Wednesday 29 January 2014

[wanabidii] JESHI LA POLISI LASAKA JAMBAZI LILILOUA WATU WANANE HUKO RORYA, TARIME

Ndugu zangu waandishi wa habari, nimewaiteni hapa kwa dharura, ili kuweza kuwafahamisha hali halisi ya mauaji yaliyotokea katika siku za hivi karibuni katika mkoa wa Kipolisi wa Tarime Rorya.
 
Mnamo tarehe 26 Januari, 2014 majira ya saa 12.00 asubuhi huko katika kijiji cha Mogabiri
katika mkoa wa kipolisi Tarime Rorya, jambazi asiyefahamika kwa jina aliwaua kwa risasi Zakaria Mwita Marwa miaka 28 na Erick Lucas Maranya miaka 24 baada ya kukutana nao njiani. Siku hiyohiyo, majira ya saa 4:00 usiku, katika kijiji hichohicho cha Mogabiri, jambazi huyo alimuua Robert Kisiri miaka 45 baada ya kuvamia Grocery inayomilikiwa na Chacha Ryoba na kumjeruhi mtu mwingine mmoja. Tarehe 27 Januari, 2014 majira ya 11:30 alfajiri katika kijiji cha Mugabiri, jambazi huyo alifanya mauaji tena kwa kumpiga risasi David Mwasi Matiko miaka 39 na kumpora simu yake aina ya Nokia. Katika tukio hilo, pia, alimjeruhi Machungu Nyamahemba miaka 19 ambaye bado amelazwa katika hospitali ya Tarime kwa Matibabu. 

Siku hiyohiyo ya tarehe 27 Januari, 2014 majira ya saa 2:00 usiku katika kijiji cha Nkende, jambazi huyo alimuua kwa kumpiga risasi Juma Marwa Nyaitara miaka 30. Baada ya kufanya mauaji hayo, jambazi huyo aliwapora simu zao za mkononi Chacha Magige na Masero Marigiri wote wa kijiji cha Nkende. Usiku wa kuamkia tarehe 28 Januari, 2014, jambazi huyo aliendelea kuua watu wengine watatu ambao bado majina yao hayajafahamika. Mtu mmoja alipigwa risasi wakati akiendesha pikipiki
katika kijiji cha Nkende na wengine wawili waliuawa baada ya kukutwa na jambazi huyo wakiwa wanatengeneza gari lililokuwa limewaharibikia katika kijiji cha Mogabiri.

Hadi sasa juhudi kubwa za kumsaka jambazi huyo zinaendelea kufanyika na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama pamoja na wananchi.  Aidha, mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernesti Mangu, ametuma timu maalum kutoka makao makuu ya jeshi la Polisi inayohusisha kamisheni ya Oparesheni, Upelelezi na Intelijensia kwenda kuongeza nguvu katika juhudi zinazofanyika na ngazi ya mkoa kuhakikisha kwamba, jambazi huyo anakamatwa upesi ili kuondoa hofu kwa wananchi.

Jeshi la Polisi nchini, linatoa wito kwa wananchi wote kutoa ushirikiano ili jambazi huyo aweze kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria haraka. Mwananchi mwenye taarifa za mhalifu huyo anaweza kutumia namba ya simu ifuatayo 0754 785557.

Mkuu wa Oparesheni wa Jeshi la Polisi,
 Kamishna Paul Chagonja

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment