililo wazi.
Mathalani, kulikuwa na
matumizi makubwa ya fedha katika uchaguzi mkuu wa mwaka
2005.

Baada ya kutangazwa mshindi wa kiti
cha urais katika
uchaguzi huo, Rais Jakaya

Mrisho Kikwete, akizindua
Bunge Desemba 30, 2005,
alisema: "Yameanza mawazo kuwa uongozi unaweza kununuliwa
kwa fedha. Tusipokuwa
waangalifu, nchi yetu inaweza kuwekwa rehani kwa watu wenye
fedha za kununua
uongozi au wanaoweza kupata fedha za kufanya hivyo, maana
unaweza kufadhiliwa
na mtu ili ununue uongozi, ni vema sasa tulishughulikie
suala hili".


Nchi kuwekwa rehani kwa
matajiri ni jambo la hatari sana,
kwa maana serikali itaongozwa na matajiri na haitawajibika
kwa wananchi.
Demokrasia itakoma na udikteta utatawala. Jambo
linalojitokeza hapa na ambalo
ni matokeo ya matumizi makubwa ya fedha na rushwa kwenye
chaguzi, ni kupatikana
kwa viongozi ambao hawakuchaguliwa na wananchi bali
walinunua uongozi au
waliotoa rushwa kushawishi wapiga kura wawape uongozi.


Pia Mwalimu Nyerere, wakati
wa uhai wake, aliwahi kuonya juu
ya hatari ya watu wachache wenye pesa kujaribu kutafuta
uongozi kwa manufaa
yao. Alisema: "Tanzania halijawa taifa imara sana na
adilifu kiasi cha kuruhusu
matajiri kuingia kwenye uongozi wa nchi kama ilivyo Marekani
na Ulaya. Wakati
huo bado uko mbali sana na tukitaka kuuvuta kwa kamba huko
ndiko kuliingiza
taifa letu changa kwenye kiwango cha ufisadi kama ilivyo
sasa.


Katika kitabu cha Uongozi
Wetu na Hatma ya Tanzania, Mwalimu
J.K Nyerere, alisema hivi: "Utajiri unaweza kupatikana
kutokana na rushwa kwa
watumishi wa umma au kutokana na wafanyabiashara ambao
wanawania nafasi za
kisiasa ili wawe wadeni wa rais aliyeko madarakani". Maana
ya maneno haya ni
kwamba kiongozi akipatikana kwa kupewa fedha na matajiri,
atapaswa alipe
fadhila kwa matajiri hao waliokifadhili chama chake au yeye
mwenyewe wakati wa
uchaguzi.


Serikali inayopatikana kwa
rushwa haiwajibiki kwa wananchi.
Hutumikishwa na matajiri walionunua uongozi na waliotoa
rushwa. Serikali hiyo
huwaabudu matajiri walioiweka madarakani, haiwezi kufanya
maamuzi yenye maslahi
kwa wananchi. Serikali hiyo hulinda maslahi ya watu
wachache, haiwezi kuchukua
hatua dhidi ya ufisadi.


Hivi karibuni tumeshuhudia
uteuzi wa hovyo wa wakuu wa
wilaya, pia siku za nyuma tumeshuhudia kwenye utawala wa
Kikwete uteuzi wa kushangaza
wa mawaziri , watendaji wa serikali na taasisi za serikali.
Uteuzi wa ajabu
kabisa hadi unajiuliza watoto wetu wanajifunza nini kwa watu
wa aina hiyo
wanaopewa dhamana kubwa wakati hawana uwezo na wamepungukiwa
maadili?


Ni bayana walipewa dhamana
hizo kwa kulipa fadhila kwani
walikuwa kwenye mtandao uliomwingiza Kikwete madarakani.
Mtandao wa sasa wa
Lowassa ni mkubwa kuliko wa mwaka 2005 uliomwingiza Kikwete
madarakani na fedha
zinatumika sasa pia ni nyingi kuliko zile zilzotumika mwaka
2005. Je Watanzania
tunategemea nini baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015 ikiwa
Lowassa atakuwa
Rais?


Hivyo ninashawishika
kukubaliana na wale wanaotabiri kwamba
utawala wa Lowassa utakuwa mgumu kuliko wa Kikwete kwani
utaendeleza yale yale
ambayo Kikwete ameyafanya, mfano kulipa fadhila kwa
wanamtandao waliomwingiza
madarakani bila kujali uwezo wao wa kuongoza.


Rais wetu ambaye pia ni
Mwenyekiti wa CCM anao wajibu na
nafasi ya kusaidia kutoa ufafanuzi na hatimaye kufikia
maamuzi ya kuliponya
taifa letu kama alivyofanya Mwalimu Nyerere. Nyerere
alipotanguliza utaifa
kwanza, akasema ukweli na maamuzi sahihi yakafanyika. A
friend in power is a
friend lost. Taifa letu kwanza urafiki baadaye. Kikwete
amshauri Lowassa aache
kugombea urais kwa ajili ya kuliponya Taifa letu.


Madhumuni ya makala hii ni kuendelea
na ushawishi na ushauri
wangu nilioutoa katika makala iliyopita kwa kuzingatia
falfasa ya Plato na
ushauri wa Mwalimu Nyerere alioutoa kwenye kitabu
chake.


Tunamhitaji Mtanzania ambaye ana uwezo
wa kuongoza lakini ambaye
anajua Ikulu ni mahali patakatifu na hakimbilii au
halazimishi kwenda huko kwa
kujua ugumu wa kazi hiyo na si kazi ya kuomba kienyeji kwa
matakwa yake
binafsi. Tunahitaji mtu mwadilifu wa mkweli siyo kama watia
nia wengine
wanavyoigiza kukubalika na jamii na wanatumia uwezo wa
kifedha kuutafuta urais.


Hivyo, ningependa kusisitiza ushauri
wa Mwalimu Nyerere
unaozingatia falsafa ya Plato kwamba ni muhimu wananchi
waelimishwe ili waweze
kuchagua viongozi wenye uwezo wa kuongoza na wanaofaa na
wasio na tamaa ya
kwenda Ikulu kwa kuwahonga watu.


Ikulu ni mahali patakatifu na hakuna
biashara Ikulu bali ni
mahali pa kuwatumikia watu. Si kila tajiri ana uwezo wa
kuongoza.
Chanzo Raia Mwema
Toleo la 402

22 Apr 2015





--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.



--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


0 comments:

Post a Comment