Saturday, 26 April 2014

Re: [wanabidii] UMOJA WA WAZANZIBAR WANAOISHI TANZANIA BARA WALAANI UKAWA KUSUSIA BUNGE


Lakini kuangalia hela zinavyotumika vibaya kwa watu kuangalia ubinafsi wao, kupeana mipasho isiyo adabu nao ni watu wazima, kuangalia uchama, urafiki nimuunge nani mkono aliyesema nini na nimkashifu nani hata kama alichosema kina mantiki inatushangaza. Utanzania haupo bali ni ubinafsi ndio sasa tunaangalia mihela waliyopewa. Lodging Dodoma ni kiasi gani? Kula kutwa moja anakula laki. Yaani kima cha chini kwa GVT worker apewacho kila baada ya mwezi mmoja yeye anapata per day na bla makato maana kodi ndio zinamaliza mishahara ya GVT workers.

Wengine wanatoka nje eti waliowengi wamesena serikali 3 CCM haitaki. Wasomi hao!! Jamani, sisi wananchi tunaweza kupiga kura kwa wingi kuchagua kitu tukisukuwa na ubinafsi na chuki, influence ya chama, udini, ukabila nani kasema nini nimfuate huu wa kabila, dini, chama changu, wa kutoka kwetu au kufuata mkumbo wowote ule. Huko wamechanganywa wa elimu na uzoefu mbali mbali na michanganyo ya kila aina ili kuleta maamuzu ya kufaa taifa. kazi yao ktk kutumia mihela yetu isiwe mzozo au kukubali tu walichosema wananchi (sio kumchagua mtu hapa ni masuala ya manufaa kwa Taifa), bali wayachambue, kuangalia prons and cons na realities za issues hizo na hizo aina zote za serikali na muungano. Wakiangalia nchi nyingine mifano ya miungano ya serikali kibao; kisha kuangalia utata uliopo TZ katika serikali ya muungano iliyozaa nchi mbili ndani ya muungano moja ikiwa nchi tu ndani ya muungano si nchi yenye katiba yake pekee ya maamuzi yake. Halafu watushauri wananchi kwa kutuelimisha kipi kinatufaa kwa mifano halisi kutuonyesha misingi ya maamuzi yao. Hata katika utafiti wa kawaida wa kupanga mipango ya maendeleo jamii, kuangalia athari ya uwekezaji wa namna fulani-utafiti unatumika tu kufungua macho kuona hali halisi iivyo na maoni, vipaumbeli ambavyo navyo vipaumbele hupimwa kwa weighted average and pairwise comparison kuvitapa vipaumbele hivyo. Kisha maamuzi yanafanyika kutokana na realities za target group na mazingira, raslimali na uendelevu wa kitakiwacho (sustainability); sera, mikakati, malengo ya nchi, sheria zilizopo; zile za ulimwengu na zile za mhisani, malengo na matakwa yake mhisani kama yupo anahusika na suala hilo.

Hii ya tume ya warioba kusema 3 isikiukwe au 2 ikubalike-SIO Tija au suala la kutugombanisha-ni matokeo ya utafiti sasa tujadili what best kinatufaa kwa kuchanganua kama nilivyochangia hapo juu?

Kila kizuri hupatikana kwa gharama sio kwa dezo. Hivyo hiyo mihela inatuuma lakini imeanza kutuuma baada ya kuona bunge maalum la katika linakuwa kilabu cha pombe na genge la malumbano ya simba na yanga, ManU na Manchester. Nasi tuna njaa, tunazitamani hiyo mipesa kama inapatikana kirahisi hivyo kwa kuufyata na kuufyatua.
On Sunday, 27 April 2014, 7:40, Mike Zunzu <mikezunzu@yahoo.co.uk> wrote:
Kwa hiyo ninyi mnacho jail ni pesa zilizotumika kuandaa shughuli za bunge la katiba, siyo umhimu wa kutengeza katiba inayowafaa Wanzania kuanzia sasa na miaka ijayo? kuna msemo ya kilugha unasema "Mahela macholwa." Maana yake pesa hutafutwa, lakini hekima itaipata wai? Au kwa mfano sasa kukifanyika makosa kukatengenezwa katiba mbovu, kwa tabia ya viongozi wa kiafrika unategemea lini tena watakuja kuruhusu katiba nyingine kuundwa?
Watu msiangalie mnahali gani sasa, fikiria miaka mia moja mbele je vizazi vijavyo wataishije.
On Sunday, 27 April 2014, 0:06, "'ELISA MUHINGO <elisamuhingo@yahoo.com>' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Hawa wanastahili kutangulia kumlaani Rais Mstaaf Karume na Kikwete kwa kupitisha katiba ambayo ilivunja muungano. Nina maana katiba ya sasa ya Zanzibar. hapo watakuwa wanasema kweli na kuonyesha uzalendo
On Thursday, April 24, 2014 12:11 PM, Fakhi Karume <fkarume@gmail.com> wrote:
UMOJA WA WAZANZIBAR WANAOISHI TANZANIA BARA (UWTB)
P.O. BOX 1019 DAR ES SALAAM TELL: 0718344443/0762812681

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TUNALAANI UKAWA KUSUSIA BUNGE

Ndugu waandishi, sisi Wazanzibari tunaoishi Tanzania Bara tumestushwa, tumehudhunishwa na tumekerwa mno na kitendo cha Wabunge wa vyama vya upinzani vya NCCR, CUF na CHADEMA kutoka nje ya Bunge maalum la Katiba linaloendelea mjini Dodoma na kususia vikao vya Bunge hilo.

Ikumbukwe kuwa Bunge hili limeandaliwa kwa fedha nyingi za walipa kodi wa Taifa hili kwa madhumuni ya kuhakikisha kuwa Tanzania inapata Katiba mpya itakayoleta maendeleo kwa wananchi. Kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa kuhusu mchakato wa upatikanaji wa Katiba, mahali pekee pa kujadili na kupitisha hoja mbalimbali za kutunga Katiba hiyo ni Bungeni.

Sasa inashangaza na kustaajabisha kuona Wabunge hao wakiacha kutumia fursa hiyo ya kutumia Bunge kutoa maoni yao, badala yake wanatoka na kuzurura Mitaani huku tayari wakiwa wameshalipwa mamilioni ya fedha za wananchi. Je, kitendo hiki si usaliti kwa wananchi? Tunalaani kitendo hiki kwa nguvu zote na kutaka wananchi wote wa Bara na Visiwani kulaani kitendo hiki. Sisi tunaamini kuwa Katiba mpya haiwezi kupatikana kwa maandamano na mikutano ya hadhara, bali ni kwa kutumia Bunge Maalum linalogharamiwa na wananchi. Hivyo tunawataka Wabunge hao warejee haraka Bungeni ili wasitucheleweshe kupata Katiba mpya kwa ubinafsi wao.

Sababu walizozitoa kwa ajili ya kususia vikao vya Bunge hilo eti wanatukanwa na kubaguliwa, hazina mashiko. Kwa sababu kama ni matusi ndiyo ingekuwa sababu za kususia vikao vya Bunge hilo, basi Wabunge wote wangesusia pale Wabunge wa Upinzani walipowatusi na kuwakashfu Waasisi wa Taifa letu Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Karume. Lakini hata baada ya wao kuwatusi Waasisi hao, Bunge hilo liliwavumilia na kuendelea na wala hakuna aliyesusa.

Kuhusu muundo wa Serikali, sisi Wazanzibari tunaoishi na kufanyia shughuli zetu Tanzania Bara, bado tunasisitiza kuwa muundo peke utakaodumisha umoja wetu, mshikamano wetu na amani iliyopo, ni muundo wa Serikali mbili na si vinginevyo. Tunapinga muundo wa Serikali tatu kwasababu utaongeza gharama kubwa za uendeshaji na kusababisha mzigo mkubwa wa ulipaji kodi kwa wananchi.

Hivi sasa tupo katika muundo wa Serikali mbili tu, lakini hali ya kiuchumi kwa wananchi wa kawaida siyo ya kuridhisha. Je, tutakapoongeza idadi ya Serikali hadi ziwe tatu hali ya maisha itakuwaje? Mbali ya suala la gharama lakini pia tunaamini kuwa usalama wa muungano huu upo ndani ya Serikali mbili. Kinyume chake, muungano huu utavunjika na kusambaratika. Kitu ambacho hatupendi kitokee.

Mwisho:
Sisi Wazanzibari tunaoishi Bara tutaendelea kuufurahia Muungano wetu na kuwa pamoja na wale ambao wanautakia mema Muungano wetu. Tunawasihi na kuwaomba Watanzania wenzetu kuwapuuza Viongozi wa UKAWA kwa jambo lolote watakaloambiwa kwa nia ya kuwachukia Viongozi wetu wanaoongoza nchi hii pamoja na bunge linaloendelea, ni wazi hawana nia njema na Taifa letu, machafuko yatakapotokea wao ndio watakuwa wa kwanza kukimbia nchi hii na matokeo yake wananchi wa kawaida ndio watakaopatwa na matatizo. 
Tunamuomba mwenyezi Mungu kuendelea kuulinda Muungano wetu pamoja na Viongozi wetu wakiongozwa na Rais wetu Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Dr. Alli Mohamed Shein

Mungu ibariki Tanzania

……………………………….
SWALEHE OMARY
MWENYEKITI
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


0 comments:

Post a Comment