Wednesday 29 May 2013

[wanabidii] Taarifa ya Polisi kuhusu habari ya Barlow iliyoandikwa kwenye gazeti la Jamhuri

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
Anuani ya Simu "MKUUPOLISI"    
Ofisi ya  Inspekta  Jenerali wa Polisi,
Simu : (022) 2110734, 
Fax Na. (022) 2135556
Makao Makuu ya Polisi,
S.L.P. 9141,
DAR ES SALAAM.
Unapojibu tafadhali taja:   
TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI
28 MAY, 2013

Jeshi la Polisi nchini linapenda kutoa ufafanuzi juu ya taarifa ambayo imekuwa ikiripotiwa katika gazeti la Jamhuri la siku ya Jumanne tarehe 21 – 27 Mei, 2013 toleo No. 81 na la tarehe 28 Mei -Juni 3, 2013 toleo No. 83, yenye kichwa cha habari "MTANDAO WA MAUAJI YA BARLOW WATAJWA NA IGP MWEMA AMPA HIFADHI MUUAJI WA BARLOW".

Taarifa hiyo siyo sahihi, kwa sababu mtu aliyehojiwa na gazeti hilo anayejulikana kwa jina la Mohamed Edward Malele ni mgonjwa wa akili ambaye mpaka hivi sasa amelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu. Mara kadhaa mtu huyo amekuwa na tabia ya kuwatuhumu viongozi na watu mbalimbali juu ya tuhuma zisizo na ukweli wowote kutokana na ugonjwa wake wa akili.

Jeshi la Polisi nchini linatoa rai kwa gazeti la Jamhuri kuwa makini na habari wananzoziandika ambazo hazijafanyiwa uchunguzi wa kutosha zenye lengo la kupotosha jamii.

Imetolewa na:-
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment