Wednesday 29 January 2014

[wanabidii] Kero ya ujenzi wa barabara ya Morogoro: Serikali na Kamati ya Bunge zichukue hatua

TAARIFA KWA UMMA

Taarifa inatolewa kwa umma kwamba kwa nafasi yangu kama Mbunge wa Jimbo la Ubungo, nimemtumia ujumbe Waziri wa Ujenzi, Ndugu John Magufuli ili atoe kauli ya Serikali juu ya ujenzi wa Barabara ya Morogoro, ambao umegeuka kuwa kero kubwa kwa wakazi wa jimbo hilo na watumiaji wengine kwa ujumla;

Katika ujumbe huo ambao hadi naandika taarifa hii Waziri Magufuli hajaujibu, nimeitaka Serikali iweke wazi mkataba wa 
ujenzi huo ili wananchi waweze kujua iwapo kampuni ya Strabag, Wakala wa Mabasi Yaendayo Kasi (DART) na Wakala wa Barabara (Tanroads) wanazingatia masuala ya kitaalam katika kufanya upanuzi na ukarabati wa barabara kama hiyo.
Ujenzi huo wa Barabara ya Morogoro unalalamikiwa na watumiaji wote, kuanzia watembea kwa miguu, waendesha baiskeli, pikipiki na magari, hasa katika maeneo kadhaa;

  • Kusababisha foleni kwa kiwango ambacho ujenzi umegeuka kuwa kero na usumbufu mkubwa.
  • Kukosekana au kuzibwa kabisa kwa barabara za kuingia na kutoka barabara kuu.

Aidha, kutokana na adha kubwa wanayoipata wakazi wa Jimbo la Ubungo, Jiji la Dar es Salaam na watumiaji wengine kwa ujumla wa barabara hiyo, nimemtumia ujumbe Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Peter Serukamba, kuhusu umuhimu wa kamati yake kulifanyia kazi suala hilo kwa haraka.

Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Miundombinu amejibu ujumbe wangu, akiahidi kwamba wataingiza katika ratiba ya shughuli za kamati, ikiwa ni pamoja na kutembelea eneo husika kujionea namna ambavyo wananchi wanahangaika kuingia na kutoka Dar es Salaam au kwenda maeneo mengine ya jiji kwa kutumia barabara hiyo.

Kwa niaba ya wananchi wa Ubungo na watumiaji wote wa Barabara ya Morogoro, natarajia Kamati ya Bunge itaona umuhimu wa kuisimamia na kuiagiza Serikali kuhakikisha hatua za haraka zinachukuliwa ili kuhakikisha ujenzi huo haugeuki kuwa kero na usumbufu mkubwa kama ambavyo imekuwa hivi sasa.

Imetolewa leo Januarri 29, 2014 na;
John Mnyika (MB)

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment