Friday 31 May 2013

RE: [wanabidii] NJAMA ZA CCM NA KINANA KUMVUA UBUNGE TUNDU LISSU.

Mwanangu Dr.Kigwangwala,
Hoja hapa ni je ni kweli  anavyodai DR. Slaa au Mr. Slaa kuwa kuna  njama za kutumia mahakama zetu kumwondoa Mh Tundu Lissu  Bungeni? Wewe changua tu unataka kumwita Dr Slaa Dr Slaa au Mr. Slaa, (au   hata Padre Slaa, kama bado mpango wa kuimiza  udini bado CCM inataka kuuendeleza!) hiyo ni hiari yako, ila tusaidie kujibu hoja iliyopo uwanjani ndugu yangu. Sisi wengine tunamwita Dr Slaa kama wewe tunavyokuita Dr Kigwangala. Hiyo title ya DR. si muhimu kiasi hicho ndugu yangu!!!  Wewe muite chochote unachopenda lakini jibu hoja kuhusu matumizi ya mahakama kufuta ubunge wa Mh. Tundu Lissu, ni kweli si kweli? Kama ni kweli basi viongozi wa juu wa CCM wanatumia vibaya fedha za wanachama wao.  Badala ya kuzitumia pesa hizo kuwalipa mawakili  kufungua kesi za kutungwa kama hizi wawalipe vizuri watendaji wao ngazi za chini wapite huko na huko wakitetea sera za CCM.  Heshima ya mahakama zetu ikiruhusiwa kudidimia kwa kiwango kikubwa  kama ilivyo ile ya polisi  mwisho wa siku wananchi watapoza kabisa imani  na utendeaji wa haki wa vyombo vyote vya dola na watafanya mambo kama ya wale wa Mtwara ya kujichukulia sheria mkononi. Ilo halina tija kwa Watanzania wote pamoja na viongozi wa CCM, siku itakapowadia huko mbele ya safari.
Mwl. Lwaitama


From: Francis.Kasili@nmbtz.com
To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: RE: [wanabidii] NJAMA ZA CCM NA KINANA KUMVUA UBUNGE TUNDU LISSU.
Date: Fri, 31 May 2013 15:11:05 +0000

Kigwangalla
Hapa swala si prefix wala nini, usitake kukwepesha mada nzuli na elekevu ya Dr Slaa. huku kujali chama zaidi katika nchi hii badala ya maslahi ya nchi kunaturudisha nyuma sana kimaendeleo. Hapa kweli umechemsha HK nenda ukajipange upya na ukiri kuchemka kwako.
 
Regards
F.Kasili
Mob: 0784850583 or 0755850583
Always darkness will never comprehend light

From: wanabidii@googlegroups.com [wanabidii@googlegroups.com] on behalf of Dr. Hamisi A. Kigwangalla [hkigwangalla@gmail.com]
Sent: Friday, May 31, 2013 5:43 PM
To: wanabidii
Subject: Re: [wanabidii] NJAMA ZA CCM NA KINANA KUMVUA UBUNGE TUNDU LISSU.

Hivi pamoja na maelezo yote yale na mjadala wote ule mrefu kiasi kile, Wilbrod Slaa bado anatumia prefix ya 'Dr.' nyuma ya jina lake? Mhh, haya.....au naomba mnijuze labda kama aliwahi kupewa Doctorate ya heshima miaka ya hivi karibuni


2013/5/31 Mohamedi Mtoi <mouddymtoi@gmail.com>
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO
(CHADEMA)
TAARIFA KWA UMMA
KINANA, CCM WANAPANGA NJAMA ZA KUMVUA LISSU UBUNGE MAHAKAMANI!!!
Dar es Salaam, 31 Mei 2013...
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimelaani vikali njama za Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana kufufua kesi ya uchaguzi dhidi ya Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Mh. Tundu Lissu. Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr. Wilbroad Slaa amedai kwamba CHADEMA imekamata nyaraka zinazoonyesha kwamba Katibu Mkuu wa CCM Kinana amewaelekeza waliowakuwa mawakili wa makada wa CCM waliomfungulia Mh. Lissu kesi ya kupinga matokeo ya Uchaguzi wa Ubunge katika Jimbo la Singida Mashariki mwaka 2010 wafungue rufaa katika Mahakama ya Rufaa ya Tanzania ili kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dodoma iliyotupilia mbali kesi ya makada hao wa CCM dhidi ya Lissu. Kesi ya Mahakama Kuu ilitupiliwa mbali tarehe 27 Aprili mwaka jana.

Dr. Slaa alisema kwamba lengo la njama za Kinana na CCM ni kuhakikisha kwamba Mh. Lissu anafutiwa Ubunge ili asiweze kushiriki katika mchakato wa Katiba Mpya kama mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba litakalojadili na kupitisha rasimu ya Katiba Mpya baadaye mwaka huu. Dr. Slaa alisema: "Kwa kipindi kifupi ambacho amekuwa Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mbunge, Mheshimiwa Lissu amekuwa mwiba mkali kwa CCM na Serikali yake ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano. Amefumbua macho ya mamilioni ya Watanzania kuhusu masuala makubwa ya kikatiba na kisheria kwa hoja zake Bungeni. Uelewa wake mpana wa masuala hayo na wa Kanuni za Bunge umekuwa kikwazo kikubwa kwa CCM na Serikali yake pamoja na uongozi wa Bunge kupitisha mambo yao kinyume cha sheria, Kanuni za Bunge na maslahi ya nchi yetu. Uwepo wake ndani ya Bunge na ujasiri wake katika kutetea hoja mbali mbali umemzuia Spika wa Bunge na uongozi mzima wa Bunge kuwaonea Wabunge wa Upinzani na hasa CHADEMA. Mtu huyu amekuwa adui mkubwa wa CCM ndio maana Kinana anataka aondolewe Bungeni ili asiwepo kabisa katika mjadala wa Katiba Mpya Bungeni."

Kwa mujibu wa Dr. Slaa, mara baada ya Mh. Lissu kuwasilisha hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni juu ya bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria tarehe 3 mwezi huu ambapo aliishambulia Tume ya Mabadiliko ya Katiba na CCM kwa kuvuruga mchakato wa uundaji wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya kwa lengo la kuhakikisha Mabaraza hayo yanakuwa ya wanachama wa CCM tu, Kinana alimwita wakili wa kujitegemea Godfrey Wassonga wa kampuni ya mawakili ya Wassonga Associates Advocates ya mjini Dodoma na kumwelekeza afungue rufaa dhidi ya Lissu katika Mahakama ya Rufaa ya Tanzania haraka iwezekanavyo. Siku nne baadaye yaani tarehe 7 Mei, 2013, Wakili Wassonga alifungua rufaa hiyo katika Masjala Ndogo ya Mahakama ya Rufaa ya Tanzania mjini Dodoma.

Ijapokuwa rufaa hiyo inaonyesha kufunguliwa na Shabani Itambu Selema na Paschal Marcel Hallu waliokuwa walalamikaji katika kesi iliyotupwa na Mahakama Kuu, Dr. Slaa alidai kwamba watu hao hawahusiki kwa namna yoyote ile na kufunguliwa kwa rufaa hiyo. "CCM na mawakili wao wanawatumia tu wanakijiji hawa bila hata kuwapa taarifa au kuwashirikisha kwa namna nyingine yoyote. Huyu Shabani Itambu Selema amekula kiapo mahakamani Dodoma kwamba yeye na mwenzake ambaye bado ni Katibu Kata wa CCM huko kwao, hawakuambiwa chochote juu ya kufunguliwa kwa rufaa hiyo. Hawakutoa maagizo yoyote kwa Wakili Wassonga kufungua rufaa kwa niaba yao dhidi ya Lissu; hawajamruhusu Wakili huyo kupinga maamuzi ya Mahakama Kuu iliyoridhika kwamba uchaguzi wa Mbunge Lissu ulikuwa halali; hawajamlipa Wakili Wassonga kwa ajili hiyo. Huyu Wakili anafunguaje kesi au rufaa bila kuambiwa au kulipwa na 'wateja' wake? Kama huku sio kukosa maadili ya kiuwakili ni kitu gani?", alihoji Dr. Slaa.

