Thursday 30 January 2014

Re: [wanabidii] Re: MRITHI WA JK HUYU HAPA/ MIZANI TOLEO 31/01/2014

Kiukweli bila ya unafiki mm c muungi mkono lowasa kwan nadhan hata
ninyi mnamfaham kilicho mfanya ajiudhuru, ufisadi, ujuma ya mali za
umma, alafu leo tuwe wajinga tumpe nchi atuongoze c atazidi kutibia,
au si atawakaribisha tena richmond waje washirikiane naye kuinyonya na
kama c kuiuza tanzania?. Kama alifanya mahasi akiwa waziri mkuu
atashindwa je kuyafanya akiwa rais.

Watanzania wenzangu tumuogope lowasa kama ukoma. Kuwaambia watu
kumkubali lowasa ni human abuse, and it must be abolished or otherwise
to hell

On 1/30/14, Steven Stey <parokostey@gmail.com> wrote:
> Kweli waje waone
> On Jan 30, 2014 12:05 PM, "Fadhili Terri" <snochetelion@gmail.com> wrote:
>
>> Hii nchi inahitaji mtu mwenye msimamo asiyeyumbishwa yumbishwa na mtu,EL
>> is a very serious man,sio mtu wa hohe hahe,jimboni kwake kumeendelea
>> maana
>> anajua kufuatilia....we need a president who can monitor wenzake
>> wanafanya
>> nini na anayeweza kuchukua maamuzi magumu.....hata kama ana kashfa ya
>> wizi....he has proved to be a hard worker,na anatimiza wajibu wake.go go
>> EL.....tutafika tu!!!
>> On Wednesday, January 29, 2014 7:08:15 PM UTC+3, magorah15 wrote:
>>>
>>> Rgrds
>>> Magora
>>> ---------- Forwarded message ----------
>>> From: "musa khamis" <mizan...@yahoo.com>
>>> Date: Jan 29, 2014 7:05 PM
>>> Subject: MRITHI WA JK HUYU HAPA/ MIZANI TOLEO 31/01/2014
>>> To: "Magora" <mago...@gmail.com>
>>>
>>> *TUSIUMIZE VICHWA BURE*
>>> *MRITHI WA RAIS KIKWETE HUYU HAPA*
>>>
>>> *Na Mwandishi Maalum*
>>> Mwenendo wa upepo wa kisiasa ni vigumu kuwa na utabiri wa kuaminika
>>> kutokana na ukweli kuwa wakati wowote hubadilika na kugeuza mwelekeo.
>>> Hali
>>> hii inatokana na ukweli ambao hauzuiliki unaotokana na hali ya
>>> kimaumbile
>>> ya binadamu ya kuwa daima ya hamu ya kutaka mabadiliko hata bila ya
>>> kujua
>>> atafaidikaje na mabadiliko hayo.
>>> Ni kwa silika hii baadhi ya watanzania hasa vijana wasiojua nchi
>>> ilikotoka, imefikia wapi na inataraji nini sasa na kwa mustakbali,
>>> waliweka
>>> matumaini yao kwenye vyama vya upinzani kama njia ya kufikia mapinduzi
>>> ya
>>> hali zao hasa za kiuchumi kwa dhana kuwa hali ngumu ya uchumi waliyonayo
>>> inasababishwa na chama tawala CCM.
>>> Matumaini ya wenye nadharia ya kuhitaji mabadiliko kwa mujibu kisilika
>>> ya
>>> kibinadamu tu, na ambao wengi wao ni vijana wadogo, wameweka tumaini
>>> lao
>>> kwenye vyama vya upinzani hususan chama cha Demokrasia na Maendeleo
>>> (CHADEMA), ambacho katika chaguzi zilizopita kilifanya vizuri
>>> ukilinganisha
>>> na vyama vingine vya upinzani.
>>> Hata hivyo matumaini hayo yamefifia katika kipindi cha zaidi ya mwaka
>>> mmoja uliopita, baada ya kuzuka malumbano makubwa na kutoaminiana baina
>>> ya
>>> viongozi wa ngazi ya juu wa chama hicho.
>>> Katika kipindi cha mwaka mzima wa 2013 viongozi wa Chadema
>>> wamejishughulisha zaidi na mapambano ya ndani badala ya kuimarisha
>>> chama,
>>> kitendo ambacho kimekidhoofisha na kukirejesha nyuma lakini pia
>>> kuwakatisha
>>> tamaa watanzaniajuu ya uwezekano wa chama hicho kukiangusha Chama tawala
>>> katika uchaguzi wa mwaka 2015.
>>> Hali ya mapambano ndani ya chama hiki kikuu cha upinzani kumekinufaisha
>>> chama cha Mapinduzi ambacho watendaji wake wakuu walitumia mwanya huo
>>> kukiimarisha chama chao na kuwajengea wananchi dhana ya kupuuza upinzani
>>> huku serikali ikishadidisha kusimamia miradi ya maendeleo ambayo ni
>>> mtaji
>>> wenye nguvu kisiasa mbele ya jamii.
>>> Kitendo cha kutuhumiwa Mbunge wa Kigoma kaskazini Zitto Kabwe na wenzake
>>> kuwa wasaliti wa chama hicho kwa kutumiwa na CCM, kitaendeleza dhana
>>> mbili
>>> endelevu zilizo muhimu na zinazohitaji tafakuri.
>>> Kwanza ni kuwa, kuna udhaifu mkubwa ndani ya uongozi wa Chadema ngazi ya
>>> Taifa kwa kiasi kwamba CCM imeweza kupenya na kuingia ndani na kufaulu
>>> kujenga dhana ya kutoaminiana na kuusambaratisha uongozi.
>>> Pili, Chadema watapaswa kufahamu kuwa ikiwa vyanzo vyao vya uchunguzi
>>> vimebaini kuwa CCM ilijipenyeza ndani yao kwa kiasi kinachoelezwa, ni
>>> wazi
>>> pia bado ndani ya Chadema kuna CCM wengine ambao wana jukumu la
>>> kuendeleza
>>> wimbi la kutoaminiana na hivyo hali ya mambo bado si shwari.
>>> Kwa ujumla katika uwanja wa siasa za vyama vingi bado CCM inatawala kwa
>>> kigezo cha ukweli kuwa inamiliki serikali na vyombo vyake na hakuna
>>> shaka
>>> kuwa vyombo hivyo kwa pamoja vitaendelea kuhakikisha vinailinda Ikulu
>>> kuangukia mikononi mwa wapinzani na njia mojawapo ni kuwasambaratisha
>>> wapinzani kama walivyofanya kwa NCCR-Mageuzi.
>>> NCCR-MAGEUZI ni chama kilichokuwa na nguvu kubwa lakini kama ambavyo
>>> kila
>>> mmoja wetu anafahamu hadi leo chama hicho kinachechemea baada ya
>>> kutokea
>>> machafuko ya ndani kama haya tunayoyaona sasa ya Chadema ambayo kuna
>>> kila
>>> dalili inayoonyesha virusi vya ugonjwa huu kiasili vinategenezwa na CCM.
>>> Chama cha Wananchi (CUF) kama vyama vingine vya upinzani kinaendelea
>>> kushuka chati baada ya kuwa na magomvi ya ndani ambayo tunaweza kuyaita
>>> ni
>>> maradhi ya wapinzani. Chama hiki katika sura yake halisi kinaonyesha
>>> uhai
>>> wake uko mikononi mwa mtu binafsi.
>>> Ukiondoa visiwani Zanzibar ambako Maalim Seif Shariff Hamad ni
>>> mwanasiasa
>>> nyota anayeng'ara kwa siasa za upinzani visiwani humo, CUF hakina mvuto
>>> wa
>>> kisiasa popote Tanzania Bara na kila uchaguzi mkuu wa Rais unapofanyika
>>> Chama hicho huzidi kupoteza umaarufu wake na kudidimia.
>>> Kwa upande wa demokrasia ndani ya vyama vyote viwili vikuu vya upinzani
>>> CUF na Chadema havina demokrasia ya kweli ndani yake ukilinganisha na
>>> CCM.
>>> Mfano mdogo ni huu kwamba haihitajiki mkutano mkuu ndani ya Chadema wala
>>> CUF kumtambua nani atakuwa mgombea wa kiti cha Urais kwa Bara au
>>> Visiwani
>>> na anayejaribu kuhoji jambo hilo hapana shaka atafukuzwa si tu uongozi
>>> bali
>>> hata uanachama wa chama chenyewe.
>>> Sasa kama nilivyotanguliza kusema awali upepo wa kisiasa hubadilika,
>>> lakini hadi sasa kuelekea uchaguzi Mkuu wa Rais wa mwaka 2015 hakuna
>>> matumaini yanayoonyesha kuwa mrithi wa Dk Jakaya Kiwete atatokea chama
>>> cha
>>> upinzani, bali bado upepo unaashiria kuendelea utawala wa CCM.
>>> Kuwapo kwa wanasiasa wengi wenye kujikweza kwenye dhana ya sifa za
>>> kugombea nafasi hiyo, kunakiweka chama cha Mapinduzi katika wakati mgumu
>>> kutokana na makundi yaliyomo ndani kugombea nafasi hiyo muhimu katika
>>> taifa.
>>> Ukweli wenyewe ni kuwa Rais JK ana wakati mgumu sana katika shughuli ya
>>> kuutua mzigo wa uongozi wa Chama chake kwa sababu huenda chama hicho
>>> kikasambaratika kabisa au kikapata ushindi kiduchu utakaokipa serikali
>>> dhaifu yenye kutegemea maridhiano na upinzani endapo vita ya kugombea
>>> urithi wa kiti cha rais ndani ya CCM haitodhibitiwa.
>>> Ndani ya CCM kuna hazina kubwa ya viongozi wenye maadili na uwezo mkubwa
>>> kiuongozi lakini wamekuwa kimya na hawaoni busara ya kujitokeza na
>>> kujitangaza kufaa kwao kwa sababu maadili mema hayamfundishi mtu
>>> mwadilifu
>>> kujitukuza na kujinaki kwa kujipa sifa mwenyewe.
>>> Pengine wapenzi wa wanasiasa wa kambi mbali mbali hawawezi kufurahia
>>> uchambuzi huu, lakini ni ukweli usioepukika kuwa Edward Lowassa kwa sasa
>>> anatambulika kuwa ndiye mwana-CCM aliyejipanga na kufanikiwa kuwarubuni
>>> wana-CCM wengi kuamini kuwa yeye ndiye rais ajaye.
>>> Lowassa anafahamika kama mwanasiasa hodari, mwenye haiba na shakhsiya,
>>> hutambulika pia kama mtu mwenye maamuzi na uwezo mkubwa wa kusimamia
>>> maamuzi yake. Mwandishi wa uchambuzi huu ni mmoja wa watu ambao
>>> wasingependa Lowassa ashike nafasi ya Urais, lakini chuki na utashi wake
>>> binafsi hauna nguvu ya kuzuia ukweli kusimama mahala pake.
>>> Lowassa ameshikilia turufu kutokana na uwezo wake mkubwa kifedha ambao
>>> ameutumia bila ajizi kuugawa kwa mahitaji ya kijamii hususan kupitia
>>> taasisi za kidini na kumfanya Lowassa kukubalika zaidi Makanisani.
>>> Lakini hata hivyo Lowassa bado hajamaliza tofauti zake na Waislamu
>>> wanaomtazama kama mdini kutokana na kusaini mkataba (Memorandum of
>>> understanding) baina ya Serikali na Wakristo unaoipa jamii hiyo fursa ya
>>> kufaidika na fedha kutoka serikalini.
>>> Lowassa ambaye alijiuzulu nafasi ya waziri mkuu kutokana na kashfa ya
>>> kampuni iliyodaiwa kuwa hewa ya kufua umeme ya Richmond, licha ya kugawa
>>> mamilioni ya fedha kila anapoalikwa bila ukomo, amekuwa akikanusha kuwa
>>> yeye si tajiri na kwamba nyuma yake wako watu ambao anawaita marafiki
>>> wanaochangia mamilioni hayo.
>>> Jambo ambalo wengi wanajiuliza bila kupata jibu kuhusu suala la fedha
>>> anazogawa Lowassa ni je, hawa marafiki zake wanaojitolea mamilioni haya
>>> wana nia gani katika utoaji wao? Marafiki hawa wema kiasi hicho ni
>>> watanzania au ni raia wa kigeni? Nini madhumuni yao katika kumjenga
>>> Lowassa
>>> kupitia njia ya kumwaga mapesa?
>>> Wanategemea kupata nini kwa Lowassa akishaingia Ikulu? Akiwa Ikulu
>>> Lowassa anategemea kuwa na hiyari juu ya wafadhili wake hao? Wafadhali
>>> hao
>>> hawawezi kuwa na kauli yoyote juu ya mfadhiliwa? Je haiwezi kuwa watu
>>> hawa
>>> wana nia ya kumfanya Lowassa akubalike ili baadae ajikute kuwa rais
>>> wakala
>>> wa wawezeshaji wake?
>>> Uchunguzi wa uhakika wa mwandishi wa dodoso hili unaonyesha kuwa uongozi
>>> wa CCM katika mikoa mingi unamuunga mkono Lowassa kwa kiwango kwamba
>>> kuna
>>> tetesi kuwa kuna baadhi ya viongozi kimkoa wanapata posho zao ama kwa
>>> Lowassa mwenyewe au kwa watu wanaodhaniwa kuwa wapenzi wake.
>>> Kwa kuzingatia udhaifu wa vyama vya upinzani, na dhana kuwa mgombea wa
>>> CCM ndiye mwenye nafasi kubwa ya kuwa rais, na kwa namna Lowassa
>>> alivyojipanga ndani ya chama, na ukweli kuwa endapo jina la Lowassa
>>> litaingizwa katika mkutano mkuu hakuna wa kumshinda, basi hapana shaka
>>> Lowassa ana nafasi ya kuwa mrithi wa Rais Jakaya Kikwete.
>>> Hii si maana yake kuwa Edward Lowassa ndiye pekee mwana-CCM anayefaa kwa
>>> nafasi hiyo. Wapo wengine wanaotajwa tajwa na ambao wana sifa bila
>>> dosari
>>> za wazi japo hawana mamilioni ya kumwaga akiwemo Benard Membe, Dk
>>> Hussein
>>> Mwinyi, Dk Emmanuel Nchimbi na Dk Asha Rose Migiro.
>>> Wengine ambao wanatajwa kuwa wanafaa ni pamoja na Dk Harison Mwakyembe,
>>> Anne Makinda, Dk John Magufuli, na pia kuna wengine kama Samuel Sitta na
>>> waziri mkuu mstaafu Fredirick Sumaye.
>>> Kwa kadiri ya mjadala huu utakavyoendelea jambo kubwa la msingi
>>> linaloweza kutokea ni CCM kusambaratika baada ya jina la Lowassa
>>> kuondolewa
>>> katika kinyang'anyiro cha urais na Lowassa naye akajibu kwa kuamua
>>> kujiondoa ndani ya chama hicho.
>>> Endapo jambo hilo litatokea CCM itagawanyika vipande ambavyo ama
>>> vitawapa nguvu wapinzani kuchukua nchi au CCM kupata ushindi kiduchu
>>> utakaokifanya kuwa na rais atakayekuwa na wabunge wachache na hivyo
>>> kuongoza serikali dhaifu.
>>> Naomba nihitimishe makala hii kwa kuwakumbusha wanaogombea nafasi ya
>>> urais na wapambe wao kuwa mbali na kampeni zao wenyewe wasije wakasahau
>>> kuzihusisha jitihada zao na matakwa ya Rais Kikwete kama kiongozi wa
>>> nchi,
>>> lakini pia Kikwete kama mtu mwenye shakhsiya na mvuto maalum wenye nguvu
>>> na
>>> ushawishi wake binafsi.
>>> Lakini kubwa kuliko yote msilolijua wagombea masikini na matajiri, ni
>>> hilo la kuwa Rais wa Tanzania atakayemrithi Jakaya Kikwete ni huyo hapa,
>>> *"Mgombea
>>> ambaye ataungwa mkono na Jakaya mwenyewe iwe wakati huo kikatiba
>>> anaruhusiwa kumfanyia kampeni au haruhusiwi. *
>>> Nafahamu kuwa wako watakaosema ya kuwa hata viongozi waliomtangulia JK
>>> walishindwa kuwaweka warithi waliowataka wao kwa kuwa walikinzana na
>>> upepo
>>> wa kisiasa. Lakini upepo wa kisiasa unaotoa ishara ya kubadilishana
>>> uongozi
>>> baina ya Rais Kikwete na mrithi wake uko wazi kuwa miongoni mwa watu
>>> anaowafikiria yeye basi mmoja wao ndiye atakayemrithi. Kama wengine
>>> walishindwa kuna kila uwezekano JK hatoshindwa. Kwa hiyo usisumbuke na
>>> kuumiza kichwa chako bure atakayeungwa mkono na Kikwete mwenyewe ndiye
>>> rais
>>> ajaye.
>>>
>>>
>>>
>>>
>>>
>>>
>>>
>>>
>>>
>>>
>> --
>> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>>
>> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
>> ukishatuma
>>
>> Disclaimer:
>> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any
>> legal
>> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must
>> be
>> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree
>> to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>> ---
>> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
>> "Wanabidii" group.
>> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
>> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>>
>
> --
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment