Friday 31 January 2014

Re: [wanabidii] TAMKO LA JOHN SAMWELI MALECELA KUUNGA MKONO KAULI YA PAUL MAKONDA

Daaah Reuben umenifurahisha sana, ati umesahau Jina la JUMANNE unasema nani nani sijui??!! ha ha haaaaa usizuge ni JUMANNE kaka. Kinachowasibu hawa ndugu zetu ni kwamba, ile taasisi yao walishaigeuza kuwa kama kampuni tu yaani mwenye mtaji mkubwa anafanya transaction sasa wale wenye mitaji midogo wanapiga kelele!! lakini hakuna mtu mwenye ujasiri wa dhati wa kuweza kumbananisha jamaa, mbona timu ni ileile iliyoshindwa kuvua ati nini vileeee!!!?? magamba enhee?? yeah magamba sasa kama gamba lilishindikana jamaa kapenya, kwenye nec ana  ushawishi mkubwa japo ulchaguzi uliitishwa mpya sasa timu ileile inawezaje kuzuia leo?????

Tafakari chukua hatua

On Friday, January 31, 2014 8:36 AM, Reuben Mwandumbya <ipyana75@yahoo.com> wrote:
Lutgard;
Ni kweli a pair of wrongs cant make a single right, kitu kibaya ni kwamba, hawa Waheshimiwa huwa wanajua tumesahau/tumesamehe kwa maana kwamba,dhambi ile ile ya John anaitumia kumhukumu mwenzake as kwamba alipoifanya yeye haikuwa dhambi au tumesahau.

Ni aibu kwa Watu wazima kama hawa pamoja na washauri wao.
 
Reuben

From: Lutgard Kokulinda Kagaruki <lutgardk@yahoo.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Friday, January 31, 2014 8:27 AM
Subject: Re: [wanabidii] TAMKO LA JOHN SAMWELI MALECELA KUUNGA MKONO KAULI YA PAUL MAKONDA

Reuben,

Two wrongs don't make one right! John, Eddy, wote sawa tu!! LKK

On Friday, January 31, 2014 8:07 AM, Reuben Mwandumbya <ipyana75@yahoo.com> wrote:
Comrades;
Phrase hii ya Mh. John imenivuta kukumbuka Mwaka 1995'

''Sisi tulikijenga chama hiki kwa taabu sana hapakuwa hata mtu mmoja aliyediriki kutumia fedha zake kutaka madaraka. Nidhamu, busara na uchungu wa rasilimali za taifa hili kwa maslahi ya wananchi ndio vilituongoza kufuata misingi na maadili ya uongozi ndani ya chama na serikali, ndio maana tunaumia sana kuona chama sasa kinataka kutekwa na wenye fedha kwa uchu wa madaraka, mpaka tunashangaa na kujiuliza hizi pesa wanatoa wapi? Na haya madaraka wanayotaka kwa kununua ni kwa maslahi ya nani? Huku watanzania wakiendelea kuwa maskini''.

Mh. Mwl JKN alikuwepo wakati huu na moja ya mambo yaliyo mdisqualify John ilikuwa ni hizi fedha anazoziona kwa wenzake kwamba zina madhara kwa Taifa na Chama,kama nakumbuka vizuri nazani alifikia hatua ya kusilimu na kuitwa nani nani sijui!
Sasa je yeye wakati huo alikuwa bado mdogo? Mana kuna kausemi kanasema 'kua uyaone'

Reuben

From: Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Thursday, January 30, 2014 4:42 PM
Subject: [wanabidii] TAMKO LA JOHN SAMWELI MALECELA KUUNGA MKONO KAULI YA PAUL MAKONDA

----- Forwarded Message -----

Boxbe This message is eligible for Automatic Cleanup! (hamisznz@gmail.com) Add cleanup rule | More info
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI --30/01/2014

Ndugu zangu waandishi wa habari, awali ya yote naomba niwasalimie na niwapongeze kwa kufika -mwaka mpya 2014, pia naomba niwapongeze kwa kazi kubwa ambayo mmekuwa mkiifanya hasa kuhakikisha watanzania wanapata habari kwa kila jambo linaloendelea kila kona ya taifa letu la Tanzania.

Ndugu waandishi wa habari nimewaita hapa ili kuzungumza nanyi na mnisaidie kufikisha ujumbe kwa watanzania hasa kuhusu jambo hili ambalo limekuwa gumzo kwa watanzania wengi la mbio za urais 2015 kwa baadhi ya watu ndani ya chama changu cha mapinduzi (CCM), kilichonisukuma zaidi na kupata hamu ya kuongea nanyi ni baada ya kumsikia -na kumuona kijana wetu ndani ya chama cha mapinduzi bwana Paul Makonda akiwa na ujasiri wa kukemea vitendo mambo haya yanayofanywa na baadhio ya viongozi bila uwoga wowote naomba tuchukue fursa hii kumpongeza sana kijana huyu.

Nadiriki kusema nampongeza kijana huyu hasa kwa kauli zake nzito na za kijasiri kwa maslahi ya chama changu cha CCM ili chama kiendelee kupendwa na kuchaguliwa na watanzania.

Pia itakuwa si busara kama sitawapongeza vijana wangu katibu mkuu wa chama ndugu ABDULRAHMAN KINANA na NAPE NNAUYE kwa juhudi zao za dhati za kujenga chama na kuendelea kuwaeleza wananchi juu ya misingi bora ya chama cha mapinduzi (CCM) kwa kuwakemea viongozi wasiofaa bila kujali cheo na umaarufu wao ndani ya chama na serikali, nawaomba waendelee -na juhudi zao hizo nami naziunga mkono juhudi zao na kama kuna watru wanaowabeza naomba wasijali kwani kukemea viongozi wasiofaa ndani ya chama na serikali ni msingi wa chama chochote kilichounda serikali.

Aidha nawaomba watanzania wenzangu wazalendo wasikubali kukatishwa tama na kikundi cha watu wachache wasio na mapenzi mema na taifa letu ambalo limekuwa mfano wa kuigwa kwa amani, upendo, utulivu na mshikamano urithi tulioachiwa na baba yetu wa taifa mwalimu julias kambarage nyerere ndani na nje ya mipaka ya bara letu la afrika.

Ndugu zangu waandishi wa habari naomba niwaambie kuwa msemaji wa UVCCM kijana wetu Paul Makonda namuunga mkono kwa -kitendo chake cha ujasiri cha kumkemea ndugu EDWARD NGOYAI LOWASSA bila uwoga kwa jinsi anavyokivuruga chama chetu kwa lengo la kutaka urais 2015 huku secretariet ya chama ikiwa imekaa kimya wakati inajua kuwa muda wa kuanza mbio hizi bado na kufanya hivi kwa sasa ni kukiuka misingi na katiba -ya chama. Hapa najiuliza kuwa ile misingi imara ya uongozi ndani ya chama chetu cha mapinduzi iko wapi? Mpaka tumuachie mototo ndio akemee haya? Je, hapa chama kiko wapi?

Ukweli ni kwamba wanachama wetu na vijana wamekuwa njia panda huku wakitamani kusikia tamko au karipio la chama juu ya suala hili la harakati za urais 2015 bila mafanikio.

Naomba niseme kuwa bila kuwa na karipio au tamko la chama, hawa wanaotumia pesa zao hadharani kwa lengo la kutafuta umaarufu na ushawishi kwa vijana ili kupata madaraka wanaharibu misingi yetu bora ya uongozi iliyowekwa na waasisi wetu ndani ya chama.

Kinachonisikitisha zaidi ni kuona juhudu za uongozi wa sasa wa chama ngazi ya juu ikiwa ni pamoja na sekretarieti inayoongozwa na katibu mkuu ABDULRAHMANI KINANA na katibu mwenezi NAPE NNAUYE za kutetea chama hiki zinatiwa mchanga.

Ninaomba juhudi hizi zisibezwe na watu wenye nia njema na chama. Ukweli ni kwamba vijana hawa wamekuwa na juhudi kubwa sana ya kujenga na kuimarisha chama chetu -kwa wananchi kila pembe ya taifa letu kwa kukemea na kueleza misingi ya uongozi bora. Swali: Je! Chama hakioni haya mpaka vijana ndio waone?

Kwa hili ni lazima tubadilike ili kujenga chama chetu na naishauri -secretariet ya chama lazima ichukue hatua mara moja, kijana huyu paul makonda asingesema haya yote kama hana uhakika wa ushahidi wa wa haya aliyoyasema na nampongeza sana.

Vijana na wanachama wengi wa CCM wamekuwa na hamu kwa muda mrefu ya kutaka kujua msimamo wa chama chao bila mafanikio na ndio sababu ya baadhi ya-wengine kupoteza mwelekeo.

Sisi tulikijenga chama hiki kwa taabu sana hapakuwa hata mtu mmoja aliyediriki kutumia fedha zake kutaka madaraka. Nidhamu, busara na uchungu wa rasilimali za taifa hili kwa maslahi ya wananchi ndio vilituongoza kufuata misingi na maadili ya uongozi ndani ya chama na serikali, ndio maana tunaumia sana kuona chama sasa kinataka kutekwa na wenye fedha kwa uchu wa madaraka, mpaka tunashangaa na kujiuliza hizi pesa wanatoa wapi? Na haya madaraka wanayotaka kwa kununua ni kwa maslahi ya nani? Huku watanzania wakiendelea kuwa maskini.

Mfano hivi karibuni baadhi ya viongozi wa chama ngazi ya juu wamejibishana kwenye vyombo vya habari,vitendo hivi havina tija kwa chama na wala havileti umoja na mshikamano ambao umedumu ndani chama kwa muda mrefu.

Mwisho Ninaomba sekretarieti ichukue hatua haraka kama alivyoomba kijana wetu makonda na kweli kuchelewa kuchukua hatua jambo hili kumejionyesha wazi kwamba utaleta kutokuelewana ndani ya chama kusiko kuwa na lazima.

JOHN SAMWELI MALECELA

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment