KUHUSU KIKAO CHA KAMATI KUU KESHO;
Kutokana na maswali kutoka kwa wanahabari wa vyumba mbalimbali vya habari juu ya agenda za kikao cha Kamati Kuu kesho, Chama kimetoa kauli ifuatayo;
Ni kweli kutakuwa na mkutano maalum wa Kamati Kuu ya chama kesho tarehe 3 Januari 2014 Jijini Dar Es Salaam. Ajenda kuu katika mkutano huo ni tatu;
Mosi; Kupokea taarifa kuhusu mchakato na maudhui ya mabadiliko ya katiba
Kamati Kuu itapokea taarifa juu ya kupitishwa kwa marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya katiba 2013, kupitishwa kwa muswada wa kura ya maoni wa 2013, uteuzi wa wajumbe wa Bunge Maalum na kutolewa kwa Rasimu ya Katiba Mpya.
Pili; Kupokea utetezi (wa mdomo) wa wanachama watatu kuhusu tuhuma mbalimbali zilizoelekezwa kwao.
Wanachama hao walishajulishwa makosa yao kwa maandishi na wamewasilisha utetezi wao wa maandishi. Wataitwa kwenye kikao kwa kuzingatia matakwa ya kanuni 6.5.2 (b) na 6.5.2 (d) kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya kikao kinachohusika.
Tatu; Mpango Kazi wa Chama kwa mwaka 2014
Mpango Kazi wa chama ni sehemu ya hatua za utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Chama wenye dhima ya kuleta uongozi bora, sera sahihi, mikakati makini na oganizesheni thabiti kwa maendeleo endelevu ya chama na taifa.
John Mnyika
Mkurugenzi wa Mawasiliano
-- Kutokana na maswali kutoka kwa wanahabari wa vyumba mbalimbali vya habari juu ya agenda za kikao cha Kamati Kuu kesho, Chama kimetoa kauli ifuatayo;
Ni kweli kutakuwa na mkutano maalum wa Kamati Kuu ya chama kesho tarehe 3 Januari 2014 Jijini Dar Es Salaam. Ajenda kuu katika mkutano huo ni tatu;
Mosi; Kupokea taarifa kuhusu mchakato na maudhui ya mabadiliko ya katiba
Kamati Kuu itapokea taarifa juu ya kupitishwa kwa marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya katiba 2013, kupitishwa kwa muswada wa kura ya maoni wa 2013, uteuzi wa wajumbe wa Bunge Maalum na kutolewa kwa Rasimu ya Katiba Mpya.
Pili; Kupokea utetezi (wa mdomo) wa wanachama watatu kuhusu tuhuma mbalimbali zilizoelekezwa kwao.
Wanachama hao walishajulishwa makosa yao kwa maandishi na wamewasilisha utetezi wao wa maandishi. Wataitwa kwenye kikao kwa kuzingatia matakwa ya kanuni 6.5.2 (b) na 6.5.2 (d) kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya kikao kinachohusika.
Tatu; Mpango Kazi wa Chama kwa mwaka 2014
Mpango Kazi wa chama ni sehemu ya hatua za utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Chama wenye dhima ya kuleta uongozi bora, sera sahihi, mikakati makini na oganizesheni thabiti kwa maendeleo endelevu ya chama na taifa.
John Mnyika
Mkurugenzi wa Mawasiliano
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment