Friday 31 May 2013

RE: [wanabidii] NJAMA ZA CCM NA KINANA KUMVUA UBUNGE TUNDU LISSU.

 

 

Ndugu zangu,

Wanaharakati Zanzibar wamefungua kesi wanataka kuvunjwa kwa Muungano na Mahakama Kuu ya huko. Hili ndilo lingetushughulisha kwa sasa, ni baya, ni zito na si la kufanyia mzaha hata kidogo. Kwa nini kutumia nguvu na jitihada kukabiliana na mtu mmoja?

Kwanza mi nadhani habari za kesi/maelekezo ya kukata rufaa ni porojo tu. Kwa nini?

1.@Time limit

Muda unaoruhusiwa kukata rufaa umekwisha pita kitambo, na labda ikioneshwa "good cause" kwa nini rufaa haikukatwa kwa muda uliowekwa, rufaa hiyo itakuwa "still born"

2. @Wakata rufaa

Kiutaratibu, ni wale waliokuwa na kesi ndio wanaoruhusiwa kukata rufaa, na si vinginevyo. Kama baadhi yao waliotumwa kufanya kesi wamekwisha hama chama, ni nani atakuwa mrufani? Kama ilivyoelezwa ni kweli kwamba rufaa imeghushiwa ili kuonyesha kuwa waliokwa na kesi ndio waliokata rufaa wakati sio kweli, hilo ni kosa la kimaadili linalopsa wakili Wassonga kufutiwa leseni ya uwakili!

3. @ Nani anaweza kupinga matokeo ya uchaguzi?

Mahakama hiyo hiyo ya Rufani iliamua na kuelekeza kwamba wapiga kura hawawezi kupinga matokeo isipokuwa pale tu haki zao kama wapiga kura kuwa zimekiukwa. Haki hizo ni zile zinazohusu kupiga kura, km madai kuwa walizuiwa kupiga kura(labda hawajakaa kwenye shehia kwa miezi sita mfululizo kwa upande wa Zanzibar,au majina yao yaliondolewa kwenye daftari la wapiga kura, au kwa sababu nyingine yoyote iliyowanyima haki ya kupiga kura. Jaribio la kumuomba mapitio (review) ya uamuzi huo lligonga mwamba huko huko Mahakama ya Rufani. Kwa sasa hiyo ndiyo sheria (authority)

MJL

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment