Monday, 1 June 2015

[wanabidii] Re; Tunahitaji maelezo ya upande wa pili wa wanaotangaza nia

 Tumewasikia na tunaendelea kuwasikia wanaotamani kuongoza nchi yetu miaka 5 ijayo. Wanaeleza mambo mengi watakayofanya kwa mbwembwe za kila aina. Kimsingi hivyo ndivyo ilivyo, ni wajibu wao. Vyombo vya habari vina kazi kubwa kufahamisha umma haya yote. Ombi langu kwa vyombo vya habari, sambamba na kutujuza wanayosema hawa waheshimiwa tunatarajia kusikia pia yale wasiyosema. Upande wa pili wa shillingi...wa kuwasaidia kueleza udhaifu wao wa nyuma ambao kwa namna moja unaweza kuwa umechangia kushidwa kwa utawala unaondoka, na hasa waow akiwa sehemu ya utawala hu. Tusaidieni kuweka hadharani tetesi zinazohusu udhaifu wao ambao hawawezi kusema. Hii itasaidia wa-Tz kufanya maamuzi sahihi.

Makongo    
----------------------------------------------------------------
Japhet Maingu Makongo
Director, Ubunifu Associates Ltd
P.O. Box 32670, Dar es Salaam,
TANZANIA
Website: www.ubunifu.co.tz, info@ubunifu.co.tz,
Tel: +253 24 2732125+253 24 2732125, Mobile:+253 758 270 254+253 758 570 253

0 comments:

Post a Comment