Kuhusu ushiriki wa Kinana katika sakata hilo, Dr. Slaa alisema kwamba mara baada ya rufaa hiyo kufunguliwa, Wakili Wassonga alimwandikia Katibu Mkuu huyo wa CCM barua yenye kumbu kumbu Na. NO/KM/CCM/01/2013 kwa ajili ya "MADAI YA MALIPO YA AWALI YA SHAURI LA RUFAA KESI YA UCHAGUZI JIMBO LA SINGIDA MASHARIKI SHABANI ITAMBU SELEMA NA MWENZAKE DHIDI YA MH. TUNDU LISSU." Barua hiyo inamkumbusha Kinana juu ya 'makubaliano' kati ya Wassonga Associates Advocates na CCM kuhusu kusimamia kesi ya wanachama hao wa CCM dhidi ya Mh. Lissu ambayo baadae ilitupiliwa mbali na Mahakama Kuu. "Baada ya shauri husika nilipata maelekezo kutoka kwa wanasheria wa CCM kwamba tukate rufaa Mahakama ya Rufaa kazi ambayo tumekamilisha." Wakili Wassonga anamweleza Kinana "... katika shauri la mwanzo nilikuwa nalipwa na CCM Singida Mkoa na hawakumalizia malipo." Barua hiyo imeambatana na hati ya madai ya malipo (invoice) kwa ajili ya 'malipo ya awali' ya shilingi milioni mbili.

Dr. Slaa alidai kwamba kazi ya Lissu na wabunge wa CHADEMA ndani ya Bunge inawatisha CCM na Serikali yake ndio maana sasa Kinana anataka Lissu aenguliwe kwa kutumia Mahakama ya Rufaa ya Tanzania. "CCM inatapatapa, Bungeni hapakaliki kwa sababu ya hoja za Lissu na Wabunge wengine wa CHADEMA. Kila siku Bunge linaahirishwa ili kukwepa mijadala mikubwa juu ya matukio muhimu yanayoisibu nchi yetu. Njama za kuizima CHADEMA kwa kuipunguzia muda wa kuzungumza Bungeni zimeshindikana; mikakati ya kuvuruga hoja za CHADEMA kwa kuingilia hotuba za Kambi Rasmi ya Upinzani na kutaka sehemu za hotuba hizo zifutwe zimegonga mwamba; vitisho vya Spika Makinda na Naibu Spika Ndugai kuwasimamisha wabunge wetu hazijafua dafu. Sasa tuna taarifa kwamba Kinana anataka kuwahonga majaji ya Mahakama ya Rufaa ya Tanzania mamilioni ya fedha ili wamfutie Kamanda wetu Lissu ubunge. Naye atashindwa pia."

Akizungumzia hati ya kiapo ya Shabani Itambu Selema ambaye alihama CCM na kujiunga na CHADEMA baada ya kesi yao kutupiliwa mbali na Mahakama Kuu mwaka jana, Dr. Slaa alisema: "Tutaishangaa sana Mahakama ya Rufaa kama itaisikiliza rufaa hiyo hata baada ya aliyekuwa mhusika wa kesi ya msingi kusema kwa kiapo kwamba yeye na mwenzake hawajakata rufaa bali ni mambo ya Kinana na CCM yake!" Dr. Slaa alisema itakuwa ajabu kwa Mahakama ya Rufaa kusikiliza rufaa iliyofunguliwa zaidi ya mwaka mmoja tangu Mahakama Kuu ilipotupilia mbali kesi ya msingi. "Kwa mujibu wa kifungu cha 115 cha Sheria ya Uchaguzi, Sura ya 343, Mahakama ya Rufaa inatakiwa kusikiliza rufaa dhidi ya uamuzi wa Mahakama Kuu ndani ya kipindi cha mwaka mmoja tangu rufaa ilipofunguliwa. Huyu Kinana na CCM yake wamesubiri mwaka umepita tangu Mahakama Kuu ilipokataa kufuta matokeo ya Lissu ndio wafungue rufaa. Kama huku sio kukanyaga spirit ya Sheria hiyo ni kitu gani?", alihoji Dr. Slaa.

Aliongeza kuwa katika kesi ya Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA), Mh. Godbless Lema aliyekuwa anashtakiwa na wanaCCM pia, Mahakama ya Rufaa ilipiga marufuku wapiga kura ambao hawakunyimwa haki zao za kupiga kura kufungua malalamiko ya kupinga matokeo ya uchaguzi mahakamani. "Hata wino wa Mahakama ya Rufaa katika hukumu ya Lema haujakauka Kinana na CCM yake wanataka Mahakama ya Rufaa iyale matapishi yake kwa kusikiliza rufaa ya wapiga kura wanaodai kwa kiapo kwamba walielekezwa na wakubwa wao katika CCM kufungua kesi iliyokataliwa na Mahakama Kuu na sasa rufaa imefunguliwa kwa maelekezo ya Kinana bila hata wao kujulishwa au kushirikishwa kwa namna yoyote ile."

Dr. Slaa alisema kwamba rufaa ya sasa inathibitisha kauli inayodaiwa kutolewa na Rais Jakaya Kikwete juu ya Tundu Lissu wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu uliopita ambapo Kikwete alidaiwa kuwaambia wanaCCM mjini Singida kwamba ni afadhali Dr. Slaa achaguliwe kuwa Rais kuliko Tundu Lissu kuwa Mbunge! "Kwa kazi zake ndani na nje ya Bunge Lissu amethibitisha umahiri na uzalendo wake kwa Tanzania na kwa chama chetu. Ametetea wabunge na viongozi wetu dhidi ya njama za CCM kuwachafua kwa kuwafungulia mashtaka ya uongo mahakamani; ametetea Watanzania kila mahali nchini, na ameelimisha wananchi kwa hoja zake Bungeni. Ni mmoja wa Wabunge hodari, jasiri na wachapa kazi katika Bunge hili. Huyu ndiye Mbunge ambaye Kinana na CCM wanataka aondolewe Bungeni kwa mbinu za kishetani za aina hii. Hatutakubali na tunawataka Watanzania wasikubali!"

Rufaa dhidi ya Lissu bado haijapatiwa namba ya usajili licha ya kwamba imeshalipiwa ada ya kuifungulia na tayari imeshapokelewa na Masjala Ndogo ya Mahakama ya Rufaa ya Tanzania, Dodoma. Aidha, rufaa hiyo haijapangiwa majaji wa kuisikiliza wala tarehe ya kusikilizwa kwake haijapangwa.





---------------------------------------------------
Dr. Wilbroad P. Slaa
KATIBU MKUU
CHADEMA


Sent from my BlackBerry® smartphone provided by Airtel Tanzania.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.





--
"Vision is the ability to see the invisible!"
Hamisi A. Kigwangalla, MD, MPH, MBA
P.O.Box 22499,
Dar es salaam.
Tanzania.
Phone No: +255 754 636963
                +255 782 636963
website: www.peercorpstrust.org or www.hamisikigwangalla.com
Email: hamisi.kigwangalla@peercorpstrust.org or info@hamisikigwangalla.com
Skype ID: hkigwangalla
Blog: blog.hamisikigwangalla.com 


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 
*************************************************************************************** *************************************************************************************** This e-mail and any attachments are proprietary to NMB PLC. Any unauthorized use or interception is illegal. The views and opinions expressed are those of the sender, unless clearly stated as being those of NMB PLC. This e-mail is only addressed to the addressee and NMB PLC shall not be responsible for any further publication of the contents of this e-mail. If this e-mail is not addressed to you, you may not copy, distribute or disclose the contents to anyone nor act on its contents. If you received this in error, please inform the sender and delete this e-mail from your computer.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment