Wednesday 29 January 2014

Re: [wanabidii] MAELEZO YA Mwl Lwaitama baada ya Kushushwa kwenye Ndege ya PrecisionAir

Nakubaliana nawe Mwijage kuwa pande zote lazima ziangaliwe. Kwa kuangalia kwa makini utagundua kwamba hili swala halikuwa jepesi kama tunavyolijadili hapa. Najua kuna mambo yametokea katika ya Dr Lwaitama na wahudumu wa ndege kabla ya kwenda kwa rubani. Ila pia hata rubani sidhani kama alikurupuka bila kutathmini hili jambo wakijua kuwa wanaweza ksuhtakiwa kama hawatafuata sheria. Kwa hiyo nafkiri mzee naye amekuwa sababu kubwa ya yaliyotokea. Swala la lugha msafiri haliwezi kuwa tatizo hata siku moja kama wewe una nia ya kusafiri kufika kwenu maana lugha ya maelezo haiwezi kuwa sababu ya kuahirisha safari yako. Wakati mwingine mtu akiona moto umewaka anaomba msamaha ila hapa hatuoni kama aliomba msamaha baada ya hayo yote kutokea hata polisi kumtoa. Angeomba radhi baada ya kuona polisi angehama na kuomba msamaha asingeshuka! Of course kwa mila ya kwetu mtu mzima huwa hutoi gesi ila watoto!


On Wednesday, 29 January 2014, 7:53, Ludovick Simon Mwijage <bugabo18@hotmail.com> wrote:
Tatizo ni kwamba, wakiruhusu kila abiria kuhoji utaratibu na misingi ya utendaji wa kazi yao ndani ya ndege, haiwezi kujenga, na/au, kuimarisha mazingira bora kwa usafiri wa anga.
 
Inaelekea Rubani aliyemteremsha alizingatia utaratibu wa taaluma yake. Tuwe wakweli kidogo, ili akraba wengine wasije wakajikuta kwenye misukasuko ya namna hii. Niko upande wa Dk Lwaitama, lakini upande mwingine wa sarafu sharti utazamwe pia.


 

 
> Date: Wed, 29 Jan 2014 06:49:09 +0000
> Subject: Re: RE: [wanabidii] MAELEZO YA Mwl Lwaitama baada ya Kushushwa kwenye Ndege ya PrecisionAir
> From: elisamuhingo@yahoo.com
> To: bugabo18@hotmail.com; wanabidii@googlegroups.com
>
> Alivunja makubaliano kwa kutaka ufafanuzi kuhusu alipokaa na lugha anazozijua? Tena alitaka kuwasaidia siku nyingine kazi hiyo ifanyike wakati wa ticketing.
>
> ----------
> Sent from my Nokia Phone
>
> ------Original message------
> From: Ludovick Simon Mwijage <bugabo18@hotmail.com>
> To: "Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
> Date: Tuesday, January 28, 2014 11:29:41 PM GMT+0100
> Subject: RE: [wanabidii] MAELEZO YA Mwl Lwaitama baada ya Kushushwa kwenye Ndege ya PrecisionAir
>
>
>
>
> PrecisionAir ilimkubali Dk Lwaitama kama mteja wao ilipomuuzia tiketi na kukubali kumsafirisha hadi mwisho wa safari yake.
>
> Lakini wakati huo huo, kwa kununua tiketi ya PrecisionAir, Dk Lwaitama naye aliingia makubaliano nao kwamba angefuata utaratibu wanaoutumia wao kuwasafirisha abiria kwa njia ya anga.
>
> Inaweza kudaiwa kwamba Dk Lwaitama alivunja makubaliano hayo alipokataa kufuata utaratibu wao, baada ya kupanda ndege yao.
>
> Kama Dk Lwaitama hakuridhika na utaratibu wanaoutumia PrecisionAir, basi angetuma malalamiko yake, na mapendekezo, kwenye mamlaka yanayohusika na pengine akafuatilia malalamiko yake kwa kuvihusisha vyombo vya habari. Kufanya hivi, huenda kungeepusha rabsha kwa abiria wenzake na kadhia yote hii.
>
> Suala la lugha aliloliibua ni muhimu sana. Ndio maana wengi tuko upande wake. Lakini inaelekea aliibua suala hili kwenye jukwaa lisilo sahihi na bila kuelewa chanzo cha PrecisionAir kutumia Kingereza kwa abiria wenye kiti karibu na mlango wa dharura.
>
> Ingekuwa vizuri zaidi kama tatizo hili lingemalizikia nje ya vyombo vya kukazia sheria na mahakama. Kwamba, Dk Lwaitama anafahamu Kingereza, inaweza kutumiwa na mawakili wa PrecisionAir kutaka kujua nia yake ilikuwa nini alipokataa kupokea maelekezo kwa lugha anayoifahamu. Ingekuwa jambo jingine kama Dk Lwaitama angekuwa hafahamu Kingereza.
>
> Kwa upande mwingine, huenda PrecisionAir wasimuombe radhi kama baadhi yetu tunavyofikiri. Kwani, wakifanya hivi, watakuwa wanamkaribisha Dk Lwaitama kuwafungulia kesi ya madai. Haya labda ndio mambo tunayopashwa kuyatafakari kwa faida ya Dk Lwaitama badala ya kulaani tu mwenendo na utaratibu unaotumiwa na PrecisionAir.
>
>
>
>
>
> > Date: Tue, 28 Jan 2014 20:04:58 +0000
> > Subject: Re: [wanabidii] MAELEZO YA Mwl Lwaitama baada ya Kushushwa kwenye Ndege ya PrecisionAir
> > From: hosea.ndaki@gmail.com
> > To: wanabidii@googlegroups.com
> >
> > Yeye ndo kachelewesha ndege kusafiri na kusumbua abiria wengine, kwanza alikuwa amekaa mlango wa dharura sasa kuambiwa uhame kiti ndo azue timbwili lote hilo kweli?
> >
> > ----------
> > Sent from my Nokia phone
> >
> > ------Original message------
> > From: <bonnyluv84@hotmail.com>
> > To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
> > Date: Tuesday, January 28, 2014 9:02:11 PM GMT+0400
> > Subject: Re: [wanabidii] MAELEZO YA Mwl Lwaitama baada ya Kushushwa kwenye Ndege ya PrecisionAir
> >
> >
> > Pole sana, itakuwa imekusumbua hii hali.Muda wako, pesa uliyolipa na hukusafiri, usumbufu uliupata, hukufika Bukoba, mambo ulipanga kuyanya huko Bukoba yamekwama, umedhalilika, umesingiziwa kuwa umefanya fujo, umelazimishwa kutojua kiingereza while wa ni mwalimu wa lugha na unakifahamu zaidi yao na zaidi wamesababisha uwasababishiye wengine usumbufu.
> > Zaidi ya kukuomba radhi hawa precision inatakiwa wakulipe pesa kufidia vyote hivyo ili hiwe fundisho tosha.
> > Pole tena.
> > --
> > Sent from myMail app for Android
> > Tuesday, 28 January 2014, 03:17PM +0300 from Tracy John Kimambo <tracykwetu@gmail.com>:
> > Ndugu wanazuoni maelezo niliyotoa mtandao wa wanamabadiliko juzi Jumapili haya hapa chini. Kesho Jumatano kwenye The Citizen , kama wataichapisha makala ya column yangu, ninajadili hoja kuu ya kisanga hiki ambayo ni swala la kutumia Kiswahili kutoa maelezo kwa abiria anayekaa karibu na mlango wa dharura. Yule mhudumu alikuwa jeuri na mwenye kutoelewa maana ya kuwa mhudumu wa ndege lakini nadhani hoja kuu ni kwanini wahudumu wanaelekezwa eti lazima kutoa maelezo ya kufungua mlango wa dharura lazima kutolewa kwa Kiingereza wakati maelezo mengine kwa abiria wote ni kwa Kingereza na Kiswahili?
> > Tena MIMI NIMEWAHI KUTOA USHAURI kama HUU HUU KWA MHUDUMU MWINGINE safari nyingine na yule mhudumu
> > alinijibu kwa ukarimu kuwa yeye alikuwa anafuata maelekezo tu na mimi nikampa pole yakaisha. Huyu wa juzi alikuwa apendi kupewa maoni na mtu aliyedhani mtu wa hadhi ya chini sana kwake ...maana nilikuwa kama kawaida yangu naonekana kibabu tu kisichozoea mambo ya usafiri wa ndege.
> > Kama wahudumu wasingekuwa wamefundishwa kikasuku eti lazima kutoa maelekezo ya kufungua mlango wa dharura kwa Kiingereza hakuna tatitizo sakata llote lisingetokea. Pia rubani naye angetumiabusara na kumtuma afisa wa juu ndani ya ndege kuhoji majirani wa nilikokaa angegundua yule mhudumu alikuwa mwongo tu maana hakukuwepo hata majibizano ya kupaza sauti kabisa... mimi nilibaki mdomo wazi aliponiambia yule mhudumu wa kwanza ninaweza kusimamisha ndege ukatolewa nje kama tishio na mimi nikamjibu kwa upole ya nini yote hayo ndugu yangu maana mimi najua Kiingereza na wewe endelea na maelezo yako kwa Kiingereza... lakini nadhani siku hiyo labda aliamuka vibaya ..Bado sijaamini angeweza kutunga uongo wa eti kuna mtu anafanya fujo vile tu nilitoa maoni yangu tu tena kwa tabasamu langu la kwaida ninapokuwa na huzuni juu ya mambo yasiyo na mantiki yanayotendeka duniani. MAELEZO YANGU YA JUMAPILI HAYA HAPA CHINI.
> > "Yaliyonikuta Mwanza
> > Nawashukuru wote kwa kunipa pole. Wanasheria wa rafiki yangu binafsi Dr Antony Diallo, mmiliki wa Star Tv na Radio Free Africa, na wanasheria waliotumwa na Nd. Sungusia wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu ( Legal and Human Rights Centre, LHRC) chenye makao makuu Dar es Salaam walifika kituo cha polisi cha kiwanja cha ndege Mwanza na wakafanikiwa kuniwekea dhamana na hivyo niko nje kwa dhamana vinginevyo ningelala selo ndugu zangu _Kesho nitaripoti polisi kufuatilia juu ya kesi iliyofunguliwa dhidi yangu na Precision kama itaenda mahakamani au vipi.
> > Kilichotokea kifupi ni hivi. Nilipanda ndege Flight PW 0492 iliyotarajiwa kuondoka Mwanza saa 3 dakika 50 asubuhi kuelekea Bukoba. Nilikuwa nimekaa kiti namba 2B na mtafiti mmoja anayefanya kazi Maruku Tea Estate huko Bukoba alikaa kiti na. 2A kwenye dirisha kushoto kwangu. Wakati ndege inaanza kukuelekea inakoruka alikuja mhudumu wa kike akatuuliza na yule mwenzangu kama tunajua Kiingereza na mimi nikasema kwa utani huku nikicheka kuwa tunajua kidogo. Yule muhudumu gafla akatahamaki akasema kama sijui kiingereza aniamishe kiti.
> > Mimi nikamjibu kuwa hakukuwa na haja maana mimi najua kiingereza maana ni mwalimu wa siku nyingi wa Kiingereza lakini nilichokuwa nashangaa ni kwa nini nyie wahudumu mnapenda kutoa maelezo kwa Kiingereza wakati mgeyatoa maelezo hayahayo kwa Kiswahili mara baada ya kujua kuwa sisi ni Watanzania na tunajua Kiswahili vizuri zaidi kuliko Kiingereza. Binti huyo nikaona ametaamaki na kuanza kusema lazima niteremshwe.
> > Mimi nilidhani masihala maana niliwahi kutoa ushauri huu hapo nyuma kwa mhudumu mwingine wa Precision Air na yeye alinijibu kwa heshima kabisa kuwa wao maelezo wameambaiwa lazima wayatoe kwa Kiingereza. Mara yule mhudumu wa kwanza akaondoka akaja mhudumu mwingine wa kike akasema kama sijui Kiingereza niamishwe nikamjibu wa taratibu na tabasamu langu la kawaida ninalolitoa katika mazingira kama haya ya dalili za kukosekana busara na mtoa huduma kukimbilia kwenye mambo ya kugombana bila sababu kuwa hakukuwa na tatizo jamani kwani Kiingereza nakijua na nilichokuwa nimempa mwenzake ni ushauri tu.
> > Yeye wala hata hakuzungumza na mimi tena aliondoka ndipo nikasikia rubani akitangaza eti kuna tatizo la kiusalama na ndege itachelewa kuruka ili litatuliwe. Mara polisi wane hivi na muhudumu wa Precision wa kiume mmoja wakaingia ndani ya ndege na kusimama mbele yangu nilipokuwa nimekaa na kufunga mkanda. Mhudumu akaniambia inabidi au nikuamishwe kiti au ni ushushwe. Wakati huo huo wale polisi wakang'angania eti lazima nishuke. Nikauliza nitii amri ya nanai sasa? Polisi mmoja aliyeonekana kama mwenye kuwaongoza wale polisi wenziwe akainama akanifungua mkanda wa kwenye ndge akaninyanyua mkuku mkuku na kunitoa nje ya ndege.Hata begi zangu mbili za mkononi ilibidi niombe nikiwa chini nipewe.
> > Abiria waliokuwa karibi na nilipokuwa walishangaa na kusema kwani amefanya nini huyu baba . Lakini waliokuwa nyumba mabali hawakujua kilichotokea zaidi ya manaeno waliokuwa wamelishwa na rubani na wlae wahudu kuwa kuna baba kule mbele amnaleta fujo inabidi ateremshwe. Nikapelekwa kituo cha polisi hapo uwajani huku nikisikia wakinongonezana kuwa lazima kuniweka selo (lockup ).
> > Nikafanikiwa kumpigia Dr Antony Dialo simu akazungumza nao wale askari na wakaanza kuchukua maelezo yangu nikiwa nimeketi ofisini kwao kwenye kochi walau badala ya kuwekwa lockup... Baadaye nilipigia Ndugu Sungusia wa LHRC na Dr Antony Diallo wote wakanitumia wanasheria walionisaidia kuandika na kutia saini maelezo yangu. Wale wanasheria wakaniombea dhamana nikapata nikaruhusiwa kutoka pale kituoni lakini nikaamriwa kuripoti kituoni pale asubuhi kesho Jumatatu kwa maelekezo zaidi.
> > Wakati huo ndege ile ya Precision iliondoka ikaenda Bukoba na ikarudi tena baadaye kutoka Bukoba na ndipo nikamuona yule muhudumu wa kike wa pili eti ndiye anatoa maelezo juu ya eti mimi kufanya fujo. Yule muhudumu aliyewadanganya wenzake wote pamoja na rubani kuwa eti mimi nimefanya fujo wala hakutoka nje ya ndege iliporudi kutoka Bukoba kutoa maelezo.
> > Katika sakata lote ili yule abiria aliyeketi kushoto kwangu siti namba 2A wala hakuhojiwa na rubani wa ndege ile kujiahakikishia kama madai ya eti mimi kufanya fujo yalikuwa ya kweli na wala hata polisi waliotekereza maelekezo ya rubani yakuniondoa ndani ya ndege mkuku mkuku hawakujiangaisha kuuliza yule abiria jirani yangu aliye kuwa siti 2A kama ni kweli mimi nilifanya fujo yoyote au nilitoa maoni tu juu ya matumizi ya Kiswahili katika kutoa maelezo ya juu ya kipi cha kufanywa wakati wa dharura.
> > Hadi sasa bado sijaelewa kisa kilichomfanya yule mhudumu atahamaki na kunibambikizia tuhuma ya kufanya fujo yarabi... maana hakukuwepo hata na kubadirishana maneno kwa ukali kwa upande wake au wangu. Nimebaki nimeduwaha hadi sasa kuwa hivi ni kweli miaka zaidi ya 50 baada ya uhuru nimekatishiwa safari yangu kwa kutoa maoni tu ambayo mhudumu yule wa shirika la ndege binafsi angeweza kupuuza. Bado sipati maelezo kwa nini haya yalinitokea zaidi ya kuhisi kuwa haya ni matokeo ya mfumo wa kuandaa wahudumu wa ndege wa Precision unaowavimbisha kichwa kuwa kwa kutamka kwa rubani kuwa kuna abiria anafanya fujo hiyo inatosha abiria yule kunyanyaswa kama nilivyonyanyaswa na kudhalilishwa kwa kutuhumiwa kufanya fujo ndani ya ndege. Lazima nikiri hata hivyo kuwa maafisa Kadhaa wa kituo cha polisi cha uwanja wa ndege pale Mwanza walinionesha uungwana sana na walikuwa wakarimu kwangu kuliko hata wahudumu wale wawili wa Precsion Air.
> > Mwl. Lwaitama"
> > JANA POLISI Mwanza WALIKUWA WAKARIMU MARADUFU NA WAMENIPA SIKU KADHHA ZA ZIADA ZA DHAMANA WAKATI WAKIENDELEA NA UPELEZI WA KAMA TUHUMA ZILIZOELEKEZWA KWANGU ZILIKUWA ZA KWELI. WATAWAHOJI WALIOKAA KARIBU NA MIMI NA SIMU ZAO WAMEPATA na sina shaka ukweli ukijulikana labda hata Precision watataka kuniomba radhi maana mimi ni mteja wao mkuu.
> > Mwl. Lwaitama
> > --
> > Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
> >
> > Kujiondoa Tuma Email kwenda
> > wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
> >
> > Disclaimer:
> > Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> > ---
> > You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
> > To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> > For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out .
> >
> > --
> > Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
> >
> > Kujiondoa Tuma Email kwenda
> > wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
> >
> > Disclaimer:
> > Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> > ---
> > You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
> > To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> > For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
> >
> > --
> > Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
> >
> > Kujiondoa Tuma Email kwenda
> > wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
> >
> > Disclaimer:
> > Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> > ---
> > You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
> > To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> > For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>
>
>
> --
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>
> --
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.


0 comments:

Post a Comment