MASWALI NA MAJIBU KUHUSU KUVURUGA PROGRAMU YA WINXP
Najibu maswali haya kama mdau wa TEHAMA Kama kuna maswali zaidi yanaweza kuulizwa na nitatolea majibu na wengine wataendelea kuchangia .
1 – PROGRAMU YA WIN XP KUVURUGIKA
Sio ukweli kwamba programu ya win xp itavuruguka kama inavyoelezwa na watu wengi .
2 – KITAKACHOTOKEA
Microsoft itaacha kutoa baadhi ya huduma za kuboresha windows xp kwa jina lingine ni updates ambazo zilikuwa zinapatikana pale mtu anapojiunga kwenye mtandao bure .
Unapokosa hizi updates maana yake windows xp yako inakuwa haikostable kupambana na mengine yanayoweza kutokea kwenye kompyuta yako haswa upande wa software , kwahiyo updates ni sawa na mtu anavyokula chakula kunachoenda kuboresha afya yake aweze kuendelea kuishi na kufanya shuguli nyingine .
3 – VIPI PROGRAMU NYINGINE
Kampuni nyingi za program zimeboresha na zinaendelea kuboresha program zao ili ziweze kufanya kazi na operating system mpya za zilizoboreshwa zaidi kama windows 7 , 8 , 8.1 ETC .
Mfano sasa hivi kuna printa ambazo hazina program za win xp kwahiyo ukiwa na win xp huwezi kutumia printa hizo .
4- KWA WANAOENDELEA KUTUMIA WINDOWS XP
Kama nilivyosema Microsoft haitokuwa inatoa msaada na updates za kuboresha windows xp , ili uhamie windows 7 , 8 na nyingine zilizokuwepo katika matumizi , hii ina maanisha Microsoft haitahusika na suala lolote la kisheria litakalotokea endapo utaendelea kutumia .
5 – WENGINE WAMEFANYAJE ?
Kuna baadhi ya kampuni zimeingia mkataba na Microsoft kwa ajili ya kuendelea kuhudumia windows xp zao huku wao wakiendelea kufanya mchakato wa mabadiliko kidogo kidogo kulingana na uwezo wao wa kifedha na sera za kampuni , sherika au nchi husika , kwa Tanzania watu wangejaribu kuwasiliana na ofisi za Microsoft nchini Kenya hawa wanaweza kuwapa msaada zaidi haswa kwa mabenki na huduma nyingine kubwa kubwa .
6 – TATIZO LA AFRIKA NA NCHI MASIKINI
Hizi program za windows xp , windows 8 na 7 ni gharama sana , kwa mfano windows 7 kwa Tanzania ni dola 250 hivi ukichanganya na office unapata dola 500 ukiweka na antivirus ni dola 550 hiyo ni kama ukiamua kununua genuine na DVD zake , hii watu wengi hawana uwezo wa kununua na hizi serikali zetu na uwezo wao ni mdogo , kuwapeleka huko juu ni gharama zaidi kwa watu na serikali .
USHAURI WANGU
Serikali iingie mikataba na kampuni zinazouza program zao kwa wingi nchini Tanzania haswa Microsoft , adobe , apple , kaspersky , Symantec , oracle , ETC ili waweze kufanya mipango ya kupunguza bei kwa ajili ya soko la Tanzania hii itasaidia watu kupata program halisi kwa bei nzuri kidogo na zenye uhakika bila hivyo wananchi watakimbilia kwenye program ambazo sio halisi na wataendelea kutumia gharama kubwa kwenye matengenezo na kukumbana na karaha nyingine za kihalifu .
YONA F MARO
O786 806028
Institut d'études de sécurité - SA
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment