Swali la Katiba lilimshinda kujibu au hakulielewa? Kalikwepa?
--------------------------------------------
On Tue, 6/2/15, 'mpombe mtalika' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Subject: [wanabidii] Yaliyojiri Ukumbi wa Hyatt Regency: Frederick Sumaye atangaza nia kugombea Urais
To: "ELISA MUHINGO' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Tuesday, June 2, 2015, 5:46 PM
Waziri mkuu mstaafu muda huu
anatangaza nia akiwa katika
ukumbi wa Hyatt Regency Dar es salaam, huku akiwa na kauli
mbiu 'UONGOZI BORA,
KOMESHA RUSHWA, JENGA UCHUMI'. Anasema huwezi kukemea
rushwa na halafu na wewe
upo ndani ya rushwa.
Anaongelea mafanikio katika
katika kipindi yuko madarakani
ikiwemo televisheni ya taifa, uboreshaji elimu ya msingi.
Anasema leo badala ya
sekondari nayo kupanda ndio hio imeshuka.
Anaongelea sera ya ubinafsishaji, anasema sera hio ilikuwepo
kabla ya uongozi
wa Mkapa. Hivyo wao walikuwa watekelezaji na hawawezi
kulaumiwa. Ubinafsishaji
kama sera ni kitu muhimu na ni vizuri ilifanyika. Mashirika
zaidi ya asilimia
45 yamenunuliwa na watanzania, mengine kwa ubia na wageni na
asilimia ishirini
pekee yalinunuliwa na wageni kwa asilimia 100.
Nimekumbana na mambo magumu katika miaka hio kumi ikiwemo
ajali ya MV Bukoba na
ajali ya treni, ukame wa mwaka 1997. Niliunda kamati ya
kushughulikia jambo
hilo na kuchimba visima zaidi ya 300 Dar es Salaam. Mambo
magumu yalinikomaza
katika uongozi. Mvua za El nino zilifata baada ya ukame,
ilikuwa hali ya hatari
lakini tulijikwamua na tuliendelea na kazi wa kujenga taifa
letu. Kifo cha baba
wa taifa, mimi sikulala siku tatu nzima hata kwa nusu saa,
sijawahi kuona
kipindi cha amani kama kili, polisi waliripoti hata uhalifu
haukuwepo.
Wakati waziri mkuu, sikuweza kusikia watu wanapigana,
asubuhi nisiwepo pale,
leo wakulima na wafugaji wanapigana miezi sita sasa. Mfano
mgogoro wa waancholi
na wahadzabe.
Huwezi kuzungumzia amani wakati watu wana njaa, tatizo la
uchumi, watu
wanaangalia takwimu badala ya uhalisia. Tunatakiwa
tuendeleze kilimo, hata
wakati wa Nyerere tulileta matrekta lakini tuliendelea?
Kuleta matrekta ni
jambo jema sasa nitalima heka 50, lakini uwezo wa mbegu heka
3 na kupalilia
heka 3.
Eneo lingine muhimu ni masoko, lazima kiendelezwe katika
ukubwa wake. Wakulima
watauza kwa bei ya hasara na bei ikiwa vizuri hawana tena
mazao. Leo viwanda
vya sukari, hatuwezi kuingiza sukari kutoka nje bila kodi,
lazima tulinde
viwanda vyetu vya ndani. Mazao yetu yote, kama tutakua na
juhudi za kusindika
mazao, hili tatizo la ajira ambalo tunapiga nalo kelele
sana, litapungua. Pia
pengo kati ya walionacho na wasio nacho litapungua.
Nimeona shule binafsi wanafanya vizuri, wanataka wazipunguze
nguvu, ongeza
juhudi nawe umfikie. Katika miaka miwili au mitatu
tutapunguza kwa kiasi
kikubwa wanaoenda nje.
Rushwa na ufisadi, hili jambo sina utani nalo. Ukituhumiwa
kwa rushwa ndani ya
wiki moja unachunguzwa na wiki mbili mahakama imekuhukumu na
kama ni viboko
unapokea kabisa.
Nawashukuru ndugu zangu waandishi wa habari, nimezungumzia
Dar es Salaam na
naamini mtafikisha nchi nzima ili tumpokee rais Kikwete
kijiti ambae amefanya
vizuri. Kama kuna maswali pia niko tayari.
Matangazo haya yalikuwa yanarushwa na ITV, Star TV, Mlimani
TV, Radio free
Africa, radio one ila bahati mbaya sehemu kubwa ya nchi
umeme hamna ikiwemo
mikoa mitano
=========
MASWALI
Tanzania Daima: Katika
awamu hio ufisadi mwingi ulitokea, uuzwaji NBC,
EPA, Radar Kiwira Kama mshauri mkuu wa rais na mtendaji
Mwananchi: Umenukuliwa
mara kwa mara kuwa ikitokea ameteuliwa mla rushwa
kupitia CCM wewe utajitoa
Mariam Mziwanda, gazeti la
Uhuru: Kabla hujaachia uongozi wa uwaziri
mkuu ulitajwa kama kiongozi unaemiliki mali nyingi, kupitia
fursa hii
MAJIBU
Swali la Kwanza
Kwanza kama waziri mkuu naweza kumshauri wa rais, Ameziita
kashfa lakini mimi
siziiti kashfa. Kama NBC ni ubinafsishaji wa kawaida. Sijui
watu wanatoa wapi
taarifa kuwa walikuwa wanapata faida, regulator wa benki
zote ni BOT hivyo ndio
ana taarifa sahihi. Hakuna kwamba tuliuziana benki hotelini
Hizo zingine zote
zinafanana, Radar na ndege ya rais, unatakiwa utofautishe
maamuzi ya serikali
na kama kuna ufisadi, nchi ilikuwa haina radar. Katika
ununuzi ule kama kuna
mtu alifanya foul anatakiwa akamatwe, ilimradi imethibitika
mtu alifanya ovyo
ni jukumu la serikali kumkamata sio Sumaye,
Swali la michezo ni muhimu ni ukosefu wa muda ndio maana
sikuigusa ila katika
kitabu changu cha sasa mtaiona.
Mimi na wala rushwa ni maji na mafuta, nitatoka ndio lakini
naamini chama
changu hakiwezi kuchagua mla rushwa. Sitegemei kutoka kwa
sababu hawatachagua
mla rushwa.
Sasa Mariam, muda unatoa jawabu, mimi leo watanzania
wananijua, watoto wangu
mnawajua wanafanya kazi za kawaida za serikali. Mtikila
ambae alinituhumu mambo
mengi sana, baadae akasema watu wasafi nchi hii ni Sumaye,
Warioba na
Mwakyembe. Hela nyingine ambayo nilipata nilisomesha
waandishi wa habari nyie
mnajua. Mimi nina moral authority kwa muda mrefu.
Kuhusu nani tishio katika mbio za urais, hakuna hata
mmoja.
MASWALI
Pendo: Katiba mpya
kuna mkwamo, ukipata ridhaa unawaahidi nini wananchi
ambao maoni yao yametupwa
Mtanzania: Uumekua
unaongelea umiliki wa ardhi bila faida, wewe
unatuhumiwa kumiliki maeneo makubwa na mengine
hayajaendelezwa
Radio Iman:
Umezungumzia vipaumbele vingi, walimu wana kilio cha muda
mrefu tangu wewe ukiwa madarakani kuhusu stahiki zao
Kubenea: Nyumba za
serikali ziliuzwa wakati uko madarakani, tamko lako!
Mimi sidhani tatizo ni katiba, tatizo ni usimamizi wa
sheria, kwa mfano
kiongozi mla rushwa, katiba haikupi fursa ya kumuhukumu?
Tatizo sio katiba,
hatuhitaji li-document likubwa kama tuliloliandika.
Swala la ardhi, wapo
watanzania wengi tu wana ardhi kubwa kuliko mimi,
haya mambo yanakuzwa tu, nimeshindwa kuendeleza baadhi ya
maeneo kwa sababu
sijapewa hati bado. Hela ya kujenga kibanda Dar unaweza
kununua ardhi kubwa
sana mikoani.
Swala la kuboresha walimu, tulifanya hayo na msiwe na
wasiwasi nalo kwa upande
wa mafao.
Nyumba za serikali ni uamuzi wa serikali, sababu yake kubwa
ilikuwa ni nini,
kwa sababu ungozi wa Mkapa ulikuwa ni uwazi na ukweli.
Kamati ilisema nyumba za
serikali ni nyingi mno hivyo pesa nyingi zinaingia
kuzikarabati. Tulikua kwenye
ubinafsishaji, mashirika yalikuwa na nyumba nyingi, nyumba
nyingi tuliamua
kuziondoa. The highest bid secured, tulijaribu kutetea hata
ma-general managers
lakini ilishindikana.
Rushwa ni rushwa, mtu hata uwe mkubwa namna gani, yani mnipe
Urais nimshindwe,
hakuna mkubwa kuliko Rais, wote nitawashughulikia.
ndugu
nawasilisha tuwachambue hawa watangaza nia mmoja baada ya
mwingine tuwajue na udhaifu wao
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment