Sunday 30 August 2015

Re: [wanabidii] Kuelekea uchaguzi Mkuu 2015: UKAWA yadhibitisha-Lowasa anaumwa.

Sawa, lete na Cheti chako ulichopimwa Virusi vya UKIMWI ili uwe mfano.Maana ni vema tuongelee afya za wengine kwa  vizuri  na hasa afya za wagombea . Usiongee bila wewe kuwa wa mfano. Maana hata hapa jukwaani, wewe naona ndo kiongozi wetu, kwa kuwa unajibu hoja zoooote!

On Aug 30, 2015 9:02 AM, 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
>
> Ninajua naweza kufa wakati wowote na niko tayari. Hata leo ukienda hospitali watu wamekufa. Siyo agenda hapa. Ukifikiri kwa kifua sawa (kwa moyo) ukifikiri kwa kichwa huwezi kuandika hayo uliyoandika. Aliyejadili afya ni Sumaye. unasema nilichoandika (kutolazimisha watu kujadili afya za watu) Watanzania hawawezi kumpeleka mtu machela ikulu. Kibaki alikuwa kapata shida iliyoeleweka. Hii si ile. Soma tena nilichoandika.
> --------------------------------------------
> On Sun, 8/30/15, 'jbifabusha' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
>
> Subject: Re: [wanabidii] Kuelekea uchaguzi Mkuu 2015: UKAWA yadhibitisha-Lowasa anaumwa.
> To: wanabidii@googlegroups.com
> Date: Sunday, August 30, 2015, 9:03 AM
>
> Mihingo
> Mungu atakupiga kofi na unaweza kufa kabla ya Lowasa. Hata
> hivyo ukome kujadili afya za watu. Hata ww hapo ulipo ni
> mgonjwa. Suala alilosema Sumaye ni kwamba Ikulu siyo mahali
> pa kubeba zege mtu yeyote mwenye akili timamu anastahili
> kuongoza. Hata ndugu zetu wenye Ulevavu wanaweza, hata
> wagonjwa Kama Kikwete sasa hivi anaongoza.
>  
>
>
> -------- Original message --------
> From: 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii
> <wanabidii@googlegroups.com>
> Date: 
> To: wanabidii@googlegroups.com
> Subject: [wanabidii] Kuelekea uchaguzi Mkuu 2015: UKAWA
> yadhibitisha-Lowasa anaumwa.
>  
>
> Watanzania wamekuwa na mashaka makubwa juu ya afya ya
> mgombea urais kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo
> CHADEMA. Sababu kubwa ya mashaka ni kuwa wasije wakamchagua
> mtu ambaye mbele akasababisha kurudiwa kwa uchaguzi kutokana
> na rais kushindwa kutimiza madaraka yake. Jambo hili kamwe
> halistahili kuwa hoja ya majukwaani. Haistahili kuanza
> kujadili afya ya mtu maana ikifikia hatua hiyo inakuwa si
> swala la itikadi. Kila mmoja anaguswa. Ni vibaya kabisa
> kugeuza afya ya mtu jambo la jukwaa la kisiasa. Kwa kweli si
> ustaarabu kuanza kujadili Fulani anaumwa. Hakuna shida
> kusema Fulani hafai kutokana na tabia au mwenendo wake.
> Lakini si afya. Afya mtu haamui bali hujikuta anaumwa.
> Katika jukwaa la kisiasa Waziri Mkuu mstaafu Fredrick Sumaye
> amewaeleza watanzania kutohoji afya ya Lowasa kwa sababu
> hata marais waliotangulia waliwahi kwenda kutibiwa.
> Amewataja Rais mkapa na Kikwete. Ameeleza kuwa mtu
> akishafika miaka 50 basi afya yake lazima itakuwa na
> matatizo. Kitu ambacho hakusema ni kuwa Lowasa haumwi.
> Amewaacha watanzania kutafsiri na kuamua alimaanisha nini.
> Mimi ninadhani alitaka kututaarifu kuwa anaumwa kweli. Maana
> yake mfumo tulio nao hautusaidii kuwapima na kuwajua watu
> afya zao. Hii kwa kweli inastahili kuwa kazi ya Tume ya
> uchaguzi. Kuhakikisha haituletei wagonjwa.
> Sumaye ni kiongozi mwandamizi wa taifa hili. Anastahili
> kuonyesha upeo wa kufikiri. Sijui kwa nini ameshindwa
> kuonyesha hilo. Au hatumjui huyo ndiye Sumaye.
> Hivi tunaweza kumchagua mtu mgonjwa asiyejimudu kwa sababu
> mtu Fulani alipokuwa madarakani aliumwa? Sumaye haoni
> tofauti kati ya JK au Mkapa walioingia madarakani wakiwa
> wazima halafu wakaumwa wakiwa kazini? Huyu kiongozi wetu ana
> upeo gani? Haoni kuwa hili si swala la kushindaniwa
> majukwaani? Yeye anasema Ikulu hawabebi zege? Yaani hajawahi
> kusikia kuna mazingira rais anaweza kushindwa kumudu
> majukumu yake? Majukumu ya kubeba nini? Hiki kifungu tena
> kimo kwenye katiba ambayo Sumaye aliwahi kuapa kuilinda
> Jamani UKAWA kuzoa zoa kutakuja kuwaaibisha siku moja!
>
> Kama CHADEMA inataka kuja kubadili mfumo inastahili kumleta
> mtu anayetiliwa shaka kuwa rais wetu? Au inataka kuingiza
> mfumo wa kusimamisha wagonjwa. Ningeelewa kama wangesema
> tunataka watu wapimwe afya kabla ya kugombea yaani kuondoa
> mfumo wa kusimamisha wagombea tusiowajua au tulio namashaka
> nao. Kama tunahakikisha hatupitishi mgombea aliyewahi
> kuhukumiwa makosa ya jinai tunashindwa kumzuia mgonjwa
> kugombea urais?
> Nakumbuka sana 2005 Mtikila akiwa anajiandaa kumlipua JK
> kuwa ameathirika yeye (JK) akawahi kupimwa na kutangaza afya
> yake. JK angesema na Mbowe ni mgonjwa (2005 JK alishindana
> na Mbowe kwa karibu zaidi) tusingemuelewa maana hapo
> asingetoa mashaka yetu. Lakini alipopimwa na akatangaza afya
> yake watu wakajua wanachagua kiongozi atakaye maliza kipindi
> chake na ikitokea asimalize ni bahati mbaya.
> Mashaka ya watanzania kuhusu afya ya Lowasa yanaongezeka
> kila kukicha. Hata zilipotoka habari kuwa serikali imepiga
> marufuku usafiri wa helicopter kwenye uchaguzi mimi
> nilidhani (kama ni kweli) basi ni njama kutaka kumchosha
> Lowasa kwa kusafiri na barabara. Jana aliposema anakaa Dar
> kwa sababu ndicho kitovu na akawataka watu wa Dar wamuombee
> kura mikoani nikawaza hivi asiposafiri kwenda kuomba kura
> itakuwaje? Kwa nini CDM ikafanya maamuzi magumu kabla
> kampein hazijapamba moto? Inataka kutuletea ya 2005 uchaguzi
> kucheleweshwa tena?
>
>  
>   --
>  
>   Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>  
>    
>  
>   Kujiondoa Tuma Email kwenda
>  
>   wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
>   Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>  
>    
>  
>   Disc

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment