Saturday 29 August 2015

Re: [wanabidii] Huku Sumaye na Lowassa, kule Mengi na Rostam, tusubiri

Watanzania wameikasirikia CCM. Wamekasirika na kuweka bifu vifuani mwao. Tuombe kuja kufika uchaguzi wawe wameamua kuua kunguni wala si kuchoka kitanda chote. Watakosa pa kulala.
Ni haki na kweli kuwa mchanganyiko wa Lowasa na Sumaye utakuja kuleta ya Sudani ya kusini. Yaani ugomvi kati ya Kir na machari. Hawa wamepatanishwa na nini na lini? Wote walikuwa CCM. hao wao ndiyo CCM. Wakishatoka CCM basi inabaki CCM mpya. Lakini kwa umbumbumbu wa wengine wanaweza kuendelea kuishambulia CCM kumbe CCM iko UKAWA inaendesha uCCM huko.
Kila mtanzania anatarajia mabadiliko. Na lazima atayapata. Yanaweza kuletwa na UKAWA (CCM B) au CCM original. Yani CCM iliyorekebishwa. Tunahitaji kuwasaidia watanzania kuliona hilo. Bahati nzuri wameanza kuliona.
--------------------------------------------
On Sun, 8/30/15, 'mpombe mtalika' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: [wanabidii] Huku Sumaye na Lowassa, kule Mengi na Rostam, tusubiri
To: "ELISA MUHINGO' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Sunday, August 30, 2015, 7:56 AM



Huku Sumaye na
Lowassa, kule Mengi na Rostam, tusubiri

AMA kweli Wahenga walisema; ndugu
wakigombana chukua jembe
ukalime,siku wakipatana chukua kapu ukavune.


Lakini pia upo usemi wa wanasiasa kote
duniani wa kwamba
katika siasa,hakuna urafiki wala uadui wa kudumu, bali
kinachoangaliwa zaidi
nimaslahi ya kisiasa!

Historia inashuhudia misemo yote hiyo
miwili kwa sasa
ikitimia katikakipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa
Oktoba 25, mwaka huu.


Huku tunawaona wanasiasa wawili
mahasimu, Edward Lowassa na
FrederickSumaye wakiungana na kuwa wamoja, kule tunawaona
wafanyabiasharawawili
mahasimu, Dk. Reginald Mengi na Rostam Aziz nao
wakiwawameungana. Tusubiri
tuone huko tuendako!


Wiki iliyopita, Agosti 22,
mwaka huu, waziri mkuu mstaafu,
Sumaye,alitangaza
rasmi kuachana na Chama cha Mapinduzi
(CCM), akisemaameamua
kujiunga na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), unaoundwa
navyama vinne vya
siasa nchini vya Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD kwa lengo
kuongeza nguvu ya
kisiasa upande wa Upinzani ili hatimayekupatikane huko chama
chenye nguvu na
kinachoweza kuaminiwa
naWatanzania.


Niseme mapema hapa kwamba binafsi,
hadi sasa sijui ni
Watanzaniawangapi wanaweza kushawishika na kukiamini chama
chochote cha
Upinzani katika idadi ya vyama hivi tulivyonavyo
atakachojiunganacho
Sumayeambaye hakuwahi kuaminiwa na Watanzania hao hata
katika miaka yakeyote 10
ya uwaziri mkuu.

Ninachokikumbuka, huyu ndiye waziri
mkuu pekee katika
uongozi wakealiyepachikwa jina la waziri mkuu zero au sifuri
na Watanzania hao
haopamoja na wachora vikatuni katika baadhi ya magazeti
yetu.


Ninachoamini bado, kama alivyosema
Sumaye mwenyewe wakati wa
akitoatamko lake hilo la kuhama CCM wiki iliyopita, huyu ni
mwanasiasasisimizi
tu katika wanasiasa wa nchi hii!

Ndugu zangu, huko Ukawa alikokwenda
Sumaye ndiko aliko
aliyekuwahasimu wake mkuu wa kisiasa katika siasa za ndani
ya CCM,
Lowassa,ambaye alitangaza rasmi kuhamia huko Julai 28, mwaka
huu, kabla yaumoja
huo kumkabidhi mikoba ya kuwa mgombea pekee wa urais wa
Jamhuriya Muungano wa
Tanzania kwa tiketi ya Ukawa.


Kabla ya wawili hao kuchukua uamuzi
huo, wakiwa bado makada
wa CCM,wote walijitokeza na kuwa miongoni mwa makada 38 wa
chama
hichowaliochukua na kurejesha fomu za kuomba kuteuliwa kuwa
wagombea waurais
katika uchaguzi wa mwaka huu.

Hata hivyo, kutokana na haiba yao ya
kisiasa ndani na nje ya
CCM, wotewawili hao majina yao yalikatwa katika hatua za
mwanzo kabisa, wala hayakuingia
hata ndani ya kikao cha Kamati Kuu kujadiliwa!


Kwa yeyote anayefuatilia siasa za
ndani ya CCM, anafahamu
kwambaLowassa na Sumaye, walikuwa hawaivi kisiasa. Mara
kadhaa,
Sumayeamejiapiza mbele ya chama chake na mbele ya waliokuwa
wanachamawenzake,
akisema endapo CCM ingemteua Lowassa kuwa mgombea wa
urais,basi yeye
angejitenga na chama hicho.


Kama ambavyo karibu viongozi wakuu
wote wa Chadema na kambi
yaupinzani kwa ujumla ilivyokuwa ikimtuhumu Lowassa kwamba
ni
fisadiasiyestahili kukabidhiwa madaraka ya juu ya kuongoza
nchi, ndivyo pia
Sumaye alivyokuwa akimnanga Lowassa kila anapopata fursa
yakuzungumzia masuala
ya rushwa na ufisadi.

Kwa mfano, Novemba 2013, katika
mkutano mmoja na waandishi
wa habari,Sumaye alilalamika kuhujumiwa na watu aliodai kuwa
mahasimu wake
wakisiasa katika mbio za urais za mwaka 2015, hasa kwa
kuingilia katimialiko
yake ya kijamii anayoipata ili kuwa mgeni rasmi.


Malalamiko hayo ni mbali na yale
aliyoyatoa mwaka 2012 baada
yakushindwa katika nafasi ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC)
Taifakuwakilisha
Wilaya ya Hannang, mkoani Manyara, akisema wazi kuwa
baadhiya mafisadi wa ndani
ya CCM, walitumia fedha nyingi kuhakikisha kwambamshindani
wake, Dk. Mary Nagu,
anamwangusha.


"Siwataji, hata ninyi mnawajua,"
aliwahi kukaririwa Sumaye
baada yakutakiwa na wandishi wa habari kuwataja mafisadi
wanaomjumu
kwenyemialiko yake ya shughuli za kijamii pamoja na kumwaga
fedha wilayanikwake
ili ashindwe ujumbe wa NEC.


Wakati fulani pia, mbele ya wandishi
wa habari, Sumaye, bila
kutajajina la Lowassa, aliwahi kukaririwa akisema: "Fisadi
huliibia taifafedha
nyingi kiasi cha wananchi kutaabika, halafu akiitwa
kwenyeharambee anatoa
kijisehemu tu cha fedha alizofisadi kwa njia ya
rushwakukandamiza maendeleo ya
watu.


"Rais Kikwete amesema kuwa rushwa
inaweza ikafanya CCM
ikashindwa.

Mimi naamini, kama CCM itapitisha
majina (ya wagombea wake
wa urais2015) kwa kuangalia rushwa, chama kitaanguka, bahati
nzuri
Mwenyekitiameliona hilo, siamini kama watapitisha watu ambao
watakiangusha.


Wakipitishwa hao, sitaweza kukaa nao,
hata kama sitahama."

Hizo ni baadhi tu ya nukuu za Sumaye
katika matukio na
nyakatimbalimbali akizungumzia msimamo wake kuhusu rushwa na
mafisadi,
lakininyingi ya kauli zake hizo, kwa vyovyote vile
akizielekeza kwa Lowassa.


Hata hivyo, Sumaye huyu wa sasa,
aliyeamua kumfuata Lowassa
Ukawa,amekaririwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini
katika tukio hilo
lawiki iliyopita akisema: "Ambaye ameshakaa serikalini
katika nafasi mbalimbali
ni Lowassa. Hawa wengine (aliogombea nao urais ndani yaCCM)
hawajaendesha
Serikali, wamekwenda shule tu."

Kwamba Lowassa ambaye siku zote Sumaye
alikuwa akikiaminisha
chamachake, CCM, kwamba ni fisadi na mtoa rushwa mkubwa,
akisema kama
CCMitampitisha mwanasiasa huyo kugombea urais, yeye hatakuwa
sehemu yachama
hicho, leo hii ndiye tunayeambiwa na Sumaye kwamba
alikuwaanafaa kuteuliwa kwa
sababu tu amekwishashika nafasi mbalimbali

serikalini, anafahamu kuendesha
Serikali!


Huyo ni Sumaye na Lowassa, wanasiasa
ambao huko nyuma
walikuwa katikamkoa mmoja wa Arusha, wakiwa na uhasama
mkubwa wa kisiasa, kabla
yaMkoa huo kugawanywa na kupatikana mkoa mwingine wa
Manyarauliowatenganisha
kiutawala.


Katikati ya mshangao huo wa Sumaye na
Lowassa, katika
kipindi hikihiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2015,
tunawaona pia mahasimu
wawiliwa kibiashara hapa nchini, Dk. Mengi na Rostam Aziz
wakiweka tofautizao
za muda mrefu pembeni na kuungana kumtafuta mgombea wao wa
uraismwaka huu.


Kwa wenye kumbukumbu na wanaofuatilia
matukio mbalimbali
yanayoendelea nchini watakuwa wanakumbuka tukio la Mei 26,
mwaka huu, siku
ambayo wafanyabiashara wawili hao maarufu nchini walivyokaa
mezakuu moja. Hilo
lilikuwa tukio la kutano wa wamiliki wa vyombo binafsi
vyahabari nchini,
kupitia umoja wao wa MOAT na waandishi wa vyombo vya habari
vya ndani na nje,
uliolenga kuzungumzia, pamoja na mambo mengine, hisia za
MOAT kuhusu miswada
miwili iliyokuwa ikitazamiwa kuwasilishwa na Serikali
bungeni ili kuwa sheria
kamili. Muswada wa Huduma za Vyombo vya Habari pamoja na
Muswada wa Haki ya
KupataHabari.


Swali kuu lililotawala vichwani mwa
baadhi ya wadadisi wa
mambowalioshuhudia tukio lile la Mei 26, 2015, la Dk. Mengi
na
Rostamkukumbatiana na kukaa meza moja, lilikuwa ni, je;
miswada hiyo miwiliya
Serikali ndiyo iliyowaleta pamoja wafanyabiashara hao wawili
maarufu katika
nchi hii au ni Uchaguzi Mkuu wa Oktoba na vitalu vya gesi
asilia na mafuta?


Kwanini swali hilo? Itakumbukwa kwamba
Aprili 23, 2009, Dk
Mengi, ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP,
alitaja kwa majina
wafanyabiashara watano akiwatuhumu kuwa mafisadi papa hatari
kwa uchumi wa
Taifa hili, miongoni mwa mafisadi wasiopungua 10 aliodai
kuuyumbisha utawala wa
Rais Jakaya Kikwete.


Katika madai yake hayo, Dk. Mengi
alikaririwa na baadhi ya
vyombo vya habari nchini akisema: "Nchi hii ina mafisadi
ambao kila kukicha
wanaiyumbisha nchi. Hawazidi hata kumi. Lakini kuna watano
ambao ni mafisadi
papa. Ukitokea kupingana nao tu kutokana na ufisadi wao,
wanakuona wewe ni adui
mkubwa."

Dk Mengi, siku hiyo akiwa kwenye
mkutano mkubwa na vyombo
vya habari, alitaja majina ya mafisadi papa hao watano,
wakiongozwa na Rostam
Aziz na wengine wanne ambao sina sababu ya kuwataja
hapa.


Baada ya kutaja orodha hiyo ya
wafanyabiashara mafisadi
papa, Dk. Mengi alieleweka vyema kwa Watanzania, hasa wale
waliokuwa
wakimwamini na kumkubali kutokana na msimamo wake wa
'uzalendo' na 'utetezi wa
wazawa.'

Wakati Watanzania hao wakiendelea
kutafakari orodha hiyo ya
mafisadi papa pamoja na matendo yao kwa Taifa hili, siku 10
baadaye, yaani Mei
2, 2009, Rostam Aziz naye aliitisha mkutano mkubwa pia wa
waandishi vyombo
mbalimbali vya habari vya ndani na nje na kumrushia
makombora mazito Mwenyekiti
Mtendaji huyo wa IPP.


Dk Mengi alitajwa na Rostam Aziz
kwamba yeye ndiye fisadi
mkubwa ndani ya nchi hii, akimfananisha na fisadi nyangumi.
Rostam alikwenda
mbali zaidi, akidai kuwa na vielelezo kibao ambavyo
angeviwakilisha mikononi
mwa Jeshi la Polisi ili waanze kumchunguza dhidi ya vitendo
vyake hivyo vya
kifisadi nyangumi.


Katika kipindi hicho cha misuguano
baina ya wafanyabiashara
hao wawili, kiasi cha kupachikana majina ya mafisadi papa na
mafisadi nyangumi,
Rostam alikuwa bado ni Mbunge wa Igunga na pia Mjumbe wa
Kamati Kuu na
Halmashauri Kuu ya CCM.


Takriban miaka mitatu
baadaye, baada ya Rostam Aziz kudaiwa
na Dk.Mengi kwamba amekuwa akishiriki katika vitendo
vinavyoiyumbisha nchi hii,
kwa maana ya Julai 13, 2011, mwanasiasa huyo aliamua
kujiuzulu ubunge huo wa
Igunga pamoja na nyadhifa nyingine zote hizo alizokuwa nazo
ndani ya CCM,
akidai kuwa dhamira yake ya dhati kabisa imemtuma

aachane na siasa uchwara za ndani ya
chama chake hicho ili
sasa aweze kutumia muda wake kushughulika na biashara
zake.


Je, uhusiano huu mpya wa Dk Mengi na
Rostam Aziz,
uliowafanya wazike tofauti zao na uhasama wao na kwa pamoja
kuamua kumuunga
mkono kisiasa Lowassa katika mbio zake za kuusaka urais,
unabeba siri gani?

Nihitimishe makala haya kwa
kuwakumbusha Watanzania kwa
ujumla wa imani zote, kwamba katika Biblia (Mathayo 7:6,
12-14), imeandikwa
hivi: "Msimpe mbwa kilicho kitakatifu, wala msiwape
nguruwe lulu zenu wasije
wakawakanyaga, wakawageuka na kuwararua."


Ikulu ni mahali patakatifu, watu wasio
wasafi si mahali pao.
Gesi asilia na mafuta yaliyopatikana Mtwara pamoja na maeneo
mengine ya nchi
hii, Bara na Visiwani, ni lulu ya uchumi wa nchi hii, ambayo
kamwe Watanzania
hawawezi kuitoa lulu yao hiyo na kuwakabidhi wasiofaa!
Tutafakari sasa na hata
Oktoba 25.

Chanzo RaiaMwema

Toleo la 420,28 Aug 2015





--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment