Wednesday 29 January 2014

[wanabidii] Diwani wa CHADEMA Majengo, Kahama avuliwa uanachama

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA jana kilitangaza kumvua uanachama Diwani wake wa Kata ya Majengo wilayani Kahama kwa madai ya ukiukaji wa taratibu za uongozi wa chama hicho.

Uamuzi wa kumvua uanachama diwani huyo Bobson Wambura umetangazwa na Katibu Uenezi wa Chama hicho Taifa, John Mnyika kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Kahama.

Katika mkutano huo Mnyika ameuagiza uongozi wa CHADEMA ngazi ya wilaya na MKoa kuchukua hatua haraka za 
kumfukuza diwani huyo na kutoa taarifa mapema iwezekanavyo.

Hata hivyo Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Kahama, Juma Protas amesema taratibu zote za kumfukuza diwani huyo zimekamilika na kuwa tuhuma kubwa inayomkabili ni ya kuunda njama za kuenguliwa kwa mgombea wao wa Udiwani kwenye uchaguzi mdogo wa Kata ya Ubagwe.

Kwa upande wake Bobson amesema uamuzi wa viongozi hao uko sahihi kwa kuwa ni maoni yao na kwamba haki yake itapatikana kisheria kwa kuwa kufukuzwa kwake ndani ya chama hicho kunatokana na sababu za kisiasa.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment