Thursday, 2 January 2014

Re: [wanabidii] Re: Tembo wanazid kuuwawa?

Kiwasila mimi bado sijaamini kama tatizo ni sisi na kwamba sisi ni waovu babu K, kama ulivyosema maana sisi tunatawaliwa na tunaweza
kuendeshwa kwa mujibu wa sera na taratibu zinazopangwa na viongozi wetu wakuu. Sisi tunafuata amri ya watawala
 
Naamini tatizo ni kiongozi mmoja tu ambae ndie mkuu wa wote. Kumbuka kisa hiki cha kalumekenge alipokataa kwenda shule.
Mzazi wake aliiomba fimbo imchape kalumekenge ili aende shule fimbo ilikataa. Mzazi akaomba moto uichome fimbo ili imchape kalumekenge aende shule moto nao ukakataa. Akaomba maji yazime moto ili moto uogope uichome fimbo na fimbo imchape kalumekenge ili aende shule maji nayo yakakataa. Akaomba mbuzi anywe maji ili yazime moto mbuzi nae akakataa. Tazama mzazi akampata mtu shababi mwenye nguvu akamuomba amchinje mbuzi. Yule mtu akakubali kumchinja mbuzi Unajua nini kilitokea? Mbuzi alipoona anataka kuchinjwa aliogopa hivyo akakubali kunywa maji.  Maji nayo kuona yananywewa yakakubali kuzima moto. Moto kuona unazimwa ukakubali kuchoma fimbo.Fimbo nayo kuona inachomwa ikakubali kumchapa kalumekenge . Na kalumekenge kuona anachapwa basi akakubali kuenda shule na mambo yote yakawa shwari na buheri.
Utaona Kiwasila tatizo liko wapi? kumpata mchinjaji wa mbuzi ili anywe maji ndio shida. Tatizo liko hapo tu huku kwingine kote kutakaa sawa,ndio maana kila mtu kiongozi  kwa sasa hawajibiki na lolote.
 
2013/12/31 Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk>

Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu. kama hatukubadilika sisi wananchi kutoka kaya, walioajiriwa maofisini na wenye madaraka ya usimamizi  kama vile directors, mawaziri. Wabunge na madiwani ni muhimu kwani wao wanawananchi katika majimbo na kata zao. Ni rahisi kuwashauri wananchi wasichakachue mazingira na raslimali, kutaka kipato cha rahisi kwa kukata miti, kuua wanyama bali kulima na kufuga sustaibaly, kulinda misitu kupata sio mvua tu pamoja na carbon reade money; kuacha kukaribisha, kuficha na kushirikiana na maujangili. Kiongozi Mkuu akiondolewa-haisaidii kitu maana mfumo mbovu ni pamoja na wanakaya wanaolinda uhalifu na wale matajiri wanaununua na kusafirisha. Kisha matajiri wanatajirika ila raia anaishia kulewea pombe hela akijua-kesho atawinda na atakata mbao tena atauza; atahamia na mifugo, kwa kilimo msitu huu au ule kama si Bunju atakwenda Rufiji-Lindi, Katavi etc. Kuwajibika-ni pamoja na mbuga za hifadhi kulinda tembo-askari wapewe magari mazuri, slaha na awwe wengi wasizidiwe nguvu na poachers ambao ni fully armed na mishale ya sumu na automatic guns.
Kenya miaka ya zamani walichukua sheria ya shoot and kill ya majangili wakikutwa mbuga za hifadhi. Tukawacheka tukawaona ni wanyama. Matokeo yake ni haya. Umuwahi akuue wewe au wewe umuue. Ukikuta m8ifugo hifadhini-chakaza maana wakifanya makusudi kuharibu mazingira yao hawasikii, hawapunguzi mifugo, kisha wanahamia hifadhi kuharibu na kuona wanaonewa wakifukuzwa. Ikawa tunawaona wehu. Sasa-tuamue-Piaga au beba mgongoni ili upate KURA uendelee KULA ukimaliza ardhi mwenyewe. Ahamie bondeni, mtoni eneo hatarishi mvua ikinyesha ategemee SERIKALI impigie mitaro ya kuondoa maji bondeni aishiko, Umuache azame afe au umbebe, umtafutie mahema, umlishe, umuuguze na kodi halipi, kadi ya afya hana ila pombe haikosi daily.

Watanzania tumeshindwa kuzuia uovu wa aina nyingi kwani sisi wenyewe tu washiriki wa uovu. Pili, tuna ushauri wa kisasi. Kwa vile tuna mitandao ya ufisadi hadi kaya-waziri au kiongozi akitaka kufanya kweli kutumia sheria-koo, rafiki watamwendea kwa mkubwa zaidi na kumfupisha asifanye hivyo-Tunalindana na kulinda uovu. Kuachia uovu uendelee ndio kazi yetu. Mbona tunaona wanaojengwa mabondeni, au ndani ya Hifadhi-Nyanza na Sasasaka villages Huko Maswa Game Reserve. Zimechomwa mara ngapi, wanarudi, wanajenga. Na sasa Wafugaji wamehamia ndani ya Mikumi National Park na wakipita wanaharibu mashamba ya wakulima, mifugo DSR na miji mingine inazurura mjini-mbuzi kibao. Hebu zikamate mikono yako iende upande-utaogopa tu kuchukua sheria. uovu kimatendo, kiushirikina, kisiasa kulindanaism.
Mfugaji amekuwa M-pesa, NBC, NMB ya viongozi kijiji, Kata. Wanapata fedha na kumwambia-ntakulinda hautoondolewa. anapewa mbuzi, ng'ombe au pesa taslimu na mfugaji. analishia mashamba, mnachapwa na kuuawa kisha mnapambana zaidi hakuna kesi!! Hivyo vituo vya basi vipya vinavyojengwa-vitajaa biashara ya mitumba, chakula watapanga humo kama walivyokuwa wakipanga daraja la manzese na wapangavyo njia za kupita kwa miguu. Hizo njia za miguu vilori, bajaji, pikipiki zinapita na uangalie utagongwa na kufokewa vilivyo.
Daladala ya mtanzania inaweza ikaamua haiendi ubungo foleni ikawashudha gate maji mtembee hadi ubungo-haendi. 'simple'. Mtanzania huyo anatesa mwenzake. Ingekuwa mhindi, mchina etc tungeandamana wafukuzwe wanatuonea. Ukiangalia mto ubungo darajani-malundo ya takataka, mifugo ipo zizini kando ya mto, kinyesi-mtoni. Viongozi wakapi wanapita hapo. Wananchi wanakoga mtoni na kutumia maji hayo machafu kukusha mboga na kuuza.
Mainzi kibao-samaki za kukaanga zimejaa mainzi zipo wazi. Mwambie atumie sanduku au asilifungue lina kioo tunaona biashara-hataki. Tunakula na mainzi yapo, tunanunua vya mainzi kama kawaida miaka inapita. Nini hao tembo-mainzi na uchafu ni ya kawaida kwetu.

Tembo, kiboko, ng'ombe mwitu anatoka nje kufuata maji, anaharibu mazao na kuua /kuumiza watu-kwani wasomi wa wanyama Pori mbona wapo? haiwaingii akilini kuwachimbia borehole kadhaa na kuweka windmill ya kupampu maji na kuyamwagia ktk bwawa la Kiboko, mamba na tembo na wanyama wengine wakanywa maji? Mbona GVt zonal drilling rigs zipo na TANAPA ina pesa za utalii? Wanyama pori wakitoka nje ni lazima wananchi nao watawaua. Haiingii akilini wakose maji na mabuldoza ya kuchimbwa mabwawa yako, ya kufukua mabwawa kama limejaa mchanga na drilling rigs na water engineers wapo. Biashara kichaa kuacha wanyama pori wafe kwa kukosa maji kwa kutegemea mto uliokauka wakati unaweza kutengeneza swamps na mabwawa ukapanda miti na majani. wazee wetu waliwaopa maji kwa mifereji wanyama pori kuzuia waziingie vijijini, siti tunakausha vyanzo kwa kukata miti, kuingiza mifugo, kilimo kisha kulalamika uonevu.

hatuwezi kuzuia maovu Suleiman Swalehe kwani nasi tu waovu babu k.
 
On Tuesday, 31 December 2013, 10:34, Selemani Swalehe <semkiwas@gmail.com> wrote:
Japhet nimevutiwa sana na pale uliposema;

Watanzania tumekubali kushindwa kuzuia maovu kutendeka katika hali ya kawaida, hadi tuwe na "Operesheni?
Kauli hiyo ndio imenifanya niunge mkono swali hili kwetu Watanzania na serikali yetu.
Ama kwa hakika operesheni zitaundwa nyingi lakini hazitaweza kufanikiwa kamwe maana operesheni sio za milele zina muda maalum. Wahalifu majangili na kadhalika watatulia kwa muda kupisha operesheni na ikimaliza muda wake mambo yanarudi pale pale. Kama tulivyoona katika operesheni hii ya  tokomeza ujangili. Imesimama kidogo kutafakari ripoti iliyoletwa na tume tayari tembo takriban 60 wameshauwawa katika kipindi hiki kifupi.
 
Dawa ni kuamsha uwajibikaji na usimamizi thabiti maana ni kazi ya kila siku ya hao waliopewa dhamana ndipo mambo yataenda sawa. Na hii yote inaletwa na mfumo uliopo kwa sasa,hata akitokea muwajibikaji mfumo unamvuta chini anatulia.  Mifano iko mingi tumeona mawaziri na viongozi wengine walipoingia madarakani kwa ari na  nguvu mpya na kasi mpya lakini vyote hivyo havikufika mbali mambo yakawa ni yale yale.
 
Wenzetu wameshindwa kubadili mfumo uliopo maana una maslahi kwao bila shaka tukiweka watu wengine watuongoze watabadilisha mfumo huu na hatimae wataweza kuwajibika na kusimamia dhamana zao walizopewa kuzisimamia
 
lakini katika mazingira ya sasa 2013/12/30 Japhet Makongo <makongo@yahoo.com>

Nimesikikia Mheshimiwa Nyalandu... Hii hali inasiktisha kwamba pamoja na juhudi kubwa zinazofanywa na serikali tunazidi kupoteza uhai wa mali asili na na maisha ya watu. Maana yake ni kwamba sisi Watanzania tumekubali kushindwa kuzuia maovu kutendeka katika hali ya kawaida, hadi tuwe na "Operesheni". Sipingi umuhimu wa kuwa na operesheni, lakini katika mazingira ya sasa sidhani kama inaweza kuwa suluhu ya kudumu. Hapa tunatakiwa kujitathimi kizalend, kimaadili..... na uchungu wa nchi na maisha ya watu. Siamini kwamba wanaongiza mifugo katika hifadhi hawajulikani kwa wananchi na viongozi wa vijiji husika. Hapa kuna uzembe au makusudi tu. Watu wanaoweka kambi ya ujangili katika hifadhi hawatoki nje ya nchi yetu na kama hivyo ndivyo kuna ushirika au ubia na watu wa ndani.. na wanajulikana  kwa viongozi wa ngazi husika.
 
Nionaavyo mimi yanayotokea katika hifadhi zetu, ambayo yamepelekea Mawaziri 4 kufikwa na mgogoro wa kiuongozi ni dalili tu za kushindwa kwa mfumo mzima wa utawala wa uwajibikaji. Udhaifu uko zaidi katika ngazi za usimamizi. Maovu  na mauaji ya aina hii yanafanyika katika kila sekta, ila tu hayajafumuka kama haya yaliyoundiwa tume.  Maana yake ni kwamba serikali haitaweza kuanzisha operesheni kila sekta na kuunda tume za kuchunguza umakini wa hizo operesheni. Tunahitaji watu wachache tu waliopewa dhamana ya kusimamia amani, usalama na utulivu wa nhci kuanzia ngazi ya vijiji/mitaa na hata taifa, na tena bila gharama  kukubali kuwa sasa imetosha. Wajitoe kusimamia na kuzuia maovu haya ya watu wachache wenye uchu na choyo kwa dhati na nidhamu, hata kama italazimu wao kuwa wahanga wa matendo yao.  
 
Mheshemiwa  Raisi, Kama ilivyokuwa katika hadithi ya Kalumekenge, angalia safu yako tena bila woga na umpate shujaa wa kushika kisu cha kumchinja mbuzi ili anywe maji, maji yazime moto na moto uchome fimbo na fimbo imchape kalumekenge apate kwenda shule.
 
Mungu Inusuru Tanzania
 
----------------------------------------------------------------
Japhet Maingu Makongo
Director, Ubunifu Associates Ltd
P.O. Box 32971, Dar es Salaam,
TANZANIA
Website: www.ubunifu.co.tz, info@ubunifu.co.tz,
Tel: +255 22 2762027, Mobile:+255 754 571 256
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment