Thursday 14 July 2016

Re: [wanabidii] Bavicha kutoa malezi ya kihanaharakati ya Mbowe hadi ya malezi ya kisanii ya Lowassa

Nisinependa kujadili hoja hii wa kwanza lakini nitafanyaje!
Nimemhurumia mwandishi wa makala maana anaonyesha wazi anavyotamani Tanzania kuwa na vyama vya siasa makini.
Lakini anakatishwa tamaa na mwenendo wa CHADEMA. Ninasikitika kuongezea kuwa kitendo cha BAVICHA kinatposha kuwakatisha tamaa watanzania kwa kuhisi CHADEMA itakayoongozwa na watu hawa wakishautoka ujana na lemavu wanaourithi kutoka kwa Mbowe na :Lowasa.
Jingine linalosikitisha ni ukimya wa lile baraza la wazee la CHADEMA. Ulipozuka mgogoro katiya viongozi (Zitto na Mbowe) waliingilia kati. Sasa CHADEMA inayeyuka kama peremende kwenye ulimi toka uteuzi wa mgombea urais 2015 wao wako kimya.
Hii ni kuwanyima watanzania walichotarajia-Siasa za Vyama VINGI. Katibuni vyama vingi vya siasa vitabaki ni vya Mutungi (Msajili). lakini kwa raia wa kawaida itabaki ni CCM tu
--------------------------------------------
On Wed, 7/13/16, 'mpombe mtalika' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: [wanabidii] Bavicha kutoa malezi ya kihanaharakati ya Mbowe hadi ya malezi ya kisanii ya Lowassa
To: "ELISA MUHINGO' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Wednesday, July 13, 2016, 11:18 PM

Ndugu zangu,



Nalazimika kujadili kujadili umuhimu wa Jumuiya za Vijana
katika vyama
vyovyote vya siasa, lakini maana ya Jumuiya yenyewe hiyo
katika uongozi
wa chama na Taifa kwa ujumla, kutokana na hali ninayoiona
ikiendelea
ndani ya Baraza la Vijana, wa Chadema.



Kwa maoni yangu sasa na mtazamo wangu, Bavicha ya sasa, hasa
ngazi ya
taifa, imeathiriwa kwa kiasi kikubwa kimtazamo tofauti wa
kisiasa
iliyopo baina kati ya viongozi wakuu wawili Mwenyekiti
Freemani Mbowe na
Mgombea wa wa urais katika uchaguzi ujao 2020, Edward
Lowassa.



Bavicha yay a sasa, ipo kwenye kipindi cha mpito, kutoka
umoja wa vijana
wanaharakati chini ya malezi ya Mbowe kwenda kwenye umoja
wa vijana wa
wasanii chini ya Lowassa. Ni kipindi kigumu sana kwa vijana
wanaopitia
katika makuzi ya mabadiliko ya mwili, ya kutoka utotoni
kwenda ukubwani,
kwa maana ya balehe.



Viongozi wa sasa wa Bavicha wameamua kuendesha siasazao
kisanii, kwa
kumwigiza mgombea urais wao mtarajiwa wa mwaka 2020,
Lowassa, pengine
baada ya kubaini kwamba siasa za kihanaharakati za kina
Mbowe, haziwezi
kuwafikisha Ikulu mwaka 2020 kama ambavyo qwalivyoshindwa
kuingia
Magogono katika uchaguzi wa mwaka wa jana 2015.



Wote tumeshuhudia hivi karibuni mvutano wa jeshi la polisi
na bavicha
ambao waliazimia kwenda Dodoma kuisaidia polisi kuzuia
mkutano wa CCM
kwa madai nya kuungamkono kauli ya Rais Magufuli ya kuzuia
mikusanyiko
haramu hadi 2020 inakiukwa na chama chochote.



Kutoka upeo mdogo wa Bavicha na kushindwa kumwelewa Rais
Magufuli
wakatafsiri ndivyo sivyo kauli ya rais, kwamba haiwezekani
CCM ifanye
mkutano wake wa ndani tena mkutano mkuu maalum unaoruhusiwa
kikatiba.



Usanii wa Bavicha ninaousema unapatika hapa, kuwa Bavicha
hawajui
tofauti ya kimaudhuikati ya mkutano wa ndani na mkutano wa
hadhara,
wakati huo huo viongozi hao hao wa Bavicha tena kwa nafasi
zao ndani ya
umoja wao huo walikuwa wametoka Mwanza katika mkutano mkuu
na baraza kuu
la Chadema kujaza nafasi katibu mkuu wa chama chao,
iliyoachwa wazi na
Dr. Slaa, bila bugugha yeyote kutoka kwa vyombo vya dola kwa
kuwa
ulikuwa mkutano wa ndani na sio mkutano wa hadhara na
mkutano huo ndipo
alipopatikana Dr. Mashinji.



Bavicha wanaleta usanii kwa kuwa mkutano maalum uliompata
Dr. Mashinji
ulikuwa wa halali ila mkutano wa CCM wa kukabidhiwa kijiji
Rais Magufuli
na Mwenyekiti wa sasa wa CCM na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete
ni haramu
na unapswa kuzuiwa?



Bavicha hii ya sasa inayohamanika kujitoa katika siasa za
kiuhanaharakati za Mbowe na kwenda katika siasa za maigizo
za Lowassa
hawana budi kujitazama upya na staili yao ya maigizo kwani
wanajiondolea
credibility kwa watanzania na kuonekana kama kundi la
wahuni Fulani au
wapiga porojo mbele ya kamera za wana habari kwa kutafuta
kick kwa
kulumbana na vyombo vya dola.



Rais Magufuli hajakataza mikusanyiko wala mikutano ya
kisiasa yenye
lengo la kujadili na kufanya shughuli za kisiasa kwa kwa
mujibu wa
Katiba ya nchi. Alichokataza Rais Magufuli ni mikusanyiko ya
wahuni na
mikutano ya kihuni kwa kisingizio cha demokrasia.



Bavicha wanapaswa kuelewa alichopiga marufuku Rais Magufuli
ni
mikusanyiko na mikutano ya hadhara ya kisiasa inayobeba
maudhui
yaliyotangazwa na Benson Kigaila katika makao makuu ya
chadema, kwamba
Chadema kinaandaa mikutano na maandamano ya nchi nzima kwqa
lengo la
kuizuia Serikali ya Magufuli isitekeleze wajibu wake.



Rais Magufuli hajatangaza mahala kokote wala kupiga marukufu
kwa chama
cha siasa kutangaza sera zake, kutangaza itikadi yake
kuhamasisha na
kushawishi wananchi waliowengi zaidi kujiunga na vyama vyao
vya soiasa
kutumia soiasa za kiustaraabu.



Alichokikataa Rais Magufuli, ambacho kimsingi ndicho
watanzania
wanachokikataa zaidi, ni siasa za kiababe, za kutafuta shari
na
kusuguana na vyombo vya dola kama walivyokuwa wanataka
kufanya Bavicha.



--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment