Wednesday 29 January 2014

Re: [wanabidii] Taarifa ya CHADEMA kulaumu mwenendo wa kampeni za uchaguzi mdogo Kiembesamaki

Kosa kubwa ni kutofuata sheria ila sijaona vitendo vya Kijasusi kwa mujibu wa Taarifa hii. Nafikiri Maafisa Habari wakati wote wanapaswa kufikisha ujumbe unaopaswa na siyo kuongeza chumvi mahali isipohitajika. Inaongeza heshima

REF.CDM./HO/ZNZ/VOL .2.07/2014     
                                
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI  
 
YAH: MWENENDO WA KAMPENI ZA UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA KIEMBESAMAKI WILAYA YA MAGHARIBI UNGUJA  

CHADEMA kimezindua kampeni zake tarehe 21/01/2014 katika viwanja vya matrekta mbweni, za kumnadi mgombea wake wa uwakilishi jimbo la kiembesamaki katika uchaguzi mdogo utakao fanyika tarehe 02/02/2014.

CHADEMA imesikitishwa na mazingira yaliojitokeza katika uzinduzi wa kampeni zake  hizo kwa vitendo vilivyofanywa na 
vijana wa chama cha mapinduzi kwa kutaka kuzuia kutumia kwa kiwanja cha mpira ambacho kilipangwa na ratiba ya Tume ya uchaguzi na kusababishia usumbufu na kuchelewesha kuanza kwa mkutano huo hadi viongozi kuingilia kati  ndio vijana hao walipo ondoka na mandalizi ya mkutano huo kuendelea .

CHADEMA  imesikitishwa na vurugu zilizo endeshwa na vijana hao wa CCM kwa kuivamia ofisi ya Chadema majira ya saa tano na robo za usiku  jimbo la Kiembesamaki  iliopo Chukwani na kung’oa mlingoti wa bendera na kuondoka na bendera yetu ya chama.

Kwa vitendo hivyo vilivyofanywa na vijana hao wa CCM imeonekana kabisa kwamab chama cha mapinduzi wameshindwa kuendesha kampeni za kistaarabu na za kiungwana ,jambo ambalo linatishia kuwepo kwa amani na utulivu katika uchaguzi huo mdogo jimbo la kiembesamaki.

CHADEMA kwa vile ni chama kinachoelewa sheria na kuheshimu sheria za nchi tayari viongozi wetu wa wilaya ya magharibi walisha liarifu jeshi la polisi katika kituo cha Mazizini wakitaka uchunguzi wa kina ufanyike na hatua za kisheria zichukuliwe ili waliohusika wafikishwe katika vyombo vya sheria .

Kwa matukio hay tunalitaka jeshi la polisi kutokufanya kazi zao kwa utashi wa kisiasa ,kwani kufanya hivyo kutalishushia hadhi jeshi hilo lakini watakua na wao tutawatuhumu kuwa wanakisaidia chama cha CCM katika kuleta vurugu katika uchaguzi mdogo wa jimbo la kiembesamaki, na kujakupeleka uvunjifu wa amani kam vile ilvyojitokeza katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Bububu uliofanyika tarehe 16/09/2012 

CHADEMA kinaamini katika chaguzi  zote ni vyema vyombo vya ulinzi vikawa makini katika kutenda wajibu wao,vilevile vyama pamoja na wafuasi wao havina budi kuheshimu sheria na kanuni zote za nchi na zile za uchaguzi.

CHADEMA kinakionya chama cha CCM kiache mara moja tabia zake za kijinga na kijasusi katika kipindi hiki cha uchaguzi mdogo na kiweze kushiriki uchaguzi huo wakiwa na hoja na sio vitisho na ujangiri jambo ambalo linaweza kuhatarisha amani na utulivu tulionao vilevile kuwakosesha wananchi wa jimbo la kiembesamaki kuchagua muwakilishi wanaemtaka kwa njia ya demokrasia. CHADEMA tunaiomba ZEC nao waweze kutoa muongozo juu ya matokeo kama haya yanayo endelea.

Pamoja na hayoyaliojitokeza tunawataka viongozi wetu waendelee na kampeni kama walivyojipangia na kuwatuliza wanachama wetu wasishiriki katika vitendo vya vurugu na tuendelee na kumpigia kampeni mgombea wetu HASHIM  JUMA ISSA aweze kuwa mshindi na kuwa muwakilishi wa jimbo la kiembesamaki tarehe 02/02/2014.

Wako

………………………………
DADI KOMBO MAALIM
AFISA HABARI NA UENEZI 
OFISI YA MAKAO MAKUU CHADEMA 
ZANZIBAR



23/12/2013

YAH: TAARIFA YA KUFANYIKA  MKUTANO WA HADHARA KATIKA KIWANJA CHA MAGOGONI  KWAMABATA  UNGUJA  

Tafadhali naomba uhusike na somo la hapo juu

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinafanya maandalizi ya kufanyika kwa mkutano wa hadhara katika Kiwanja cha Magogoni kwa Mabata wilaya ya  Magharibi  Unguja.

Mkutano ambao unatarajiwa kufanyika tarehe 29/12/ 2013 kuanzia saa nane 8:00 za mchana hadi saa kumi na mbili 12: 00 za jioni.

 Kwa barua hii ofisi yangu inawasilisha kwako Taaifa ya kufanyika mkutano wa hadhara kwa ajili ya Uzinduzi wa operesheni ya M4C Kanda ya Unguja  Zanzibar , Mkutano huo utahutubiwa na Katibu Mkuu Mhe. Dk  SLAA  na viongozi wa kuu wa kitaifa kutoka ofisi ya Chadema  Makao makuu Dar es-salaam .

Ninayo matarajio makubwa kwamba ofisi yako itatoa ushirikiano unaostahili  na kuwezesha maandalizi ya shughuli husika yaweze kuendelea kwa wakati.

Ninakutakia utendaji mwema wa majukumu yako katika ujenzi wa Taifa letu.

Ahsante

…………………………..
MAKAME  SALUMU ALI 
CHADEMA  /MWENYEKITI WILAYA  
UNGUJA / ZANZIBAR

NAKALA 
MAKAMO MWENYEKITI  CHADEMA ZANZIBAR
KATIBU MKUU 

.
CHADEMA
VUGUVU LA   MABADILIKO (MOVEMENT FOR CHANGE – M4C)
Wako
…………………………………….
DADI K.MAALIM
KAIMU NAIBU KATIBU MKUU CHADEMA ZANZIBAR
202723629-pol.pdf
Download File



--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment