Thursday 30 January 2014

Re: [wanabidii] Re: MAHAKAMA YA KADHI - KUPATIKANA HIVI KARIBUNI

Sidhani kama ni vyema kuliweka hili kwenye katiba maana, hata hili la vatican halipo kwenye katiba. Katiba ina toa dira, na sio kila kitu ni cja kuweka kwenye katiba. Hata hivyo katiba yetu ni kubwa sana ukilinganisha na ya taifa kama Marekani. Katiba inatakiwa kutoa dira, kisha, kila dira inatakiwa iwe na miongozo inayofafanua utekelezaji wa dira fulani iweje. Hadi hivi sasa, katiba inatambua na imeweka uhuru wa kuabudu. Hili ni sawa, na hili ni la msingi zaidi, kuliko hili  ambalo mnataka liwekwe kwenye katiba ingali nila upili!

Sorry for being this much blunt!


2014-01-25 Idd Makame <iddmakame@gmail.com>
NAOMBA TUWE PAMOJA ILITUWEZE KUELEWANA JUU YA HAYA MASUALA KWA WALE VICHWA MKUKI WASIOTAKA KUELEWA UKWELI.
1. Uhusiano wa Jumuiya za kimataifa usiwe wa kibaguzi,katiba itamke kuwa Tanzania inaweza kujiunga au kuwa na uhusiano wa kibalozi,uanachama na jumuiya ya kimataifa.Kwa msingi huu waislam waruhusiwe kujiunga na OIC kama vile wakristo walivyokuwa na uhusiano wa kibalozi na papa ambaye ni kiongozi wa dola ya kidini ya Vatcan ya kanisa katoliki.Kama hili haliwezekani kujiunga na OIC basi iwe pia ubalozi wa Vatcan nchini Tanzania usiwepo kwa sababu ni ubaguzi wa kidini.

2. Mgawanyo wa madaraka ngazi ya Taifa,mkoa,wilaya na kata pamoja na ajira zitolewazo na serikali zigawiwe kwa usawa kwa wana dini ili kusiwepo mkandamizo kwa baadhi ya wana dini kama ilivyotokea ktk baraza la mitihani (NECTA) kwa kuwafelisha wanafunzi wa kiislam kwa makusudi.

3. Mahakama ya Kadhi itambulike kisheria kuhukumu mashauri ya waislam yanayohusundoa,talaka,mirathi,waqfu,maleziyawatoto,hibba(zawadi),wosia,biashara,bima na pawekwe kipengele cha kuzuia rufaa za mahakama ya kadhi kwenda mahakama za kawaida.Pia mahakama hii ipewe nguvu za dola na iwekewe fungu la kujiendesha kutoka serikalini.

4. Ubaguzi wa kidini ufutwe kwa kuwapa haki sawa waumini wa dini kwa siku za kuabudu kwa waislam tunataka Ijumaa tupatiwe muda wa mapumziko kwa ajili ya kutekeleza ibada ya Swala.Pia waislamu wapatiwe MoU (mkataba na serikali kwa kupatiwa pato la serikali kwa ajili ya maendeleo kama wanavyopatiwa wakristo) au kama itakuwa vigumu basi MoU kwa wakristo usitishwe.

5. Nchi yetu iwe na serikali tatu,yaani serikali ya Muungano,Serikali ya Tanganyika na serikali ya Zanzibar.Pia uraisi uwe wa kupokezana kwa Tanganyika na Zanzibar na Mambo yaliyoongezwa ktk orodha ya Muungano yajadiliwe upya vile vile Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uwe wa Mkataba.
PINDI UKWELI UNAPODHIHIRI UBAYA HUKAA KANDO.

On Thursday, November 25, 2010 2:39:39 PM UTC+3, Mabwawa wrote:
Hildegarda,
 
Nakubaliana na wewe kabisa kuwa kuna mikoa yenye maendeleo sana na hiyo ni kwa sababu watu wake walisoma...........anayepingana na ukweli huu rahisi ana lake jambo.
 
Umenikumbusha rafiki yangu mmoja ambaye yeye wakati tunataniana alikuwa ananiambia " UKIZALIWA BUKOBA TU, TAYARI UMEJIHAKIKISHIA KUMALIZA FORM 4...........

2010/11/25 Hildegarda Kiwasila <khild...@yahoo.co.uk>
Sawa kabisa, ninakubaliana nawe. Na hata kuoana rasmi watu wa dini mbali mbali wanafanya hivyo siku hizi ambapo zamani ilikuwa ni kujitangazia kifo kwa muislamu aoe kanisani, au amuoe mkristu serikalini au msikitini. Na vivyo kwa madhehebu mengine wakaoe kwa sheikk kisha arudie dini yake ilikuwa balaa.
Tutunze mazuri yetu. Asiyekubali yale ambayo yapo, si mhitaji mabadiliko ya maendeleo.


From: Bartholomew Mkinga <bmk...@yahoo.com>
To: wana...@googlegroups.com
Sent: Wed, 24 November, 2010 7:58:30

Subject: RE: [wanabidii] Re: MAHAKAMA YA KADHI - KUPATIKANA HIVI KARIBUNI

Mabeya, sidhani kuwa Hildegarda alikusudia kuwa ambaye hakusoma shule za kikristu anakosa kitu fulani ila alikusudia kuelezea jinsi ambavyo tumekuwa tukishirikiana katika mambo mbalimbali katika jamii yetu bila ya kujali tofauti zetu za kidini huku kila mmoja akijitihidi kuheshimu imani ya mwenzake bila ya kumkwaza kwa lolote. Nadhani ndiyo sababu ya kueleza kuwa wakristo wamekuwa wakiwaomba waislam kuchinja wanyama wao ili waweze kuwakaribisha waislam, wakristo wakiona kuna waislam wanakuja kushiriki katika tafrija wamekuwa hawaandai kiti moto, n.k. Msingi wake mkubwa ni kuwa kama unataka kuishi vema na jirani yako au rafiki yako ujitahidi kuimarisha yale yanayowaunganisha na kuepuka kukazania kutenda yale yanayowatenganisha. Huko ndiko kufanya mambo kwa dhamira njema.
 
Kwa upande mwingine, ningependa kumwambia Hildegarda kuwa pamoja na mapenzi yake makubwa kwa Kikwete lakini ukweli ni kuwa Rais huyu alifanya kosa kubwa la kuvunja katiba kwa kuruhusu serikali kujishughulisha moja kwa moja na mambo ya imani za kidini. Hili lilikuwa ni kosa kubwa ambalo katika nchi nyingine lilitosha kumwondoa katika kiti chake. Katiba imetamka wazi kuwa masuala yote yanayohusu imani za watu yatakuwa ni mambo ya mtu binafsi na taasisi yake ya kidini. Yeye aliwezaje kuruhusu serikali kuunda kamati itakayofanya kazi na viongoza wa dini kwa masuala ya kutimiza matakwa ya imani ya dini? Kwa tendo hili Kikwete ametuingiza kwenye mijadala ya hatari sana ambayo baadaye inaweza kuathiri umoja wa watanzania. Rais sasa hivi anasema kuna udini lakini kama kuna mtu atahukumiwa kwa kuanza kupandikiza fikra za udini ni Rais Kikwete mwenyewe, ni kwa kauli na matendo yake. Bado tunamsihi sana Kikwete kuwa nchi hii ina mambo mengi anayoweza kuyafanya akakumbukwa na watanzania wote bila ya kujali imani zao, zaidi ya hili la kuiingiza serikali katika kujishughulisha na uanzishwaji wa taasisi za kidini. Kikwete hata afanye mazuri kiasi gani lakini akituingiza watanzania kwenye utengano wa kidini, Watanzania tutamlaani na kumkumbuka kwa kosa hilo vizazi kwa vizazi maana kazi waliyoifanya watangulizi wake kwa miaka mingi yeye atakuwa imeiharibu kwa miaka yake 10, tunaomba sana hilo lisitokee. Utengano wa kidini hautamnufaisha yeyote, hata yule anayetaka masuala ya imani yake yagharimiwe na serikali.
 
Bart
 

--- On Tue, 11/23/10, Mayeye, Mussa (Buzwagi) <mma...@africanbarrickgold.com> wrote:

From: Mayeye, Mussa (Buzwagi) <mma...@africanbarrickgold.com>
Subject: RE: [wanabidii] Re: MAHAKAMA YA KADHI - KUPATIKANA HIVI KARIBUNI
To: wana...@googlegroups.com
Date: Tuesday, November 23, 2010, 7:58 AM

KIWASILA,
 
MCHANGO WAKO HAUPO KUINUFAISHA JAMII, UPO KIDINI ZAIDI,      YAANI MUWAMBA NGOMA.................!!!!!!!!
 
 
Jaribu kuziweka pembeni zile kauli amabazo zinaonyesha moja kwa moja zimejenga ubinafsi haziko kimaslahi ya jambo lenyewe.
 
MASLAHI YA JAMBO Husika ni pale unapotoa kauli za
kumuelimisha au za kutaka kuelimisha katika yale unayoyajua na kuwa na uhakika nayo
na pia kuomba kuelimishwa katika yale ambayo hauna ufaham wa elimu yake.......(HIZO NDIZO HOJA ZINAZO CONSIDER MASLAHI YA JAMBO FULANI)
 
Napoona ukitoa kauli kuwa wauza samaki, waolewaji, watumiaji wa madawa ya kuelevya wametokana na kutosoma shule za kikristu HAPO unaonyesha udhaifu wa hoja zako.
 
Kwasababu tukisema tuweke into practical sidhani kama unaweza pata ushahidi wa kuaminika.
 
Mfano mzuri mimi, sikusoma shule za kikristu, lakini leo mimi ni ENGINEER.
Mbona sijakwenda kuuza au kuvua samaki?
Mbona bado madawa ya kulevya ni adui kwangu.
 
Kauli zako nazinyima point kwa kiasi fulani, zimetetea maslhi binafsi zaidi kuliko maslahi ya taifa.


From: wana...@googlegroups.com [mailto:wana...@googlegroups.com] On Behalf Of Hildegarda Kiwasila
Sent: Tuesday, November 23, 2010 6:15 PM
To: wana...@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Re: MAHAKAMA YA KADHI - KUPATIKANA HIVI KARIBUNI

 
Labda niseme kama walivyojitetea Chadema 'Hunielewi'. Kama mwana maendeleo Jamii, ninaweza nikakusapoti unapoongea la maana, lakini nikiona umekiuka huongei cha maana ninachoona mimi cha maana nitakugeuka. Hivyo, suala hili la kadhi mimi nimelipinga toka mjadala ulivyoanza humu maana kama mwana harakati ninaelewa tabu za kutoa haki zinavyokuwa kidini na kikabila sio kwa akina mama tu hata akina baba. Ninaelewa kuna madhehemu mengi nchini. Kama ikiwa kila dhehemu mambo yake yalipiwe na GVT ni tatizo kuleta mahakama ya dhehebu moja, kesho zogo la nyingine etc. Any fool knows this. Nimesoma shule za kikristu na waislamu jirani zangu. Tena wale ambao waliona watoto wao wakisoma huko watasilimishwa au kulishwa nguruwe ndio watoto wao hawakusoma wameishia kuolea au kuvua samaki na sasa madawa ya kulevya yamewatawala. Wale ambao walisema anataka wanae wasome wafaulu-watoto wao wanapeta na wala hawakubadili dini. Tena wanajua hata kusali kikristu maana tukisali wao wanakaa sisi tunasimama. Nimeishi karibu na madrasa, ninajua nyimbo kadhaa za kasda ninaweza kuimba ila sijawa muislamu. Tuna marafiki wa dini mbali mbali kazini na mashuleni. Familia tuna ndugu wa dini mbali mbali na kama kunasherehe-wale waislamu ndio wanachinja wanyama ili nao wapate kula kipikwacho na hapo kiti moto hapikwi tena. Pia, tunafahamu wakristu na waislamu jina hawa hula nguruwe na kunywa pombe (Nipa, mnazi, mapuya, kangara, mbege, beer, konyagi n.k). Hakuna sababu ya kuweka ajenda ya udini muda huu, tuangalie mambo mengine. Kujamba ushuzi sio kupumua. kama umeshaharibu au unataka kuharibu, kusemwa ni kuelekezwa ujirekebishe. Hii ya mahakama ya kadhi-NO. hata mawe nipigwe. Ni kosa kuiingiza bungeni.


From: Mike Zunzu <mike...@yahoo.co.uk>
To: wana...@googlegroups.com
Sent: Tue, 23 November, 2010 15:43:48
Subject: Re: [wanabidii] Re: MAHAKAMA YA KADHI - KUPATIKANA HIVI KARIBUNI

Niwie radhi dada Hildegarda na pia wanabidii wengine kwani nitakachoandika hapo chini siyo mchango bali ni swali kwa dada Hildegarda, kabla ya uchaguzi alikuwa mstari wa mbele kutetea Serikali ya Kikwete na siasa zake leo anaona hitilafu ndani yake, hukuamini yaliyokuwa yakisemwa wakati ule leo ndiyo umefunguka macho?

--- On Tue, 23/11/10, Hildegarda Kiwasila <khild...@yahoo.co.uk> wrote:

From: Hildegarda Kiwasila <khild...@yahoo.co.uk>
Subject: Re: [wanabidii] Re: MAHAKAMA YA KADHI - KUPATIKANA HIVI KARIBUNI
To: wana...@googlegroups.com
Date: Tuesday, 23 November, 2010, 12:26

Unayoyasema Livingstone yanaeleweka na yana matiki. Ila, ukiona masuala wazi ya namna hii yanafanywa na serikali kama vile haioni na watu wa sheria kukaa kimya-ujue imo namna. Hii ni kufirisika kisiasa na kiutaalamu unalina kula yako-tia mchuzi pangu pakavu. Nani asiyeelewa haya usemayo? Nani asiyejua mahakama za koo, mila na kabila na za dini kama zipo? Labda hana dini huyo!! nani hajui kuwa kuna mila zinaonea na dini zinanyonya binadamu na kuonea kwa bendera ya dini? Hvyo utaona, waliowengi hukimbilia serikalini kudai haki sio kimila au kidini kwani huko haki hupunguzwa. Kufirisika kisiasa ndio kunaleta haya uyaongeayo kwa mantiki hapa na huu ndio mwanzo wa udini wimbo ambao sasa unaimbwea ili ipatikane sababu ya mahakama ya kadhi. Udini upo wapi ambapo ukienda St Mary's utakuta Idadi kubwa ya wanafunzi ni waislamu na ni ndugu na watoto wa wakubwa. Ukienda madrasa na GVT school ndio utakuta hao wa wengine na akivunja ungo tu anaolewa na 'maalim' shule ndio mwisho. Shule pekee inayotoa elimu ya ufundi au ya ujasiriamali kisiwani Mafia ni ya Kardinari Pengo ambapokisiwa hicho asilimia 97-98 ni waislamu. Waliosoma zamani hadi Mh rais Kikwete wote wamesoma shule za Kikristu na hawakusilimu dini. Yupo katika mstari kapanga foleni ya shule ya Msingi Lugoba na aliyemchokonoa na kumvuta juu aje kuwa kiongozi ni Mkristu Mtakatifu J.K Nyerere. Alisema ninawaleteeni vijana (Mkapa na Kikwete) na akawaleta. Sasa hii inayoanza leo inatoka wapi? Kufirisika kisiasa na kimaadili au ni kitu gani?
Poleni!!

From: Danny Livingstone <dannyliv...@gmail.com>
To: wana...@googlegroups.com
Sent: Tue, 23 November, 2010 12:43:08
Subject: Re: [wanabidii] Re: MAHAKAMA YA KADHI - KUPATIKANA HIVI KARIBUNI

Kinachotatiza hapa wandugu si suala la uwepo au kutokuwepo kwa mahakama ya kadhi. Madhehebu mengi au hata makabila mengi yana mifumo yao ya mahakama za kidini au za kimila. Kinachozua mijadala ni kwamba katika nchi isiyokuwa na dini maalumu kama yetu watu wote bila kujali dini zao hutozwa kodi na serikali yao. Inapokuja katika mgawanyo wa mapato hayo yatokanayo na kodi - serikali hugawa kutegemea na vipaumbele vilivyopo. Kama ikianzishwa mahakama ya kadhi kwa mfumo wa kuingizwa kwenye bajeti za serikali hii itapelekea watumishi wa mahakama hizi (wanaotokana na dini ya kiislamu) na shughuli zote za mahakama hizi (kuhudumia waislamu pekee) gharama hizo zitaingizwa katika bajeti ya kawaida ya matumizi ya serikali. Kitakachofuata ni kwamba kila dini na hata makabila yatakuwa na haki ya kudai mahakama zao za kidini na hata za kimila ziingizwe nazo katika mfumo huo, hii itaingiza vurugu katika matumizi ya kawaida - hicho ndicho kinachozua hofu katika uanzishwaji wa mahakama hizi. Kama mijadala hii ingekuwa inaendeshwa katika majukwaa ya dini husika bila kuingiza uwezekano wa kutegemea serikali katika uendeshaji wa mahakama hizi kusingekuwa na tatizo kubwa kama linavyoonekana sasa.
--
Tembelea www.naombakazi.com Kwa nafasi za kazi kila siku
 
DISCLAIMER: The contents and opinions expressed in this email are solely those of the author and do not represent those of the Moderator
 
To unsubscribe from this group, send email to
wanabidii+...@googlegroups.com

--
Tembelea www.naombakazi.com Kwa nafasi za kazi kila siku
 
DISCLAIMER: The contents and opinions expressed in this email are solely those of the author and do not represent those of the Moderator
 
To unsubscribe from this group, send email to
wanabidii+...@googlegroups.com

--
Tembelea www.naombakazi.com Kwa nafasi za kazi kila siku
 
DISCLAIMER: The contents and opinions expressed in this email are solely those of the author and do not represent those of the Moderator
 
To unsubscribe from this group, send email to
wanabidii+...@googlegroups.com

--
Tembelea www.naombakazi.com Kwa nafasi za kazi kila siku
 
DISCLAIMER: The contents and opinions expressed in this email are solely those of the author and do not represent those of the Moderator
 
To unsubscribe from this group, send email to
wanabidii+...@googlegroups.com
--
Tembelea www.naombakazi.com Kwa nafasi za kazi kila siku
 
DISCLAIMER: The contents and opinions expressed in this email are solely those of the author and do not represent those of the Moderator
 
To unsubscribe from this group, send email to
wanabidii+...@googlegroups.com

--
Tembelea www.naombakazi.com Kwa nafasi za kazi kila siku
 
DISCLAIMER: The contents and opinions expressed in this email are solely those of the author and do not represent those of the Moderator
 
To unsubscribe from this group, send email to
wanabidii+...@googlegroups.com

--
Tembelea www.naombakazi.com Kwa nafasi za kazi kila siku
 
DISCLAIMER: The contents and opinions expressed in this email are solely those of the author and do not represent those of the Moderator
 
To unsubscribe from this group, send email to
wanabidii+...@googlegroups.com



--
Wasalaam
 
Denis Matanda,
Snr Eng,
RTL -  Nzega.
P.o box 390
Nzega - Tanzania.
 
" Low aim, not failure, is a crime"

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.



--
-----------------------
Fratern Kilasara
,

P. O. Box - (Home): 62810; or (Office): 65300
Dar es Salaam - Tanzania.
Telephone (Office): +255 (0)22 2700021/4 Ext No. 239; Fax: +255 (0)22 2775591
Mobile (Personal): +255 (0)715 40 41 53 or +255 (0)754 40 41 53
Emails: kilasara.fratern@gmail.com or kilasara.fratern@yahoo.com

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment